Wednesday, 29 March 2023 13:52

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 10

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo kisha ujaze nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu lifaalo zaidi.

Ufisadi ni __1__. Mtu anayejihusisha na ufisadi huitwa __2__. Ndiposa atapigiwa msemo, fulani ali __3__ Baa hili la shida __4__ kuangamiza __5__ nyingi hapa duniani __6__ maafa mengi duniani. Ni wazi kuwa asilimia yetu kubwa __7__ nao kwa njia moja ua nyingine. Ni lazima kama __8__ tushirikiane kwa __9__ kumaliza nduli huyu ili __10__

                   A                    B                       C                  D 
 1.   kumpa mtu asichostahili   kupewa kitu asichostahili   Uharibifu wa mali ya umma   kupewa pesa za nchi
 2.  ufisadi  mfisadi  fisidi  wafisadi
 3.  kula kalenda  zunguka mbuyu  kula mwande   kunywa chai 
 4.  inayotisha  linalotutishia    linaloutishia   inayotishia
 5.  jamaa  mataifa   jamii   watu 
 6.  lenye  yenye   zenye   chenye 
 7.  tumejihusisha  imejihusisha  zimejihusisha  wamejihusisha
 8.  sheria  mauti   ibada   afya
 9.  ujino na ukucha  hamu na ghamu  raghba ya mkanja  guu mosi guu pili
 10.  tugonge gogo tusikie mlio wake  tukate ubeleko kabla ya mwana kuzaliwa   tuivute ngozi kwetu  tukiwahi chuma kingali moto.

 

Ali alikuwa na __11__ kubwa ya masomo. Kiu __12__masomoni kilikuwa sawa na hamu na ghamu na mama kupata mwana. Walimu nao __13__ kumsaidia. Ali alijua na pia __14__ mwalimu mkuu angemtafutia __15__ amlipie karo ya masomo yake kwani kwao walikuwa maskini sana.

  A    B   C   D 
 11.   ari   hali   tayari   chuku 
 12.  chake   yake   lake   zake 
 13.  walimtolea   walijitoa   walijitolea   walimtolea 
 14.  kuangalia  kuamua   kutazama   kutazamia 
 15.  mthamini  mdhamini   mhadhiri   mfawidhi 

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi 

  1. Tambua aina tofauti za ki
    Ukirusha kipira hiki kitapotea. 
    1. Kitendo, chombo wakazi
    2. Mtendaji, umoja, kiashiria
    3. Nafsi, udongo, kitenzi
    4. Masharti, udongo, kiambishi ngeli
  2. Ni nomino gani dhahania?
    1. Boresha
    2. Usahaulifu
    3. Wenzo
    4. Jukwaa
  3. Ni methali gani inayolingana na maelezo haya. Ni bora kuwa na ndugu mbaya anayekusaidia wakati wa shida kuliko yule wa mbali asiyekusaidia
    1. Mui huwa mwema
    2. Damu ni nzito kuliko maji
    3. Ndugu mui heri kuwa naye
    4. Mchumia janga hula na wa kwao
  4. Uwiano wa sauti katikati na mwisho wa mshororo ni ____________________.
    1. mloto
    2. mizani
    3. kina
    4. kibwagizo
  5. Mshenga kwa posa ni kama ____________________________ kwa maji.
    1. mzegamzega
    2. topasi
    3. kungwi
    4. bawabu
  6. Chagua sentensi iliyotumia ka kuonyesha mfululizo
    1. Mwelekeze mzee akate chakula
    2. Mpira uligongwa ukadunda ukagonga kioo na kukipasua
    3. Kiti hicho kidogo kimeundika vizuri
    4. Tawi la mti lilianguka kacha lilipovunjika
  7. Maradhi mengi yameweza kuthibitiwa.
    Neno mengi limetumika kama __________________.
    1. kivumishi kimilikishi
    2. kivumishi cha sifa
    3. kivumishi cha pekee
    4. kivumishi cha idadi
  8. Andika kinyume cha
    Fahali mpole ametoka nje
    1. Ng'ombe mkali ameingia ndani
    2. Maksai mkali ametoka nje
    3. Fahali mkali ametoka nje
    4. Bakari mkali ameingia ndani
  9. Chura ni mnyama mdogo aendaye kwa kuvuka.Chura pia ni _____________________
    1. Anayefanya kazi ya kufunga mizigo chomboni
    2. Anayetumwa kupeleka ujumbe wa posa
    3. Anayetunza na kufunza farasi
    4. Anayeibuka wa mwisho katika mchezo wa watoto
  10. Taja umbo hili.
    C8swaT1SF23002Q25

    1. mchinjo kali
    2. hiram
    3. tufe
    4. mche
  11. ______________________ ni kiungo ambacho husaga chakula katika mwili wa ndege.
    1. Firigisi
    2. Kongosho
    3. Nso
    4. Wengu
  12. Chagua sentensi inayoonyesha istiara
    1. Mlo tulioula ulikuwa mtamu kama hahoe
    2. Mwizi alikamatwa na kubebwa hobelahobela
    3. Alimwangalia shashimamishi bila ya kunionea huruma
    4. Maswali yote yalikuwa mboga tu
  13. Andika kwa umoja
    Nyenzo madhubuti hutumiwa kuinulia majabali
    1. Nyenzo dhubuti hutumiwa kuinulia jabali 
    2. Uwezo madhubuti hutumiwa kuinulia jabali
    3. Wenzo madhubuti hutumiwa kuinulia jabali 
    4. Uwenzo dhubuti hutumiwa kuinulia majabali 
  14. Mwana wa punda huitwa ________________________
    1. kihongwe
    2. kiwavi
    3. kivinimbi
    4. kipunda
  15. Shungi ni kwa nywele kama vile bumba ni kwa
    1. pesa
    2. nguo
    3. pamba
    4. nyuki

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40.

Anda alikuwa kijana yatima. Wazazi wake waliuaga ulimwengu yeye akiwa mkenibe. Jambo lililompa moyo kijana huyu ni ahadi ya mjombawe kuwa angemlea vyema.

Wahenga walitueleza kuwa ahadi ni deni lakini Sango mjombake Anda hakuweka ahadi yake. Alipomchukua Anda alimpa kila aina ya mateso. Sango alimwambia mkewe kuwa hakukuwa na haja ya kumlisha mtoto asiyefanya kazi yoyote. Hatimaye alikataa kumlipia karo ya shule, jambo lililomfanya aache kusoma. Aliachia darasa la tano.

Kumtoa Anda shuleni hakukotosha, yeye na mkewe walimpa kazi ya sulubu nyumbani. Kila asubuhi alishurutishwa kufua mtumba wa nguo, kuosha vyombo na kupiga deki. Isitoshe Sango na mkewe walimpiga na kumtupia vipande vya matusi. Mtoto wa pekee wa Bwana Sango aliitwa Koto. Alikuwa akisoma shule ya Bweni jijini. Shule zilipofungwa alirudi nyumbani akiwa na huzuni kubwa. Sababu ya kujawa na biwi la simanzi ni kuwa alikuwa mkia katika somo la Hesabu na Kiswahili. Wazazi wake walimkaripia. Kwa nini ushindwe na watoto wengine shuleni?" Babake alimkemea.

Anda alihuzunishwa na hali hiyo. Jioni yake alimwambia Koto kuwa angemsaidia kudurusu. Anda alikuwa mwerevu na shuleni alikuwa akiongoza tangu darasa la kwanza. Kila siku walijifungia chumbani na kumfunza Koto hadi likizo ikaisha. Mwalimu wa Koto aliona maajabu. Koto alikuwa sasa anafunza wengine Hesabu na Kiswahili. Mwalimu alitaka kujua kilichomsababisha awe mwerevu hivyo. Kofu alimweleza juu ya Anda. Kisha alimweleza kuwa yeye hasomi tena. Mwalimu alimpelekea habari Mwalimu Mkuu ambaye alitaka kumwona Anda.

Mwalimu Mkuu alipelekwa nyumbani na Koto. Walipofika tu Sango alikataa kufungua lango. Mwalimu aliwaeleza polisi ambao walifika haraka. Anda aliokolewa kutoka katika mateso hayo. Mwalimu mkuu alimpa nafasi ya kusoma shuleni kwake. Sango na mkewe wakawa na mashtaka ya kujibu.

  1. Anda hakujua kwamba ____________________________
    1. Sango aliweka ahadi
    2. Sango ni mjombake
    3. Angepata shida maishani
    4. Angesoma vizuri
  2. Maneno 'akiwa mkembe' yana maana akiwa 
    1. mdogo
    2. mchanga
    3. kubwa
    4. mnyonge
  3. Methali 'ahadi ni deni' inatufunza kuwa
    1. tunapoahidiwa tusifanye mzaha
    2. tukiombwa pesa tutoe
    3. tukiahidi mambo tutimize
    4. tusikubali kudai madeni
  4. Kwa nini Sango na mkewe walimtesa Anda?
    1. Walikuwa na wivu
    2. Walikuwa hawana mtoto
    3. Walikuwa wazee
    4. Walikuwa katili
  5. Neno 'kushurutishwa' ni sawa na
    1. alipigwa
    2. alilazimishwa
    3. aliagizwa
    4. aliombwa
  6. Ni kauli ipi si ya kweli _________________________
    1. Anda alikuwa mwerevu
    2. Sango hakumpenda Anda
    3. Mwalimu wa Koto alimwokoa Anda
    4. Sango alikuwa na watoto wengine
  7. Kulingana na taarifa, maana ya alimkemea ni
    1. alimwonya
    2. alimgombeza
    3. alimwita
    4. alimtukuna
  8. Kulingana na kifungu, methali ipi inalenga maisha ya Anda?
    1. Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.
    2. Mola hamtupi mja wake
    3. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
    4. Mla ni mla leo, mla jana kalani
  9. Ni hatia gani walifanya wazazi wa Koto?
    1. Kumfanya Anda afue
    2. Kumdharau Anda
    3. Kumkemea mwanawe
    4. Kumnyima Anda haki yake
  10. Kichwa kinachofaa zaidi kisa hiki ni?
    1. Sango na mkewe
    2. Tutimize ahadi
    3. Koto shuleni
    4. Mwalimu mkuu wa Koto

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu swali 41-50.  

Ni ukweli usiopingika kuwa hali ya mawasiliano ya siku hizi imeboreshwa na kurahisishwa sana. Sio siku za kisogoni ambapo watu wengi waliwasiliana japo kwa taabu nyingi.

Kuanzia siku za mababu zetu, hadi miaka ya hivi majuzi, watu wengi hawakuwa na vifaa vya mawasiliano ambavyo siku hizi vimepatakaa kila mahali. Ilikuwa vigumu sana kumpata mtu na simutamba labda wale mabwenyenye tu, yaani wale watu na vyao. Redio nazo hazikupatikana kila mahali kama siku hizi. Labda ungepata redio moja ikisikizwa na watu katika kijiji kizima. Runinga nayo hata usiseme.

Ile huduma iliyotolewa na Shirika la Posta na simu hapa nchini iliwaokoa wengi katika kutuma na kupokea barua. Aidha, shirika hili liliwafaa sana watu enzi hizo kwani mja angetaka kutuma ujumbe wa dharura, angetuma telegramu na ingepokelewa upande wa pili baada ya muda mfupi labda siku moja au mbili hivi. Njia hii ilionekana kama ya haraka ya kutuma ujumbe kwani barua nyakati hizo zingechukua hata wiki tatu ama mwezi mmoja kumfikia aliyenuiwa.

Hata hivyo kutokana na uvumbuzi wa teknolojia mpya mambo yalibadilika kabisa. Uvumbuzi wa tarakilishi na mitambo mingine ya teknolojia ukabadilisha kabisa sura ya mawasiliano. Kiza kilichomfunika macho mwanadamu kikaondolewa na mwanga wa teknolojia mpya. Siku hizi si ajabu kumwona hata watoto wakiwa na simu za mkono, tarakilishi za kupakata na kadhalika. Mitambo ya mawasiliano imezagaa kote. Ukitaka kusema na aliye ulaya unabonyeza tu kiduda kwenye tarakilishi yako naye anapata habari papo hapo! Maajabu yalioje!

Kwa kutumia hizo simu za mkononi, mtu anaweza kutuma ujumbe mfupi ikiwa hataki kumpigia simu anayewasiliana naye. Kwenye tarakilishi, pia waweza kutuma baruameme au barua pepe. Aidha kuna kipepesi ambacho ni kifaa kinachotumika kuitumia au kupokea ujumbe wa barua kieletroniki. Teleksi nayo ni njia ya mawasiliano ya simu ambayo husafirisha ujumbe ulioandikwa kama ulivyo. Uzuri wa njia hizi zote za mawasiliano ya kisasa ni kuwa, ujumbe unapotumwa mtu huupata papo hapo.

  1. Chagua jibu sahihi linalotoa maelezo sahihi ya neno mawasiliano
    1. upashanaji wa habari
    2. usafirisha wa bidhaa
    3. usikilizaji wa habari
    4. matumizi ya vyombo kama simu
  2. Siku za kisogoni ni _______________________________
    1. jana
    2. siku zilizopita
    3. siku zijazo
    4. siku za usoni
  3. Ipi kati ya hizi sio njia ya mawasiliano?
    1. Teleksi
    2. Barua
    3. Simu
    4. Kambarau
  4. Neno jingine la mabwanyenye ni
    1. wazee
    2. majambazi
    3. mabingwa
    4. matajiri
  5. _________________________hushughulikia mtumiaji na upokeaji wa barua kwa mujibu wa kifungu.
    1. Shirika la usambazaji umeme
    2. Shirika la reli
    3. Shirika la posta na simu
    4. Shirika la huduma za barua
  6. Shida la kutumia ujumbe kwa kutumia barua nyakati hizo ilikuwa ipi hasa?
    1. Barua zilichukua muda mrefu kuandikwa
    2. Gharama ya kutuma barua ilikuwa juu
    3. Barua zilichukua muda mrefu kumfikia msomaji
    4. Barua zilichukua siku moja au mbili hivi kufika
  7. Ni nini kilichosaidia kuboresha hali ya mawasiliano kulingana na ufahamu?
    1. Uvumbuzi wa tarakilishi
    2. Uvumbuzi wa teknolojia mpya 
    3. Mitambo mipya
    4. Shirika la posta na simu
  8. Ni njia ipi inayofaa zaidi ukitaka kuwasiliana na mtu aliye nga'mbo ukitumia tarakilishi?
    1. simu
    2. Barua meme
    3. Barua
    4. Rununu
  9. Kulingana na msemaji katika aya ya mwisho, mtu anapotumia rukono anaweza kupiga simu au
    1. atume arafa
    2. apige picha
    3. atume picha
    4. atume pesa
  10. Faida kubwa ya njia za kisasa za mawasiliano iliyotajwa ni kuwa
    1. gharama ya mawasiliani imepungua
    2. hata watoto wadogo wana simu na tarakilishi 
    3. ujumbe unawasilishwa jinsi ulivyotumwa
    4. ujumbe unapotumwa mtu hupata papo hapo

INSHA

Andika insha itakayoisha kwa maneno yafuatayo.

.........................................nilichomoka mbio kama Swara aliyejinasua kutoka mtegoni na kufululiza moja kwa moja hadi nyumbani.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. B
  3. B
  4. A
  5. C
  6. A
  7. B
  8. C
  9. A
  10. D
  11. A
  12. A
  13. C
  14. D
  15. B
  16. D
  17. B
  18. C
  19. C
  20. A
  21. B
  22. C
  23. D
  24. D
  25. D
  26. A
  27. D
  28. C
  29. A
  30. D
  31. C
  32. B
  33. C
  34. D
  35. B
  36. D
  37. B
  38. B
  39. D
  40. B
  41. A
  42. B
  43. D
  44. D
  45. D
  46. C
  47. B
  48. B
  49. A
  50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 10.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students