Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1-15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne Chagua jibu lifaalo zaidi.
Maktaba ni 1 na ambapo watu huenda 2 . 3 maktaba si lazima liwe jengo. Hakika maktaba ni mkusanyiko wa vitabu na matini mbalimbali 4 mt anaweza kupata 5 kuhusu nyanja mbalimbali 6 maisha. 7 wewe unaweza kuwa na maktaba yako nyumbani.
1 | A. chumba ambacho kina dawa za aina mbalimbali | B. jengo ambalo linafanyiwa utafiti wa kisayansi | C. chumba ambacho kina vipuri vya ujenzi | D. jengo ambalo lina vitabu vya aina mbalimbali |
2 | A. kusomeana | B. kusomesha | C. kusomea | D. kusomeka |
3 | A. Licha ya hayo | B. Hata hivyo | C. Mbali na hayo | D. Fauka ya hayo |
4 | A. ambapo | B. ambayo | C. ambao | D. ambako |
5 | A. maadili | B. maarifa | C. maswala | D. ilhamu |
6 | A. za | B. ya | C. la | D. wa |
7 | A. Ilhali | B. Hata | C. Wala | D. Isipokuwa |
Moja 8 mali ya asili 9 humfaidi sana binadamu ni madini na vitu vya 10 .Madini huchimbwa kutoka 11 na huwa na matumizi 12 . Je 13 umewahi kuwazia namna ambayo jamii 14 ingekuwa kusingekuwa na madini 15 .
8 | A. baina ya | B. miongoni mwa | C. kati ya | D. baadhi ya |
9 | A. ambapo | B. ambayo | C. ambao | D. ambako |
10 | A. dhamani | B. thamana | C. thamani | D. mdhamani |
11 | A.ziwani | B. ardhini | C. msituni | D. mbinguni |
12 | A. mingi | B. nyingi | C. anuwai | D. yote |
13 | A., | B.: | C.? | D. • |
14 | A. yake | B. yangu | C. yako | D. yao |
15 | A.? | B.! | C.O | D.... |
Kutoka swali 16-30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua kundi lenye maneno ambayo ni vielezi
- chakula, mkate, kalamu, mkoba
- ajiri, angaza, chora, andika
- mfupi, mrefu, mwembamba
- vibaya, haraka, asteaste, vizuri
- Wingi wa sentensi "Karani yule alimpelekea katibu waraka huo" ni
- Karani yule aliwapelekea makatibu waraka huo.
- Makarani wale waliwapelekea makatibu nyaraka hizo.
- Makarani wale waliwapelekea katibu waraka huo.
- Karani wale walimpelekea katibu nyaraka hizo.
- Ni jibu lipi lenye mpangilio sahihi wa aina za maneno katika sentensi ifuatayo?
Wachezaji hawa ni shupavu kuliko wengine.- nomino, kivumishi, kitenzi, kivumishi, kihusishi, kiwakilishi
- nomino, kitenzi, kiwakilishi, kivumishi, kihusishi, kivumishi
- nomino, kielezi, kitenzi, kivumishi, kiunganishi, kiwakilishi
- nomino, kielezi, kitenzi, kihusishi, kiunganishi, kivumishi
- Malizia
Insha hii imeandikwa- ikaandikwa
- ikaandikiwa
- ikaandikishwa
- ikaandikika
- Kanusha sentensi ifuatayo:
Mkeka uliofumwa na babu uliuzwa.- Mkeka usiofumwa na babu haujauzwa.
- Mkeka uliofumwa na babu haukuuzwa.
- Mkeka ambao haukufumwa na babu haujauzwa.
- Mkeka uliofumwa na babu hautauzwa.
- Parandesi hutumiwaje?
- Kutanguliza maneno katika orodha
- Kufungia maneno halisi ya msemaji
- Kuonyesha ufafanuzi wa maneno ya ziada
- Kubainisha maneno ya awali
- Badilisha sentensi ifuatayo kwa kutumia -amba
Gazeti nililolisoma ni la kusisimua- Gazeti ambayo nililolisoma ni la kusisimua.
- Gazeti ambaye nililisoma ni la kusisimua.
- Gazeti ambalo nililisoma ni la kusisimua.
- Gazeti ambalo nilisoma ni la kusisimua.
- Chagua sentensi iliyo na ki ya masharti
- Nilikuwa nikienda dukani alipowasili.
- Anatembea kikobe.
- Kitoto kile ni cha nani?
- Nikimwona nitamsalimu.
- Nomino "Nyaraka" iko katika ngeli gani?
- U-ZI
- I-I
- I-ZI
- LI-YA
- Tegua kitendawili: Juu ya mlima kuna msitu mweusi
- chungu
- nywele
- mpingo
- makaa
- Methali inayotoa funzo kuwa:
Jambo linaloonekana kuwa rahisi kwako linaweza kuwa zito kwa mwingine.- Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno
- Bahati ya mwenziwe usiilalic mlango wazi
- Kila mwamba ngoma huvutia kwake
- Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi
- Kamilisha: Maembe yamejaa sokoni
- chepechepe
- pomoni
- nomi
- tiki
- Ujanja ni kwa sungura ilhali in kwa ajali
- kawaida
- utulivu
- ghafla
- msiri
- Meno hushikiliwa na nyama zinazoitwa
- taya
- shavu
- kaakaa
- ufizi
- Kulia ni kwa machozi. Jeraha ni kwa
- usaha
- matongo
- kamasi
- damu
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 31-40.
Imesemwa na kurudiwa tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika umaskini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu. Zaidi ya Wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa katika maeneo mbalimbali kwa sasa kufuatia uhaba wa chakula nchini Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo. Imesahauliwa kuwa karibu asilimia sabini na tano ya Wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa mwananchi na pia kuletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na muazo ya mazao katika mataifa ya nje. Wataalamu wa masuala ya zaraa wanaeleza kuwa, pato la nchi linalotokana na kilimo huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja. Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi, asilimia sabini na tano ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo. Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidhaa za kilimo katika maneno haya umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia kukithiri kwa baa la njaa.
Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi maradufu katika kushabikia kilimo ili kumaliza njaa na umaskini. Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogomadogo kuhusu mihimili a zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng'ombe, mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo. Serikali itafikia lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wavyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo. Bila hilo hatutakuwa na jingine, bali kukimbilia mataifa yaliyostawi kuomba msaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa.
- Kulingana na aya ya kwanza:
- karibu ya wakenya milioni kumi wamo katika hatari ya kufa njaa
- umuhimu wa kilimo utasaidia kujiondoa katika ukata
- wananchi wote nchini wanakufa njaa
- uhaba wa chakula umesababishwa na kutokuwa na maono
- Kifungu kimebainisha kwamba
- Mapuuza ya muda mfupi katika sekta ya kilimo ndicho kiini kikubwa cha njaa
- Pato la nchi lisilotokana na kilimo haiangamizi njaa
- Wananchi wengi huishi mijini katika mataifa yaliyostawi
- Ushuru unaotokana na zaraa za mashambani ni mdogo sana
- Kulingana na aya ya pili
- asilimia ishirini na tano haitegemei kilimo nchini
- asilimia sabini na tano inaishi mijini
- pato la Kilimo huangamiza njaa mara nne
- asilimia ishirini na tano inategemea kilimo
- Kulingana na aya ya tatu:
- mchango wa shughuli nyinginezo haupiku mchango wa kilimo
- shughuli za kilimo hazilengi kuzalisha vyakula moja kwa moja
- katika mataifa yanayostawi, wananchi wote huishi mashambani
- baa la njaa linasababishwa na uhamiaji wa wananchi mjini
- Katika mataifa mengi yanayostawi:
- wananchi wachache huishi mashambani
- idadi kubwa ya wananchi huishi mijini
- wananchi wote hushiriki katika kilimo
- asilimia ishirini na tano ya wananchi huishi mijini
- Chagua jibu sahihi kulingana na kifungu:
- Ushuru wa bidhaa za kilimo ni mchache sana
- Juhudi mara mbili zinahitajika ili kushabikia kilimo
- Jukumu kuu la serikali ni kukusanya ushuru.
- Kuomba misaada kutoka mataifa yaliyostawi hakutegemei kilimo
- Kulingana na aya ya mwisho:
- kupunguza gharama za pembejeo hakutasaidia serikali kutimiza malengo yake
- kuwekwa sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi kutahimiza malengo chanya
- kupunguza bajeti ya kilimo kutaboresha zaraa
- misaada itapunguka bajeti ya kilimo ikipunguzwa
- Shughuli zifuatazo zinastahili kuimarishwa kwa wakulima isipokuwa:
- kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo
- kuwahimiza wakulima kuzalisha matunda na mboga
- kuwajulisha wakulima kuwafuga ndege
- kutoanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.
- Maana ya "Zinazodhibiti" ni
- zinazodharau
- zinazodhoofisha
- zinazovunja
- zinazotawala
- Chagua kichwa kinachovutia tarifa hii
- Ghadhabu ya njaa
- Dhima ya zaraa
- Mataifa yaliyostawi
- Kilimo cha kisasa
Soma kifungu kituatacho kisha ujibu maswali 41-50
Hapo zamani za kale, aliishi mzee mmoja aliyejulikana kama Matongo. Matongo alimwoa banati mmoja mrembo kweli na kuweza kufanikiwa kujifungua kijana mmoja tu, aliyeitwa Mapendo. Mapendo alikuwa mtoto mzuri na babake Matongo alimkabidhi maarifa yote yaliyohitajika katika maisha ya watoto. Mafunzo haya hata hivyo yaliangukia masikio yaliyotiwa komango-hasa alipozidi kubaleghe. Matongo, bibi yake na mtoto wao Mapendo waliishi katika jamii iliyokuwa na ushirikiano, kwa neema na mabaya. Jamii hii iliishi kwa kutegemea mifugo na kulima mashamba madogo madogo. Mapendo alifunzwa akawa kijana mwerevu sana katika hirimu yake. Kwa sababu hii alianza kujihisi ameerevuka kiasi cha kuwajaribu wakuu wake akili. Kweli aliyesema akili nyingi huondoa maarifa hakukanyaga chechele. Baadhi ya mafunzo aliyofundishwa na babake ni kuwa akienda kulisha kondoo kisha avamiwe au pindi amwonapo mbwamwitu apige ukemi watokeapo na atapata usaidizi haraka sana. Siku moja Mapendo alienda kulisha mifugo mbali kidogo na nyumbani. Alifikiri na akaona ni bora apige ukemi aone kutatokea nini. "Wuuwi! Wuuwi! Wanaume kujeni haraka mbwamwitu wamevamia kondoo Wuuwi! Wuuwi kujeni!!...." Mapendo alipiga kelele. Kufumba na kufumbua wanaume wa miraba minne, mashujaa wa kijiji walifika huku wameshika nyuta na mishale. Waliduwaa kuona kijana amecheka hadi mbavu zikaanza kumuuma akitokwa na mate kwa raha. Ibura iliyoje?
Wanaume walirejea kiamboni na kumweleza Matongo kisa chote. Mapendo alipowasili alitolewa taka masikioni na kukemewa na wavyele wake. Mwana muwi haongeleki mara moja. Mapendo alirudia tendo lake mara ya pili. Nao wanaume wakaja kama safari ya kwanza. Tukio hili lilikuwa mchezo mzuri wa kuchezea watu wazima. Siku ya tatu, Mapendo alipokuwa analisha mifugo, mbwa-mwitu walitokeza ghafla kama ajali. Alipiga usiahi lakini hakuona hata mtu mmoja aliyekuja kumsaidia. Watu walidhani ni mzaha ule wake wa kawaida. Maskini Mapendo, mbwa-mwitu waliwala kondoo wote na hatimaye kumuua na kumla yeye. Mzaha mzaha wake sasa ukawa umetumbukia usaha!
- Mja aliyetia komango masikioni
- husikia anayoambiwa
- hufuata maonyo
- huwa mtiifu
- hasikilizi anayoambiwa
- Kwa nini Mapendo alitaka kuwajaribu wakuu wake?
- Alikuwa mtundu
- Alijiona kama wametoshana akili
- Ni kawaida kwa watoto kufanya hivyo
- Alikuwa mwerevu kuliko watoto wa rika lake
- Mapendo alipiga kamsa ya bandia mara ya kwanza kwa sababu
- jambo hili lilimtia furaha isiyo kifani
- alikuwa amewaona mbwa mwitu
- alikuwa akifuata maagizo ya Matongo
- alikuwa amekosa jambo jingine la kufanya
- Ni jambo lipi linaloonyesha utangamano katika taarifa hii?
- Kule kwenda kumsaidia Mapendo alipopiga ukemi mwishoni
- Kule kwenda kumsaidia Mapendo alipopiga makelele na ukemi mara ya pili
- Kutoenda kumsaidia Mapendo safari ya mwisho
- Kule kwenda kusaidia Mapendo alipoitana safari ya kwanza na ya pili.
- Banati ni
- mwanamke aliyeolewa
- mtoto wa kiume
- mtoto wa kike
- bikira
- Wazazi wa Mapendo walimkemea baada ya kupashwa habari juu ya yaliyotokea kwa sababu
- kondoo wote waliliwa mbwa mwitu
- alikuwa ameonyesha utovu wa nidhamu
- alikuwa ameonyesha ushujaa
- alikuwa amefanya jambo jema
- Ni sentensi gani inayodhihirisha ukwelli wa msemo, "Akili nyingi huondoa maarifa?"
- Wanaume wote walifika kumsaidia. kila alipowaita
- Alikuwa amepewa mafunzo mengi na babake
- Alijihisi ameerevuka zaidi kuwajaribu wakuu wake
- Alikuwa kijana mwerevu zaidi katika rika lake
- Kulingana na taarifa hii mtu wa miraba minne ni
- mtu mwenye busara na hekima
- mtu wa umri wa makamo
- mtu mkubwa na mnene
- mtu mwenye vipande vinne
- Mwana muwi haongeleki mara moja inamaanisha
- Mtoto mzuri hawezi kuharibika kwa kosa moja
- Kumbembeleza mtoto si vyema
- Mtoto mwenye nidhamu hafai kukanywa
- Mtoto mbaya haachi tabia mbaya.
- Kichwa mwafaka cha habari hii ni
- Ujanja haufai maishani
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
- Maarifa ya Mapendo
- Mtoto mtukutu.
Andika insha ya kusisimua itakayomalizika kwa maneno yafuatayo
.......................kwa hakika mvua hiyo ilitusababishia madhara mengi .
MARKING SCHEME
- D
- C
- B
- A
- B
- A
- B
- C
- B
- C
- B
- C
- A
- C
- A
- D
- B
- A
- D
- B
- C
- C
- D
- A
- B
- D
- C
- C
- D
- D
- B
- C
- A
- A
- D
- B
- B
- D
- D
- B
- D
- B
- D
- D
- C
- B
- C
- C
- D
- A
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 6.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students