KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
Neema : Salaam aleikum sahibu yangu.
Juhudi : (Kwa furaha) Aleikum salaam msena wangu. Wambaje ?
Neema : Sina la kuamba.
Juhudi : Mimi pia sina neno. Ninakuomba twende nyumbani kwetu kwa matembezi..
Neema : Nashukuru kwa makaribisho. Ningetaka kwanza niwapigie wazazi wangu simu niombe ruhusa. (Anapiga simu)
Juhudi : (Akimtazama kwa makini) Je, wamekupatia idhini?
Neema : (Kwa tabasamu) Naam! Lakini baba ameniambia ikifika saa kumi na moja jioni niwe nimerudi nyumbani.
(Wote wanatembea pamoja)
Juhudi : (Akifungua mlango) Karibu nyumbani kwetu.
Neema : Starehe! Sebule yenu inavutia sana.
Juhudi : Namshukuru Mungu kwa kutubariki na fanicha kama vile: Makochi, meza, viti na kabati.
Neema : Matendegu ya samani zenu ni ya kipekee.
Juhudi : Seremala aliyeyatengeneza ni hodari. Pia alitengeneza fremu ya mlango wetu.
Neema : (Akiangalia huku na kule) Pia ninaona televisheni, mazulia, mapazia na vitu vingine vingi.
Juhudi : Kila siku mimi hupendezwa na vitu hivi vyote.
Neema : Kusema kweli nyumba yenu inapendeza.Pia ninaona balbu zenu na picha zilizo ukutani ni za kupendeza.
Juhudi : Ninaomba Mungu awawezeshe kupata vitu kama hivi.
Neema : Inshallah!
(mazungumzo yanakatika wazazi wa Juhudi wanapoingia)
- Mazungumzo kati ya Juhudi na Neema yalianza kwa
- kuagana
- kujuliana hali
- kuomba ruhusa
- matembezi
- Kulingana na mazungumzo haya neno sahibu ni sawa na:
- Laazizi
- Msena
- Ndugu
- Jirani
- Kulingana na mazungumzo uliyoyasoma ni fanicha gani haipatikani katika sebule ya akina Juhudi?
- Makochi
- Meza
- Rafu
- Kabati.
- Neema anawaheshimu wazazi wake kwa sababu?
- Ana rafiki mzuri.
- Alimtembelea Juhudi.
- Aliomba ruhusa kabla hajaenda kumtembelea Juhudi.
- Anamsalimia rafiki yake kwa heshima.
- Ni nini kilichofanya mazungumzo hayo kuisha?
- Wakati wa kurudi nyumbani ulipofika.
- Wazazi wa Juhudi kufika nyumbani.
- Giza kuingia.
- Walichoka kuongea.
Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Tedi na Njeru walisomea shule ya Baraka. Waliishi katika kijiji cha Mamboleo. Ilikuwa kawaida yao kukutana mara kwa mara ili kusoma pamoja. Jumamosi iliyopita walikutana nyumbani kwa kina Tedi. Walikuwa wamepewa kazi ya kuchora bendera ya Kenya kwenye chati. Pia walifaa kupaka bendera hiyo rangi zake.
Tedi alikuwa amefundishwa kuhusu bendera ya Kenya na kaka yake. Kaka yake anaitwa Rashid. Tedi alichukua chati nyeupe na penseli za kuchorea. Alimwelekeza Njeru jinsi ya kuchora bendera ya Kenya. Walichora bendera vizuri na kuipaka rangi. Rashid alifika akaiona bendera waliyochora. Alifurahi na kuwapongeza. 'Je, rangi za bendera yetu zinaonyesha nini ?" Njeru alimwuliza Rashid.
Rashid aliwaeleza maana ya kila rangi. Alisema kuwa rangi nyeusi inaonyesha rangi ya ngozi yetu. Nyeupe nayo inaonyesha amani na uaminifu. Tedi na Njeru waliendelea kusikiliza kwa makini. Rashid aliendelea kuwaeleza kuwa rangi nyekundu inasimamia damu iliyomwagika wakati wa vita vya kutafuta uhuru. Nayo rangi ya kijani inaonyesha ardhi. Tedi na Njeru walifurahi. Walimshukuru Rashid kwa kuwaelimisha.
- Tedi na Njeru waliishi wapi?
- Kijiji cha Mamboleo
- Shule ya Baraka
- Nyumbani kwao
- Shuleni
- Tedi anamjali Njeru. Toa sababu.
- Alimtembelea
- Walisoma pamoja
- Alikuwa rafiki yake
- Alimsaidia kuchora bendera ya Kenya
- Ni watu wangapi waliotajwa katika kifungu hiki?
- Wawili
- Watatu
- Wannne
- Mmoja
- Kukutana mara kwa mara inamaanisha nini
- Kukutana mara nyingi
- Kukutana baada ya muda mrefu
- Kukutana mara moja
- Kukutana bila kutarajia
Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Karibu wangu mwandani, twende sote ziarani,
Tutazunguka shambani, kuna matunda mitini,
Nina mimea bondeni, na miche kando mtoni,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.
Michungwa ni tele kwangu, tena yote imezaa,
Miembe ninayo kwangu, maembe yaning'inia,
Minanasi mingi kwangu, nanasi zimezagaa,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.
Minazi ni ile kule, ina nazi na madafu,
Mipera ni ile pale, inazaa maradufu,
Mianzi nayo ni ile, kimo chake ni kirefu,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.
Ziara tumemaliza, miche ninakupa shika,
Naomba kama waweza, panda kwako ukifika,
Maswali nayo uliza, upate kufaidika,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.
- Msimulizi anamwalika mwandani wake waende wapi?
- Safari ya shambani
- Sherehe ya shambani
- Kazi ya shambani
- likizo shambani
- Kwa nini miche ilipandwa kando ya mto?
- Ili isipate magugu
- Ili isiharibiwe na wadudu
- Ili ipate maji
- Ili ipate kivuli
- Jina lingine la shambani ni gani?
- Mtoni
- Ziarani
- Kondeni
- Safarini
Swali la 13 hadi la 15.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Shangazi Naomi hututembelea kwetu kila likizo. Likizo iliyopita, nasi tuliruhusiwa kwenda kumtembelea. Tulimpelekea sukari, unga na matunda. Shangazi alifurahi sana. Mimi na kakangu pia tulifurahi kumwona.
Shangazi alituandalia chakula kilichonukia kama ruhani. Alitukaribisha mezani. Kila mmoja aliketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwenzake.Tulizingatia maagizo ya Wizara ya Afya. Kaka aliombea chakula kisha tukanawa mikono. Kila mmoja alijipakulia chakula kiasi cha kumtosha.
Shangazi alitupongeza kwa kuzingatia adabu mezani. Alitupongeza tulivyokula kwa heshima. Aidha, alisema tumelelewa vizuri. Hakuna aliyebakisha chakula kwenye sahani. Shangazi alitushukuru nasi tukamuahidi kumtembelea tena.
- Shangazi Naomi alipelekewa bidhaa zifuatazo isipokuwa
- Ugali
- Unga
- Sukari
- Matunda
- Katika kifungu hiki ni nini kinachoonyesha kuwa wahusika wanajali afya zao?
- Kuombea chakula
- Kuketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwingine
- Kujipakulia chakula cha kutosha
- Kula chakula cha kutosha
- Shangazi aliwapongeza wapwa wake kwa sababu ya
- Kula chakula na kumaliza
- Kulelewa vizuri
- Kumtembelea
- Kuzingatia adabu mezani
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Je, ___16___unajua mavazi mbalimbali? Kuna mavazi ya wanaume na ya___17__. Nguo___18___ jinsia ya kike pekee ni kama vile__19__na shimizi. Mavazi__20___ faida nyingi kwa watu.
A | B | C | D | |
16 | sisi | wewe | nyinyi | mimi |
17 | wanawake | wasichana | wavulana | wazee |
18 | wa | la | za | ya |
19 | kaptura | mashati | suruali | marinda |
20 | zina | ina | yana | una |
Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.
- Ni neno gani limeambatanishwa vizuri na aina yake?
- Mrefu- Nomino
- Gilasi -Kitenzi
- Kimbia- Kielezi
- Vizuri- Kivumishi
- Jaza nafasi kwa jibu sahihi. Yai ____ meliwa na mtoto.
- li
- i
- u
- a
- Andika sentensi hii katika hali ya umoja. Wapishi wamepika vyakula.
- Mpishi amepika chakula
- Wapishi wamepika vyakula
- Wapishi wamepika chakula
- Wapishi amepika vyakula
- Ni kundi gani lina mpangilio mzuri wa maneno kama yatakavyofuatana katika kamusi?
- Kula, pakua, pika, nawa
- Salamu, salama, salimu, sala
- Kinu, kisu, mwiko, mchi
- Zulia,tumbuu, pazia, fremu
- Pita aliukata mti huo. Katika kukanusha tunasema, Pita_____
- hataukata mti huo
- hakuukata mti huo
- hajaukata mti huo
- hakati mti huo
- Jaza nafasi kwa jibu sahihi. Wachezaji watapewa zawadi
- sasa
- jana
- kila siku
- kesho
- Chagua kiunganishi katika sentensi ifuatayo: Nitaosha matunda ili nimpe mama;
- matunda
- ili
- mama
- nitaosha
- Jaza pengo kwa jibu sahihi. Mimi nina mpira wangu. Yeye ana mpira
- yake
- wake
- lake
- chake
- Kisan ana mazoea ya kufanya mambo upesi. Mara nyingi anakosea. Je, Kisao anaweza kuambiwa methali gani ili awe makini?
- Haraka haraka haina baraka.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. kipindi cha mwisho.
- Chagua jibu sahihi. Wanafunzi walifagia darasa ______ kipoindi cha mwisho.
- kati ya
- baada ya
- ndani ya
- juu ya
INSHA
Andika insha kuhusu mada ifuatayo:
SHULE YETU
Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 2 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students