Monday, 06 March 2023 12:36

Shughuli za Kiswahili - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp
  • Kusikiliza na Kuzungumza
  • Kusoma na Kujibu Maswali
  • Sarufi


Maswali

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mwajuma na Juma wamekutana kijijini wanakoishi. Wanazungumza kuhusu machache yanayowahusu.)
Juma: Mwajuma, we, Mwajuma, Jamani hata hunisikii. Masikio ulipeleka wapi? (huku akitabasamu).
Mwajuma: Ah Jamani, pole sana Juma. Upepo ni mkali ndiyo maana sikukusikia. Hali yako vipi lakini?
Juma:  Hali yangu njema dada. Je wewe? Natumai kwema.
Mwajuma: (Kwa huzuni) Ndiyo ila si sana. Kabla tu ya kuuvuka mwaka, mlezi wangu alipata ajali na kuumia vibaya miguu. Sasa yuko hospitalini.
Juma: Pole sana Mwajuma. Maskini Bwana Shani aliumia akiwa wapi?
Mwajuma: Alikuwa akitoka dukani alipogongwa na pikipiki kisha mwendeshaji akajiendea zake. (Kwa hasira) Afadhali angesimama amsaidie.
Juma: Usijali Mwajuma. Nitakupa msaada wowote ambao utahitaji kwa kuwa wewe ni rafiki yangu. (Muda unapita) Na kuhusu shuleni?
Mwajuma: (Kwa furaha) Nafurahi kuwa sasa tumejiunga na gredi ya nne. Nilitamani sana nifike katika darasa hili.
Juma: Hata mimi vivyo hivyo (wote wanaonyesha nyuso za furaha) Dada Mwajuma, hebu twende tukamtazame mlezi wako hospitalini (wanaondoka).

  1. Kulingana na Mwajuma, ni kwa nini hakumsikia Juma alipomwita?
    1. Kulikuwa na jua kali.
    2. Juma alimwita kwa sauti ya chini.
    3. Kulikuwa na upepo mkali.
    4. Mwajuma alikuwa na huzuni nyingi.
  2. Hali ya Mwajuma haikuwa njema sana kwa sababu
    1. alikuwa amepata ajali.
    2. mzazi wake alikuwa mgonjwa.
    3. Juma alikuwa amepata ajali.
    4. mlezi wake alikuwa amepata ajali.
  3. Kulingana na mazungumzo haya, Bwana Shani alikuwa
    1. mlezi wa Mwajuma.
    2. mzazi wa Juma.
    3. mlezi wa Juma.
    4. mzazi wa Mwajuma.
  4. Bwana Shani alipata ajali wapi?
    1. Alipokuwa akielekea shuleni.
    2. Baada ya kutoka sokoni.
    3. Alipokuwa akitoka dukani.
    4. Alipokuwa pale dukani.
  5. Kilichowafurahisha Juma na Mwajuma ni
    1. kuumia kwa mlezi wa Mwajuma.
    2. kuondoka kwa mwenye pikipiki.
    3. kujiunga na gredi ya tatu.
    4. wawili hao kujiunga na gredi ya nne. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Zamani kidogo, aliishi mfalme aliyekuwa akiitwa Kinara, kumaanisha kiongozi wa wengi. Alikuwa jasiri kweli kweli. Baba yake alimwonea fahari kwa sababu ya ujasiri wake. Hakutaka mwana wake apatwe na tatizo lolote. Alimkanya mwanawe asiende vitani lakini mwanawe hakumsikiliza. Aliwashambulia majirani wanyonge katika jamii zao na kuwapokonya mashamba. Baba yake aliogopa kuwa huenda angeuawa akamwambia kuwa, badala ya kuwaua na majirani hao, ni vyema zaidi ashirikiane nao. Baadaye, Kinara alimsikiliza baba yake na kuishi kwa amani na wenzake.

  1. Kulingana na taarifa hii, jina Kinara lilimaanisha nini?
    1. Mfalme mwenye kuheshimiwa.
    2. Kiongozi wa wengi.
    3. Kiongozi mnyonge.
    4. Mfalme anayewanyanyasa wengine.
  2. Ni kwa nini baba wa Kinara alikuwa na fahari kuu kwake?
    1. Alikuwa jasiri kweli kweli.
    2. Aliwanyanganya wengine inashamba.
    3. Aliwatesa watumishi wake.
    4. Alikuwa na nguvu nyingi.
  3. Ni kwa nini baba wa kinara hakutaka mwana wake aende vitani?
    1. Mwanawe alikuwa mfalme mnyonge sana.
    2. Wanakijiji walikuwa na nguvu zaidi ya mwana wake.
    3. hakutaka mwana wake apatwe na tatizo lolote.
    4. hakukuwa na silaha za kutosha.
  4. Mwisho kabisa, kinara aliamua
    1. kuwashambulia wanakijiji.
    2. kumsikiliza baba yake.
    3. kuwavamia majirani zake.
    4. kukataa mawaidha ya baba yake. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Katika ukingo wa mbali wa msitu wa Suramawe, aliishi sungura, fisi na mbwa wanyama hawa walikuwa marafiki wa kufa kuzikana au wa chanda na pete. Wanyama wengine walishangazwa na kuwa walikuwa marafiki hata ingawa walikuwa tofauti kabisa. Siku moja, fisi alialikwa shereheni na wazazi wa mke wake kama marafiki wazuri, sungura na mbwa walikubali kumpeleka shereheni. Walipofika, walipokelewa kwa furaha tele. Baada ya kupokelewa, waliandaliwa vyakula murua na vinywaji vya kudondosha mate. Wote walikula na kunywa kwa furaha hadi wakatosheka.

  1. Ni wanyama wangapi waliokuwa wakiishi katika msitu wa suramawe?
    1. Watatu
    2. Wanne
    3. Wawili
    4. Watano
  2. Wanyama wale wengine walishangazwa na nini kuhusiana na marafiki wale?
    1. Walikuwa wakipendana hata kama walifanana.
    2. walikuwa maadui hata kama walifanana.
    3. walipendana hata kama walikuwa tofauti.
    4. walikuwa inaadui ambao walikuwa tofauti.
  3. Wageni wa fisi walipokelewa vipi?
    1. Waliandaliwa vyakula pamoja na vinywaji.
    2. walipewa mahali pazuri pa kulala.
    3. walipewa maji baridi ili wazime kiu.
    4. walipewa maji moto ili waoge kwa furaha.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Kismati aliangalia saa yake ya kiwiko, nayo ikamjulisha kuwa muda wa kuenda nyumbani ulikuwa umefika. Ijumaa hiyo, alitarajia wageni kutoka kaunti ya Jipemoyo. Ilimbidi aabiri basi ili afike nyumbani haraka. Basi lililoitwa Haraka lilitokeza ghafla. Alipomwashiria dereva alisimamisha, dereva alitii na kuliegesha kwenye stani. Alipoingia, Mwendo ukaanza kuelekea Bwagamoyo, alikoishi Kismati. Kondakta alipomtaka Kismati kulipa nauli, Kismati aligundua kuwa kibeti chake hakikuwa mfukoni. Maskini Kismati!

  1. Baada ya kuangalia saa yake, Kismati alitakiwa kwenda wapi?
    1. Nyumbani. 
    2. Kazini
    3. Basini
    4. Stanini
  2. Je, kisa hiki kilitokea lini?
    1. Jumapili
    2. Ijumaa
    3. Alhamisi
    4. Jumanne
  3. Inawezekana kuwa kibeti cha Kismati
    1. kilikuwa mbali
    2. hakikuwa mbali.
    3. kilikuwa mfukoni mwake.
    4. kilikuwa kimeibwa. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua Jibu lifoglo zaidi kati ve vale uliyopewa.

Panya ni .........16......... mdogo na mharibifu. Yeye huishi........17.........ya shimo. Hutoka shimoni wakati ana njaa. Yeye ........18......... mahindi, karatasi, vitabu na nguo. Huwasumbua watu sana lakini watu wametafuta njia za kumnasa na........19.........Wengine hutumia sumu na wengine huurmia ........20.........

  1.                                    
    1. ndege
    2. mtu
    3. mnyama
    4. nyama
  2.                    
    1. nje
    2. ndani
    3. juu
    4. mbele
  3.              
    1. hataki
    2. hali
    3. hapendi
    4. hula
  4.                  
    1. kumwua
    2. kumpenda
    3. kumshtaki
    4. kumla
  5.                  
    1. mashimo
    2. mahindi
    3. mitego
    4. chakula 

Katika swali la 21-30. jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Ni chombo gani kati ya hivi hupatikana sokoni?
    1. Nyundo
    2. Rejesta
    3. Ubao
    4. Ratili
  2. Tumia kihusishi bora zaidi kukamilishia sentensi ifuatayo:
    Ndege mkubwa ametua...............................mti.
    1. ndani ya
    2. juu ya
    3. miongoni mwa
    4. katikati ya
  3. Wanyama walioshiba walilala
    ...................................mti kwenye kivuli.
    1. chini ya
    2. kati ya
    3. katikati ya
    4. juu ya
  4. ............................ni ndege wa nyumbani.
    1. Mwewe
    2. Heroe
    3. Korongo
    4. Bata
  5. Chagua sentensi iliyo na kikomo.
    1. Je, mliwaona walimu wangapi?
    2. Lo! Kumbe alikuwa mwizi!
    3. Leo ni siku ya Jumapili.
    4. Wazazi wameanza mkutano
  6. Mtu anayetengeneza vifaa vya mbao huitwaje?
    1. Dereva.
    2. Seremala.
    3. Fundi.
    4. Askari.
  7. Chagua sentensi iliyo katika wakati ujao.
    1. Wanyamapori watalindwa vyema.
    2. Mwalimu alisahihisha makosa yangu.
    3. Mtoto anapenda kunywa maziwa.
    4. Paka wetu alimnasa panya mnono.
  8. Mwezi wa Julai hufuatwa na mwezi gani?
    1. Septemba.
    2. Juni
    3. Agosti
    4. Mei
  9. 79 kwa maneno ni
    1. tisini na saba.
    2. tisini na nne.
    3. sabini na sita.
    4. sabini na tisa.
  10. Je, ni sentensi gani iliyo katika nafsi ya kwanza?
    1. Alisema atamletea miwa.
    2. Wageni wao wote walikwa warefu.
    3. Nilichora picha nzuri ubaoni.
    4. Umeamua kufanya bidii.


Majibu

swa

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili - Grade 4 Opener Exams Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students