Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall -
(Mwalimu na wanafunzi wamo darasani wakijadiliana kuhusu wanyama na umuhimu wao.)
Mwalimu: Haya wanafunzi wangu wakati ule mwingine niliwaeleza kuwa kunavyo vikundi viwili vya wanyama.
Tobi: Naam, na kumbuka jana baba yangu aliniambia kuwa wanyama wengine huishi na wanadamu nyumbani huku wengine wakiishi misituni. Mwalimu: Hakika. Wanaoishi na wanadamu nyumbani huitwa wanyamahowa ilhali wanaoishi misituni ndio wanyamapori. Wengi wa wanyamapori huhifadhiwa katika mbuga za wanyama.
Huna: Nawapenda wanyama hawa kwa kuwa wao hutusaidia. Ng'ombe, mbuzi na ngamia hutupa nyama na maziwa, nguruwe hutupa nyama nao kondoo hutupa nyama na manyoya.
Tim: Naam, tena baadhi ya wanyamahowa hufugwa kwa ajili ya huduma. Mbwa ni mlinzi mizuri wa nyumbani, punda hutusaidia kukokota mikokoteni yenye mizigo nao paka huwakamata na kuwala panya waharibifu.
Mwalimu: Kwa upande mwingine, wanyamapori huwavutia watalii ambao huitembelea nchi yetu. Wanapowaona, wao hulipa pesa za kigeni ambazo hutumika kuijenga nchi. Kwa hivyo, wanyama wote wana umuhimu mkubwa kwetu.
- Kulingana na mazungumzo uliyoyasoma, wanyama huweza kugawanywa katika
- waishio na wasioishi.
- wanyamapori na wanyamahowa.
- vikundi vinne.
- wale wa asili na wale wa kigeni.
- Wanyama wasioishi na wanadamu nyumbani
- huitwa wanyamahowa.
- butusaidia katika shughuli za nyumbani.
- huishi mbugani.
- hutupa vyakula murua.
- Watalii wanapoitembelea nchi yetu, wao
- hulipa pesa za kigeni.
- hulipwa pesa za kigeni.
- hurudi na wanyama wetu katika nchi
- huja na wanyama kutoka katika nchi zao.
- Ni kundi gani la wanyama hutupa vyakula vya aina moja?
- Paka, mbwa na punda.
- Kondoo, nguruwe na mbuzi.
- Ngamia, mbuzi na paka.
- Mbuzi, ngamia na ng'ombe.
- Kulingana na mwalimu, umuhimu mkuu wa wanyamapori ni kwamba wao
- huwavutia watalii wa humu nchini.
- huiwezesha nchi yetu kupata pesa za kigeni.
- huwa walinzi wazuri wa nyumbani.
- hutusaidia kukokota mikokoteni.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Hapo zamani za kale, wanyama wote waliishi msituni. Walifanya kazi zao pamoja ili wapate chakula cha kuwatosha. Chakula kilichopatikana kiligawanywa kwa usawa miongoni mwao. Kila siku, walirauka kwenda shambani. Mbwa, Fisi na Simba walienda kuwawinda ndege ambao baadaye waliwaleta na kuwagawia wenzao.
Paka alikuwa mvivu asiyependa kufanya kazi. Hakutaka kuchafuka. Alishinda siku nzima akiisafisha miguu yake kisha baadaye kwenda kula. Kuona hivi, wanyama wale wengine wakakasirika sana. Waliamua kuficha chakula chote. Hata hivyo, Paka alinyemelea na kuingia katika ghala polepole akala chakula chote. Wanyama waliamua kumkamata Paka huyo mvivu. Walimwambia Mbwa awe mlinzi wa ghala. Paka alipokuja, mbwa alibweka kwa sauti. Wanyama wote waliamka na kumfukuza Paka. Paka aliamua kwenda kwa binadamu kuishi. Aliahidi kuwashika panya. Wakawa marafiki.
- Wanyama hawa walipata chakula chao kwa
- kufanya kazi pamoja kwa bidii.
- kuwaibia wanyama wengine.
- kuwawinda wanyama wadogo.
- kuishi pamoja kwa amani.
- Wanyama wale wengine walimkasirikia Paka kwa sababu
- alikila chakula chote ghalani.
- hakufanya kazi kama wao.
- aliiba chakula kutoka ghalani.
- aliwasumbua wenzake.
- Je, Mbwa alifanya nini Paka alipoenda katika ghala?
- Alibweka kwa sauti.
- Aliwaita wanyama wale wengine.
- Aliwakamata panya.
- Alimfukuza paka.
- Paka alimwahidi nini mwanadamu?
- Kuwa rafiki yake mkubwa.
- Kuwakamata ndege.
- Kufanya kazi shambani.
- Kuwashika panya.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Ilikuwa siku ya Jumamosi karibu saa tano hivi asubuhi. Pendo, kaka yake Ali na mama yao walianza safari kuelekea katika soko la kijijini mwao, soko la Malimengi. Soko hilo lilikuwa karibu na uwanja wa ndege. Ilikuwa ndiyo Juniamosi ya kwanza tangu shule zilipofungwa. Siku hiyo, walipaswa kununua bidhaa kama vile sukari, mchele, mafuta na nguo za kuwapelekea nyanya na babu yao walioishi huko Konoike.
Walipofika sokoni, waliwapata watu wengi sana. Kwa sababu ulikuwa nisimu wa sherehe za Idi, mavazi yalikuwa ya bei ghali sana. Iliwabidi wanunue mchele, sukari na mafuta pekee. Nguo wangenunua kwingine.
- Karibu saa tano hivi asubuhi,
- safari ya kuenda kijijini ilianza.
- safari ya kwenda sokoni ilianza.
- kina Pendo walifika nyumbani.
- shule zilifungwa.
- Kina Pendo walipaswa kununua
- nguo, sukari na mchele.
- mafuta, sukari na mchele.
- mafuta, sukari, nguo na mchele.
- nguo, sukari na mafuta.
- Safari hii iliandaliwa katika msimu wa sherehe gani?
- Krismasi
- Pasaka
- Jumamosi
- Idi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Asubuhi hiyo, niliamka nikiwa nimechelewa. Nilijua kuwa rafiki zangu, Rama na Veli walikuwa wakiningoja katika stani. Siku zote, tulishindania kiti cha mbele katika basi letu la shule. Mara nyingi nilikuwa wa kwanza katika stani. Kwa hivyo mara nyingi nilikiwahi kiti hicho. Tuliahidiana kuwa yeyote ambaye alikiwahi kiti hicho cha mbele angegawiwa vipande vya mikate na wenzake waliochelewa wakati wa mapumziko. Upesi, niliunawa uso wangu na kuvalia sare zangu nikatandika kitanda changu na kukisafisha chumba changu. Baadaye, nilielekea sebuleni kupata kiamshakinywa. Niliteremsha chai kwa sambusa upesi na kuondoka.
- Ni nini ambacho mwandishi alijua kuwahusu Rama na Veli? Kuwa
- walikuwa katika basi la shule.
- walikuwa wakimngoja.
- wangekuwa wa kwanza kukiwahi kiti cha mbele.
- tayari walikuwa wamefika shuleni.
- Ni nini ambacho mwandishi na wenzake walikishindania?
- Kufika shuleni mapema.
- Kula vipande vya mikate.
- Kuabiri basi la shule.
- Kukiwahi kiti cha mbele.
- Kabla ya msemaji kupata kiamshakinywa, alifanya haya yote ila
- kukiwahi kiti cha mbele.
- kukisafisha chumba chake.
- kukitandika kitanda chake.
- kuunawa uso wake.
Soma kifungu kifuatacho. Chagua Jibu lifaalo zaldi kati ya yale uliyopewa.
Maji ni uhai. Bila maji, ___16___ binadamu hata mmoja ambaye anaweza ___17___. Binadamu ___18___ huyategemea maji moja kwa moja. Maji hayo hutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kunywa, kupikia, kuoshea vyombo na shughuli nyingine za nyumbani. ___19___ inapokosekana, maji hutumika kunyunyizia ___20___. Maji yatumiwayo kunyunyizia huweza kupatikana mitoni, mabwawani na maziwani.
A | B | C | D | |
16. | hakuna | kunaye | kuna | wapo |
17. | kuisha | kufa | kuishi | kufariki |
18. | sote | wote | zote | yote |
19. | Mvua | Maji | Mimea | Mawingu |
20. | shamba | wafu | mvua |
Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Ni shughuli gani hapa haipatikani nyumbani?
- Kupalilia mimea.
- Kusafisha nyumba.
- Kufua nguo.
- Kuosha vyombo.
- Katika sentensi Mbwa mdogo amebeba mfupa katika meno yake, nomino ni zipi?
- Mdogo, mfupa, yake
- Mbwa, mfupa, meno
- Mdogo, amebeba, katika
- Yake, katika, mfupa
- Tisini na sita ni
- 69
- 66
- 99
- 96
- Ni gani hapa ni maelezo sahihi kuhusu matumizi ya kikomo katika sentensi?
- Hutumiwa mwanzoni mwa sentensi.
- Huweza kuwa katikati ya sentensi.
- Hutumiwa mwishoni mwa sentensi.
- Haiwezi kutumiwa sentensi ikianza kwa herufi kubwa.
- Ni yupi hapa ameambatanishwa na kazi yake kwa usahihi?
- Dereva - hutengeneza magari yaliyoharibika.
- Mpishi - hukuza mimea na kuwafuga wanyama
- Mwalimu - huwalea watoto majumbani mwao.
- Seremala - hutengeneza vifaa kwa kutumia mbao.
- Je, ni mwezi gani huwa baina ya Julai na Septemba?
- Agosti
- Oktoba
- Juni
- Mei
- Nywele huota ___________________ kichwa.
- ndani ya
- katikati ya
- juu ya
- chini ya
- Tumia kihusishi bora zaidi kukamilisha sentensi hii.
Mti mrefu uko _______________________ darasa letu.- chini ya
- nje ya
- ndani ya
- juu ya
2
- Ili kuwaangamiza wadudu waharibifu shambani, wakulima
- hupalilia.
- huvuna.
- hunyunyiza maji.
- hupiga dawa.
- Ni sentensi ipi iliyo katika nafsi ya tatu?
- Mwanaisha ataimba jioni.
- Mimi niliimba jioni.
- Nyinyi msiimbe jioni.
- Sisi hatutaki kuimba jioni.
MARKING SCHEME
- B
- C
- A
- D
- B
- A
- D
- A
- D
- B
- C
- D
- B
- D
- A
- A
- C
- B
- A
- D
- A
- B
- D
- C
- D
- A
- C
- B
- D
- A
Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End Term 1 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students