Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 hadi 5.
ZOEZI: 1
KUSOMA KWA UFAHAMU
Swali la 1 hadi la 5.
Sasha: (Akimtazama) Sabalkheri Kiki!
Kiki : (kwa furaha) Aheri rafiki yangu!
Sasha: Nina furaha kubwa kujiunga na gredi ya tano.
Kiki : Mimi pia sijawahi kuwa na furaha kama niliyo nayo.
Sasha : Tutafanya nini ili tuwe wanafunzi bora mwaka huu?
Kiki : (akijikuna kichwa) Ni lazima tuwe na nidhamu. Unakumbuka mwaka jana....
Sasha ; (akimkatiza) Mwaka jana tuliwasumbua walimu sana kwa tabia zetu mbaya.
Kiki : Huu ukiwa mwaka mpya lazima tutabadilisha.
Sasha : Naam! Tutakuwa wavulana wenye adabu.
Kiki : Ndiyo sahibu. Tutakuwa tukikamilisha kazi, kumsikiliza mwalimu, kutulia darasani.
Sasha : (Akimdakiza) na kuwaheshimu wenzetu.
Kiki : Isitoshe ni vyema kutunza mazingira yetu darasani na nje ya darasa.
Sasha : (Akimkazia macho) Unakumbuka ulivyokuwa ukitupa taka ovyo mwaka jana!
Kiki ; Hayo yote yamepita. Nimeamua kuwa mwanafunzi bora zaidi shuleni.
Sasha : Mungu atakujalia.
Kiki : Asante sana. Sasa tujiandae kwa kipindi cha kwanza.
Sasha : Tutazungumza zaidi wakati wa breki.
- Mazungumzo uliyoyasoma yalifanyika wakati gani?
A. jioni B. Adhuhuri C. Asubuhi D. Magharibi - Sasha na Kiki walikuwa darasa gani mwaka jana?
A. Gredi ya tatu B. Gredi ya sita
C. Gredi ya nne D. hatujaambiwa - Si kweli kusema kuwa Sasha na Kiki
A. ni wa jinsia tofauti. B. ni wavulana.
C. hawakuwa na maadili mwaka jana. D. wameamua kubadilika, - Ni maadili gani hayajatajwa katika mazungumzo haya?
A. Kutunza mazingira B. Kutulia darasani
C. Kuwaheshimu wengine D. Kusoma kwa bidii - Neno rafiki lina maana sawa na
A. jirani B. adui C. sahibu D. jinsia
Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Sitawahi kuusahau muhula wa tatu nikiwa katika Gredi ya nne. Shule yetu ya Waridi ilituandalia safari ya kuzuru mbuga ya wanyama ya Masai Mara. Mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa na furaha isiyo na kifani.
Mbugani, tuliwaona wanyama wa kila aina. Tuliwaona wanyama wala nyasi kama vile: Nyati, ndovu, kifaru, twiga na swara. Isitoshe tulibahatika kuwaona wanyama walao nyama mathalani simba na chui. Licha ya hayo kulikuwa na fisi na tai ambao hula mizoga. Tulifurahia sana kuwaona kongoni wakivuka Mto Mara. Kongoni ni kivutio kikuu cha watalii katika mbuga hii.
Mwelekezi wa ziara yetu mbugani alitueleza kuhusu faida za wanyama pori kwa taifa letu. Kwa mfano, wanyama wa pori huvutia watalii wengi nchini. Watalii wakija, huiletea nchi yetu pesa za kigeni zinazosaidia kukuza uchumi wetu. Ziara hii ilitufunza kuwa, kutembea kwingi ni kuona mengi.
- Safari iliyosimuliwa ilifanyika muhula gani?
- Muhula wa mwisho wa mwaka
- Muhula wa pili
- Muhula wa kwanza
- Muhula wa kufungua mwaka
- Kati ya wanyama hawa ni gani hajaambatanishwa na chakula chake?
- Nyati-Nyasi
- Simba-Nyama
- Tai- Mizoga
- Chui- Nyasi
- Je, ni mnyama gani ametajwa kama kivutio kikuu cha watalii nchini?
- Twiga
- Kongoni
- Ndovu
- Kifaru
- Faida ya watalii kwa nchi yetu ni gani?
- Kuwaona wanyama.
- Kufurahisha wanafunzi.
- Kusaidia kukuza uchumi.
- Kuzuru mbuga ya wanyama.
Swali la 10 hadi la 12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Kwanza ni mwanafunzi anayependa kutumia wakati wake vizuri. Kila siku katika likizo yake alikuwa na ratiba. Hakupenda kuupoteza wakati wake hata kidogo. Ifuatayo ni ratiba ya siku yake moja
Asubuhi | Adhuhuri | Magharibi | Usiku nchanga |
Kula kiamshakinywa |
kulachamcha | kusoma vitabu vya hadithi | kutazama habari za jion |
kufanya kazi ya ziada |
kutazama habari za adhuhuri kwenye runinga |
kucheza kandanda | kula chajio |
kucheza | kupumzika | kuoga | kwenda kulala |
- Kinachomsaidia kwanza kutumia wakati wake vizuri ni.
- ratiba
- saa
- wakati
- siku
- Ni shughuli gani inayopatikana katika kila kipindi?
- Kucheza
- Kusoma
- Kula
- Kutazama habari
- Kwanza hutunza usafi wa mwili wake wakati gani?
- Asubuhi
- Usiku mchanga
- Adhuhuri
- Magharibi
Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Kijiji cha Busara kina wakazi wengi sana. Wakazi hawa walifurahia utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima. Bi. Adili ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Inua Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi. Adili alitumia nafasi hii kuwashauri. Bidii ya Bi. Adili ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika, wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi.Adili. Waliandaa sherehe kubwa walimtuza Bi. Adili kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.
- Wanakijiji cha Busara walifurahia ,kwa muda mrefu.
- fujo
- hali ya amani
- vijana
- Bi. Adili
- Vijana wa kijiji cha Busara walibadilika vipi baada ya kushauriwa?
- Walivalia mavazi yasiyofaa
- Walikataa kwenda shuleni
- Walianza kuwatii watu wazima
- Walikosa heshima
- Waliandaa sherehe inamaanisha:
- Walitayarisha sherehe
- Walisafiri shereheni
- Walizuru sherehe
- Walimaliza sherehe
ZOEZI 2:SARUFI
Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo Zaidi kati ya yale uliyopewa.
Mchezo 16 kandanda hupendwa na watu 17 . Kila mtu huwa na 18 kumi na 19 Timu ambayo hushinda ni ile iliyofunga 20 mengi.
A | B | C | D | |
16. | wa | ya | cha | la |
17. | mingi | vingi | wengi | nyingi |
18. | waimbaji | waigizaji | mashabiki | wachezaji |
19. | moja | mmoja | wamoja | kimoja |
20 | mabao | alama | maksi | mikwaju |
- Tazama picha hizi kisha ujibu swali.
Ni jibu gani lililoambatanisha nomino za picha na ngeli zake?
Ng'ombe (a) Kiti (b)- KI-VI A-WA
- A-WA U-I
- I-ZI KI-VI
- A-WA KI-VI
- Juma amempata mwalimu wake majilisini asubuhi akamwamkua, "Shikamoo mwalimu." Je. mwalimu alimjibu vipi?
- Binuru
- Marahaba
- Salama
- Aleikum salaam
- Kati ya maneno haya ni gani lililo katika hali ya ukubwa.
- Mto
- Jito
- Kijito
- Mito
- Tazama picha hii kisha utumie kihusishi mwafaka.
Mpira uko Meza.- juu ya
- kando ya
- chini ya
- mbele ya
- Chagua kundi ambalo lina vitenzi pekee.
- Nyumba, kiti, simul
- Chora, imba, lala
- Safi, kubwa, dogo
- Polepole, haraka, sana
- Badilisha sentensi hii katika wingi: Mgeni amefika kwangu leo.
- Wageni wamefika kwetu leo.
- Wageni wamefika kwangu leo
- Mwenyeji amefika kwetu leo.
- Mgeni hajafika kwangu leo.
- Chagua jibu sahihi. Rafiki yangu amekuwa
- mfupi
- mnene
- mjanja
- mrefu
- Chagua jibu linalofaa kujaza nafasi.
Lila ameosha nguo. Nguo .na Lila.- zimeoshewa
- zimeoshwa
- zimeoshea
- zimeosheka
- Kanusha sentensi hii:
Ninasoma kitabu sasa.- Sisomi kitabu sasa.
- Hatusomi kitabu sasa
- Sitasoma kitabu sasa.
- Sijasoma kitabu sasa.
- Umefika katika dukakuu. Kabla hujaingia, mlinzi amekukumbusha uvae barakoa, utamwambiaje?
- Karibu
- Asante
- Hongera
- Salimini
INSHA
Kuandika(Alama 10)
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha kuhusu mada ifuatayo:
SIKUKUU YA KUPENDEZA
MWONGOZO KISWAHILI
- C
- C
- A
- D
- C
- A
- D
- B
- C
- C
- C
- D
- B
- C
- A
- A
- C
- D
- B
- A
- D
- B
- B
- C
- B
- A
- C
- B
- A
- B
Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 set 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students