Soma kifungu hiki Cha mazungumzo kisha ujibu swali la 1-5.
Onyango: Sabalkheri Lucia?
Lucia: Aheri Onyango. Habari za likizo?
Onyango: Njema sana, labda yako.
Lucia: Yangu pia ilikuwa njema. Wakati wa likizo wavyele wangu walinipeleka kwa nyanya.
Onyango: (Kwa furaha) Inaonekana kuwa likizo yako ilijawa na mema.
Lucia: Naam! nyanya alinisimulia hadithi chungu nzima za kusisimua. Baada ya kila hadithi ningepata
mafunzo mengi.
Onyango: Nami ningependa kujua mafunzo uliyopata.
Lucia: Ngano ya sungura na fisi ilinifunza umuhimu wa kushirikiana na wengine.
Onyango: (Huku akitikisa kichwa) Likizo ijayo nami pia nitahakikisha nimeenda kumzuru nyanya.
Lucia: Hakika sahibu yangu. Hilo ni wazo zuri sana. Naomba kwenda darasani. Kuwa na siku njema.
Onyango: Nawe pia Lucia.
Maswali
- Sabalkheri ni salamu za wakati upi?
- Jioni
- Wakati wowote
- Adhuhuri
- Asubuhi.
- Onyango na Lucia walipatana lini?
- Kwa nyanya yao
- Wikendi
- Baada ya likizo
- Disemba.
- Taja hadithi moja iliyotajwa kwenye kifungu hiki
- Onyango na Lucia.
- Nyanya na Lucia.
- Sungura na fisi.
- Nyanya na wavyele.
- Tambua kisawe cha 'wavyele' kama ilivyotumika kwenye mazungumzo
- Mama
- Wazazi
- Abu
- Rafiki.
- Lucia alifurahia nini alipokuwa kwa nyanya yake kulingana na kifungu?
- Hadithi za nyanya.
- Kulisha mifungo.
- Kupalilia mimea.
- Kupiga deki.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 6-10.
Dawa za kulevya pia huitwa mihadarati. Dawa hizi huwa na madhara mengi hasa kwa siha zetu. Dawa hizi husababisha vifo pia. Hivyo basi, tunapaswa kuepuka matumizi ya dawa hizi kabisa.
Baadhi ya njia za kuepuka matumizi ya mihadarati ni kusikiliza na kufuata ushauri tunaopewa shuleni na walimu wetu. Walimu huwashauri wanafunzi kuhusu madhara ya dawa za kulevya na jinsi ya kujiepusha na dawa hizi. Mwanafunzi pia anaweza kuingizwa katika matumizi ya dawa hizi na marafiki wapotovu. Ni vyema wanafunzi kuwachagua marafiki wao kwa uangalifu sana.
Wanafunzi pia hawapaswi kutazama filamu na vipindi vinavyopotosha mitandaoni. Vipindi hivi huonyesha wanaotumia dawa hizi kama mashujaa na ni kinyume na maadili.
Hatimaye vijana wanahimizwa kujihusisha na shughuli na michezo mbalimbali wakati wao wa mapumziko ili kujiepusha na fikra za kutaka kujaribu dawa hizi.
Maswali
- Kulingana na aya ya kwanza mihadarati ni nini?
- Dawa za afya.
- Dawa za kulevya.
- Dawa za nguvu.
- Dawa mbovu.
- Ili wanafunzi wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya, wanafaa kufuata ushauri wa nani?
- Mwalimu
- Marafiki
- Rika
- Mitandao.
- Wanafunzi hutazama wapi vipindi na filamu zinazohusu dawa za kulevya?
- Nyumbani
- Shuleni
- Mtandaoni
- Vitabuni.
- Ipi kati ya njia hizi itasaidia kuepuka matumizi ya dawa za kulevya?
- Kusikiliza ushauri wa mwalimu.
- Kuwa na marafiki wapotovu.
- Kutazama filamu na vipindi vinavyoimarisha matumizi ya dawa za kulevya.
- Kutumia muda wa mapumziko kutumia dawa za kulevya.
- Tambua mada inayofaa zaidi kwa kifungu hiki
- Dawa za kulevya.
- Maafa ya dawa za kulevya.
- Wanafunzi na dawa za kulevya.
- Ushauri.
Soma kifungu hiki kwa makini kisha ujibu Swali la 11-15.
Mapambo ni vitu vinavyovaliwa mwilini ili kufanya mtu awe wa kuvutia. Mapambo huvaliwa katika sehemu mbalimbali za mwili. Kuna mapambo ambayo hutumiwa kwa kupaka. Mapambo hasa hutumiwa mtu anapohudhuria sherehe kama za harusi na kadhalika.
Kuna mapambo ya aina mbalimbali ya kike na kiume. Aidha kuna mapambo kama vile ushanga, pambo ambalo huvaliwa na wanawake shingoni. Mapete na vipuli huvaliwa sikioni na wanawake. Pete huvaliwa kwenye kidole cha pete na wanawake kwa wanaume. Hina nayo hupakwa mikononi na miguuni. Ni vizuri kuyatumia mapambo ifaavyo.
Maswali
- Kwa nini watu hutumia mapambo?
- Ili kuvutia
- Ili kusafiri
- Ili kulala.
- Ili kuchukiza.
- Mapambo hutumiwa kwa kuvaa na
- kuangalia
- kula
- kupaka
- hakuna.
- Taja pambo linalotumiwa kwa kupaka
- Kipuli
- Hina
- Ushanga
- Mapete
- Pete huvaliwa wapi?
- Shingoni
- Vidoleni
- Puani
- Mkononi.
- Tambua pambo linalovaliwa sikioni
- Mapete
- Ushanga
- Kipini
- Pete.
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 16-20 ukitumia jibu sahihi
Asubuhi hiyo watu wengi walikuwa ___16___kwenye ___17___cha polisi. Wanawake kwa wanaume walikuwa wakizungumza kuhusu ___18___waliokuwa wakiwavamia usiku na mchana kwenye kijiji chao. Sajini wa polisi aliyekuwa akiyapokea malalamishi ___19___aliyaandika kwenye shajara na kutuliza ___20___wa watu uliojawa na hasira.
A | B | C | D | |
16. | anafika | wakifika | walifika | watafika |
17. | kituo | shule | darasa | mahali |
18. | watu | watalii | wanakijiji | wezi |
19. | zao | yao | wao | yake |
20. | umati | mlolongo | tita | halaiki |
Tambua aina za nomino zilizopigiwa mstari.
- Umati wa watu ulihudhuria mkutano.
- Nomino ya wingi.
- Nomino ambata.
- Nomino ya makundi.
- Nomino ya kawaida.
- Ipi ni nomino tofauti kati ya hizi?
Maji, Maua, Manukato, Maziwa- Maua
- Maukato
- Maziwa
- Maji.
- Andika sentensi ifuatayo kwa wingi.
Sabuni ilinunuliwa jana.- Masabuni yalinunuliwa jana.
- Sabuni zilinunuliwa jana.
- Sabuni ilinunuliwa jana.
- Sabuni yalinunuliwa jana.
- Tambua sentensi iliyoakifishwa vyema.
- juma alisafiri Jana
- wanafunzi wamenunua vibati kalamu na vifutio
- Kitabu kipi kilinunuliwa?
- mwalimu amefika shuleni.
- Kamilisha methali ifuatayo.
Asiyesikia la mkuu huvunjika ______________________- mkono
- shingo
- mguu
- guu
Tumia maneno ya heshima.
- Mama ana mimba
- mawe
- mtoto
- mjamzito
- mlevi
- Mtoto anahara
- anatapika
- anaendesha
- anakimbia
- anazama
- Tumia amba- kukamilisha sentensi ifuatayo.
Chakula ____________________ kimepikwa ni kitamu.- ambayo
- ambacho
- ambalo
- ambao
- Tambua ngeli ya neno lililopigiwa mstari.
Chupa imeanguka ikavunjika.- I-ZI
- A-WA
- U-I
- LI-YA
- Mwezi wasaba huitwaje?
- Agosti
- Juni
- Julai
- Aprili.
INSHA
Ufuatao ni mwanzo wa insha. Iendeleze kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Mvua ilinyesha sana siku hiyo. Mimi na rafiki zangu tulikuwa...
MARKING SCHEME
- D
- C
- C
- B
- A
- B
- A
- C
- A
- A
- A
- C
- B
- B
- A
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- A
- B
- C
- D
- C
- B
- B
- A
- C
Download Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students