Thursday, 03 August 2023 08:05

Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti Questions and Answers - CBC Grade 1 End Term 2 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA          (Alama 5)

Mwalimu atamwamkua mwanafunzi kisha amwambie

"Leo tutajifunza kuhusu mwili wangu. Nitakuuliza maswali nawe uyajibu kwa Kiswahili."

  1. Una macho mangapi?   (Alama 1)
                                     (Mwanafunzi ajibu)
  2. Ni sehemu gani hutumika kutembea?  (Alama 1)
                                     (Mwanafunzi ajibu)
  3. Masikio yanatumiwa kufanya nini?   (alama 1)
                                     (Mwanafunzi ajibu)
  4. Unatumia pua kufanya nini?   (alama 1)
                                     (Mwanafunzi ajibu)
  5. Mkono wako mmoja una vidole vingapi?      (alama 1)
                                     (Mwanafunzi ajibu)

                     KUSOMA KWA SAUTI              (alama 10)

                   Soma hadithi hii kwa sauti.

                            GRADE1kiswahiliSET1ET22023Q10

Shangazi alisema kuwa mimi ni mtoto mzuri, Alinituma kwa babu kuleta mapera. Babu alikuwa ameketi chini ya mti. Alikuwa akisoma gazeti. Alinipa mapera. Nilirudi nyumbani upesi. Njiani sikuongea na mtu yeyote. Nilifika nyumbani mapema.

MARKING SCHEME

  1. mawili
  2. miguu
  3. kusikiza
  4. kupumua
  5. tano
.