Monday, 27 February 2023 11:53

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 2 Opener Exams Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

This paper contains both complete questions and answers for this set 1.

Find more exam sets (1 - 4) here: Term 1 2023 sets for Grade 2

Mwalimu ajaze jedwali hili baada ya kusahihisha kazi ya mwanafunzi

Sehemu ya   Alama  Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio  Kukaribia Matarajio  Mbali na Matarajio 
 1  Kusikiliza na kuzungumza          
 2  Kuspma          
 3  Sarufi          
 4  Kuandika          


Maswali

SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

  1. Familia yako ina watu wangapi?
  2. Je, wewe na familia yako mnaishi wapi?
  3. Ni nani huwapikia katika familia yako?
  4. Je, unaye ndugu yeyote katika familia yako?
  5. Wewe husaidiaje katika familia yako ukiwa nyumbani?

SEHEMU YA 2: KUSOMA
Zoezi la 1: Kusoma kwa sauti.
Jioni moja, mama alikuja nyumbani akiwa na furaha nyingi. Aliniambia kuwa baba angesafiri kuja nyumbani siku iliyofuata. Niliposikia hivyo, nilirukaruka kwa furaha.

Zoezi la 2: Kusoma kwa Ufahamu.
Soma hadithi na ujibu maswali yafuatayo.
Sami na Kiki ni marafiki wakubwa. Wao wanapendana sana. Wao ni wanafunzi wa gredi ya pili katika shule ya Mamboleo. Mwalimu wao anaitwa Bi. Rukia. Mwalimu huyo hufundisha kwa bidii sana. Wanafunzi wake humpenda kwa sababu bidii yake kazini. Siku zote, yeye huwaambia kuwa wafanye bidii kwa sababu bidii hulipa.

  1. Sami na Kiki wanasoma katika shule ya................................................................
  2. Mwalimu aliyetajwa anaitwa Bi................................................................
  3. Wanafunzi humpenda mwalimu wao kwa sababu ya................................................................
  4. Sami na Kiki ni wanafunzi wa gredi ya................................................................
  5. Siku zote, mwalimu huyo huwaambia wanafunzi wake kuwa................................................................

SEHEMU YA 3: SARUFI
Chagua jibu sahihi kutoka mabononi.

  1. Mwanafunzi ameketi................................ya mwalimu wake. (katikati, ndani, mbele)
  2. Mafuta yamo................................ ya chupa. (ndani, juu, katikati)
  3. Paka amekaa................................yameza na kiti,(chini, ndani, katika) 
  4. Wageni wameingia................................ya nyumba. (juu, ndani, nje)

Jaza Jedwali hili kwa usahihi.

  Umoja  Wingi 
20  Nimeokota kalamu  
21   Tunaanika nguo.
22 Ninapenda maziwa  
23   Tutanunua penseli.

Pigia mistari viambishi vya nafsi

  1. Ninapenda kuchora.
  2. Tunaandika vizuri.

SEHEMU YA 4: KUANDIKA
Andika sentensi zifuatazo kwa hati nzuri.

  1. Juma amechora baiskeli kubwa.

    ................................................................
  2. Wanafunzi wameenda uwanjani kucheza.

    ................................................................
  3. Mama alituletea matunda mabivu.

    ................................................................
  4. Meza ya baba ilikuwa mpya.

    ................................................................
  5. Matunda ni bora kuliko vibanzi.

    ................................................................


Majibu

  1.  Mamboleo
  2.  Rukia
  3. bidii yake kazini
  4. pili
  5. wafanye bidii kwa sababu bidii hulipa
  6.  mbele
  7. ndani
  8. chini
  9. ndani
  10. Tumeokota vilamu.
  11. Nimeanika nguo.
  12. Tunapenda maziwa.
  13. Nitanunua penseli.
  14.  Ni
  15. Tu

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 2 Opener Exams Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.