MASWALI
Imla
- ..............................
- ..............................
- ..............................
Andika wingi
- kitabu ..............................
- Mti ..............................
- Ua ..............................
Tumia "huyu" au "hawa"
- ..............................ni wasichana.
- ..............................ni mtoto.
Chagua jawabu sahihi kujaza nafasi
- Mgeni..............................amaingia leo.
(langu, wangu, yangu) - Matunda..............................yameoza.
(yangu, wetu, yetu) - Kiti ..............................kilivunjika.
(kizuri, mazuri, wazuri) - Watoto .............................. walichuna matunda yote.
(mazuri, vibaya, wabaya)
Kanusha sentensi hizi
- Mimi ninasoma
- Sisi tunalima
Andika kinyume cha maneno haya
- Ingia ..............................
- Safi ..............................
Andika wingi wa maneno haya
- Kitabu hiki
- Tunda hili
- Mzazi huyu
- Chakula hiki
Chagua jibu sahihi kujaza nafasi
- Viti .............................. vitanunuliwa.
(hiki, hivi, hili) - Kichana ..............................kimevunjika.
(hivi, huyu, hiki) - ..............................nitafagia.
(sisi, mimi, yeye) - ..............................anavua nguo.
(wewe, yeye, wao) - Gari ..............................limeharibika.
(hili, huyu, hiki)
Soma hadithi kisha ujibu maswali
Jamila anapoamka asubuhi anasugua meno. Kisha anaweka maji kwenye karai. mama yake humfunza kuoga vizuri kwa kutumia sabuni na maji. Yeye huoga sehemu zote za mwili. Nguo zake za shule hufuliwa na mama. Dada yake Sidi hanawi mikono vizuri.
- Jamila husugua ..............................anapoamka asubuhi.
- Jamila hutumia nini kuoga?
- Ni nani hufua nguo za Jamila za shule?
- Je, dadake Jamila huitwa nani?
- Jamila huweka maji yake ya kuoga kwa kifaa kipi?
Majibu
- vitabu
- miti
- maua
- Hawa
- Huyu
- wangu
- yetu
- kizuri
- wabaya
- Mimi sisomi.
- Sisi hatulimi.
- toka
- chafu
- Vitabu hivi
- Matunda haya
- Wazazi hawa
- Vyakula hivi.
- hivi
- hiki
- Mimi
- Yeye
- hili
- meno
- sabuni na maji
- mama
- Sidi
- karai
KUSOMA
Soma habari hii
Omari ni mtoto. Baba yake ni Otieno. Mama yake anaitwa Kanini. Omari hukaa na dada katika kaunti ya Nairobi. Omari huletewa mayai na kaka yake Kimtai. Nyanya mkuu humpa mabuyu. Omari hutamani chakula kitamu zaidi ya mabuyu. Omari hupenda kucheza sana. Yeye ana mpira mzuri.
Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 4.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students