MASWALI
SEHEMU 1: KUSIKILIZA NA KUONGEA
Mwalimu amuulize mwanafunzi4maswalLyafuatayo.
- Habari yako?
(Mwanafunzi ajibu) - Taja tunda unalolipenda.
(Mwanafunzi ajibu) - Tunda hilo linapatikana wapi?
(Mwanafunzi ajibu) - Kabla ya kula tunda unafaa ufanye nini?
(Mwanafunzi ajibu) - Tunda hilo huwa tamu likiwa bivu au bichi?
(Mwanafunzi ajibu)
SEHEMU 2: KUSIMA KWA SAUTI
Soma kifungu hiki kwa sauti
Niliamka asubuhi na mapema. Kulikuwa na utulivu kwa sababu watu wengi hawakuwa wameamka. Hata wazazi wangu bado walikuwa wakilala. Nilienda bafuni nikaoga. Kisha nikaenda jikoni kutayarisha staftahi. Sikutaka nichelewe kufika shuleni. Baada ya kupata staftahi, nilipiga meno mswaki kisha nikavaa sare za shule. Nilitoka mbio hadi shuleni. Siku hiyo ilikuwa siku ya kuzuru mbuga ya wanyama.
SEHEMU 3: UFAHAMU
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, kuku na mwewe. Walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walikuwa wakiishi pamoja. Kila asubuhi walienda kulima katika shamba lao. Kuku alikuwa na vifaranga watano naye mwewe alikuwa na makinda wawili.
Siku moja kuku alimkanyaga kinda mmoja hadi akaaga dunia. Ingawa ilikuwa ajali, mwewe aliapa kulipiza kisasi. Kuku aliamua kutoroka hadi kwa binadamu. Tangu siku hiyo, mwewe huwashika vifaranga wa kuku kulipizd kisasi.
- Kila asubuhi kuku na mwewe walienda wapi?
- Kuku alikuwa na vifaranga wangapi?
- Mwewe alikuwa na makinda wangapi?
- Nani alimkanyaga kinds?
- Kuku alitoroka hadi wapi?
SEHEMU 4: SARUFI
Kanusha sentensi.
- Enda nyumbani.
- Mtoto anakula ndizi.
- Baba analima shambani
- Kaka amepika chakula
- Soma kitabu hiki.
Andika kinyume.
- Shuka
- Rudi
- Keti
- Funika
- Jenga
Andika tarakimu kwa maneno.
- 86
- 92
- 126
- 74
- 225
Andika majina ya maumbo haya.
Andika maneno kwa wingi
- Uzi
- Ukuta
- Meza
- Tunda
- Mwanafunzi
SEHEMU 5: KUANDIKA
INSHA
Andika insha juu ya:
DARASA LETU
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
Ufahamu
- Kwa shamba
- Watano
- Wawili
- Kuku
- Kwa binadamu
Sarufi
- Usiende nyumbani
- Mtoto hali ndizi
- Baba halimi shambani
- Kaka hajapika chakula
- Usisome kitabu hiki
- Panda
- Enda
- Simama
- Funua
- Bomoa
- Themanini na sita
- Tisini na mbili
- Mia moja, ishirini na sita
- Sabini na nne
- Mia mbili, ishirini na tano
- Pembe tatu
- Mstatili
- Duara
- Duara dufu
- Mraba
- Nyuzi
- Kuta
- Meza
- Matunda
- Wanafunzi
Download Kiswahili Activities Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 1 Exams 2022 SET 2.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students