Thursday, 02 March 2023 07:50

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 Opener Exams Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Maswali

SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

  1. Mwanafunzi anapewa shuleni akisoma, yeye huwa anafurahia haki gani?
  2. Mtoto anapopewa chakula bora na mzazi wake, yeye hupata haki gani?
  3. Mtoto akiwa mgonjwa anafaa kusaidiwaje?
  4. Haki ya kucheza hupatikanaje?
  5. Ni kwa nini watoto hawafai kuvalia nguo zilizoraruka?

SEHEMU YA 2: KUSOMA
Zoezi la 1: Kusoma kwa sauti.
Soma hadithi hii kwa sauti.
Samira ni mvuvi katika kijiji cha Saragambo. Yeye hupenda kuvua wakati wa asubuhi. Samaki hao yeye huwauza katika soko la Uyoma. Anao watoto watatu ambao anawapenda sana. Samira ana bidii sana. Watu wa kijiji chake humpenda sana Samira.
Alama 10

Zoezi la 2: Kusoma kwa ufahamu
Soma hadithi hii na ujibu maswali
Jumamosi iliyopita, shangazi yangu alitutembelea. Hakuwa ametutembelea kwa muda wa wiki mbili. Aliniletea peremende na biskuti. Baba na mama walifurahi sana kwa kumwona. Hata hivyo, nilikuwa na furaha kuliko wao. Siku iliyofuata, Jumapili, mimi na shangazi tulienda kanisani ambapo tuliimba na kumchezea Mungu. Ilikuwa ni siku njema.

  1. Shangazi wa mwandishi aliwatembelea siku ya ......................................
  2. Shangazi wa mwandishi alimietea mwandishi......................................
  3. Mwandishi alienda kanisani pamoja na......................................
  4. Kina mwandishi walienda kanisani siku ya......................................
  5. Walipokuwa kanisani, waliimba na kumchezea......................................

SEHEMU YA 3: SARUFI
Chagua jibu sahihi kutoka mabanani.

  1. Wavulana......................................liokuja wapewe viti (tu, ni, va). 
  2. Sisi sote......................................tapewa zawadi (ni, wa, tu).
  3. Yeye......................................pendi kunywa maziwa (si, hu, ha)

Andika sentensi hizi katika umoja au wingi.

  1. Wageni wanakula samaki. ......................................
  2. Mvulana amesimama mezani. ......................................
  3. Watu wanaimba kwa sauti. ......................................
  4. Mjomba amenunua simu. ......................................

Pigia mistari viambishi vya nafsi.

  1. Ninataka kununua simu. ......................................
  2. Tunaandamana na wao hadi uwanjani. ......................................
  3. Ninapongezwa kwa ujasiri wangu. ......................................

SEHEMU YA 4: KUANDIKA
Ziandike upya sentensi hizi kwa hati nadhifu.

  1. Tulikuwa tukitaka kuandika.
    ......................................
  2. Tuko katika gredi ya tatu.
    ......................................
  3. Mwalimu akija tutafurahi.
    ......................................
  4. Wanafunzi wote wameanza safari.
    ......................................
  5. Wageni walifika jana jioni.
    ......................................

Majibu

  1. Jumamosi
  2. peremende na biskuti
  3. shangazi
  4. Jumapili
  5. Mungu
  6. wa
  7. tu
  8. ha
  9. Mgeni anakula samaki.
  10. Vijana wamesimama mezani.
  11. Mtu anaimba kwa sauti.
  12. Wajomba wamenunua simu.
  13. Ni
  14. Tu
  15. Ni
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 Opener Exams Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.