0 votes
3.2k views
in Chozi la Heri by
edited by
Jadili kwa hoja nane suala la ukoloni mambo leo lilivyoshugulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri

1 Answer

0 votes
by
  1. Watoto wa walowezi wa kikoloni kumiliki mashamba yaliyomilikiwa na familia zao-shamba la Tengenea,wazungu wanamiliki mashamba ya michai na mibuni pamoja na mashirika ya utengenezaji wa mazao ya mimea nchini.
  2. Baadhi wa Wahafidhina wanamiliki mashamba huku Waafrika wengine wakiwa maskwota au wafanyikazi-Kangata anafanya kazi na kuishi katika shamba la Kiriri.Watoto wa Kangata hata wanajitambulisha kwa jina la Kangata.
  3. Wahafidhina inaendeleza umilikinafsi wa ardhi ulioanzishwa na mzungu.
  4. Wageni kuamua kitakachokuzwa Wahafidhina.
  5. Unyonyaji-wenyeji kukuza zao na kuwapa wageni kuwasagia huku wakiwauzia kwa bei ghali.
  6. Mifumo kandamizi ya utawala- uongozi unatuma vyombo vya dola kudhibiti upinzani
  7. Utegemezi. Wanahafidhina wanawategemea washiria wa kimaendeleo wakati mikasa inapotokea. Kudhibitiwa na malengo ya kimataifa- Tila anamwambia Ridhaa kwamba wangependa kufikia Malengo ya Kimilenia. Haya ni matakwa ya kimataifa ambayo nchi hujifunga kutimiza.
  8. Kampuni za kigeni kuchimbua madini katika sehemu za mashambani na fedha kuwaendea hao hao wageni. Raia wanaoajiriwa kuchimbua madini kulipwa mshahara duni.Tila analalamikia haya.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...