0 votes
737 views
in Kigogo by

Onyesha uhusiano uliopo baina ya wahusika hawa na maudhui ya hadithi. 

  1. Majoka
  2. Tunu

1 Answer

0 votes
by
  1. Majoka: 
    1. Kielelezo cha viongozi dhalimu- anamuua Jabali, kumjeruhi Tunu, kumfungia Ashua kizuizini, n.k.
    2. Ni mfano wa kiongozi mwenye bezo- anamweleza Ashua alikataa uchumba wake sasa amekuwa ombaomba
    3. Ni mfano wa kiongozi asiyethamini wanyonge- anawatusi- Alimwita Sudi zebe, Tunu na Sudi makunguru (uk 38) na kuwarejelea wanasagamoyo kama wajinga.
    4. Ni kielelezo cha viongozi wanaowatishia raia- anaposikia Tunu anaongoza maandamano, anatoa vitisho kwake kuwa atawafundisha mambo ambayo hakufundishwa nyumbani.
    5. Ni kielelezo cha cha kiongozi mnafiki- Husda ni mkewe ila hampendi na anampenda Ashua.
    6. Ni mtu asiyewajali wengine- Anaendeleza ubinafsi. Anatumia cheo chake kujinufaisha kwa mfano kwa kunyakua ardhi ya umma.
    7. Anaendeleza maudhui ya uzinifu- licha ya kuwa ana mke, anamtongoza Ashua ambaye ni mkewe Sudi.
    8. Ni mfano wa kiongozi mjinga ambaye anakubali ushauri potovu kutoka kwa vibaraka wake kama vile Kenga. Hatambui kuwa wanampotosha.
    9. Ni mfano wa viongozi ambao hawawathamini wanawake- (uk. 27) anasema wanawake ni wanawake tu. Anamweleza Husda, "Shut up woman!" Anamwita mkewe "woman" kama mtu asiyefahamu jina lake.
    10. Anaendeleza usaliti- anamsaliti babake Tunu na kumuua ingawa walikuwa marafiki . Anawasaliti wananchi kwa kulifunga soko.
    11. Anawakilisha kundi la viongozi wanaopata madaraka kutokana na uhusiano wa kinasaba na viongozi watangulizi.
    12. Ni mfano wa kiongozi jeuri- Kwenye ndoto, babu yake anajaribu kumnasihi kutenda mema lakini anapuuza. 
  2. Tunu:
    1. Ni kielelezo cha vijana wazalendo wanaopigania haki za jamii yao. Anashirikiana na Sudi kupigania wanyonge.
    2. Ni mfano wa vijana wenye msimamo dhabiti- anakataa kuozwa kwa Ngao kwa vile hautaki uhusiano na ukoo unaowanyanyasa raia.
    3. Ni kielelezo cha raia jasiri- Anamkabili Majoka bila woga na hata kumwita muuaji (uk 47) 
    4. Anaendeleza maudhui ya utu- anawahurumia wanoa Sudi na Ashua. Anapendekeza wapelekwe kwao ambako mamake angewatunza.
    5. Anaendeleza maudhui ya uadilifu- Yeye hapendi ulevi. Hajihusishi kimapenzi na Sudi kinyume na tetesi za watu.
    6. Ni mfano wa vijana wanaofanya bidii masomoni na kufaulu. Anasoma na kuhitimu na shahada ya uzamili na kisha uzamifu katika sheria.
    7. Ametumiwa na mwandishi kuonyesa umuhimi wa msamaha na maridhiano. Mwishoni mwa mchezo, Mamapima anaomba msamaha na Ashua anamsamehe.
    8. Anaonyesha dhima ya ukakamavu pale anapohutubia umma kwenye lango la soko bila kuogopa Majoka na walinzi wake.
    9. Ametumiwa kama njia ya kuhamasisha umma dhidi ya kuwachagua viongozi fisadi ambao hawaonei fahari maendeleo ya jamii yao.
    10. Ni mfano wa mzalendo kamili katika jamii licha ya kuumizwa na wahuni, aliendelea kupigania haki za wanyonge kwa kutumia kigari cha magurudumu.
    11. Ametumiwa na mwandishi kuwahimiza watu kutenda mambo kwa busara - anapinga wazo la Majoka kuwatenganisha na Sudi pale ofisini.
    12. Mwandishi amemtumia kusuta uongozi wa jamii yake ambao hauthamini elimu ya kisasa. Majoka na Kenga walikashifu juhudi zake za kupata elimu. Aidha uongozi huu unashindwa kubuni nafasi za kazi kwa vijana waliohitimu.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...