0 votes
2.4k views
in Chozi la Heri by
Jinsi maudhui ya umaskini yamejitokeza katika chozi la heri

1 Answer

0 votes
by
Umaskini ni ukata. Ni hali ya kukosa fedhamali nk. Tunapata kuwa waafrika wanajikuta katika hali ya umasikini;

• Uk 7,"Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo, maskini, wasio na ardhi " Uk 25,"Nyinyi ndio vikaragosi wanaotumiwa na wasaliti wa nia zetu kuendelea kutudidimiza kwenye lindi hili la ukata "

•  Ridhaa pia anajikuta kwenye lindi la umaskini baada ya mali yake yote kuchomwa, ikiwemo familia yake. Uk 1,"Ridhaa alisimama kwa maumivu makali, mikono kairudisha nyuma ya mgongo wake uliopinda kwa uchungu. Macho yake yaliyotanda ukungu alikuwa kayatunga juu angani, akitazama wingu la moshi lililojikokota kwa Kedi na mbwembwe; wingu lililomwonyesha na kumkumbusha ukiwa aliozaliwa nao na ambao alihofia kuwa angeishi na kuzikwa nao"

• Tunapata pia kuwa watu wengi wanaiaga dunia wakijaribu kujikomboa kutokana na hali hii ya ukata, wanapoenda kuchota mafuta kwenye lori ambalo limebingirika kisa na maana alienda kuwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori, ambalo lilikuwa limebingiria lnasemekana kuwa umaskini uliwasukuma watu hawa kuchukua kisichokuwa haki yao!"

Related questions

Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...