0 votes
923 views
in Chozi la Heri by
Fasiri jinsi maudhui ya mabadiliko yalivyoijenga riwaya ya Chozi la Heri.

1 Answer

0 votes
by
Hii ni hali ambapo mambo yanaenda kinyume na jinsi yalivyokuwa yakienda mbeleni. Hali ya kufanya mambo inabadilika na kuwa tofauti ya kawaida yake.

Katika ukurasa wa 10; "Hatua ya mkoloni ya kupuuza sera za Mwafrika za umiliki wa ardhi, na kuamua kujumuisha pamoja ardhi iliyomilikiwa na mtu binafsi, na kuidhinisha umiliki huu kwa hati miliki, ilivuruga mshikamano wa kijamii. Katika sera ya kijadi ya umiliki na matumizi ya ardhi, raiya wote, hata wageni, walikaribishwa na kugawiwa mashamba, hivyo kupata mbinu ya kuyaendeshea maisha. Sera mpya ya umilikaji nafsi wa ardhi ilimaanisha kwamba wale waliokosa pesa za kununulia mashamba wangekosa mahali pa kuishi. Na hata wale waliobahatika kuwa na pesa za kununulia mashamba daima walichukuliwa kama wageni wasiopasa kuaminiwa Tunapata kuwa mfumo uliokuwepo hapo awali wa kumiliki mashamba barani Afrika ulipigwa marufuku na kukawa na mfumo mpya wa umiliki wa mashamba uliohusisha kupewa kwa hati miliki. Haya ni mabadiliko yanayokuja katika jamii.

Katika ukurasa wa 11; "Pengine hata ni mzaha tu. Kesho nitakurudisha shuleni. Nitazungumza na mwalimu ili awaelekeze Zaidi 'Huo ndio uliokuwa mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa. Baada ya mwalimu kuzungumza na wanafunzi na kuwasisitizia umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano dhihaka na masimangoyaliisha "Kuna mabadiliko yanayofanyika katika shule baada ya mamake Ridhaa kuzungumza na mwalimu wake kuhusu umuhimu wa kuwajuza wa nafunzi ushirikiano na kuishi kwa umoja. Mabadiliko haya yanakuwa ya maana sana kwa Ridhaa kwani elimu yake inaendelea kwa ufasaha na anahitimu hadi chuo kikuu.

Katika ukurasa uo huo wa 11 tunasoma; "Mimi binafsi nimefanya juu chini kuhakikisha kuwa kijiji kizima kimepata maji ya mabomba. Eneo ambalo awali likiitwa Kalahari, sasa limetwaa rangi ya chanikiwiti. Miambakofi, mivule na miti mingine mingi imepandwa. Mvua inanyesha majira baada ya mengine "Haya ni mabadiliko yanayofanyika katika mtaa huu ambao ulikuwa hapo awali umekauka sana lakini baada ya maji ya mabomba kufikishiwa watu, tunapata kuwa kunabadilika na ile hali ya kuwa jangwa inaisha, miti mingi inapandwa na hata mvua nyingi kunyesha.

Katika ukurasa wa 84,"Maisha ya Umu yalichukua mkondo mpya. Siku ile baada ya kuwapigia polisi ripoti, ilibainika kuwa wanuna wake walikuwa wametekwa nyara na Sauna "

Maisha ya Ridhaa pia yanachukua mkondo mpya au kubadilika wakati familia yake inapoangamia kwenye janga la moto, na mali yake yote kuishia hapo. Maisha yaliyokuwa ya furaha pamoja na familia yake yanabadilika na kuwa uchungu mtupu na kilio cha kufiwa na wapenzi wake.

Katika ukurasa wa 40 tunasoma; "Ridhaa: Na nani akasema viongozi waliopo hawajajikuna wajipatapo?Huoni hata wahasiriwa wa magonjwa sugu kama vile iri na hata UKIMWI wana dawa za bei nafuu za kuwawezesha kudhibiti hali hizi?Je, serikali haijaanzisha sera ya elimu bila malipo kwa Shule zote za msingi?Haijagharamia karo za Shule za kutwa katika Shule za upili?kumbuka pia na ule mradi wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la kwanza ana kipakatalishi chake?Ushaona?Hivi karibuni, nchi inafikia ile vision 2030 hata kabla ya 2030 yenyewe!Je, ni tume ngapi za kuchunguza kashfa za kifisadi ambazo zimeundwa?Hizo si juhudi za kupigana na ufisadi?" Maelezo haya yote yanatuonyesha jinsi taifa limepiga hatua mbele kimaendeleo. Kumekuwa na mabadiliko mengi sana katika serikali na pia hali ya maisha ya raia, bila kusahau elimu.

Katika ukurasa wa 63 tunasoma; "Usicheze na binadamu apatapo nyenzo ya kujiinua!kabla ya miaka miwili kuisha, mahali hapa palikuwa pamepata sura mpya-majumba yenye mapaa ya vigae, misitu ya mihindi na miharage, maduka ya jumla, viduka vya rejareja almuradi kila mtu alijifunga mkaja kutunisha kibindo chake; kufidia alichokuwa amekipoteza hapo awali "Haya ni mabadiliko yanayoendelea katika msitu wa Mamba. Tunaambiwa kuwa msitu huu uligeuka na kuwa nyumbani mwa maelfu ya watu waliogura makwao bila tumaini ya kurudi. Maduka na majumba yanajengwa, na ile hali ya kuwa msitu inabadilika, na mashamba ya watu ndiyo yanayoonekana kwa sasa.

Pia katika ukurasa wa 148 tunasoma; "Maisha yangu yalichukua mkondo mwingine nilipojiunga na darasa la saba. Katika jamii yangu, inaaminika kuwa msichana akishaisha kupashwa tohara, ameingia utu uzimani, hivyo ataipaka familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume "
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...