0 votes
1.8k views
in Chozi la Heri by
Jamii katika riwaya ya chozi la heri imebaidiwa (tenganishwa) na utabaka. Tetea kauli hii.

1 Answer

0 votes
by
Utabaka ni hali ya kuwa na kundi fulani katika jamii linalotofautiana na kundi lingine katika jamii iyo hiyo, kwa misingi ya kiuchumi, kielimu na kadhalika. Utabaka mara nyingi hujitokeza wakati kunapopatikana matajiri na masikini katika jamii. Pia kuna matabaka ya wasomi, wafanyakazi, wafanya biashara, na kadhalika. Katika ukurasa wa 14 uliopo ni ule wa hali, mazoea na silika. Hapa tulipo tupamwe na wamwe na walokuwa nacho na wachochole. Unaweza kusema kuna kiasi fulani cha usawa watu husema kuwa binadamu hawawi sawa ila kifoni! Kile ambacho hawajuia ni kwamba hata katika kifo, hamna usawa. Pana tofauti kati ya mandhari wanamofia. Kuna wanaokufa wakipewa na wauguzi katika zahanati za kijiji. Wapo wanaolala maumivu yao yakiwa yamefishwa ganzi kwenye hospitali za kifahari, wakiliwazwa na mashine, kila mmoja akihimiza wenzake kuushikilia kukutu uhai wa mheshimiwa huyu. Hawa wafapo sura zao huwa tulivu; wameziachilia huru roho zao kwa faraja. Huwezi kuzilinganisha nyuso zao na za wanaokufa kwa hamaniko wakizingirwa na jamaa ambao hawana hata hela za kununulia sindano ya kuingiza dawa mwilini!Kuna wale ambao hufia kwenye vitanda vya mwakisu vitongojini baada ya kupiga maji haramu. Hawa husemekana kuwa wamekuwa nzi ambao hufia dondani sio hasara. Hulaumiwa kwa kujitosa katika msiba wa kujiwekia. Tofauti hizi zote unazijua. Unajua pia kuna tofauti hata katika mitindo ya mazishi, viviga vinavyohusishwa na sherehe za mazishi na hata mavazi ya "mwenda zake" na wafiwa. Hata majeneza yenyewe huhitilafiana!" Kuna matabaka mawili yaliyoangaziwa sana hapa, yale ya walala hoi, na walala heri. Matabaka haya mawili yanatofautiana sana kihali, na jinsi ya kufanya mambo yao.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...