0 votes
1.9k views
in Sarufi na Matumizi ya Lugha by
recategorized by

Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.

  1. Maafisa hao walipewa uhamisho. Maafisa wengine hawakupewa uhamisha
    (Unganisha kuunda sentensi ambatano.)    
  2. Hadithi hiyo ilitungwa vizuri ikawavutia wengi.
    (Badilisha vitenzi vilivyopigiwa mstari kuwa nomino.)    
  3. Tunda halitaoshwa vyema. Tunda halitalika.
    (Unganisha kuwa sentensi moja kwa kutumia 'po'.)     
  4. Kengewa alitoa ahadi. Wengi waliiamini ahadi hiyo.
    (Unganisha kuwa sentensi moja inayoanza kwa: Ahadi.)      

1 Answer

0 votes
by
edited by
  1. Maafisa hao walipewa uhamisho ilhali wengine hawakupewa uhamisho
  2. Mtungo huo ulikuwa mzuri ukawa na mvuto mkubwa
  3. Tunda lisipooshwa vyema halitalika
  4. Ahadi ambayo Kengewa alitoa uliaminika na wengi
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...