0 votes
1.5k views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
Sifa za wahusika katika Mkubwa

1 Answer

0 votes
by

Mkubwa

  • Mwenye bidii
    Alikuwa akishughulisha na kazi ya kuuza pweza wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi ili kuingia uongozini.
  • Mwenye utani
    Anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo lililomfanya utingo kukimia kwa kuchekwa na abiria.
  • Ni mtambuzi
    Aliweza kuelewa maana ya unga japo hakuwahi tu kuona vituko vyake.
  • Mwenye utu
    Alimpigapiga kijana mbwia unga aliyekuwa ameinama kama kwamba anarukuu na kumuuliza iwapo anaumwa.
  • Mwenye tamaa ya mali
    Alipotanabahi namna viongozi wanavyotajirika kwa kuuza unga , maneno 'unga na utajiri' yalimkaa moyoni kiasi chake kukosa usingizi usiku huo.
  • Ni maskini
    Alikuwa akifanya biashara ya kuuza pweza iliyokuwa na kipato kidogo . vilevile kabla ya kupata uongozi, alikuwa na suruali na shati kipande papa.
  • Ni fisadi
    Baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya biashara ambayo huonekana kama ya kishetani. Vile vile alitoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea na ndipo akaupata ushindi.
  • Mwenye msimamo dhabiti
    Baada ya kuyatia moyoni maneno aliyopewa na kijana yule kuhusu utajiri na unga aliamua kutafuta kwa udi na uvumba na ndipo akamwendea rafikiye kwa jina Mkumbukwa.
  • Ni msiri
    Mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake kuutafuta uongozi.
  • Mwenye wasiwasi
    Aliogopa kuwa huenda kisomo chake kingemzuia kupata uongozi.

Mkumbukwa

  • Rafiki wa dhati
    Mkumbwa alimwendea kwa mawaidha baada ya kuamua kuugombea uongozi na ndipo Mkumbukwa akamshauri Mkubwa augombee.
  • Mkakamavu
    Alimweleza Mkubwa bila kupepesa macho wala kugugumizi kuwa pesa na ukaragosi wa chama ndiyo mambo muhimu pale Mchafukoge yatayomwezesha kuupata uongozi.
  • Mwenye kutimiza ahadi
    Alimwambia Mkubwa kuwa akitafuta milioni kumi kisha ampe yeye ataupata uongozi na kuapa kuwa iwapo ataukosa amuue.
  • Ni mwenye bidii
    Baada ya Mkubwa kujaza fomu; alianza kazi ya kuingia /kupita nyumba baada ya nyumba kumtafutia kura mkubwa.
  • Mwenye busara
    Alifahamu fika kuwa ili kufanya kazi vyema ni lazima angemtafuta Bi Kibwebwe (Sada) na kumhusisha katika harakati za kumtafutia Mkubwa kura.
  • Mwenye majuto
    Aliponaswa na askari wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevya alijuta kimoyomoyo.
  • Mwenye kulalamika
    Alipotiwa ndani alikuwa akilalamika kupuuzwa kwa haki za mahabusu.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...