Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya uliyopewa.
__1__ husema kuwa __2__. Ulimi huu ulidhihirika __3__ hivi majuzi humu nchini pale ambapo mchungaji mmoja maarufu aliwahadaa wafuasi wake kwa kuwaagiza kususia chakula na maji kwa muda wa siku arubaini ili kumwona Mungu. Hatua hii __4__ mauti ya wengi wa wafuasi hao wake huku miili yao ikipatikana katika shamba la mchungaji huyo la zaidi ekari themanini. Iliaminika kuwa mchungaji huyo alikuwa na nia __5__ ambayo haikubainika kwa wakati ufaao. Wengi walisikika wakidai kuwa kuwaamini baadhi ya wachungaji sasa ni sawa na __6__. Baadhi hawaaminiki. __7__.
A | B | C | D | |
1. | wasemavyo | waemayo | wasemao | wanaposema |
2. | kosa moja halimwachishi mke | papo kwa papo kamba hukata jiwe | papo kwa papo kamba hukata jiwe | uzuri wa kuyu ndani mabuu |
3. | tenge tahanani | dhahiri shahiri | daima dawamu | liwalo na liwe |
4. | ilipelekea | ilielekeza | ilileta | ilisababisha |
5. | fiche | bora | bayana | njema |
6. | kutarajia manufaa baada ya bidii | kuchezea shilingi katika tundu la choo | kuwarai waumini kujiunga na madhehebu | kumtegemea Mungu katika shughuli zetu |
7. | Wamevalia ngozi ya chui | Wamezifichua kucha zao | Wamevalia ngozi ya kondoo | Matendo yao yako wazi |
Dunia ya sasa inaenda mbio na maisha ya vijana wetu nayo pia __8__ kwa kiasi mithili ya duma. Ugumu wa maisha na __9__ kwa uchumi vinawasukuma baadhi yao __10__ katika uhuni ili __11__. Ni afadhali __12__ na kidogo walicho nacho kuliko kutamani kingi wasicho nacho kwani __13__. Pia, wanaweza kujianzishia miradi ya __14__ badala ya __15__.
A | B | C | D | |
8. | yakitimika | yakiimarika | yakizorota | yakidumaa |
9. | kuporomoka | kujengeka | kubomoka | kuimarika |
10. | kujitoma | kujiondoa | kujitosa | kujikuta |
11. | kusaka ukata | kusumbua riziki | kuasi umaskini | kutafuta umaarufu |
12. | watosheleza | wasiridhike | wakinaishwe | wasikinai |
13. | haba na haba hujaza kibaba | apelekaye mkono kutamalaki si kazi | bura yangu sibadili na rehani | njia mbili zilimshinda fisi |
14. | kutusaidia | kuniauni | kujikimu | kukuokoa |
15. | kujikaza kisabuni | kuuma uzi | kujifunga kibwebwe | kupakata mikono |
Kutoka swali la 16 hadi 30, jibu swali kulingana na maagizo.
- Chagua sentensi iliyo na tashbihi jozi.
- Dada yake ana maringo kama tausi.
- Rudisha ana mbio mithili ya duma.
- Bahasha yangu ni nyeupe ja theluji.
- Wanafanana kama kurwa na doto.
- Tumia sifa "geni" kusanifisha sentensi ifuatayo;
Wazo alilotoa kuhusu nchi yake ni- ngeni.
- mgeni.
- ligeni.
- geni.
- Chagua ala ya muziki ambayo huchezwa kwa uta mdogo.
- Firimbi
- Zeze
- Marimba
- Zumari
- Kiulizi "ngapi" huwa tasa katika ngeli gani?
- I - ZI
- LI-YA
- KI-VI
- KU-KU
- Tenga silabi katika neno "mafunzo"
- m-a-f-u-n-z-o
- ma- fu- n - zo
- mafunzo
- maf - un-zo
- Kamilisha methali;
Kukopa harusi- isiyo na vigelegele.
- ingawa kulipa ni kugumu.
- kulipa matanga.
- lakini hakuna raha,
- Chagua sentensi iliyo sahihi kisarufi.
- Wewe na Musa ndio viranja wa darasa letu.
- Utajua aje hesabu bila kufanya mazoezi?
- Upande huu ni mpana kuuliko ule.
- Kwamba atakuja au atasusia, kwangu ni mmoja.
- Je, ni sentensi ipi iliyotumia kiunganifu-a- kwa usahihi?
- Rafiki ya Abdala ni Salim.
- Katikati mwa jiji kuna msongamano wa magari.
- Uwanjani kwa watoto kuna nyasi ndefu.
- Shauri ya Omari, hakumaliza kazi ya mwalimu.
- Chagua orodha yenye vivumishi pekee.
- Yangu, kivivu, yeye, juu ya
- Lini, ovyo, ya, ala!
- Pona, ona, safi, ghali.
- Wao, hiki, nyembamba, mwa
- Chagua maneno yaliyo katika ngeli ya I-ZI.
- Dahalia, korti, kawa.
- Maabara, kalamu, chupa.
- Maeneo, mizani, simu.
- Kimbilio, maskani, nyumba.
- Nomino kudhoofika lina konsonanti ngapi?
- 4
- 5
- 3
- 6
- Eleza matumizi ya “na”
Wana huzuni tangu wafiwe na mkoi wao.- Umiliki
- Mtendaji
- Hali
- Kiunganishi
- Ni sayari gani kati ya hizi iliyo angavu zaidi?
- Mshtarii
- Zuhura
- Utaridi
- Zohali
- Nahau enda magamaga ina maana ya
- enda kwa kutanua miguu.
- aga dunia.
- enda upesi.
- tembea polepole.
- Kimelea gani hupatikana katika maskani ya kuku?
- Siridado
- Funza
- Papasi
- Utitiri
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 hadi 44.
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Rafiki yangu, Bwana Kenzi almaarufu "mkereketwa❞ alihitaji tuonane uso kwa macho katika eneo la Shambahola siku mbili tatu zilizopita. Maadamu nilikuwa waya, sikuwa na budi ila kuhesabu hatua kuanzia kwangu hadi alipokuwa Kenzi. Si mtu hujikuna ajipatapo bwana!
Njiani walikuwapo wale ndugu zetu wanaoishi na ulemavu wakiwa katika hamsini zao za kuomba chochote kutoka kwa wapitanjia. Wengi wa wapitanjia waliwavalia miwani na kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa. Nilipowatazama, niliwahurumia na kuwasikitikia. Vitoto vyao je? Maskini, moja... mbili... tatu, mbavu hizo!
Nilifahamu kuwa sikuwa na chochote kwa hivyo, ili kuchelea kuunguzwa ndani kwa ndani, ilinipasa kukaza mwendo ili nisiwaone tena. Mara, nilikuwa nimewapa kisogo na kuyoyomea mbali. Moyoni nilijiambia kuwa iwapo Kenzi angenipa hela kidogo, ningepitia mahali pale ili angalau niwaachie kitu.
Baada ya kukinzana na misongamano ya watu na magari, nilijipenyeza hadi katika lango la Shambahola nikaichomoa rununu yangu kuukuu ili nimwarifu Kenzi kuwa nilikuwa nimetia guu. Naam, sifuri, saba, mbili, mbili.... mara shwa! Yarabi! Wewe.... mwizi... mshikeni! Kaniibia simu, mwi... Ikiwa umewahi kubeba maji kwa gunia, basi unafahamu ninachomaanisha. Kumbe mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi tu! Ama kweli, chambacho Kenzi, mjini ni shuleni.
Nilibaki nimejishika kichwa kwa mikono huku nikitweta si haba. Si lazima niandike kuwa nilikuwa nimenyong'onyea ungedhani konokono aliyenyunyiziwa chumvi. Ingawa ni muhimu sana kuyapokea yajayo, iliniwia vigumu kukabiliana na hali hiyo kwa muda huo. Nilihisi nimenyanyaswa na kuonewa pakubwa.
Haidhuru, nilipoingia Shambahola, sikuwa na jingine ila kuangazaangaza macho huku na kule kama pengine ningeangukiwa na nyota ya jaha kumwona Kenzi. Baada ya kuzurura kwa muda, nilimwona jamaa kwa mbali akinipungia mikono. Nilifurahi sana kumwona, Mbio, nilimwelekea ili nimsimulie yaliyojiri.
Nilipomaliza kumweleza yote, alicheka na kutingishika nusuru ya meno yake yaanguke kama si kule kuyashikilia kwa kiganja. Ala! Kwani nini kilichochekesha badala ya kusikitisha? Alicheka nini hasa? Baadaye alinieleza kuwa hiyo ilikuwa desturi kwa wageni mjini. Aliendelea kunifahamisha kuwa shababi huyo aliyenipokonya simu alikuwa mmoja wa wale "walemavu" .... ah
- Uhusiano baina ya Kenzi na msimulizi ni kwamba
- walikuwa ndugu wa toka nitoke.
- kulikuwa na urafiki mkuu kati yao.
- walikuwa wafanyakazi huko Shambahola.
- kulikuwa na uhasama mkuu baina yao.
- "...nilikuwa waya..." ni
- nahau inayomaanisha kuwa msimulizi hakuwa na pesa.
- istiara inayomaanisha kuwa msimulizi alikuwa mwembamba.
- msemo wenye maana kuwa ilibidi msemaji kuchukua hatua aliyoichukua.
- sitiara inayomaanisha kuwa msimulizi alikuwa mchovu.
- Msemaji alisafiri vipi hadi Shambahola? Kwa
- matwana.
- bodaboda.
- matatu.
- miguu.
- Kulingana na aya ya pili,
- wapitanjia hawakuwajali wale waliokuwa wakiomba.
- msemaji aliwahurumia bila kuwasikitikia wale ombaomba.
- baadhi ya wapitanjia walikuwa katika hali ya ulevi.
- msimulizi wetu aliwahurumia na kuwasikitikia watoto wale.
- Dondoo "moja... mbili... tatu, mbavu hizo! inatoa dhana gani?
- Mbavu za watoto wale ziliweza kuhesabika.
- Afya ya watoto wale iliyumba.
- Familia za ombaomba wale zilikuwa katika afya mbaya.
- Watoto wale walidhoofika kupindukia.
- Mwishoni mwa aya ya tatu mna dhan kuwa
- gae huwa chombo wakatiwe.
- ndo ndo ndo hujaza ndoo.
- kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
- ukiona vyaelea jua vimeundwa.
- Chagua kauli iliyo ya kweli kulingana na ufahamu.
- Lengo kuu la msimulizi kutoa simu ilikuwa kumwarifu Kenzi mjo wake.
- Rununu ya msimulizi haikuwa ndogo.
- Wazalendo walimsaidia msemaji katika kumkamata mkwepuzi yule.
- Watu wa Shambahola hujalishwa na matatizo ya wenzao.
- Ni hali gani iliyomwia vigumu mwandishi kukubaliana nayo? Hali ya
- kuyapokea yajayo.
- uchovu, wasiwasi na sintofahamu.
- kutafakari dhuluma aliyotendewa.
- kumsimulia Kenzi kisa kilichomkabili.
- ".... alicheka na kutingishika nusura meno yake yaanguke...."
- ni fani tu ya lugha ya kutilia chumvi.
- inamaanisha kuwa Kenzi alibahatika kwa kuwa meno yake yangeanguka.
- inatoa dhana kuwa kisa cha msemaji kilikuwa cha kuchekesha.
- ni mojawapo ya njia za kujieleza ueleweke vyema.
- "Walemavu"
- walihitaji kuonewa huruma.
- walikuwa sawa na chui ndani ya ngozi ya kondoo.
- walikuwa sawa na kuku mgeni asiyekosa kamba mguuni.
- waliwaibia watu simu, hasa wageni mjini.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 hadi 50.
Wakazi wa mitaa ya mabanda huogelea katika bahari kubwa sana ya changamoto. Baadhi ya changamoto zinazowakabili ni zile ambazo kwa yakini, wana uwezo wa kuzisitisha. Hata hivyo zipo nyingine ambazo kwa kweli juhudi za kuzisitisha zipo nje ya uwezo wao.
Mojawapo kati ya masaibu tumbi akidi yanayowatafuna ni hali duni ya usafi. Mingi ya mitaa hii hujulikana na kutambulika katika udororaji wa viwango vya usafi humo mitaani mwao. Si siri kuwa mitaa mingi ya mabanda haina misala, hivyo, huwalazimu wenyeji kutimizia haja zao kokote, hata vyumbani mwao! Ajabu iliyoje? Haya ni baadhi ya masaibu ya vitongoji duni.
Tatizo jingine ni la ukosefu wa usalama miongoni mwa wakazi wa mitaa husika. Wananchi wengi huamini na kusadiki kuwa baadhi ya wezi na majambazi sugu ambao majina yao hugonga vichwa vya habari kila wakati huishi mumo humo mitaani mwa mabanda. Utovu huu wa usalama umekithiri kiasi cha wakazi kuishi maisha ya roho mikononi. Dua za wakazi hawa daima huwa, "Nakuche tukushukuru, ewe Manani...."
Si suala la mjadala 'uwa asilimia kubwa sana vya watoto humo mitaani haitazamiki kwa mara ya pili. Si lolote, si chochote, vimbaumbau hasa! Ni nani atajali ilhali wazazi wao hupata wajaliwalo tu na wala si watakalo? Msamiati kama sodo kwa vitoto vya kike vilivyovunja ungo humo mitaani huwa ndoto. Si ajabu kurekodi kuwa kuishi huku gizani kwa wasichana hao maskini ndiko chimbuko hasa la ongezeko la visa vya utungwaji mimba mapema.
Ni jambo la kutia simanzi sana kuona kuwa katika mitaa mingi ya mabanda, viwango vya elimu viko chini sana ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchi. Hali hii huchangiwa na kuwa wazazi wengi humo hawana ajira za kutajika. Ni zile familia za "bora mate tumboni". Ndiyo, upo mpango wa elimu ya dezo katika shule za umma nchini. Swali ni: ikiwa ni pesa za kujipatia angalau kibaba cha unga ili kuokoa majahazi ya familia yanayozama ni kizungumkuti, seuze hiyo koto?.... Sare je?
- Mitaa ya mabanda ni sawa na
- maeneo ya umaskini.
- majumba mabovu mabovu.
- vitongoji duni.
- vijiji vinavyohangaika.
- Ni neno lipi halina maana sawa na kuzisitisha?
- Kuzikomesha.
- Kuzitamatisha.
- Kuzihitimisha.
- Kuzikatiza.
- Ni kitambulisho gani huweza kutumiwa kuijulia mitaa ya mabanda?
- Hali duni ya usafi.
- Usafi uliokithiri.
- Uchafu wa wakazi.
- Usafi wa mazingira.
- Chagua kisawe cha neno misala kulingana na habari.
- Choo.
- Mkeka.
- Mikeka.
- Vyoo.
- Kutokana na uhaba wa usalama miongoni mwa wakazi wa mitaa ya mabanda, wenyeji huishi
- katika hali ya sintofahamu.
- katika hali ya woga mwingi.
- wakiwa na wasiwasi mwingi.
- maisha ya ajabu sana.
- "...asilimia kubwa sana ya watoto humo mitaani haitazamiki kwa mara ya pili...." kwa sababu
- wanakera na kukirihi.
- wanatia aibu kwa mtazamaji.
- wanahuzunisha pakubwa.
- wao hulialia kila mara.
- Wakazi wengi wa mitaa ya mabanda ni
- walalahai.
- walalahoi.
- walalaheri.
- walanguzi.
- Mimba za mapema kwa wasichana humo mitaani huchangiwa na
- wasichana husika kutoielewa miili yao vyema.
- wasichana hao kutofahamu matumizi ya sodo.
- watoto hao wa kike kushiriki ngono kiholela.
- watoto hao wa kike kutojua namna ya kutumia sodo.
- Suala la viwango vya elimu kuwa duni humo mitaani mwa mabanda
- linafurahisha.
- linasumbua.
- linahamasisha.
- linahuzunisha.
- Wazazi huenda wasimudu karo na sare kwa kuwa
- pesa zao zatosha chakula tu.
- pesa zao zatosha sare tu.
- hawana pesa za kutosha.
- hawana pesa.
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Kamilisha insha ifuatayo kwa maneno yako mwenyewe na uifanye iwe ya kusisimua.
Si rahisi kuyasahau yaliyonikumba katika msitu wa Ngomeni. Awali, wazazi wangu walikuwa wamenikanya dhidi ya kwenda humo msituni, nami nikatia komango masikioni. Asubuhi hiyo,.............................................................................................................
MARKING SCHEME
- C
- D
- B
- D
- A
- B
- A
- A
- A
- A
- C
- C
- C
- B
- D
- D
- D
- B
- A
- B
- C
- D
- C
- D
- B
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- A
- D
- A
- B
- C
- A
- C
- A
- B
- C
- C
- A
- D
- C
- C
- B
- A
- D
- C
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 2 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students