Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.
Mazoezi ya viungo vya mwili.__1___uzingatiaji wa lishe bora___2__ ni njia muhimu ya kuimarisha___3__ zetu. Mtu___4__ viungo vyake mazoezi yafaayo___5___ vibaya kiafya.___6__, watu wengi____7__ kuwa kutofanya kazi zozote, hata zile nyepesi ni___8___cha ustaarabu wao. Si ibra, yaani si___9___ kwa waja kama hawa kudhoofika kiafya.
A | B | C | D | |
1 | dhidhi ya | mithli ya | mbali na | kinyume na |
2 | , | : | ___ | ; |
3 | sifa | miili | ari | siha |
4 | asipozifanyia | asipovifanyisha | akifanya | akifanyisha |
5 | huathirika | huathirikia | huathiri | huathirishwa |
6 | IIhali | Japo | Hata hivyo | Ingawa |
7 | hujua | husadiki | huelewa | hung'amua |
8 | kizingiti | kizuizi | kikwazo | kitambulisho |
9 | hoja | nadra | vigumu | ajabu |
Maimuna___10___kuenda shuleni kama____11___ ada yake. Safari yake ya masomo___12____ na changamoto za kila aina. Hata hivyo, alizidi kujikaza huku akielewa kuwa____13___. Aliiona elimu kama njia ya pekee ya____14___ jamii yake kutokana na umaskini___15___hali zao.
A | B | C | D | |
10 | alishika tariki | alitia nanga | alichana mbuga | aliweka nadhiri |
11 | iliyokuwa | iliokuwa | ilivyokuwa | ilipokuwa |
12 | ilikabidhiwa | ilikabiliwa | alikabiliwa | alizongwa |
13 | msasi haogopi miiba | msafiri hana miiko | hamadi kibindoni silaha mkononi | heshima haiji bali huletwa |
14 | kuliokoa | kuwaokoa | kumwoka | kuiokoa |
15 | uliowazorotesha | uliozizorotesha | uliyoizorotesha | uliyowazorotesha |
Kutoka swali 16 - 30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.
- Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
- Sogora waliwatumbuiza sana kwa kigoma hivyo.
- Masogora walikutumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
- Sogora walikutumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
- Masogora waliwatumbuiza sana kwa vigoma hivyo.
- Chagua jozi iliyo tofauti na nyingine.
- Sabalkheri -Akheri.
- Alamsiki -Binuru.
- Buruani - Buriani dawa.
- Usiku mwaka - Majaliwa.
- Ni sentensi ipi iliyotumia kiambishi 'ka` kuonyesha kusudi?
- Komu alijikwaa akaumia kidole gumba.
- Deya aliamka akaandaa kiamshakinywa akala akaondoka.
- Salma ameenda nyumbani akawaone wazazi wake.
- "Tutaanza safari kesho asubuhi," akasema.
- Konokono ni kwa kombe ilivyo kuku kwa
- zeriba
- kizimba
- kifukofuko
- kitala.
- Bainisha orodha yenye vihusishi pekee.
- Kando ya, licha ya, mbali na, katika
- Polepole, vibaya, jioni, kwa sauti
- Mithili ya, karibu na, dhidi ya, kwenye
- Maridadi, gumu, nyepesi, vyenyewe.
- Tegua kitendawili kifuatacho.
Nyumba yangu ina milango mingi.- Kichunguu
- Kiota
- Uyoga
- Kibuyu.
- Chagua sentensi yenye maana sawa na hii.
Hakuenda mjini wala hakununua mboga.- Asingalienda mjini asingalinunua mboga.
- Akienda mjini hatanunua mboga.
- Angeenda mjini asingenunua mboga.
- Angalienda mjini angalinunua mboga.
- Kipi ni kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi?
- Andika - Maandishi.
- Legevu - Ulegezaji.
- Uhodari - Hodari.
- Angalia - Mwangalifu.
- Bela ni dadaye Patu. Maria ameolewa na Patu. Bela atamwitaje Maria?
- Mwamu
- Mpwa
- Wifi
- Mwanyumba.
- Andika katika usemi wa taarifa;
Kaka! Ukinipa nafasi nitakufunza kuuimba wimbo huu.- Kaka alimwomba ampe nafasi ya kufunzwa wimbo huu.
- Kaka alimwambia kuwa iwapo angempa nafasi angemfunza wimbo huo
- Kaka alimwambia kuwa kama atampa nafasi atamfunza wimbo huu.
- Kaka alimwambia kwamba iwapo angempa nafasi angemfunza wimbo huu.
- Meza, dawati na kochi, kwa jina moja ni
- samani
- viti
- ala
- pembejeo
- Kanusha sentensi ifuatayo.
Mkono uliotibiwa umepona kabisa- Mkono usiotibiwa haukupona kabisa.
- Mkono uliotibiwa haukupona kabisa.
- Mkono usiotibiwa haujapona kabisa.
- Mkono uliotibiwa haujapona kabisa.
- "Gae huwa chombo wakatiwe" ni kwa watu wanaowadharau wale waliowahi kuwasaidia. "Mzigo wa chungu ni chembe moja ya mchele" ni kwa watu
- wanaopuuza thamani ya vitu vikubwa
- wanaotishwa na matatizo ya wenzao
- wanaoviona vitu vidogo kuwa na thamani kubwa
- wanaovidharau vyao kwa kutamani vya wenzao.
- Zipi ni nomino za wingi?
- Magari, nyuzi
- Ufuta, marashi
- Njaa, hamaki
- Kombamwiko, askarikanzu.
- Sentensi ifuatayo imetumia tamathali gani za usemi?
Rajab ni kinyago, alituvunja mbavu kwa masimulizi yake- Tashhisi, chuku
- Kinaya, tashbihi
- Sitiari, kinaya
- Sitiari, nahau.
Soma ufahamu ufuatao kwa makini kisha ujibu maswali 31-40.
Nilikuwa chumbani mwangu nikijisomea novela ili kukinaisha uraibu wangu. Mama aliniita ghafla, nikaukunja ukurasa niliokuwa nikisoma kabla ya kutoka. Alikuwa ameshika noti ya shilingi mia tano. "Nenda kwa Bwana Mauzo uninunulie kilo ya sukari, maziwa na paketi ya unga," aliniambia huku akinikabidhi fulusi zile. "Hewala mama," niliitikia huku niking'oa nanga kuelekea kwenye duka hilo lililokuwa takriban kilomita mbili kutoka pale nyumbani.
Njiani nilimkuta rafiki yangu, Aviza akiendesha baiskeli yake. Nilimwamkua naye akaniitikia kwa ucheshi kama ilivyokuwa ada yake. Nilimweleza kuwa mama alikuwa amenituma dukani na kwamba nisingethubutu kuwa kihongwe kwa kuwa sisi watoto tunao wajibu wa kuwaauni wavyele wetu. Huku akikubaliana nami, alijitolea kunisaidia. "Kwa kuwa sina ujuzi zaidi yako katika kucharaza baiskeli, utaendesha wewe nami niketi kwenye karia," alisema kisha akanikabidhi baiskeli ile.
Tuliichupia baiskeli tukaiendesha kwa uangalifu katika barabara ile yenye kuruba nyingi. Siku zote nilizingatia kauli ya wahenga kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Muda si muda tulifika
dukani.
Umayamaya wa washitiri ulikazania kununua bidhaa. Wanyonge walikaa kando kusubiri muujiza angaa wanunue. Wenye misuli kama mimi nao waliwasukuma wenzao almradi wapate fursa ya kununua bidhaa walizohitaji. Jambo moja lililowavuta wateja kwa Bwana Mauzo ni kwamba hakudiriki kuwapunja wateja wake licha ya kuwa na duka la kipekee pale kijijini. Wema nao hauozi. Hali ilikuwa hivyo siku zote katika duka lake.
Baada ya kujipenyezapenyeza, nilijipata nimekabiliana ana kwa ana na mwenye duka. Usoni, alionyesha tabasamu yake ya kawaida. Pindi tu tulipotazamana, niliuona uso wake ukibadilika ghafla, akawa kama aliyeona mzimu mbele yake. Hali hiyo ilinitia wahaka kidogo. Nilishuku kuwa labda alifikiri nimeenda kumkopa. Falsfa ya Bwana Mauzo ilikuwa wazi kwa wote "Lipa leo nitakukopesha kesho." Ili kumwondolea hofu yake, nilitabasamu, nikaunyosha mkono huku nikimwonyesha noti aliyonipa mama. Ajabu ni kuwa hakuipokea.
Mara noti ile ilinyakuliwa na mkono mzito kama nanga. Kwa udhia mwingi, niligeuka kumwona hasidi huyo aliyenuia kuchuma riziki kutoka mkononi mwangu pasipo kutoka jasho. Lo! Maneno yalinikauka kinywani, macho yakanitoka pima nisiweze kutamka 'be' wala 'te'. Uso wangu ulikumbana na mtutu wa bunduki. Tuliagizwa kulala sakafuni huku majambazi wale wakijiandaa kutupora. Acha mtafaruku uingie! Hakika angurumapo simba mcheza ni nani?
Wahalifu wawili walijitoma dukani wakaanza kupakia pesa za Bwana Mauzo katika mkoba. Mwanaume mmoja aliyekuwa nyuma yangu alimtazama mmoja wao aliyebaki nje akitutishia kwa bunduki. Sijui alikuwa akiwazia nini. Alitazamana na mwanamume mwenye bunduki akasimama na kupiga hatua akienda kwake.
"Nitakufyatulia risasi kichwani mpumbavu wewe!" Jambazi yule alifoka kwa ukali. “Nina hakika kuwa huna uwezo huo," alijibu mwenzetu huku akitabasamu. Jambazi alibabaika. Kumbe mteja mwenzetu alikuwa askari polisi, kwa hivyo alitambua kuwa bunduki ile ilikuwa bandia. Sote tulipandwa na mori, wengine wetu wakiwashambulia kitutu wahalifu hao. Hofu ilituondokea tuliposikia kuwa bunduki ile ilikuwa bandia.
Kamba zilitolewa pale dukani, wakafungwa kitita na kupelekwa marshimarshi hadi kituoni mwa polisi. Noti yangu ilitolewa mfukoni mwa jambazi aliyeniibia. Nilinunua bidhaa alizonituma mama, Bwana Mauzo akawahudumia wachache kisha akafunga duka ili akaandikishe taarifa kituoni. Japo nilichelewa kurudi nyumbani, nilikuwa na uhondo wa kusimulia aila yangu
kuhusu tukio lile.
- Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza.
- Mama hakufurahishwa na mazoea ya msimulizi
- Msimulizi alikuwa na mazoeza ya kusoma vitabu vya hadithi
- Bwana Mauzo alimiliki duka la pekee kijijini.
- Aviza alizoea kucheka kila alipomwona msimulizi.
- Dukani alikotumwa mwandishi
- kulikuwa zaidi ya kilomita mbili kutoka kwao
- kulikuwa kilomita mbili kamili kutoka kwao
- kulikuwa karibu kilomita mbili kutoka kwao
- kulikuwa pua na mdomo kutoka kwao.
- Kwa nini Aviza alimpa msimulizi baiskeli yake?
- Msimulizi alikuwa hodari zaidi katika kuendesha baiskeli.
- Msimulizi alionyesha hamu kubwa zaidi ya kuendesha baiskeli.
- Aviza hakujua kuiendesha baiskeli vizuri.
- Dukani walikonuia kuenda kulikuwa mbali sana.
- Maneno 'Kuwa kihongwe' yametumia tamathali gani ya usemi?
- Tashbihi
- Chuku
- Tashhisi
- Sitiari.
- Sifa gani zinamwafiki zaidi msimulizi wa kifungu?
- Mwenye nguvu, afanyaye mambo kwa uangalifu.
- Mwerevu, asiyewadhulumu wanyonge.
- Mtiifu, hodari katika mambo mbalimbali.
- Mwenye udaku, anayejulikana kijijini.
- Wateja walifurika dukani kwa Bwana Mauzo kwa kuwa
- hapakuwa na maduka mengine
- aliendesha shughuli zake kwa uadilifu
- aliuza bidhaa za aina mbalimbali
- aghalabu waliendea bidhaa kwa mkopo.
- Kulingana na aya ya tano
- Bwana Mauzo aliwataka wateja walipie bidhaa papo hapo
- mtu alihitajika kununua angaa mara moja ndipo akopeshwe
- shaka ya mwenye duka iliondoka alipoonyeshwa pesa
- uso wa mwenye duka ulibadilika pindi tu alipomwona msimulizi.
- Mwanaume aliyetajwa hakujali alipotolewa vitisho kwa sababu
- alikuwa afisa wa usalama
- jambazi alikuwa mwoga
- alikuwa na uwezo wa kujihami
- alitambua kuwa bunduki ile isingemdhuru.
- Ni methali gani inayofaa zaidi kupigia mfano kifungu hiki?
- Mwenye nguvu mpishe.
- Pwagu hupata pwaguzi.
- Akili nyingi huondoa maarifa.
- Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
- Neno 'hewalla' kama lilivyotumika A. ni kiingizi cha kusisitiza jambo B. ni kihusishi cha wakati C. ni kihisishi cha kukubaliana na jambo D. ni kielezi cha kufafanua jambo.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 41 hadi 50.
Hakuna jambo litakalohatarisha maisha yetu humu duniani kuliko ukataji wa misitu. Hakika, ukataji huu si jambo jipya kwetu. Hata mababu na nyanya zetu walikata miti. Walifanya hivyo kwa matumizi mbalimbali kama vile ujenzi, dawa, mavazi na kadhalika. Ukataji miti siku hizo, hata hivyo, ulifanywa kwa uangalifu. Baadhi ya miti ilikatwa kwa ajili ya kafara na kwa matumizi mahsusi lakini leo, miti hukatwa bila kusudi maalum.
Si ajabu kupata miti ikikatwa milimani kwa kusudi la kupanda dawa za kulevya kisiri ili isijulikane na serikali. Aidha, miti imekatwa ili kujenga majumba yetu katika mazingira yaliyo na hewa mwanana bila kujali madhara tunayosababishia mandhari yetu. Tumekata miti kando ya mito ili kulima vishamba vya mboga karibu na chemichemi ya maji. Kile ambacho binadamu hafahamu ni kuwa miti hii ndiyo inayoshikilia udongo usimomonyoke.
Inafahamika kuwa misitu ni asili ya chakula na maskani ya wanyama. Misitu inapokatwa, ama wanyama watakufa au watahamia kwingine. Huko kwingine kunaweza kuwa kwenye makao yetu binadamu. Watavamia mashamba yetu na kuhatarisha maisha yetu na ya wanetu.
Tusisahau kuwa misitu huvuta mvua. Tunapokata miti tunapunguza mvua na tunaharakisha ukame. Bila mvua, mito na maziwa yatakauka. Bila maji sisi hatutakuwa na uhai. Mifugo wetu nao watafuata mkondo uo huo.
Hebu fikiria utafanyaje uamkapo asubuhi na kuambiwa kuwa mfadhili wako ameachishwa kazi katika kiwanda cha karatasi kilichopo hapo karibu. Kuna uwezekano wa hayo kutokea iwapo ukataji wa misitu utaendelea. Viwanda vitakosa malighafi, hivyo vitafungwa na watu kumwaga unga. Basi vitu kama karatasi, mbao, gundi na viberiti vitakosekana au kupanda bei.
Vilevile, misitu inapokatwa, dawa za kienyeji na za kisasa zitapotea kwa maana nyingi kati yazo hutokana na miti. Wagonjwa wengi watatangulia mbele ya haki kwa kukosa dawa. Je, wakataji miti wenyewe wajua wao pia wataangamia?
Misitu mingi yenye manufaa makubwa huchukua muda mrefu kukomaa. Kwa hivyo, tunapoikata bila mpango tunavinyima vizazi vya kesho urithi huu wa kimaumbile. Vijana wengi watakuwa wakizisoma habari za misitu vitabuni bila kuiona misitu yenyewe. Utafiti wa miti pia utakwama na elimu itakoseshwa mahali pa uvumbuzi nyanjani. Sasa iko wapi faida ya kufunza taaluma ya misitu katika shule na vyuo kinadharia tu kama misitu yenyewe haipo?
Miti isipokuwepo hakuna kitu kitakachozuia mmomonyoko wa udongo wetu wenye rutuba. Mimea itadhoofika ajabu. Mchanga nao utajaa kwenye mito na maziwa. Hali hii ikiendelea maziwa yatapotea.
Hakuna mandhari yavutiayo kama yale yenye rangi ya kijani. Mtu atembeapo karibu na miti jioni, hufurahia harufu tofauti; harufu ya maua na mzizimo wa upepo mwanana. Miti ikipotea ghafla hubaki visiki butu vyenye rangi ya hudhurungi au kijivu isiyovutia. Badala ya mzizimo huwa upepo mkali uliobeba vumbi jingi. Matokeo yake ni mawili. Kwanza, upepo huu waweza kusababisha uharibifu kama vile kuangusha miti na hata kung'oa mapaa ya nyumba.
Hasara nyingine ni kuwa upepo husafirisha viini vinavyoeneza magonjwa chungu'nzima ya macho, koo na mapafu. Hewa itachafuka maana hakuna miti ya kuisafisha. Mnaona! sisi wenyewe tunajiua. Tamaa mbele mauti nyuma.
- Ni kweli kusema kuwa
- ukataji wa misitu ni hatari pekee inayoweza kuwaangamiza watu duniani
- hapo awali, ukataji wa miti haukuwa ukifanyika kiholela
- wazee wa zamani hawakuthubutu kuikata misitu asilani
- awali, miti ilikuwa na matumizi mbalimbali, kinyume na ilivyo sasa.
- Wanaokata miti milimani hufanya hivyo ili
- wapate miti iliyo bora zaidi
- waharibu misitu makusudi
- wakuze mboga karibu na chemichemi
- washiriki kilimo cha mimea haramu.
- Kulima kwenye kingo za mito kuna athari gani kulingana na kifungu?
- Kusababisha memonyoko wa udongo.
- Kusababisha kukauka kwa vyanzo vya maji.
- Kufariki kwa viumbe wa majini.
- Kuchafua maji yanayofanikisha kilimo.
- Kulingana na aya ya tatu
- kukata miti ovyoovyo husababisha mgogoro wa binadamu na wanyama
- kukata miti ovyoovyo ni kichocheo kikuu cha ukame
- maeneo yasiyo na misitu hayana binadamu wala wanyama
- watu wengine huharibu mazingira kwa nia ya kuanzisha makao yao.
- Kufungwa kwa viwanda katika kifungu husababishwa na
- ukosefu wa wafanyakazi
- hali ngumu ya kiuchumi
- kukosekana kwa malighafi
- kupungua kwa mvua.
- Chagua msemo mwingine wenye maana sawa na 'watatangulia mbele ya haki'.
- Watakula mwata.
- Wataenda na ulele ngoma.
- Watakufa moyo.
- Wataenda nguu.
- Manufaa ya misitu kulingana na makala haya ni
- kufanikisha elimu na dawa za kulevya
- kuhifadhi maji na kuzuia mmomonyoko wa udongo
- urithi wa vizazi na kubuniwa kwa mitambo
- kuongeza nafasi za kazi na kusafisha hewa.
- Matokeo ya upepo mkali yanaweza kuwa
- magonjwa ya mapafu na ardhi kukosa mvuto
- kuvunja miti na kutatiza starehe za watu
- kuporomoka kwa majengo na kueneza maradhi
- mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa maziwa.
- Kauli 'sisi wenyewe tunajiua' inaonyesha kuwa
- binadamu wanauana wenyewe kwa wenyewe
- tunajiangamiza kwa matendo yetu
- bila misitu vizazi vijazo havitakuwepo
- binadamu amevamiwa na maradhi chungu nzima.
- Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
- Faida za misitu.
- Mmomonyoko wa udongo.
- Tamaa mbele mauti nyuma.
- Madhara ya uharibifu wa misitu.
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa. Ufuatao ni mwanzo wa insha. Iendeleze kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Mchana kutwa sikuweza kupata utulivu. Nilitamani kurudi nyumbani haraka ili............................
MARKING SCHEME
- C
- A
- D
- B
- A
- C
- B
- D
- D
- A
- C
- B
- A
- D
- B
- D
- A
- C
- B
- C
- A
- D
- D
- C
- D
- A
- D
- C
- B
- D
- B
- C
- A
- D
- A
- B
- A
- D
- B
- C
- B
- D
- A
- A
- C
- B
- D
- C
- B
- D
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 2 Exams 2023 Set 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students