Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, chagua jibu sahihi kati ya yale manne uliyopewa.
Yena__1___kofia aina ya__2___kichwani: Jasho lilikuwa likimtiririka tiriri kwa kuwa kulikuwa na joto__4___mno. Alimwangalia__5___ yake na kushindwa la kufanya. Ajali hiyo ilimwacha mwenzake bila___6__ mmoja. Alipoona watu walimtania na kumbandika jina "kikono." Kutoka siku aliyoipata ajali, rafiki_____ Yona hakuendesha pikipiki tena. Alipowaona vijana wakiendesha pikipiki kwa__8___ aliwaonea__9___ na alipopata nafasi, aliwashauri kuwa haraka haraka haina baraka.
A | B | C | D | |
1 | alivaa | alifua | alivua | alifaa |
2 | kikuba | kikoi | joho | chepeo |
3 | pake | mwake | yake | kwake |
4 | nyingi | jingi | mingi | kingi |
5 | sahibu | mwendani | hasimu | msena |
6 | mwili | mguu | sikio | mkono |
7 | ya | wa | la | cha |
8 | mbio | haraka | polepole | kasi |
9 | mayo | wivu | huruma | kinyama |
Kiongozi___10___alizifuja pesa____11__ za umma na kujenga___12____kubwa ambacho kiliuzwa vinywaji vya aina mbalimbali.__13___ walikasirika na kugoma. Aliliwa___14__ na kupelekwa___15___ ambako alikaa kwa saa kumi. Siku iliyofuata alipelekwa mahakamani.
A | B | C | D | |
10 | shupavu | mihiri | katili | mwadilifu |
11 | lote | wote | yote | zote |
12 | baa | mkahawa | klabu | hoteli |
13 | Waliomwajiri | Waliomchagua | Waliochaguliwa | Aliowapenda |
14 | mbaroni | pengu | shime | ufunguo |
15 | kortini | jalani | rumande | korokoroni |
Kutoka nambari 16 hadi 30, chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua wingi wa;
Uwanja wangu una nyasi ndefu.- Nyanja zangu zina nyasi ndefu.
- Nyanja zetu zina nyasi ndefu.
- Uwanja wetu una nyasi ndefu.
- Uwanja wetu una unyasi mrefu.
- Chagua jina ambalo ni tofauti na mengine.
- Nasaba
- Jamaa
- Mbari
- Nikahi
- Uadilifu, wema, ubora ni aina gani ya nomino?
- Nomino za wingi
- Nomino za dhahania
- Nomino za makundi
- Nomino za kuhesabika
- Chagua kielezi ambacho hakijaambatanishwa vyema na aina yake.
- Mwakani - wakati
- Haraka - namna
- Kidogo - jinsi
- Mara mbili - idadi
- Je, jina mede huwa katika ngeli gani?
- I-ZI
- U-YA
- A-WA.
- I-I
- Mimi ni kifaa cha mkulima. Kazi yangu ni kutandaza mchanga au mbolea. Wakati mwingine mimi hukusanya takataka. Mimi ni nani?
- Beleshi
- Reki
- Jembe
- Mundu
- Kamilisha takanali hii ya sauti. Yeye alifunga mzigo wake
- mwaa
- nga
- ji
- ndi
- Tambua umbo hiii.
- Mistari sulub
- Mistari sambamba
- Mistari mshazari
- Mitari butu
- Ni sentensi gani inayoonyesha majuto?
- Ningalifanya bidii ningalifaulu maishani
- Ningekuwa na hela ningenunua kalamu
- Nisingefuata ushauri wake nisingefaulu
- Nikifuata mawaidha nitafua dafu maishani
- Ugonjwa unaofanya mgonjwa kukoja damu huitwaje?
- Kaswende
- Upele
- Safura
- Kichocho
- Tegua kitendawili hiki:
Chaenda mbali lakini hakiondoki.- macho
- jua
- njia
- mto
- Ni mdudu yupi ambaye hafyonzi damu?
- Bunzi
- Kiroboto
- Chawa
- Mbu
- Ni sentensi gani inaonyesha ngeli ya KU-KU?
- Chumbani inle mlikuwa na kukurukakara
- Kule jehanamu kutakuwa na mateso tele
- Shuleni petu kuna madaraka mengi sana
- Kucheza kwake kuliwafurahisha mashabiki
- Ng'ombe hurarama lakini chui
- huluza
- huvuma
- hunguruma
- hukorokocha
- Neno dunia lina sauti ngapi?
- Tano
- Tatu
- Mbili
- Nne
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.
Vitabu vyote vitakatifu vinatufunza tuwe waaminifu na tusithubutu kamwe kuzungumza uongo kwani mambo ya uongo hayadumu. Nadhani ni kwa sababu hii wahenga wakaeleza kuwa njia ya mwongo ni fupi. Mzee siambiwi alitanabahi kuwa uongo haufai baada ya kuona mambo yamemzonga kama chafu anavyomzonga mbuzi.
Kijiji cha Maganya kiliangukiwa na nyota ya jaha kubwa baada ya wafadhili kujenga chuo cha mafunzo ya watoto yatima na shule. Kila mtu aliyekuwa na watoto yatima alitakiwa kwenda kuwasajili chuoni. Hapo wangesomeshwa mafunzo ya kawaida pamoja na kufunzwa taaluma za ufundi wa kila fani. Kulikuwa na kazi za uashi. Uhadisi, taaluma ya tarakilishi mingoni mwa kazi nyingine. Nafasi zilikuwa wazi kwa mtoto yeyote nchini muradi awe yatima na kufiwa na mzazi mmoja au wote wawili. Vilevile kulikuwa na sehemu ya walemavu wa aina zote katika chuo hicho. Hawa nao walikuwa na rabiba yao ya masomo kulingana na uwezo waliokuwa nao.
Mzee Siambiwi, aliyekuwa mtu bahili na mwenye kupenda kuyakwepa majukumu yake ya malezi alipiga bango vile angefaidika kwa fursa hiyo. Siku moja asubuhi Siambiwi alimwita mkewe na kumketisha kitako. "Sharti nimpeleke kitindamimba wetu nasari ya yatima." Siambiwi alimwambia mkewe huku macho ameyatoa ungedhani ni ya bundi.
Mkewe alikiona hicho kama kioja kikubwa kwani wote walikuwa hawajakata kamba, isitoshe mumewe alijiweza kifedha. Ubishi mkubwa ulizuka. Mzee Siambiwi alisisitiza kuwa kutompeleka mwanawe . asome hapo bure ni sawa na mtu mpumbavu ambaye huacha jua lichomoze ashindwe kuliota kisha alitafute waka wa jioni.
Majadiliano yakakomea hapo kama sentensi iliyowekwa kikomo. Majonzi hayo yalimchoma sana mama inoyoni hadi akapata maradhi ya shinikizo la damu yaliyompeleka jongomeo, bila nauli wala matwana. Asubuhi ya majogoo Mzee Siambiwi na mkembe wake mikononi alikuwa kwenye lango la nasuri ya yatima. Alipokelewa kwa heshima kubwa na bawabu na kuelekezwa alikostahili kwenda huko alimwandikisha mtoto kwa mwalimu mkuu kuwa yeye alimwokota njiani na hivyo ni msamaria mwema. Mtoto alipokelewa na kupewa yaya wa watoto wadogo.
Miaka ilipeperuka ungedhani imepachikwa mbawa. Kitimtim alikua na kuwa mkubwa. Inasomekana alikuwa na bongo la sumaku. Aliongoza kwenye mitihani yake yote hadi akaingia chuo kikuu. Huko alifuzu na kupata kazi ya uhandisi. Alikuwa mhandisi mkuu nchini. Siambiwi wakati huo pesa zilikuwa zimemwishia na kubaki maskini hohehahe.
Siku moja alifunga safari kwenda jijini kumtafuta mwanawe ili akamwombe usaidizi na pia amweleze kuwa yeye ni mzazi wake. Kitimtim alishangaa kukiona kizee kilichodai kuwa mzazi wake kikimlilia machozi kupukupu. Alifahamu tangu utotoni mwake kuwa yatima. Siambiwi alidinda kutoka ofisini na ikabidi polisi waitwe kumtoa nje. Alimshika koti mwanawe na kukatalia kumwachia. Palizuka kizaazaa patashika. Uchunguzi wa kitaalamu wa hospitali na ushahidi ulitolewa. Mzee Siambiwi akawa na bahati kama mtende.
- Kulingana na aya ya kwanza ni bayana kuwa
- njia ya mwongo huwa ndefu
- uongo humletea mtu mambo
- mbuzi huzongwa kwa uongo wake
- kuna vitabu ambavyo huenzi uongo
- Bahati iliyowapata wanakijiji ni gani?
- Waliangukiwa na nyota za angani
- Walifundishiwa watoto bure bilashi
- Walijengewa vyuo vya ufundi
- Walipata watu wakusaidia viokote
- Waliofaa kujiandikisha chuoni
- walikuwa wamepewa barua za mwaliko
- walikuwa na watoto wengi
- walihitaji msaada wa wafadhili
- walitaka kupewa elimu nzuri
- Neno jingine lenye maana sawa na uhandisi ni
- uinjinia
- uhesi
- uhasibu
- usanii
- Chuo hiki cha ufadhili hakikubagua kwa kuwa
- kiliwaalika watoto wote wa kijiji
- kiliwapa wazazi wote nafasi sawa
- kiliwasaidia mayatima na walemavu
- kiliwapa mafunzo ya aina mbalimbali
- Unafikiri ni kwa nini ratiba nyingine huwa na tofauti?
- Vyuo hufunza kozi tofauti
- Uwezo wa wanafunzi hutofautiana
- Huwa mayatima na wengine wamelemaa
- Ulezi wa watoto wote si sawa
- Mkewe Siambiwi alienda jongomeo kwa kuwa
- mumewe alitaka aoge
- mwanawe alienda shule ya yatima
- aliugua ugonjwa uliomweza
- alilipa nauli ya kwenda jongomeo
- Siambiwi ni jina linalolingana na tabia ya mzee huyu. Mbinu hii huitwaje?
- Majuzi
- Lakabu
- Kupanga
- Somo
- Kitimtim alikuwa mtoto mwerevu kwa kuwa
- alimkana babaye ambaye alimtekeleza
- alipewa kazi pamoja na ofisi kubwa
- alielewa mambo haraka na akawa fundi
- alimsaidia babaye na wanakijiji pia
- Kulingana na kifungu hiki ni kweli kusema kuwa
- Kitimtim alihitaji kusaidiwa ili asome
- mamaye Kitimtim alikuwa na pesa nyingi
- chuo hicho kilijua Kitimtim ana wazazi
- Babaye Kitimtim alikuwa mtu mchoyo sana
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50
Je, umewahi kutafakari kuhusu namna wanafunzi wengi, ukiwemo miongoni mwao, wanavyosafiri kwenda shuleni? Yumkini jibu lako kwa swali hili litadhihirisha kwamba asilimia kubwa hutembea kwenda shuleni, wengine hutumia baiskeli, magari ya umma na ya kibinafsi, pikipiki na gari mosi. Bila shaka aina ya usafiri hutofautiana kulingana na uwezo wa kiuchumi na umbali baina ya mwanafunzi na shule yake.
Kila aina ya usafiri ina changamoto maalum. Mathalani ikiwa umezungumza na wenzako ambao hutembea kwenda shuleni, haikosi wamekueleza dhiki wanazokumbana nazo. Licha ya safari za aina hii kuwachosha wanafunzi, ni wazi kuwa wanafunzi wengine hata hukosa masomo kwa sababu ya kutopitika kwa njia wakati wa mvua nyingi.
Pengine hata wewe umewahi kujipata katika njia panda baada ya daraja unalovukia kusombwa na maji ya mto uliofurika. Isitoshe, watembeao huweza kuathirika kiafya wakati wa kipupwe. Baridi huweza kuwasababishia pumu au hata kichomi. Wengine huwa katika hatari ya kuteleza kwenye njia zenye matope na kuvunjika viungo vya mwili. Hawa pia wamo katika hatari zaidi ya kutekwa nyara na hata kunyanyaswa kimapenzi.
Wanafunzi wengine huwahusudu wale ambao husafiri shuleni, ama kweli gari la sule, au la kibinafsi. Wakiulizwa kuhusu kiini cha husuda hii, wanasema kwamba wenzao hawa hawachoki kwani magari haya yanawachukua kutoka mlangoni mwa nyumba zao. Hata hivyo ukichunguza vyema utapata kwamba hata hawa wana matatizo sugu. Kwa vile magari ya shule huwabeba wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali, magari haya hayana budi kuanza safari mapema. Hii huwalazimu wanafunzi nao kuamka alfajiri na mapema ili kuyawahi magari haya. Matokeo ni kwamba wanafunzi wengi hawadiriki kulala usingizi wa kutosha. Kuna wale ambao hulala saa nne usiku baada ya kukamilisha kazi za darasani, kisha wanaraushwa saa kumi ili kijitayarisha basi la sa kumi na moja. Wanafunzi wa aina hii hukumbwa na uchovu, na bila shaka husinzia darasani.
Isitoshe, wanafunzi wanaotumia usafiri wa umma hulalamikia msongamano wa magari ambao unawafanya kukawia njiani, na hata kupewa adhabu kwa kuchelewa kufika shuleni. Wengine hata hukataliwa na magari ya abiria, eti wanalipa fedha kidogo na kuwasababishia wenye magari hasara. Wanafunzi hawa huaibika na kulazimika kutembea hadi shuleni. Hali kadhalika magari ya umma humpa mwanafunzii mazingira ya kujifunzia tabia mzuri na mbaya. Pamoja na wanafunzi hawa hupata fursa ya kutengamana na wenzao kutoka shule nyingine, wao pia huweza kuathiriwa vibaya na hulka za wasafiri wengine. Kuna wale ambao huiga lugha, mitindo ya mavazi, namna ya kutembea na hata mienendo mingine ya madereva na utingo. Wengine huishia kuwa waraibu sugu wa vileo kutokana na vielezo wanavyopata kwenye magari haya. Muziki, picha na video na mazungumzo kupitia vyombo vya habari vilivyo kwenye magari haya huchangia kuzorotesha tabia ya wanafunzi. Hii ni kwa sababu baadhi ya maswala yanayozungumziwa ni ya aibu na hayapaswi kusikilizwa na watu wa umri mbichi.
Nihahiri kwamba kila aina ya usafiri ina athari zake. Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Usafiri unaitajika katika kufanikisha masomo ya wanafunzi na katika uchukuzi wa bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanahitaji shuleni. Ni jukumu la kila mwanajamii kuhakikisha kwamba mikakati ifaayo imewekwa ili kukinga dhidi ya madhara yanayoandahana na kila aina ya usafiri. Wanafunzi nao wakae ange kutambua watu ambao huenda wakatosa katika maovu. Wachujo ya kuiga na ya kukataa.
- Ni bayana kuwa usafiri wa wanafunzi
- hauna changamoto nyingi
- huwa sawa kulingana na mwandishi
- huwa rahisi kwa wanaotembea
- hutegemea uchumi na umbali
- Kulingana na mwandishi ni wazi kuwa kila aina ya usafiri
- huwa na changamoto ambazo ni nzuri
- humtatiza mwanafunzi kwa njia fulani
- humtunza mwanafunzi na kumfanya bora
- huweza kumnoa mwanafunzi kimaadili
- Wanafunzi hasa wanaotembea huathirika vipi kulingana na kifungu hiki?
- Kutekwa nyara na kusikiliza nyimbo mbaya
- Kunyanyaswa kimapenzi na wanafunzi wenzao
- Kupatwa na magonjwa yanayolewa na baridi
- Kutazama runinga na kuvunjika viungo
- Ni nini maana ya huwahusudu kulingana na kifungu hiki?
- Huponda kwa sababu fulani
- Huhimizwa kwa sababu fulani
- Huchukia kwa hali fulani
- Huvuliwa na starehe fulani
- Kulingana na aya ya pili, mwanafunzi huchanganyikiwa iwapo
- njia ni mbili na hajui ya kupitia
- wachoka na kusombwa na maji
- njia anayotumia haipitiki hata kidogo
- kuna baridi kali na watekanyara
- Ni kauli gani sahihi kulinana na kifungu hiki?
- Wanafunzi huraushwa mapema ili wasichelewe .
- Wanafunzi wote wanazo changamoto zinzaofanana
- Wanafunzi wengi huchoka na hufeli mtihani
- Wanaosafiri kwa magari wana starehe sana
- Tabia za mwanafunzi zinaweza kuathiriwa na nini?
- Madereva wa magari ambao huwa wema
- Aina ya usafiri na wanaosoma nao
- Wasafiri na mitandao anayoitumia mwanafunzi
- Mazingira na watu anaotangamana nao
- Kuchelewa kwa mwanafunzi anayesafiri kwa magari ya umma husababishwa na nini?
- Madereva na utingo husukisha watu kila stani
- Kukaa sana njiani kwa sababu ya msongamano
- Kupewa adhabu ya kuchelewa na walimu shuleni
- Kukataa kuwabeba wanafunzi na kuwabeba abiria wengine
- Hata hivyo, baniani mbaya kiatu chake dawa. Kauli hii inamaanisha
- mtu ambaye huwa mbaya huwa mwema siku moja
- Usafiri ni mbaya lakini hutufanya watu wema
- Tunafaa kuenzi usafiri wa miguu tusipatwe na maafa
- Hata kitu kikiwa na madhara, kina umuhimu wake
- Kulingana na aya ya mwisho, mwandishi ana mtazamo upi?
- Jamii yote yafaa kuona madhara ya usafiri
- Tunafaa kuweka mikakati itakayotufaidi safarini
- Kusoma kutaimarika tukiimarisha usafiri wetu
- Wanafunzi wanafaa kujichagulia namna ya usafiri
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Andika insha yakusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.
Wewe ni kiranja mkuu shuleni. Andika hotuba utakayotoa katika siku ya michezo shuleni........................
MARKING SCHEME
- C
- B
- A
- B
- A
- D
- A
- D
- C
- C
- D
- C
- A
- A
- C
- B
- D
- B
- C
- C
- B
- D
- B
- A
- D
- A
- A
- D
- A
- B
- B
- C
- A
- A
- C
- B
- C
- B
- C
- B
- D
- B
- C
- C
- C
- A
- D
- B
- D
- C
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term 2 Exams 2023 Set 5.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students