Friday, 10 March 2023 13:52

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo, vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.   

Siku hiyo___1___Jumamosi niliamka nikiwa mzima kama ___2___. Mzazi wangu alikuwa ___3___ katika maonyesho ya kilimo. Tulipofika katika lango kuu, ilitubidi kulipa ___4___ baada ya kupanga ___5___ kwa muda wa nusu saa. ___6___  na wanyama wa kuvutia humo kwa mfano ___7___ farasi, twiga simba, chui na wengineo. Nilivutiwa pia na ___8___ mpya ya kilimo. Ulipowadia wakati wa ___9___ tulirudi nyumbani nikiwa na furaha ___10___.

   A   B   C   D 
 1.   za   la   wa   ya 
 2.  kigongo   kaburi   kinyonga   ibada 
 3.  atanipeleka   angenipeleka   akinipeleka   hunipeleka 
 4.  nauli  kiingilio  fola  karo
 5.  laini  nguo  vyombo  foleni
 6.  Mlikuwa  Palikuwa  Kulikuwa  Pangekuwa 
 7.  ; . : /
 8.  uinjinia  teknolojia  ufundi  maarifa
 9.  macheo  mawio  alfajiri  machweo
 10.  riboribo  kwikwikwi  tiki  pomoni

 

Ajali za barabarani ___11___ shida kubwa humu nchini. Idadi kubwa ya watu ___12___ maisha yao huku wengine wakijeruhiwa ___13___. Sababu kuu ni kuwa madereva wamekuwa ___14___ sana.  Tushirikiane ili kupunguza ajali nchini kwani ___15___.

   A   B   C   D 
 11.   limekuwa   zingekuwa   ilikuwa   zimekuwa 
 12.  haijapoteza   imepoteza   haipotezi   wamepoteza 
 13.  vizuri   vyema   vibaya   zaidi 
 14.  wapotovu  waaminifu   waangalifu   wema 
 15.  ajali haina kinga   jifya moja halinjiki chungu   haraka haraka haina baraka    jungu kuu halikosi ukoko.

 

Kutoka swali la 16 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Chagua sentensi iliyo katika hali timilifu
    1. Mvua ilinyesha tukapanda.
    2. Nchi ingelindwa ingestawi
    3. Mashindani yakikamilika tutaondoka
    4. Mgeni wetu hajawasili
  2. Andika akisami  6/7 kwa maneno
    1. Tusui sita
    2. Thumuni saba
    3. Subui sita
    4. Tusui saba
  3. Ni orodha ipi yenye vitenzi pekee?
    1. Cheza, imba, soma
    2. Mtiifu, zuri, karimu
    3. Polepole, vibaya, haraka
    4. Juu ya, katika, kwenye
  4. Chagua nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi nyamaa
    1. nyamazia
    2. unyamavu
    3. nyamaza
    4. nyamavu
  5. Ni mdudu yupi husababisha ugonjwa wa malale?
    1. Mbu
    2. Chawa
    3. Mbung'o
    4. Konokono
  6. Shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti huitwa
    1. Tarbia
    2. Takhmisa
    3. Tathnia
    4. Tathlitha
  7. Andika kwa wingi:
    Rafiki yangu amemkamata koo na jogoo.
    1. Rafiki zetu wamewakamata koo na jogoo
    2. Marafiki zetu wamewakama makoo na majogoo
    3. Rafiki wetu wamewakamata makoo na majogoo
    4. Marafiki zangu wamewakamata koo na jogoo
  8. Ni orodha ipi yenye vitate?
    1. Baba-papa
    2. Mvulana - barobaro
    3. Jenga - bomoa
    4. Panda - vua
  9. Ni methali ipi yenye maelezo kuwa vitendo vizuri hupongezwa na mtu husifiwa kwa matendo yake mema?
    1. Dua la kuku halimpati mwewe
    2. Haba na haba hujaza kibaba
    3. Chanda chema huvikwa pete
    4. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo
  10. Kanusha sentensi ifuatayo
    Mwalimu aliyefika ametufunza vyema
    1. Mwalimu asiyefika hakutufunza vyema
    2. Mwalimu hakufika wala hakutufunza vyema
    3. Mwalimu aliyefika hajatufunza vyema
    4. Mwalimu aliyefika hatatufunza vyema
  11. Msimu wa baridi nyingi bila ya mvua huitwa
    1. kiangazi
    2. masika
    3. vuli
    4. kipupwe
  12. Maneno, waraka, nyasi na uo huwa katika ngeli gani?
    1. U-ZI
    2. I-ZI
    3. U-YA
    4. I-I
  13. Mtu huyu ni kinyonga. Maneno haya yametumia fani ipi ya lugha?
    1. Tashbihi
    2. Istiara
    3. Msemo
    4. Nahau
  14. Tegua kitendawili
    Huku mwamba na kule mwamba.
    1. Giza
    2. Ardhi
    3. Jeneza
    4. Kaburi
  15. Karibu imetumikaje katika sentensi?
    Darasa letu lina karibu wanafunzi thelathini.
    1. Kuonyesha wakati
    2. Kuonyesha nusura
    3. Kuonyesha takribani
    4. Kuonyesha makaribisho

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Hapo zamani za kale, paliishi mzee mmoja aliyeitwa Maarifa. Maarifa alimwoa mke mmoja na kuweza kufanikiwa kupata mwana aliyeitwa pendo. Pendo alikuwa mtoto wa pekee katika aila hiyo. Mabonge ya nasaha aliyopewa na baba yake yaliangukia masikio yaliyotiwa nta.

Maarifa, mke wake na mtoto wao Pendo waliishi katika jamii iliyokuwa na ushirikiano kwa wema na mabaya. Jamii hii ilishi kwa kutegemea mifugo na kulima mashamba madogo madogo. Pendo alipoendelea kukua alijihisi ameerevuka kiasi cha kuwajaribu wakuu wake akili. Kweli aliyesema akili nyingi huondoa maarifa hakukosea.

Baadhi ya mafunzo aliyopewa na baba yake ni kuwa akienda kulisha kondoo apige ukemi pindi mbwa mwitu watokeapo na atapata usaidizi haraka sana. Siku moja Pendo alienda kulisha mifugo mbali kidogo na nyumbani. Alifikiri na akaona ni bora apige ukemi aone kutatokea nini.

"Uuuwi! Uuuwi! Uuuwi! Njooni haraka, mbwa mwitu wamevamia kondoo." Punde si punde wanaume wa miraba minne, mashunjaa wa kijiji walifika huku wamejihami kwa nyuta na mishale. Waliduwaa kuona Pendo akicheka huku akiwa na raha. Ni ibra iliyoje?

Wanaume walirejea nyumbani na kumweleza Maarifa kisa chote. Pendo alipowasili alioswa na kukemewa na wazazi wake. Mwana muwi haongeleki mara moja. Pendo alirudia tendo lake mara ya pili. Nao wanaume wakaja kama safari ya kwanza. Tukio hilo lilikuwa mchezo mbaya wa kuchezea watu wazima.

Siku ya tatu, Pendo alipokuwa akilisha mifugo, mbwa mwitu walitokeza ghafla. Alipiga mayowe lakini hakuona hata mtu mmoja aliyekuja kumsaidia. Watu walidhani ni mzaha ule wake wa kawaida. Maskini Pendo, mbwa mwitu waliwala kondoo wote na hatimaye kumjeruhi vibaya. Pendo alijuta kwa kutofuata mawaidha aliyopewa na wakuu wake.

  1. Ni nini maana ya maneno Pendo alikuwa mtoto wa pekee kulingana na habari?
    1. Pendo alikuwa na tabia tofauti na wenzake
    2. Pendo alizaliwa wa kwanza katika jamaa yake
    3. Pendo hakuwa na dada wala kaka
    4. Pendo alikuwa wa mwisho kuzaliwa kwao
  2. Mawaidha ambayo pendo alipewa na baba yake
    A hakuyasikiliza wala hakuyafuata
    B. aliyatilia maanani
    C. hakuyasikiliza bali aliyafuata
    D. aliyazingatia yote 
  3. Ala ya mzee Maarifa ilishi katika
    1. jamii iliyotangamana wakati wa furaha
    2. jamii iliyoishi kwa utengano
    3. jamii iliyoshirikiana wakati na dhiki pekee
    4. jamii iliyoshirikiana wakati wa heri na shari
  4. Tendo la Pendo kujihisi ameerevuka kiasi cha kuwajaribu wakuu wake linaonyesha
    1. ni kawaida watoto kufanya hivyo
    2. alikuwa mkaidi
    3. alikuwa mwerevu kuliko watoto wa rika lake
    4. alikuwa ameerevuka kuliko wavyele wake
  5. Baadhi ya mafunzo aliyopewa Pendo ni yapi?
    1. Akiwa malishoni apige mayowe akiwaona mbwa mwitu
    2. Akipiga mayowe wakati wowote akiwalisha kondoo
    3. Asithubutu kwenda malishoni peke yake
    4. Mbwamwitu wakitokea apambane nao
  6. Ni nini maana ya maneno wanaume wa miraba minne kulingana na habari?
    1. Wanaume jasiri na dhaifu
    2. Wanaume dhaifu na shujaa
    3. Wanaume wanene na wenye nguvu
    4. Wanaume wenye nguvu na woga
  7. Unadhani ni kwa nini wazazi walimkemea Pendo baada ya kupashwa habari?
    1. Alikuwa amefanya jambo la aula
    2. Alikuwa ameonyesha ushujaa 
    3. Kondoo wote waliliwa na mbwamwitu 
    4. Alikuwa ameonyesha utovu wa nidhamu
  8. Ni jambo lipi linaloonyesha kuwa wanakijiji walikuwa wamechoshwa na tabia za Pendo? 
    1. Kutoenda kumsaidia safari ya mwisho
    2. Kutomjulisha baba yake kuhusu tabia zake 
    3. Kumsaidia alipopiga ukemi mara ya pili
    4. Kutomfahamisha baba yake kuhusu kuvamiwa na mbwamwitu
  9. Mwana muwi haongeleki mara moja ina maana kuwa
    1. Mtoto mzuri hawezi kuharibika kwa kosa moja
    2. Mtoto mbaya haachi tabia zake mbovu
    3. Kumbebeleza mtoto si vyema.
    4. Mtoto mwenye nidhamu hafai kukanywa
  10. Kichwa mwafaka cha habari hii ni kipi?
    1. Maarifa na Pendo
    2. Kikulacho ki nguoni mwako.
    3. Majuto ni mjukuu
    4. Dawa ya moto ni moto

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Kilimo ndicho uti wa mgongo nchini Kenya. Ukulima huchangia pakubwa katika jumla ya pato la taifa. Asilimia sabini na tano ya Wakenya walio katika umri wa kufanya kazi ni wakulima ingawa nusu ya mzao haya hutumika kwa kukidhi mahitaji ya kimsingi.

Nchi ya Kenya ikiwa na chini ya asilimia ishirini ya ardhi inayofaa kwa ukulima ndiyo inayoongoza katika ukuzaji wa kitunguu na maembe kwa mataifa ya nje. Kwa ujumla, sekta ya kilimo inachangia takriban asilimia sitini na tano ya bidhaa za nchi zinazouzwa katika mataifa ya nje.

Hata hivyo ukulima wa nchi ya Kenya umekabiliwa na changamoto ainati. Ukosefu wa mvua hutatiza wakulima nchini. Hii ni kwa sababu kilimo nchini hutegemea mvua. Majira ya mvua yanaendelea kubadilika kwa kiasi cha kuyafanya yasitegemewe. Mvua inayonyesha haitoshi na mimea hukauka kabla ya kukomaa na kupata mazao. Iwapo wakulima wametayarisha mashamba na kupanda mbugu, huweza kupata hasara kubwa.

Wakulima wengi nchini hawatumii teknolojia ya kisasa ili kuboresha mapato yao. Hii ni kwa sababu utafiti hauhusishi wakulima ili kuboresha mapato yao. Wakulima wengi hivyo basi huendelea kutumia njia zilizopitwa na wakati katika uzalishaji wa mazao na hivyo kupata mapato yasiyoweza kukidhi haja ya mkulima na nchi kwa jumla.

Wadudu na magonjwa yanayoathiri mimea ni changamoto nyingine inyokabili wakulima. Wengi wao wamekosa elimu kuhusu jinsi ya kuzuia magonjwa na wadudu wanaoharibu mimea na mazao au mavuno yao. Wengi hawajui jinsi ya kuzuia wadudu wanaoyaharibu. Mahali wanamoweka mazao au mavuno yao hamfai na husababisha uharibifu unaoleta hasara kuu. Wataalamu wanaowatembelea wakulima ni wachache sana na hawafikii wakulima wengi. Jambo hili husababisha ukosefu wa ujuzi wa kutosha wa kuendeleza kilimo kwa njia za kisasa.

Wakulima wanaweza kuwa na ujuzi wa kuzuia magonjwa na wadudu wanaoharibu mimea na mazao au hata matumizi ya teknolojia ya kisasa lakini wakose fedha za kutekeleza mambo haya. Gharama ya mbegu, viuadudu na mbolea yaweza kuwa juu kwa mkulima wa kawaida.

Ukosefu wa miundomsingi mathalani barabara umesababisha usafirishaji wa mazao ya mkulima kuwa ghali. Hili hufanya mazao kuharibika mashambani na yakifika sokoni yanauzwa kwa bei duni kwa kuwa hali yake si nzuri. Hivyo basi wakulima wanaendelea kupata hasara zaidi. Serikali inafaa isaidie sekta ya kilimo kwa kuongeza wataalamu zaidi wanaotembea mashambani kuwaelekeza wakulima. Wakulima wapewe mikopo ya kukidhi mahitaji ya zaraa. Miundomsingi pia iboreshwe.

  1. Kilimo ndicho uti wa mgongo ina maana
    1. kimefanikiwa sana
    2. ni tegemeo kubwa
    3. wananchi wengi ni wakulima
    4. kina faida na hasara nchini
  2. Chagua jibu sahihi
    1. Asilimia sabini na tano ya Wakenya ni wakulima
    2. Takribani Wakenya wote hupenda kilimo
    3. Zaidi ya nusu ya mapato ya nchi ni ya wakulima
    4. Robo tatu ya wafanyakazi nchini ni ya wakulima
  3. Nchi ya Kenya inaongoza kwa
    1. asilimia kubwa ya ardhi ya kulima 
    2. uuzaji wa kahawa na chai kwa wenyeji 
    3. ukuzaji wa kahawa na majani chai 
    4. kilimo bora cha kitunguu na maembe
  4. Ni kweli kusema kwamba
    1. Kenya hutegemea tu mauzo ya bidhaa za kilimo
    2. Kenya hainunui bidhaa za kilimo maadamu ziko tele
    3. Bidhaa nyingi zinazouzwa nje ya nchi ni za kilimo
    4. Nchi yetu imeweza kujitosheleza kupitia kilimo
  5. Ipi si mojawapo ya changamoto zinazowakabili wakulima nchini?
    1. Mvua kunyesha kupita kiasi
    2. Ukosefu wa mvua ya kutosha
    3. Ukosefu wa soko la bidhaa
    4. Kupungua kwa thamani ya bidhaa
  6. Elimu humsaidia vipi mkulima
    1. kuimarisha mazao na kupunguza hasara
    2. kujifanyia utafiti na kupiga hesabu za pesa
    3. kutumia njia za kiasili na kuepuka hasara
    4. kufahamu manufaa ya kilimo na kuboresha miundomsingi
  7. Ni methali ipi inayolingana na ya sita?
    1. La kuvunda halina ubani
    2. Jitihada haiondoi kudura maelezo katika aya
    3. Kidole kimoja hakivunji chawa
    4. Dau la mnyonge haliendi joshi
  8. Miundomsingi inahitaji zaidi katika
    1. utoaji wa elimu
    2. uchukuzi wa bidhaa
    3. uimarishaji wa soko 
    4. uuzaji wa bidhaa
  9. Serikali inafaa kuwapa wakulima mkopo ya kukidhia mahitaji ya kilimo. Mkopo usiotozwa riba huitwaje?
    1. Arbuni
    2. Ridhaa 
    3. Karadha
    4. Fidia
  10. Kichwa kinachofaa zaidi kifungu hiki ni kipi?
    1. Umuhimu wa kilimo nchini
    2. Ukulima nchini na changamoto zake
    3. Namna ya kuinua uchumi nchini
    4. Faida za ukulima

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.

Endeleza insha hii

Ulikuwa ni usiku wa manane ambapo niliamshwa na mayowe.............................



MARKING SCHEME

  1. D
  2. A
  3. C
  4. B
  5. D
  6. A
  7. C
  8. B
  9. D
  10. A
  11. D
  12. B
  13. C
  14. A
  15. B
  16. D
  17. C
  18. A
  19. B
  20. C
  21. D
  22. B
  23. A
  24. C
  25. C
  26. D
  27. A
  28. B
  29. D
  30. C
  31. C
  32. A
  33. D
  34. B
  35. A
  36. C
  37. D
  38. A
  39. B
  40. C
  41. B
  42. D
  43. C
  44. C
  45. A
  46. A
  47. D
  48. B
  49. C
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students