Soma taarifa ifuatayo Kisha ujibu maswali 1 - 5
Mbu ni mnyama anyonyaye damu usiku tunapolala. Juzi, Maria alipokuwa amelala aliumwa na mbu. Aliamka ghafla na kuwasha taa. Mbu huyo aliruka na kutua kwenye ukuta. Alionekana amefura kwa damu aliyokuwa amefyonza.
Kwa upande mwingine wa ukuta kulikuwa na mbu mwengine. Mbu huyo hakuwa amenyonya damu. Alionekana mwembamba. Maria alipomwona mbu yule aliyekuwa ameshiba, alimpiga na kumwua. Mbu yule aliyekuwa na njaa aliruka na kujificha.
Maria alirudi kitandani na kulala tena. Mbu yule mwembamba alirudi kitandani na kumwuma Maria. Maria aliamka kwa mara ya pili na kuanza kumtafuta mbu huyu wa pili. Maria alikasirika sana kwa sababu usingizi wake uliharibika kwa mara ya pili. Kama Maria angemwua mbu aliyekuwa na njaa, asingeamka mara ya pili.
Maswali
- Chakula kikuu cha mbu ni
- damu
- maziwa
- kunyonya
- maji.
- Maria alipoumwa na mbu
- alijifunika vizuri
- aliamka na kuomba
- aliamka na kuwasha taa
- aliamka, akawasha taa kisha akamfukuza mbu huyo.
- Mbu husababisha ugonjwa gani?
- Tauni
- Malale
- Malaria
- Upele
- Ni kosa gani alilolifanya Maria?
- Kumwua mbu aliyekuwa na njaa.
- Kutomwua mbu mwenye njaa.
- Kutomwua mbu aliyeshiba.
- Kumwua mbu aliyeshiba.
- Ili kujikinga na mbu lazima tujifunike kwenye
- chandarua
- hewa
- blanketi
- leso
Soma kifungu kifuatacho Kisha ujibu maswali 6-11
Mwanamke mmoja alikuwa akisafiri katika gari la abiria wakati wa usiku. Kwa bahati mbaya hakuwa na pesa za kutosha za nauli. Kondakta alipofika kwa mwanamke huyo, alimwomba atoe nauli yake. Mwanamke yule akatoa pesa alizokuwa nazo, lakini kondakta akasema kuwa hazikutosha.
Mama yule alimwelezea bwana huyo kuwa hakuwa na pesa zaidi, akamwomba amsamehe. Bwana huyo alikataa kabisa na kusema kwamba mama huyo atoke katika gari. Wasafiri wengine waliona uchungu sana hata mmoja wao akajitolea kumlipia bibi yule nauli. Kondakta alisema kuwa hangekubali pesa za mtu mwingine yeyote kwani yule mama alikuwa na pesa, ila alitaka kufanya mzaha tu. Mama huyo alizidi kulia hata akatokwa na machozi. Mtu yule aliyejitolea kumlipia alisema hakuwa akifanya mzaha. Mama alitoka huku analia.
Aliposhuka gari tu akanaswa na kushambuliwa na simba. Kwa bahati, palitokea gari la polisi. Walilifukuza like gari la abiria mpaka wakalishika. Walipoulizwa kiini cha kisa hicho yule kondakta alitaka kukana, lakini abiria wote walisema kwamba mwanamke huyo alikuwa katika basi hilo. Hapo yule kondakta akashikwa na kupelekwa mahakamani. Akashtakiwa na kufungwa kwa miaka kumi pamoja na viboko ishirini.
Maswali
- Mwanamke alikuwa akisafiri wakati wa
- mchana
- asubuhi
- usiku
- jioni.
- Neno nauli linamaanisha
- pesa za kusafiria
- chakula cha jioni
- nguo za safarini
- wasafiri.
- Watu wanaosafiri katika gari huitwa
- abiria
- kondakta
- watalii
- makanga.
- Mwanamke alitolewa nje ya gari wapi?
- Kituoni
- Nyumbani
- Mtoni
- Njiani
- Kondakta alishikwa na kupelekwa
- mahakamani
- jela
- stanini
- gerezani
- Neno 'mzaha' limepigwa mstari. Linamaanisha?
- Kumchezea mtu.
- Kumtembelea mtu.
- Kumwibia mtu.
- Kuliwa.
Soma habari hii kisha ujibu maswali 12-15
Katika kijiji cha Waso aliishi Mzee mmoja aliyeitwa Mtoro. Mzee huyo alikuwa mwenye tabia nzuri, tena mpole sana. Alipendwa na majirani zake wote. Walikuwa wakimwendea ili wapate mawaidha juu ya mambo na hasa wakiwa na matatizo ya kinyumbani.
Mzee Mtoro alikuwa na mke mmoja na mtoto mmoja tu. Mtoto huyo alikuwa msichana aliyeitwa Mrembo. Alikuwa mrembo sana. Watu wa kijiji chake walimpenda mtoto huyo kama vile walivyompenda baba yake.
Familia hii ilikuwa ikiishi maisha ya raha, furaha na amani. Kwa bahati mbaya, siku moja mama yake Mrembo alishikwa na maradhi ya kipindupindu na baada ya kuugua kwa siku chache alifariki. Jambo hili lilihuzunisha sana baba yake Mrembo na wanakijiji wote kwa jumla.
Maswali
- Majirani walimwendea Mtoro ili
- wabarikiwe
- wamfurahishe
- wapewe mawaidha
- awapende.
- Mzee huyu alikuwa na wake wangapi?
- Mmoja
- Wawili
- Hakuwa ameoa
- Watatu.
- Bahati mbaya iliyoipata familia hii ni
- Mrembo kufa
- Mtoro kufa
- ajali ya barabarani
- mamaye Mrembo kufa
- Maana ya neno 'kufariki' ni
- kufa
- kuugua sana
- kulazwa
- kupata afueni.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 16-20, kwa kutumia jibu bora zaidi.
__16__ huu chifu alikuja kutuongoza __17__ sherehe ya kupanda miti. Mgeni huyo alipofika alikaribishwa na mwalimu mkuu na __18__ na wanafunzi. __19__ watoto __20__ nyimbo nzuri kisha mwalimu mkuu akamkaribisha mgeni kutoa hotuba fupi.
A | B | C | D | |
16. | Wiki | Juma | Mwaka | Siku |
17. | katika | kwa | na | mwa |
18. | kupiga | kushangaliwa | kukemewa | kupendwa |
19. | Baada ya | Baadae | Baadaye | Baadawe |
20. | walimwibia | waliiba | waliimbiana | walimwimbia |
Kutoka swali la 21-30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.
- Watu huagana vipi usiku?
A. Tuonane
B. Alamsiki
C. Habari
D.Ndoto mbaya - Jina kondoo' liko katika ngeli gani?
- A-WA
- KI-VI
- I-ZI
- LI-YA
- Kamilisha sentensi ifuatayo.
Ningekusaidia _________________________ sina uwezo.- wala
- kwa sababu
- lakini
- na
- Samaki huishi majini kama vile ng'ombe huishi katika
- kizimba
- kombe
- zizi
- mzinga.
- Sehemu ya mwili inayosaidia kupumua huitwa
- masikio
- ini
- moyo
- pua
- Andika sentensi ifuatayo kwa wingi.
Yeye hutumia kisu kikali.- Nyinyi hutumia kisu kikali.
- Wewe hutumia visu vikali.
- Wao hutumia visu vikali.
- Sisi hutumia visu vikali.
- Kamilisha methali ifuatayo.
Asiyesikia la mkuu- huvunjika mkono
- huvunjika guu
- huvunjika mkono
- ni mbaya.
- Nguo ya ndani inayosetiri uchi wa sehemu ya siri ni
- shimizi
- kizibao
- chupi
- kanzu.
- Tegua kitendawili kifuatacho.
Fatuma mchafu- Nzi
- Choo
- Mbwa
- Ufagio.
- Mtu asiyeweza kusikia huitwa
- bubu
- kiziwi
- kipofu
- kiwete.
KUANDIKA: INSHA
Andika insha kuhusu;
USAFI WA MAZINGIRA.
____________________________________________________________________________________________

Download Kiswahili Questions - Grade 4 Opener Exams Term 2 2023 Set 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students