Tuesday, 27 June 2023 12:08

Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3

Share via Whatsapp

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 1 hadi 5.

G4SwaMT2S32023Q1

Nyumba ni makao ya mwanadamu. Kuna aina nyingi za nyumba. Kuna nyumba zinazojengwa kuelekea juu, vibanda, msonge, mapango, hema, tembe, za mawe, za udongo, za zege na kadhalika. Sehemu za nyumba ni sakafu, kuta, milango, vizingiti, madirisha, dari na paa.

Katika nyumba kuna makabati, makochi na viti. Mekoni kuna majiko, majokofu, karo, chanja, susu, sahani, vijiko, mabakuli na vinginevyo. Anayejenga nyumba za kawaida huitwa mjenzi na anaye jenga nyumba aushi za mawe ni mwashi.

Mwanadamu hutumia nyumba kama pahali pa kuishi, kulala, kupumzika, kujificha, kula na kupikia. Wasomi hutumia nyumba kwa masomo. Watu wengine pia hutumia nyumba kwa biashara.

Maswali

  1. Makao ya wanadamu ni
    1. makochi
    2. sakafu
    3. nyumba
    4. msitu
  2. Nyumba zinazojengwa nyingine zikiwa juu ya nyingine huitwa
    1. vibanda
    2. ghorofa
    3. vizingiti
    4. hema 
  3. Ni aina ngapi za nyumba zilizotajwa kwenye kifungu?
    1. Tisa
    2. Saba
    3. Nane
    4. Sita.
  4. Sakafu iliyo juu ya nyumba huitwaje?
    1. Paa
    2. Dari.
    3. Kuta
    4. Gorofa.
  5. Anayejenga nyumba za mawe ni
    1. mjenzi
    2. mwokaji
    3. mjengaji
    4. mwashi.

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi 10.

Je, kwa nini mbuni ana shingo ndefu? Wajua kwa nini shingo hiyo haina manyoya? Zamani Mbuni na mamba waliishi pamoja. Walikuwa marafiki wakubwa. Waliishi kama ndugu lakini sidhani kama walipendana kwa dhati. Siku moja Mamba alihisi njaa. Alitafuta mizoga ya kula akakosa. Mbuni alikula mizizi ya miti na matunda ya porini. Yeye hakuwa na shida ya njaa,

Mamba alifikiri kitu ambacho angekula, akaona kuwa nyama ya karibu naye ni Mbuni. Akajifanya mgonjwa na kumwita Mbuni. Alimwambia kuwa jino lake lilikuwa linauma. Alimwomba aingize kichwa chake kwenye mdomo wake aone shida ya jino hilo.

Mbuni kwa kumhurumia Mamba akakubali. Alipoingiza kichwa mdomoni, Mamba alifunga kinywa ghafla. Mbuni alijivuta kwa nguvu sana hadi akatoka mdomoni mle. Ubaya ni kuwa, manyoya ya shingo yake yalibaki mdomoni mwa Mamba. Pia, shingo yake ilirefuka zaidi

Maswali

  1. Zamani, Mbuni na Mamba waliishi ______________________________
    1. majini
    2. pamoja
    3. kwa furaha
    4. nyumbani.
  2. Kwa kawaida chakula cha Mamba kilikuwa
    1. mbuni
    2. ndege
    3. mizizi
    4. mizoga.
  3. Mamba alipowaza sana alifanya nini?
    1. Alimla Mbuni.
    2. Aliingia majini.
    3. Alitamani kumla Mbuni.
    4. Alimkamata Mbuni.
  4. Kwa nini Mamba alijifanya kuumwa na jino? Alitaka
    1. kuling'oa jino
    2. kumnyoa Mbuni 
    3. kumla Mbuni
    4. kuumwa na jino.
  5. Mbuni alikubali kufanya nini?
    1. Kumtibu Mamba.
    2. kumla Mamba
    3. Kung'oa jino.
    4. Kukiingiza kichwa kinywani mwa Mamb

Soma hadithi hii kisha ujibu maswali 11-15.

G4SwaMT2S32023Q2
Kila asubuhi wakulima huenda kwenye makonde yao kulima. Baada ya siku nyingi wao hupanda mbegu. Mbegu zikiota hutokea miche. Miche hugeuka na kuwa mimea. Mimea hustawi kisha ikapaliliwa. Baada ya hayo, magugu yote hung'olewa. Mimea inazaa mazao. Mazao ya mimea yakikomaa huvunwa. Mavuno ya mimea hutumiwa kama chakula sana. Wengine huuza ili kupata pesa za kutumia nyumbani. Kazi ya ukulima ni nyingi na huchosha lakini ina faida sana! Kila kitu huanza mbali na hutengenezwa ili kiwe kizuri baadaye.

Maswali

  1. Wakulima huenda kulima kwenye ________________________________.
    1. ngumi
    2. mashamba
    3. mabonde
    4. makundi 
  2. Baada ya kulima shamba mkulima hufanya nini?
    1. Huvuna
    2. Hupalilia.
    3. Hupanda mbegu.
    4. Huuza. 
  3. Katika kupalilia, mkulima hutoa shambani magugu au ___________________________________.
    1. miche
    2. mbegu
    3. kwekwe
    4. mimea
  4. Wakulima hupalilia nini?
    1. Mazao
    2. Mimea
    3. Magugu.
    4. Mauzo.
  5. Wakati wa mavuno, wakulima huvuna
    1. mimea
    2. miche
    3. chakula
    4. mazao.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujaze pengo 16 - 20 kwa jibu lifaalo zaidi.

Unga ___16___ ngano hutengeneza vyakula ___17___ kama vile ,chapati na ___18___. Jana nilikula andazi moja ___19___ chai kikombe __20__
nikashiba.

   A   B   C   D 
 16.    ya   za   la   wa 
 17.  tamu   mamo   vitamu   matamu 
 18.  maandazi   wali   vibanzi   mtama 
 19.  na  kwa   ya   pamoja 
 20.  moja  mbili   mmoja   kimoja 

Jibu maswali kulingana na maagizo.

  1. Tegua kitendawili hiki.
    Ajenga ingawa hana mikono. 
    1. Kobe
    2. Ndege
    3. Konokono
    4. Kilema. 
  2. Kinyume cha kumeza ni _________________________
    1. kutapika
    2. kutoa
    3. kula
    4. kutema.
  3. Bainisha neno lililopigiwa mstari. Nilienda ila sikumpata.
    1. kihusishi
    2. kiunganishi
    3. kihisishi
    4. kitenzi.
  4. Ipi ni nomino katika ngeli ya A-WA?
    1. Kiti
    2. Kitabu
    3. Kidole
    4. Kipepeo.
  5. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Mwaka umeanza.
    1. Miaka zimeanza
    2. Mamiaka imeanza
    3. Miaka imeanza
    4. Mamiaka yameanza.
  6. Jaza pengo kwa neno la adabu linalofaa.
    ____________________________ Vicky, naomba kupita.
    1. Simile
    2. Samahani
    3. Tafadhali
    4. Songea.
  7. Sehemu ya kompyuta inayoonyesha picha au maandishi huitwa
    1. kitufe
    2. kipanya
    3. kiwambo
    4. mashine.
  8. Tambua kivumishi katika sentensi hii.
    Watoto wadogo walipata zawadi nyingi. 
    1. nyingi
    2. watoto
    3. zawadi
    4. pata
  9. Jaza pengo kwa usahihi.
    Nzi ___ meruka
    1. i
    2. u
    3. ki
    4. a
  10. Barua ya kindugu huwa na anwani moja ya
    1. rafiki
    2. mwandishi
    3. mwandikiwa
    4. msomi.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha ya maelezo kuhusu;

                                                                                     UMUHIMU WA MAJI.   

______________________________________________________________________________________________________

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. B
  5. D
  6. B
  7. D
  8. C
  9. C
  10. D
  11. B
  12. C
  13. C
  14. B
  15. D
  16. D
  17. C
  18. A
  19. B
  20. D
  21. B
  22. A
  23. B
  24. D
  25. C
  26. A
  27. C
  28. A
  29. D
  30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 4 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students