Thursday, 09 November 2023 12:11

Kiswahili Questions - Grade 6 KPSEA 2023 Exams

Share via Whatsapp

Swali la 1 hadi la 5

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

(Ni jioni. Leni na Kibo wamekutana mtoni. Ni msimu wa kiangazi.)

Leni: (Akitabasamu.) Bingwa, hujambo? Ha! Ha! Ha! Umejitwika mtungi kichwani kutafuta maji!
Kibo: (Akionyesha kukasirika.) Sijambo, lakini mimi si bingwa. Ubingwa gani na hata tone la maji sina?
Leni: Samahani kaka. Sikudhani unaweza kukosa maji. Ajabu! Matangi yako makubwa yamekauka?
Kibo: Bila shaka. Unavyoona kiangazi kimetuathiri sisi sote. Hali ya anga isipobadilika tutaangamia.
Leni: (Akionyesha kuhuzunika.) Ni kweli unavyosema mwenzangu. Lakini hiyo anga itabadilikaje ilhali miti inakatwa ovyo?
Kibo: Ipo haja ya sisi kushirikiana ili kutunza na kuhifadhi mazingira yetu. Kumbuka tusipoziba ufa...
Leni:  (Akikubaliana naye.) Tutajenga ukuta. Nasikitika hali hii ikiendelea tutakosa chakula. Wanyama na ndege nao watakosa makao.
Kibo:  Mwandani wangu, hakika utunzi wa mazingira ni wajibu wetu.
Leni:   Kweli kabisa. (Wanaagana na kuondoka)

  1. Leni alimwamkua Kibo, hujambo? Ni salamu gani nyingine ambayo Leni angetumia kumwamkua Kibo?
    1. Chewa?
    2. Masalkheri?
    3. Sabalkheri?
    4. Shikamoo?
  2. Leni alitumia lugha ya adabu alipokuwa akizungumza na Kibo. Chagua kauli aliyoitumia inayoonyesha adabu.
    1. Umejitwika mtungi kichwani kutafuta maji!
    2. Wanyama na ndege nao watakosa makao.
    3. Matangi yako makubwa yamekauka?
    4. Ni kweli unavyosema mwenzangu.
  3. Katika mazungumzo, msikilizaji anaweza kukamilisha kauli ya anayezungumza. Chagua kauli iliyotumiwa kukamilisha nyingine katika mazungumzo haya.
    1. Bila shaka.
    2. Tutajenga ukuta.
    3. Kweli kabisa.
    4. Samahani kaka.
  4. Leni alimweleza Kibo athari za kutotunza mazingira. Ungekuwa Kibo, ungetaja athari gani nyingine?
    1. Kiwango cha joto kuongezeka.
    2. Wanafunzi kuacha shule.
    3. Mahusiano baina ya watu yataharibika. 
    4. Vyombo vya usafiri wa umma vitapungua.
  5. Neno mwandani limetumika katika mazungumzo. Chagua neno lenye maana sawa na mwandani.
    1. Ndugu.
    2. Jirani.
    3. Sahibu.
    4. Mwenza.

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Ushuru ni malipo yanayotozwa na serikali kama ada ya kuingiza bidhaa ndani ya nchi au kuziuza nje ya nchi. Pia, ni ada inayotozwa raia kwa kuuza au kununua huduma mbalimbali. Nchi yetu hutegemea ushuru ambao wananchi hutozwa ili kuendesha shughuli zake.

Shirika lenye jukumu la kukusanya ushuru nchini Kenya ni Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru almaarufu KRA. Shirika hili limepewa mamlaka ya kikatiba kukusanya aina zote za ushuru: ushuru wa mapato, ushuru wa forodhani, ushuru kutokana na shughuli za kitalii na nyinginezo.

Serikali huandaa bajeti kila mwaka ili kuhakikisha matumizi yafaayo ya fedha. Bajeti huwa na makadirio ya mapato na mgao wa fedha kwa matumizi mbalimbali. Makadirio hayo husomwa bungeni na Waziri wa Hazina ya Kitaifa kisha kuidhinishwa.

Ni wajibu wa kila mwananchi kulipa ushuru ili taifa letu liweze kujitegemea. Tukifanya hivyo, tutaweza kupiga hatua kimaendeleo. Tutakuwa na miundomsingi bora, huduma nzuri za kimsingi kama vile afya na elimu na hata nafasi zaidi za ajira

  1. Kulingana na kifungu, maendeleo ya taifa hutegemea:\
    1. bidhaa zinazouzwa.
    2. bajeti ya taifa.
    3. huduma za kimsingi.
    4. ushuru unaotozwa.
  2. Kifungu kimeonyesha kuwa ni haki ya KRA kukusanya ushuru kwa sababu:
    1. bajeti huandaliwa kila mwaka.
    2. imepewa mamlaka kikatiba. 
    3. ni muhimu kuhakikisha matumizi yafaayo ya fedha.
    4. bidhaa nyingi huuzwa ndani na nje ya nchi.
  3. Miundomsingi ikiimarika:
    1. viwanda vya uzalishaji bidhaa vitaimarika.
    2. wakulima watapata mazao mengi. 
    3. idadi ya watu itaongezeka.
    4. uharibifu wa mazingira utapungua.
  4. Chagua maana ya neno kuidhinishwa kama lilivyotumiwa katika kifungu.
    1. kuwasilishwa.
    2. kuchunguzwa.
    3. kukubaliwa.
    4. kukamilika.

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Likizo iliyopita nilitumia muda wangu wa mapumziko kumsaidia mlezi wangu kuwatunza mifugo wetu. Jambo hilo lilimfurahisha sana mlezi wangu akanizawidi ndama wa kike. Nilimpa ndama wangu jina, Simati.

Nilijitolea kwa hali na mali kumtunza Simati. Anapendeza kwa rangi yake nyeupe na madoa meusi. Matarajio yangu ni kwamba siku za usoni atapata ndama wake. Wakati huo utakapofika, nitamkama maziwa.

Maziwa nitakayoyapata nitayagawa kwa matumizi ya nyumbani na mengine nitayauza kwa usaidizi wa mlezi wangu. Hela nitakazopata kutokana na mauzo ya maziwa hayo, nitaziweka kama akiba kwani akiba haiozi.

  1. Kulingana na kifungu, msimulizi alipewa zawadi kwa sababu:
    1. alifika nyumbani kwa likizo.
    2. alimsaidia mlezi wake.
    3. alimpa ndama jina Simati.
    4. alitamani kuuza maziwa.
  2. Chagua jibu linaloonyesha kuwa msimulizi anafahamu uwekezaji.
    1. Anatumia likizo yake vizuri.
    2. Anatarajia Simati atapata ndama.
    3. Anafurahisha sana mlezi wake.
    4. Anapanga kuuza maziwa ili apate pesa.
  3. Msimulizi alimsaidia mlezi wake kuwatunza mifugo wao. Kuwatunza ni:
    1. kuwalinda.
    2. kuwatayarisha.
    3. kuwapenda.
    4. kuwafurahisha.

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

Kesho ni Ijumaa. Itakuwa sikukuu ya Mashujaa nchini. Kutakuwa na sherehe ya kuadhimisha siku hiyo. Jena na Joana watakariri shairi kuhusu mashujaa. Tangu juzi, wamekuwa wakifanya mazoezi ili kujiandaa. Mtondogoo watarejea shuleni. Watawasimulia wenzao kuhusu matukio ya siku hiyo.

  1. Jena na Joana watarejea shuleni mtondogoo. Mtondogoo itakuwa siku gani?
    1. Jumamosi.
    2. Jumapili.
    3. Jumatatu.
    4. Jumanne.
  2. Chagua vitendo vinavyoonyesha kuwa Jena na Joana wanapenda nchi yao.
    1. Kuhudhuria sherehe, kukariri shairi. 
    2. Kurejea shuleni, kukariri shairi.
    3. Kusimulia matukio, kuhudhuria sherehe.
    4. Kusimulia matukio, kurejea shuleni.
  3. Maana ya kujiandaa kulingana na kifungu ni:
    1. kujitambulisha.
    2. kujitayarisha.
    3. kujinufaisha.
    4. kujiburudisha.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kuwa na afya yaani ____16____  bora ni jambo muhimu kwa binadamu. Mlezi wangu husema kuwa lishe bora na mazoezi ya viungo vya mwili ni njia ____17_____ ya kutupatia afya njema. Yeye huhakikisha kwamba ____18____ matunda, mboga, mihogo na maharagwe ____19____ wingi. Tukiwa
na afya njema, tutaweza kufanya kazi kwa bidii kama ____20____.

   A  B  C  D
 16.  uhai  nguvu   kimo   siha 
 17.  kuzuri  nzuri  mzuri  vizuri
 18.  tunakula  tungekula   tukila   tulikula 
 19.  ya  kwa  ni  vya
 20.  kiwavi  mchwa   tausi   njiwa 


Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

  1. Chagua umoja wa:
    "Majembe yatatumiwa kupalilia mipapai yao michanga".
    1. Jembe litatumiwa kupalilia mipapai yake michanga.
    2. Jembe litatumiwa kupalilia mipapai yake mchanga
    3. Jembe litatumiwa kupalilia mpapai wake mchanga.
    4. Jembe litatumiwa kupalilia mpapai wake michanga.
  2. Chagua jibu sahihi kujaza pengo.
    Jakaya amekuwa akiwasaidia ______________________ zamani.
    1. hadi
    2. kisha
    3. tena
    4. tangu 
  3. Ukitaka kwenda chooni utamwomba mwalimu ruhusa kwa kumwambia unataka kwenda ________________________.
    1. bafuni.
    2. majifichoni.
    3. msalani.
    4. chumbani
  4. Matu ni fundi wa nguo. Rinda la Anna limeshonwa na Matu. Kwa hivyo, Anna __________________________ rinda na Matu.
    1. wameshonewa
    2. wameshonesha
    3. ameshonewa
    4. ameshonesha
  5. Chagua jibu sahihi kujaza nafasi.
    Mlango _______________________ darasa ni safi.
    1. za
    2. ya
    3. wa
    4. la
  6. Mjomba wako alikuletea zawadi juzi. Ikiwa leo ni Jumamosi, mjomba wako alikuletea zawadi siku gani?
    1. Jumanne.
    2. Jumatano.
    3. Alhamisi.
    4. Ijumaa.
  7. Tamu ni kwa chungu ilhali mwepesi ni kwa:
    1. mzito.
    2. mkubwa.
    3. mnene.
    4. mpana.
  8. Chagua jibu linaloonyesha ukanusho wa sentensi ifuatayo:
    Munira amesoma kitabu hicho. A
    1. Munira hasomi kitabu hicho. 
    2. Munira hatasoma kitabu hicho. 
    3. Munira hakusoma kitabu hicho. 
    4. Munira hajasoma kitabu hicho.
  9. Mtu anapomhimiza mwenzake kufanya kazi, tunasema anamtia shime. Je, mtu anapomsaidia mwenzake katika jambo fulani huwa:
    1. anamfanyia hima.
    2. anampiga jeki. zamani.
    3. anachapa kazi.
    4. anatia fora
  10. Katana na Kombo hawapendi kushirikiana na wenzao kufanya shughuli za vikundi darasani.
    Chagua methali inayoweza kutumiwa kuwashauri kubadilisha tabia hii.
    1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    2. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako.
    3. Mchagua jembe si mkulima.
    4. Jifya moja haliinjiki chungu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions - Grade 6 KPSEA 2023 Exams.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students