Wednesday, 29 March 2023 12:41

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 3

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

(Mwasia anapiga gumzo na babu yake. Mazungumzo yanakuwa hivi)
Mwasia:   Shikamoo babu?
Babu:       Marahaba. Umeshindaje mjukuu wangu?
Mwasia:   Nimeshinda vyema. Nashukuru kwa kunijulia hali. Jana ulisema kwamba leo tutazungumzia suala fulani. Ikiwa unayo                     nafasi tunaweza kuzungumza badala ya kuyaweka mambo kiporo.
Babu:       Sawa, kaa kitako tuzungumze. Nilitaka uniambie ni nini kiini cha vijana wa siku hizi kukaidi mila zetu. Kwani                                     mmesahau kwamba mwacha mila ni mtumwa?
Mwasia:   Ni kweli kwamba baadhi ya vijana wameonyesha maasi hasa kwa kuiga utamaduni wa kigeni usiofaa. Inasikitisha                           kuwaona wengine wakivaa mavazi ya aibu, kutumia lugha ya kuudhi na kushiriki ndoa za jinsia moja.
Babu:      (Akatikisa kichwa kwa masikitiko). Haya ni baadhi ya mambo yanayotukera sisi wazee. Suala la mapenzi ya kiholela                       halionekani kama mwiko siku hizi.
Mwasia:   Vijana hawa wanafaa wajirekebishe. Hata hivyo kuna mila ambazo zinafaa kuachwa nyuma kwani haziongezi thamani                   katika maisha ya jamii.
Babu:       Zipi hizo?
Mwasia:   Mila kama kurithi wajane, ukeketaji, kafara ya damu ya binadamu na kuwanyima wasichana urithi zimepitwa na wakati.
Babu:      Sisi wazee tulijiendea tu kama gari lisilo na taa wala kidhibiti mwendo. Mnapaswa kutumia elimu yenu kubadili mkondo                  wa maisha katika jamii.
Mwasia:  Hayo ni kweli babu. Pia vijana lazima watumie akili vizuri wasiwe kama ng'ombe asiye na nadhari. (Wanaendeleza                           mazungumzo kwa muda kisha wanaagana)

  1. Maneno 'kuyaweka mambo kiporo' yana maana gani?
    1. Kupuuza mambo muhimu.
    2. Kushughulikia jambo mapema. 
    3. Kuacha jambo ili lishughulikiwe baadaye.
    4. Kula chakula kilicholala.
  2. Vijana wanapotoshwa na nini kulingana na mazungumzo haya?
    1. Kuiga utamaduni wa kigeni.
    2. Kufuata sana utamaduni wao.
    3. Teknolojia inayoonyesha mambo yasiyofaa.
    4. Kuandamana na wageni wabaya.
  3. Kwa nini watu wa zamani walizingatia mila ambazo hazikuwa na manufaa?
    1. Hawakufanya mambo kwa kufikiria.
    2. Vijana walikuwa watiifu.
    3. Hawakuwa na utamaduni wa kigeni.
    4. Hawakuwa na climu ifaayo ya kuwaongoza.
  4. Mila potovu zilizotajwa si pamoja na; .
    1. tohara ya wasichana.
    2. utiifu na unyenyekevu.
    3. kurithi wake.
    4. kuwatoa watu kafara.
  5. Baba analinganisha maisha ya kale na;
    1. gari bovu barabarani.
    2. gari la zamani.
    3. gari lisilo na taa.
    4. gari lisilo na dereva.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 - 9  

Kuku na mwewe walikuwa marafiki wa chanda na petc. Walijitahidi sana kuwalea na kuwaelekeza wana wao kwa njia iliyofaa. Yamkini, walimaizi kuwa mtoto umleavyo ndiyo akuavyo. Aghalabu mwewe aliamka mapema akaanza shughuli ya kusaka riziki. Zipo nyakati, japo kwa nadra sana, ambapo kuku alijitwika jukumu la kutafuta chakula. Chochote walichopata walitumia pamoja, jambo ambalo liliwavutia sana ndege wengine.

Wakati fulani, kiangazi kikali kilivamia enco lile ikawa kwamba mwewe akitoka angekawia hata kwa juma zima kabla ya kurudi na chakula. Wakati mwingine, hata hakuwaona watoto wake kwani alifika usiku na kuamkia kazi mapema. Hata hivyo, hakuwa na wahaka kwani alijua rafikiye kuku alimtunzia wana kama ndugu. Laiti angalijua! Jambo usilolijua ni usiku wa giza totoro.

Mwewe alipitisha majuma mawili bila kuwaona wanawe. Asubuhi moja, alijihisi mchovu akashindwa kufuata shughuli zake za kawaida. Kuku alidhani kuwamwenzake ameshaelekea mawindoni. Mwewe akiwa nje kwenye mti mmoja alimwona kuku akiwapa wanawe kiamshakinywa. Watoto wa mwewe waliodhoofika kupita kiasi waliambiwa kuwa hapakuwa na chakula chao.

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi Mwewe aliteremka kwa ghadhabu, akamshika mtoto mmoja wa kuku na kumrarua vipandevipande. Kuku alipoona hayo, aliwachukua wanawe waliosalia akatorokea kwa binadamu kuomba hifadhi. Usuhuba wao ulifikia kikomo papo hapo.

  1. Chagua maelezo sahihi kuhusu kuku na mwewe.
    1. Walikaa na kulala pamoja.
    2. Walitafuta chakula pamoja.
    3. Walizingatia malezi bora ya wanao.
    4. Walipendezwa na urafiki wa wenzao.
  2. Ni kweli kusema kwamba,
    1. haikuwa kawaida ya kuku kutafuta chakula.
    2. mwewe alibaki na watoto mara kwa mara.
    3. kuku aliwatunza watoto vizuri kuliko mwewe.
    4. jukumu la kutafuta chakula ni muhimu kuliko ulezi
  3. Kwa nini mwewe hakujua hali ya wanawe mapema?
    1. Kuku alimnyima nafasi ya kuwaona wanawe.
    2. Hakuweza kutangamana nao mara kwa mara.
    3. Hakuwajali watoto wake hata kidogo.
    4. Watoto walilelewa mbali na pale alipoishi.
  4. Urafiki wa kuku na mwewe ulivunjwa na nini hasa?
    1. Ukatili wa mwewe. mwewe.
    2. Uchochezi wa majirani.
    3. Tamaa ya watoto wa mwewe.
    4. Ubinafsi wa kuku na wanawe.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 - 12  

Nchi iliyo na misitu hunufaika kwa njia nyingi. Mbali na kuwa makao ya wanyama walio kivutio cha watalii, pia hutupa mvua ya kutosha. Kilimo huendeshwa msimu baada ya msimu hivyo kukabiliana na uhitaji wa chakula. Wakazi wanaweza kutumia miti iliyojikaukia kupata kuni au kuchomea makaa. Isitoshe, wanaweza kupata mbao za kujengea na kuundia samani almradi ukataji wa miti uandamane sambamba na upanzi wa mingine.

Uharibifu wa misitu huwaacha wenyeji wakisaga meno kwa masikitiko. Vyanzo vya maji hukauka. Vivuli vya kujikinga na jua huadimika kama kaburi la baniani. Upepo nao huvuma bila kizuizi, jambo ambalo hupelekea kung'olewa kwa mimea na mapaa ya majengo. Upepo uo huo huwa na mavumbi yanayowachafua watu na kuwasabibishia shida za macho. Sote hatuna budi kuitikia mwito wa serikali wa kuilinda misitu yetu.

  1. Manufaa ya misitu kulingana na kifungu hiki ni:
    1. Kuhifadhi mvua na kuzuia upepo.
    2. Kivutio cha watalii na kuni.
    3. Makao ya wanyama na mbao za ujenzi.
    4. Kuundia samani na dawa.
  2. Si kweli kuwa nchi yenye misitu;
    1. hukabiliwa na baa la njaa.
    2. hupunguza athari za upepo mkali.
    3. wakazi hupata mahali pa kujiburudisha.
    4. wenyeji hawasumbuliwi na mavumbi.
  3. Mwito wa mwandishi ni kuwa:
    1. Tukate miti ili tupande mingine. 
    2. Tutumie kuni na makaa ya msituni. 
    3. Tuepuke sehemu zilizo na misitu.
    4. Tuitikie mwito wa serikali.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 - 15  

Usalama ni uwepo wa amani, bila tishio wala hatari yoyote. Kila mmoja hupenda kukaa palipo na usalama. Mtoto akilelewa katika hali ya vurugu maisha yake huathirika vibaya. Yeye hukosa kujiamini na akiwa mbele ya watu hugeuka bubu. Ni rahisi kumtambua mtoto kama huyo akiwa shuleni. Mara nyingi hujitenga na shughuli wanazoshiriki wenzake hasa michezo, majadiliano na shughuli za vyama vya wanafunzi shuleni.

Ni muhimu kuelewa kuwa wakati mwingine, matendo ya mtu yanaweza kumsababishia utovu wa usalama. Mifano ni wale wanaojipalia makaa kwa kudandia magari yapitayo kwa kasi, kuchezea karibu na barabara au visima vya maji. Wengine huchezeana michezo inayowaweka katika hatari ya kujeruhiana.

Jukumu la kudumisha usalama halifai kuachiwa wazazi na walezi pekee. Lazima tujaliane maslahi popote tulipo. Ukihisi kwamba unakabiliwa na tishio la aina yoyote, mjulishe mzazi, mwalimu au mtu mzima unayemthamini.

  1. Usalama ni nini?
    1. Kupata utulivu palipo na hatari,
    2. Malezi mema katika hali ya vurugu.
    3. Taarifa zinazohusiana na mambo yasiyo ya hatari.
    4. Kuwepo hali ya utulivu mahali alipo mtu.
  2. Maana ya 'hugeuka bubu' ni kuwa
    1. hupoteza uwezo wa kuongea.
    2. huwa na mazoea ya kunyamaza.
    3. huongea kwa lugha ya ishara. 
    4. huzungumza kwa sauti ya chini.
  3. Jambo lipi si tishio kwa usalama wa mtoto? A
    1. Kuchezea pale yanapopitia magari.
    2. Michezo inayosababisha majeraha.
    3. Kucheza na wenzake mbali na kwao.
    4. Vitisho na ukatili katika malezi.

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 mpaka 20. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa jibu sahihi.

Kuna aina nyingi ___16___ ndege wa porini. Ndege mmojawapo ___17___ sana na watu ni ___18___. Hii ni kwa sababu ___19___ kuyaiga maneno ___20___ na watu

   A   B   C   D 
 16.   ya   wa   za   kwa 
 17.  anayejulikana   wanaojulikana   anaojulikana   wanajulikana 
 18.  njiwa  kasuku   heroe   ninga 
 19.  ameweza  angeweza   ataweza   anaweza 
 20.  yanayosema  anayosema   yanayosemwa   wanaosema 

 

Kuanzia nambari 21 mpaka 30,chagua jibu sahihi.  

  1. Ni jozi ipi ya maneno iliyo tofauti?
    1. baba - abu
    2. barua - waraka
    3. adui - hasimu
    4. furaha - huzuni
  2. Andika kauli ya kutendea ya sentensi.
    Baba alileta zawadi akampa mwanawe.
    1. Mwana aliletewa zawadi na babaye. 
    2. Baba alimletea mwanawe zawadi
    3. Zawadi ililetwa na baba kwa mwana.
    4. Baba alileta zawadi ya mwanawe
  3. Chagua sentensi iliyo sahihi.
    1. Darasani lililofagiliwa ni zuri.
    2. Darasani mlimofagiliwa ni pazuri. 
    3. Darasani mlimofagiliwa ni mzuri.
    4. Darasani palipofagiliwa ni kuzuri.
  4. __________________ ni ugonjwa wa kutabawali damu unaosababishwa na vidudu vya konokono.
    1. Kichocho
    2. Tauni
    3. Utapiamlo
    4. Waba
  5. Andika wingi wa:
    Jani hilo lilianguka karibu na ua wak
    1. oJani hizo zilianguka karibu na maua ya
    2. Majani hayo yalianguka karibu na nyua zako.
    3. Majani hayo yalianguka karibu na nyua zao.
    4. Majani hayo yalianguka karibu na maua yao.
  6. Ni sentensi ipi iliyo katika hali ya mazoea?
    1. Shawe alimsaidia mzee kuvuka barabara.
    2. Mjomba anaipalilia miche shambani.
    3. Kamau amempelekea bibi maziwa.
    4. Mimi hula matunda siku zote.
  7. Tashbihi gani inaonyesha sifa ya mchwa?
    1. Mlafi kama mchwa.
    2. Bidii mithili ya mchwa.
    3. Mkali kama mchwa.
    4. Mwaminifu kama mchwa.
  8. Chagua methali inayohimiza ushirikiano. 
    1. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
    2. Mtoto umlcavyo ndivyo akuavyo.
    3. Mwenye nguvu mpishe.
    4. Kikulacho ki nguoni mwako.
  9. Tambua maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo:
    Vijana waadilifu wametuzwa na mwalimu wao.
    1. kivumishi, nomino
    2. kivumishi, kitenzi
    3. nomino, kitenzi
    4. kivumishi, kiwakilishi
  10. Chagua sentensi iliyoaki fishwa ipasavyo.
    1. Mwaye, anaishi, wapi?
    2. Mtoto yule. ni mtiifu.
    3. Je? Unaenda wapi?
    4. Nilipomwona jana, alikuwa akitoka sokoni.

INSHA   

Andika insha ya maelezo kuhusu:

SIKU YA MICHEZO SHULENI  

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. C
  6. C
  7. A
  8. B
  9. D
  10. C
  11. A
  12. D
  13. D
  14. B
  15. C
  16. C
  17. A
  18. B
  19. D
  20. A
  21. D
  22. B
  23. C
  24. A
  25. C
  26. D
  27. B
  28. A
  29. A
  30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 1 Exams 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students