Wednesday, 05 July 2023 08:07

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaMT2S22023Q1

Hapo zamani za kale, katika ulimwengu wa wanyama, paliishi Swara na Mbweha Swara na Mbweha walipendana kama chanda na pete. Wawili hao walikuwa na familia zao. Kila mmoja alikuwa na nyumba yake, mke pamoja na watoto. Mbweha alikuwa na watoto sita naye Swara alikuwa na watoto watano. Marafiki hao walifanya mambo yao kwa ushirikiano mkubwa. Walifuga wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe, kondoo na ngamia. Wanyama hao waliwapa faida ya maziwa na wakati fulani kuwafanyia kazi.

Tofauti kubwa iliyokuwapo ni kuwa Swara alipenda shughuli za kilimo naye Mbweha alipenda sana ufugaji. Swara alipouza maziwa yake, alipanda miche kisha akaamua kuwekeza katika kilimobiashara. Alipanda mimea kama vile michungwa, mihindi, mitufaha na mingine. Alipovuna mazao ya mimea hiyo, alitoa gharama ya ukulima huo kisha akabaki na faida kubwa mno. Kwa kuwa kazi ilikuwa nyingi shambani, aliamua kuwapa wanyama wengine ajira. Kila alipovuna mazao yake, aliyauza na kuweka pesa alizozipata katika benki. Hiyo ilikuwa njia ya kuhakikisha kuwa pesa zake zisingeibwa na wahalifu. Uzalendo wa Swara ulijulikana sana alipolipa ushuru kutokana na mapato.

Kwa sasa, marafiki hao wawili ni matajiri wakubwa. Wakazi katika eneo hilo wanapenda sana kilimo, ufugaji na biashara. Vilevile, wao hulipa ushuru wa mapato mara kwa mara. Wamejifunza kwa Swara na Mbweha kuwa kulipa ushuru kuna manufaa makubwa katika nchi.

  1. Ukirejelea maisha ya Swara, ni jambo gani lililokuwa la mwisho kati ya mambo haya?
    1. kulipa ushuru
    2. kuuza mazao ya shambani
    3. kufuga wanyama
    4. kuanzisha kilimo
  2. Maneno 'walifanya mambo yao kwa ushirikiano mkubwa' yanaonyesha kuwa Swara na rafiki yake walizingatia methali gani?
    1. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    2. Majuto ni mjukuu huja baadaye.
    3. Mkono mmoja hauchinji ng'ombe.
    4. Panya wengi hawachimbi shimo.
  3. Ni kweli kuwa kama Swara asingekuwa na mifugo;
    1. angekosa wanyama wa kumfanyia kazi shambani.
    2. angekosa pesa za kuweka katika benki.
    3. angeshindwa kabisa kulipa ushuru.
    4. angeshindwa kuanzisha kilimo chake.
  4. Benki ilimpa Swara manufaa gani?
    1. Ilimpa mkopo alipokosa pesa.
    2. Ilimtunzia pesa zake.
    3. Ilimpa ushahuri kuhusu kilimo. 
    4. Ilimsaidia kuuza mazao yake.
  5. Marafiki wanaozungumziwa katika ufahamu huu walikuwa na jumla ya watoto wangapi?
    1. 6
    2. 11
    3. 5
    4. 4
  6. Swara alikuwa mzalendo kwa kuwa;
    1. aliipenda sana nchi yake.
    2. aliwapa wenzake ajira.
    3. alilipa ushuru kutokana na mapato.
    4. alikuwa rafiki wa Mbweha.
  7. Kifungu hiki kinaeleza umuhimu wa mambo yafuatayo isipokuwa;
    1. kilimo
    2. biashara
    3. ufugaji
    4. elimu
  8. Maneno 'Swara na Mbweha walipendana kama chanda na pete' ni mfano wa;
    1. tashbihi ya umbo
    2. tashbihi ya tabia 
    3. istiara ya umbo
    4. nahau ya upendo

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

G6SwaMT2S22023Q2

Kijiji cha Ingusi kinapatikana kati ya masoko manne. Soko la Butere hujulikana sana kwa ununuzi wa mifugo kama vile mbuzi, nguruwe, kondoo na mbuzi. Katika soko lilo hilo, kunapatikana nguo za watu wa kike na kiume, watoto kwa watu wazima. Wanaotaka kununua viungo vya upishi kama vile mafuta, vitunguu, nyanya na chumvi nao wanaweza kununua katika soko hilo. Upande mwingine, utapata soko la Mumias. Kwenye soko hilo, unaweza ukanunua mifugo mbalimbali. Aidha, unaweza ukununua jezi za timu mbalimbali
kama vile Gor Mahia, AFC Leopards, Manchester United, PSG na kadhalika. Vifaa mbalimbali vinavyotumika nyumbani kama vile sufuria, vikombe, mabeseni, vijiko na visu viliuzwa sokoni hapo. Nyanya, mafuta ya kupikia, vitunguu, mdalasini na bizari pia huweza kupatikana katika soko hilo.

Soko la Imanga nalo linapatikana karibu na kijiji cha Ingusi. Kwenye soko hilo la Imanga, wanunuzi hupata bidhaa nyingi zisizopatikana katika masoko hayo mengine. Kile kinachopatikana kwenye soko hilo na lile la Butere ni viungo vya kupikia. Soko la Ugunja linafahamika kwa bidhaa moja muhimu sana. Wakazi wa Ingusi huenda kwenye soko la Ugunja kwa sababu ya kununua samaki mbalimbali kama vile mkunga, kipepeo, pweza na kambare.

  1. Ni nini kinachopatikana katika masoko matatu?
    1. vifaa vya kupikia
    2. viungo vya kupikia
    3. jezi za kuchezea
    4. mavazi mbalimbali
  2. Waliotaka kununua mifugo wangetembelea masoko gani?
    1. Butere na Imanga
    2. Butere na Mumias
    3. Mumias na Imanga
    4. Ugunja na Butere
  3. Soko lipi linalojulikana kwa bidhaa za aina moja pekee?
    1. Mumias
    2. Butere
    3. Imanga
    4. Ugunja
  4. Kifungu kimetaja samaki wa aina ngapi?
    1. 4
    2. 3
    3. 5
    4. 6

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
(Kando ya barabara, Farida anakutana na Juma akiwa amebeba jembe.)

Farida: Hujambo Juma?
Juma : Sijambo Farida. Umeadimika sana. (Wanashikana mikono wakitabasamu.)
Farida: Si sana. Je, unatoka wapi na jembe?
Juma : Mimi pamoja na vijana wenzangu tumekuwa tukichanga bia shambani. Farida
Farida: Hewaa! Jambo zuri sana. Nami ninatoka katika shughuli za kufanya mazoezi. Tangu nilipokuwa na umri mdogo, nimekuwa                           nikifanya mazoezi mara kwa mara. Kesho nitahamia kule Marekani, nimechaguliwa kuwa mchezaji katika timu moja ya kandanda. 
Juma :  Hongera. Uamuzi huo ni wa busara mwenzangu. Ningependa nifike nyumbani ili nipumzike kiasi.
Farida: Buriani Juma.
Juma :  Buriani dawa. (Wanapigana pambaja kisha kila mmoja anaondoka.

  1. Ni kweli kuwa Farida;
    1. anapenda masomo.
    2. anapenda kilimo.
    3. anapenda afya yake.
    4. anapenda nchi yake.
  2. Nahau 'tukichanga bia' ina maana gani jinsi ilivyotumika katika mazungumzo?
    1. tukilima
    2. tukifanya bidii
    3. tukishirikiana
    4. tukizungumza
  3. Ni kweli kuwa Farida na Juma;
    1. wangeonana tena shule zikifungwa.
    2. hawakutarajia kuonana hivi karibuni.
    3. walisomea katika shule moja.
    4. walikuwa marafiki kwa muda mrefu.

Chagua jibu lifaalo ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Kenya ni nchi __16__ makabila mengi. Makabila haya yanapatikana nchini__17__. __18__ tuishi vizuri, tunafaa kuwa na amani na umoja kati __19__. Umoja huo utatuwezesha kupiga hatua za kimandeleo na __20__ uchumi wetu.

   A   B   C   D 
 16.   yenyewe   lenye   yenye   lenyewe 
 17.  mote  pote   yote   kote 
 18.  Ikiwa  Ila  Ili   Lakini 
 19.  yetu  yenu   yao   yangu 
 20.  kuijenga  kuujenga   kuyajenga   kumjenga 
  1. Chagua sentensi iliyo sahihi.
    1. Mgeni mwenye amewasili ni huyu.
    2. Hii kalamu ilinunuliwa jana.
    3. Mtoto mgani mwenye mikono safi?
    4. Walitupa kalamu nzuri tukafurahi. 
  2. Ishara gani kwenye tarakilishi ambayo huonyesha chapa koza?
    1. I
    2. B
    3. X
    4. U
  3. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
    Wewe una kalamu ambayo ni nzuri.
    1. kivumishi, kivumishi, kiwakilishi
    2. kiwakilishi, kivumishi, kivumishi
    3. kiwakilishi, kiwakilishi, kivumishi
    4. kivumishi, kielezi, kivumishi
  4. Kipande cha kwanza cha mshororo wa shairi huitwaje?
    1. ukwapi
    2. utao
    3. vina
    4. mizani
  5. Tambua umoja wa;
    Makazi yao yamezungushiwa nyua nzuri.
    1. Makazi yao yamezungushiwa ua mzuri.
    2. Makazi yake yamezungushiwa ua mzuri. 
    3. Kazi yake imezungushiwa ua mzuri.
    4. Makazi yake yamezungushiwa ua zuri.
  6. Kiungo cha mwili ambacho huhifadhi mkojo tumboni huitwa _______________________.
    1. figo
    2. pafu
    3. kibofu
    4. moyo
  7. Chagua ukubwa wa;
    Mzee huyo amebeba ndoo iliyokuwa chini ya mti.
    1. Jizee hilo limebeba jidoo lililokuwa chini ya jiti.
    2. Kizee hicho kimebeba kidoo lilichokuwa chini ya kijiti.
    3. Zee huyo limebeba doo lililokuwa chini ya jiti.
    4. Zee hilo limebeba doo lililokuwa chini ya jiti.
  8. Soma ni kwa 'somewa' kama vile nyoa ni kwa ___________________________.
    1. nyoewa
    2. nyoana
    3. nyolewa
    4. nyoleka
  9. Nomino gani inayopatikana katika ngeli ya U-U kati ya nomino zifuatazo?
    1. ubua
    2. ukuta
    3. unga
    4. mkono
  10. Alama gani ya kuakifisha ambayo hutumika kuanzishia orodha?
    1. koloni
    2. ritifaa
    3. hisi
    4. koma

INSHA   

Mwandikie mwalimu wako wa darasa barua ukimweleza sababu zilizofanya ukakosa kuja shuleni juma lililopita.

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. D
  4. B
  5. B
  6. C
  7. D
  8. B
  9. B
  10. B
  11. D
  12. A
  13. C
  14. C
  15. B
  16. C
  17. D
  18. C
  19. A
  20. B
  21. D
  22. B
  23. B
  24. A
  25. B
  26. C
  27. D
  28. C
  29. C
  30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Mid Term 2 Exam 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students