Friday, 10 March 2023 09:41

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

                         (Wazazi wanajadiliana na wana wao kuhusu namna na umuhimu wa kuwa na afya bora)
Baba:                Mke wangu, ni siku nyingi hatujazungumza na kina Tina kuhusu masuala ya kibinafsi. (Kimya kinapita) Hebu waite tuzungumze nao.
Mama:              Sawa mume wangu (anasimama dirishani akitazama nje) Tinaa!..... Ramaa!
Tina na Rama: Naam mama!
Mama:               Hebu njooni humu ndani upesi (Kwa mumewe) Watoto siku hizi wakipata fursa, hawakai. Ni wao na mchezo. (Watoto wanaingia                                    wakihema)
Baba:                Wanangu, tumewaita hapa ili tuzungumze kuhusu umuhimu wa kuwa na afya bora. Ketini. (Wanaketi)
Mama:               Kwanza, Tina na Rama, lazima mjue namna ya kudumisha afya bora.
Tina:                  Nadhani njia mojawapo ni kudumisha usafi, kula vyakula salama na kamili na kufanya mazoezi.
Baba:                 Vyema Tina. Tunapokuwa na afya bora, miili yetu haipatwi na magonjwa mara kwa mara.
Rama:               Tena akili zetu hufanya kazi vyema na kuboresha matokeo ya shughuli zetu zikiwemo za masomo.
Mama:               Si hayo tu, tunapokuwa na afya bora, sisi hupendeza na kuvutia maana miili yetu huwa na maumbo ya asili, si miili iliyokonda na                                    kuonyesha mifupa.
Baba:                 Ningependa kuwa kwanzia leo kila mmoja wetu aliakikishe ubora wa afya yake kwa kutenda haya na mengine yaliyo mema.
Tina na Rama:  Sawa baba.

  1. Baba alitaka kuzungumza na watoto wao kuhusu
    1. matokeo ya mtihani.
    2. michezo waliyokuwa wakicheza.
    3. masuala ya kibinafsi.
    4. vipindi walivyovipenda.
  2. Kabla hawajaitwa, Tina na Rama walikuwa wapi?
    1. Chumbani
    2. Nje wakicheza
    3. Wakipumzika nje
    4. Sebuleni
  3. Pendekezo la kula vyakula salama na kamili lilitolewa na
    1. Tina
    2. Rama
    3. mama
    4. baba
  4. Kulingana na baba, tunapokuwa na afya bora,
    1. matokeo ya shughuli zetu huwa mazuri.
    2. miili yetu huweza kupatwa na magonjwa.
    3. miili yetu huwa na maumbo asilia isiyokonda.
    4. hatupatwi na magonjwa mara kwa mara.
  5. Kulingana na mazungumzo haya,
    1. Rama na Tina hawapendi kucheza.
    2. hakuna haja ya kudumisha afya bora.
    3. wazazi waliotajwa wanawajali watoto wao.
    4. watu wa familia hiyo wanapenda sana kucheza.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 9.   

Amina alikuwa mwanafunzi wa Gredi ya tano katika shule ya Shaurimoyo. Mama yake alimwambia awe mwangalizi pale nyumbani alipokuwa sokoni. Amina alikuwa na kaka wawili na dada wawili. Ndugu zake Amina walikuwa watiifu.

Jumamosi moja, mama yao alienda sokoni kama kawaida. Alimwambia Amina awaelekeze ndugu zake kufanya shughuli za pale nyumbani. Amina aliwaambia dada zake waoshe vyombo na kusafisha nyumba. Kaka zake walitakiwa kuyanyunyizia maua maji na kuwashughulikia mbuzi wao. Baada ya shughuli hizo zote, watoto hao walikaa na kutulia huku wakimngoja mama yao atoke sokoni.Mama yao aliporudi, alifurahi sana kuona jinsi nyumba yao ilivyokuwa safi. Aliwapa wasichana maparachichi na wavulana miwa kwa kazi nzuri walizofanya. Wote walifurahi.

  1. Familia hii ina jumla ya watoto wangapi?
    1. Wanne
    2. Sits
    3. Watano
    4. Watalu
  2. Ikiwa kila msichana alipewa parachichi moja, mama alileta maparachichi mangapi?
    1. Matano
    2. Sita
    3. Manne
    4. Matatu
  3. Baada ya kumaliza kazi zote, watoto
    1. walikaa na kumngoja mama yao.
    2. walienda nje kucheza.
    3. waliwasha runinga na kutazama vibonzo.
    4. walifurahia maparachichi na miwa.
  4. Mama alipotoka sokoni alifurahishwa na 
    1. utulivu wa watoto wake.
    2. usafi wa nyumba yao.
    3. bidii ya watoto wake.
    4. ladha ya matunda aliyoleta.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.    

Moto! Moto! Hii ilikuwa sauti ya kutisha kwelikweli. Ingawa nilikuwa na usingizi kiasi, nilinyanyuka kutoka kitandani kuangalia ilipotoka sauti ile. Nilichungulia dirishani. Nje, kila mmoja alikuwa akikimbia huku na kule kujaribu kuuzima moto katika nyumba ya Bi. Faya.

"Siachwi nyuma!" Nilijiambia huku nikishuka vidato. Nilipofika, kila mmoja alikuwa mbioni kuokoa hali. Ghafla, nilichukua ndoo iliyokuwa na mchanga nikampa mzee Mapunda. Naye hakusita. Aliumwaga kwenye kitovu cha moto ule. Haikutosha, Mwang'ombe akaleta ndoo nyingine huku kipusi akimimina mapipa kadhaa ya maji motoni. Baada ya muda mfupi, moto wote ukawa umezima.

  1. Mwandishi aliposikia sauti ya kutisha, alikuwa wapi?
    1. Kitandani akilala.
    2. Chumbani akifanya usafi.
    3. Nje akizima moto.
    4. Sebuleni akitazama runinga.
  2. Mwandishi aliamua kuwa haachwi nyuma kwa kuwa alikuwa
    1. na usingizi kiasi
    2. na moyo wa kusaidia.
    3. na ndoo yenye mchanga.
    4. mwenye bidii kwelikweli.
  3. Wakati wa ajali hii ya moto, Bi Faya alikuwa wapi?
    1. Sokoni
    2. Dukani
    3. Chumbani
    4. Hatujaelezwa

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.  

Siku iliyofuata, mfalme simba alikuwa ameandaa mashindano yaliyotakiwa kuwahusisha wanyama wote. Hata hivyo, kunao wengine waliokuwa wameomba ruhusa kuwa wasingeshiriki. Jioni ya siku ya Ijumaa, mbweha alipita kote huku akipuliza firimbi ya kutangaza mashindano ya siku iliyofuata, mashindano ya kucheza muziki.

Wanyama waliotakiwa kushiriki walikuwa pundamilia, kinyonga na sungura. Watatu hawa walifika wakiwa wamejipodoa vilivyo. Pundamilia alikuwa amepakwa rangi nyeupe na nyeusi kwa namna ya mistari, sungura alikuwa amenyolewa mtindo wa shore na kuliacha shungi la nywele utosini huku kinyonga akiwa na mavazi mapya yaliyomkaa sawasawa.

Baada ya kila mmoja kuchukua nafasi yake na ngoma kuanza, mvua kubwa ilianza kunyesha. Kila mmoja alitimua mbio kumwacha maskini kinyonga akinyeshewa na nguo zake mpya!

  1. Mashindano haya yangefanyika siku ya
    1. Ijumaa
    2. Alhamisi
    3. Jumamosi
    4. Jumapili
  2. Wanyama wangapi walitarajiwa kushiriki katika mashindano haya?
    1. Watano
    2. Wawili
    3. Wanne
    4. Watatu
  3. Unadhani ni kwa nini kinyonga alibaki wenzake wakikimbia?
    1. Hawezi kuenda haraka.
    2. Alitaka kubaki pale.
    3. Alitaka anyeshewe.
    4. Alikataa kuwafuata mbio.

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.   

Siku hiyo tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu. Sote tulifika ___16___ tukiwa tayari kuabiri___17___kuelekea mjini Meremeta. Hii ilikuwa mara yangu ya ___18___ kuenda huko. Sikuwa nimewahi kuenda huko. Tuliingia ___19___ tukiwa na furaha sana. Mara dereva alitia gari ufunguo na safari
___20___.

   A   B   C   D 
 16.   asubuhi   shuleni   adhuhuri   usiku 
 17.  baiskeli  basi   ndege  meli 
 18.  moja  mwisho   tatu   kwanza 
 19.  njiani  safari   basini   barabarani 
 20.  ikaanza  ikaisha   ikaendelea   ukaanza 


Katika swali la 21-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.  

  1. Katika sentensi chura mnono aliteleza akazama, nomino ni
    1. mnono.
    2. chura.
    3. aliteleza.
    4. akazama.
  2. Chagua orodha ya vitenzi pekee. A
    1. Kiazi, bata, daftari.
    2. Chota, peleka, kataa. 
    3. Sana, zaidi, polepole.
    4. Chini ya, kando ya, mbele ya.
  3. Ni gani kati ya maneno haya ni kihisishi? 
    1. Lo!
    2. Katikati ya
    3. Mweupe
    4. Leo
  4. Kati ya orodha hizi, ni ipi ina mavazi, kike na kiume
    1. Kamisi, chupi, soksi.
    2. Koti, rinda, kofia
    3. Suti, soksi, tai
    4. Suruali, kaptura, sidiria
  5. Kamilisha methali:
    Mwana akibebwa 
    1. usilevyelevye miguu. 
    2. ndivyo akuavyo.
    3. kuzimu enda kiona.
    4. hutazama kisogo cha nina.
  6. Ni upi wingi wa sentensi ifuatayo?
    Mkoba wenyewe ni huu.
    1. Mikoba zenyewe ni hizi. 
    2. Mikoba yenyewe ni hii. 
    3. Mkoba zenyewe ni hizi. 
    4. Mkoba yenyewe ni hii.
  7. Ni rangi gani hapa haipo katika bendera ya taifa la Kenya?
    1. Nyeupe
    2. Nyeusi
    3. Manjano
    4. Kijani
  8. Nomino mayai inaweza kuorodheshwa katika ngeli gani?
    1. U-I
    2. KI-VI
    3. LI-LI
    4. LI-YA
  9. Kitenzi chapa katika kauli ya kutendea huwa
    1. chapia.
    2. chapwa.
    3. chapisha.
    4. chapiwa.
  10. Kamilisha tashbihi hii
    Bwana Murefu ni mfupi kama
    1. mlingoti.
    2. nyundo.
    3. kasuku.
    4. nguruwe.


MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. D
  5. C
  6. C
  7. D
  8. A
  9. B
  10. A
  11. B
  12. D
  13. C
  14. D
  15. A
  16. A
  17. B
  18. D
  19. C
  20. A
  21. B
  22. B
  23. A
  24. C
  25. D
  26. B
  27. C
  28. D
  29. A
  30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 1 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students