Maagizo ya mwanafunzi
- Karatasi hii ina mazoezi matano.
- Jibu maswali yote kulingana na maagizo uliyopewa.
Jedwali la Alama
Zoezi | Kusikiliza na kuzungumza | Kusoma kwa sauti | ufahamu wa kusoma | sarufi | kuandika |
Upeo | 5 | 10 | 5 | 25 | 10 |
Alama za mwanafunzi | |||||
Kiwango cha utendaji |
MASWALI
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu aulize maswali. Mwanafunzi ajibu kwa sauti.
- Bendera ya nchi yetu ina rangi ngapi?
Mwanafunzi ajibu. - Taja rangi moja inayopatikana kwenye bendera yetu.
Mwanafunzi ajibu - Taja siku ambazo bendera hupandishwa juu.
Mwanafunzi ajibu - Bendera inapopandishwa watu wanaimba wimbo upi?
Mwanafunzi ajibu - Taja majina ya raisi wa nchi ya Kenya.
Mwanafunzi ajibu
KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi ifiuatayo kwa sauti
Leo ni siku ya Jumapili. Tunajitayarisha kwenda kanisani na watu wa familia yangu. Nimevaa mavazi ya rangi ya samawati na shati jeupe. Nimevalia soksi za rangi nyeusi. Mama yangu anataka nivae viatu vyangu vipya. Baba ndiye alininulia viatu hivyo. Baba amevaa suruali ndefu na shati ambalo ni ya rangi sawa na yangu. Amejifunga tai shingoni. Mimi na baba tumevaa mavazi yanayofanana.
Mama amevaa rinda la rangi nyekundu. Yeye anapenda rangi nyekundu. Amevaa viatu vinavyomotamota. Anapendeza sana. Kila siku ya Jumapili sisi huhudhuria ibada kanisani. Huwa tunavaa mavazi yetu yanayopendeza.
UFAHAMU
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
Mimi ninaitwa paka. Mimi pakasipendi uchafuchafu hufanya umbo lisokote. Mimi hujifuta mikono kila mara. Sirambi kucha zangu ovyoovyo. Huwa nasafisha kucha zangu vizuri. Ninapenda usafi. Ninapotaka kujisaidia ninachimba shimo. Nikimaliza kujisaidia ninalifunika. Nina kazi nyingine muhimu sana kwa binadamu. Mimi hufukuza panya nyumbani. Panya huharibu nguo za binadamu na mahindi waliyovuna. Binadamu hunipatia maziwa kwa kazi yangu nzuri. Mimi hufurahia kazi hiyo.
Maswali
- Paka anapenda nini?
- Uchafu hufanya tumbo lifanye nini?
- Paka hufanya nini akitaka kwenda haja?
- Paka hufanyia nini kucha zake?
- Paka hapendi nini?
SARUFI
- Andika jibu sahihi.
Ni vizuri.........................kila siku. (kuoga, kucheza)
......................hutuzuia kupata magonjwa. (Usafi, Uchafu)
Watu hupangusa kamasi kwa..............................(taula, hancifu) - Chagua jibu sahihi kujaza mapengo.
[Mwili Kuoga mswaki Kukatwa]
Kila mtu anafaa kufanya usafi wa.....4.......Kila asubuhi ni vizuri ....5......Kupiga....6....huua wadudu kwenye meno. Kucha pia zinafaa ....7.....ili zibaki fupi kila wakati. - Jaza nafasi kuunda maneno ya heshima
P_I_
_s_nt
s_m_h_n_
t_f_dh_ - Andika sentensi ukitumia picha hizi
............................
............................ - Jaza mapengo kwa kuchagua jibu sahihi.
Salam aleikum..........................................(aleikum salaam, vizuri).
Shikamoo..........................................(salama, marahaba). - Kanusha vitendo hivi.
Keti..................................
Lia..................................
Inuka................................. - Andika maneno haya kwa herufi kubwa au ndogo.
mwalimu - .................................
DAKTARI - .................................
Andika sentensi tano kuhusu;
UMUHIMU WA MAJI
Majibu
UFAHAMU
- usafi
- lisokote
- ninachimba shimo
- safisha kucha zake vizuri
- uchafu
Sarufi
- kuoga
Usafi
hancifu - mwili
kuoga
mswaki
kukatwa - pole
asante
samahani
tafadhali - Mtoto alibeba mkoba.
Ufunguo ulianguka chini. - aleikum salaam
marahaba - simama
cheka
inama - MWALIMU
daktari
Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 3.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students