Maswali
- UFAHAMU (Alama 10)
- Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo. (alama 5)
Bj. Musa ana duka. Yeye huanza shughuli zake mapema ili wateja wake wampate dukani. Katika duka lake ameweka bei kwenye bidhaa na pia bidhaa zote zimepangwa kwenye rafu. Yeye hupima bidhaa zake kwa kutumia ratili. Bidhaa ambazo Bi. Musa huuza ni kama maziwa, mikate, mchele, sukari na chumvi. Bi. Musa huwakaribisha wateja wake vizuri.- Bi. Musa ana nini?
- Yeye huanza shughuli zake saa ngapi?
- Bidhaa zimepangwa wapi?
- Andika vitu viwili ambavyo Bi. Musa huuza. (alama 2)
- Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo. (Alama 5)
Bwana na Bi. Juma ni wakulima. Shambani mwao kuna mifugo na mimea ya aina tofauti. Bwana Juma hulima shamba lake kwa kutumia trekta. Wakati wa kupalilia wao hufanya kazi na watoto wao. Bwana Juma hutegemea shamba lake kwa mahitaji yake yote.- Bwana Juma hufanya kazi gani? (alama 1)
- Kwenye shamba lao kuna nini? (alama 2)
- Yeye hutumia nini kulima? (alama 1)
- Ni nani huwasaidia kupalilia? (alama 1)
- Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo. (alama 5)
- SARUFI (Alama 15)
- Tumia kimilikishi sahihi kujaza pengo. (alama 5)
langu, yake, wako, chake- Mkoba ............................. utaanguka.
- Baba ............................. alimpeleka shuleni.
- Jino ............................. linauma.
- Kalamu ............................. imepotea.
- Kikapu ............................. kimepotea.
- Tumia alama ya kiulizi (?) au kikomo (.) kukamilisha sentensi hizi. (alama 5)
- Unataka nani
- Nilimtembelea nyanya
- Leo ni Jumapili
- Unaenda wapi
- Unaitwa nani
- Kanusha sentensi hizi. (alama 5)
- Jana nilienda sokoni.
- Kesho nitafua nguo zangu.
- Leo ninamsaidia mama.
- Nilimtembelea babu shambani.
- Nitacheza na rafiki yangu.
- Tumia kimilikishi sahihi kujaza pengo. (alama 5)
- KUANDIKA (alama 10)
Andika insha kuhusu
"DARASA LANGU"
Maswali
Ufahamu
-
- duka
- mapema
- kwenye rafu
- maziwa
mikate
mchele
sukari
chumvi
-
- mkulima / hulima
- mifugo na mimea
- trekta
- watoto wa bwana na bi Juma.
Sarufi
-
- wako
- yake
- langu
- yake
- chake
-
- (?)
- (.)
- (.)
- (?)
- (?)
-
- Jana sikuenda sokoni.
- Kesho sitafua nguo zangu.
- Leo simsaidi mama.
- Sikumtembelea babu shambani.
- Sitacheza na rafiki yangu.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Download Shughuli za Kiswahili Ufahamu, Sarufi na Kuandika - CBC Grade 3 End of Term 3 Exam SET 2 2022.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students