0 votes
808 views
in Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine by
"...dunia imenikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza fimbo yake aushi yangu yote."

Eleza jinsi dunia ilimcharaza fimbo msemaji kwa kutolea hoja kumi na nne.

1 Answer

0 votes
by
  1.  Mamake Mashaka kufariki punde tu baada ya kumkopoa.
  2. Babake pia anafariki punde tu baada ya mamake.
  3. Kuambulia mama mlezi maskini.
  4. Kuanza kufanya kazi za kijungu jiko kujikimu yeye na mama mlezi.
  5. Licha ya bidii yao mara kwa mara walikosa ikamlazimu Kidebe kutumia akiba yake.
  6. Kufiwa na mama mlezi.
  7. Kufungishwa ndoa ya mkeka na Mzee Rubeya.
  8. Kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa sababu ya umasikini wake.
  9. Kuishi katika mtaa duni.
  10. Chumba chake ni duni - kinavuja paa inyeshapo.
  11. Alikosa samani chumbani – hana meza,viti,kitanda wala godoro.
  12. Kazi ya usiku.
  13. Mshahara duni .
  14. Kukopoa pacha mara tatu.
  15. Kulazimika kuomba nafasi ya malazi ya wana kwa jirani.
  16. Mazingira yenye harufu mbaya ya chooni.
  17. Mke na wana kumkimbia.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...