Login
Remember
Register
EasyElimu Questions and Answers
Questions
Unanswered
Tags
Users
Ask a Question
Ask a Question
Mwalimu Mstaafu- (Dumu Kayanda) “Hiari na mukhitari ni juu yako. Lakini yeye kafika nyumbani”. Eleza mambo makuu ambayo mwandishi anayaibua kabla na baada ya kutolewa kwa usemi huu.
0
votes
733
views
asked
Jul 6, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anony mous
Mwalimu Mstaafu- (Dumu Kayanda)
“Hiari na mukhitari ni juu yako. Lakini yeye kafika nyumbani”. Eleza mambo makuu ambayo mwandishi anayaibua kabla na baada ya kutolewa kwa usemi huu.
Ndoto ya Mashaka- (Ali Abdulla Ali)
Anwani "Ndoto ya Mashaka” inaakisi barabara yaliyomo kwenye hadithi. Fafanua.
hadithi fupi
tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
mwalimu mstaafu
ndoto ya mashaka
Please
log in
or
register
to answer this question.
1
Answer
0
votes
answered
Jul 6, 2021
by
anony mous
Utu- Jamii ya Mwalimu Mstaafu kumzawadi Mwalimu Mosi alimiminiwa sifa na waliohutubu kwenye sherehe ya kumuaga.
Ubaguzi-Wanyonge hawakupewa nafasi ya kuhutubu kwenye sherehe ya kumuaga Mwalimu Mosi. Aidha hawakutengewa mahali maalum pa kukaa kama wastaarabu walioketi kwenye hema.
Utabaka- Kuna watu matajiri katika jamii hii. Kwa mfano, wanafunzi wa zamani wa Mwalimu Mosi wanaendesha magari ya kifahari. Kuna watu maskini walitamauka kama vile Jairo anayeingia jukwaani na mavazi yaliyochanikachanika (uk.121)
Unafiki. Kati ya wale waliotoa hotuba kumhusu Mwalimu Mosi, wote walimsifia sana. Walimuona kama mtu kamilifu asiye na taksiri (uk. 126) walimuona kama Mungu.
Ufisadi- Rais alipokuja kuchangisha pesa kwenye shule ya upili ya Wangwani, pesa hizo zililiwa na wakora. (uk. 122)
Anasa- Jairo hunywa pombe na kulewa sana. Hata anatembea bila viatu kutokana na ulevi wake.
Ubabedume/taasubi ya kiume- Mwanamke kufuata amri ya mumewe bila ya kukaidi- mkewe Jairo anakubali kutolewa kwake na kukabidhiwa Mwalimu Mosi kama zawadi pasi na kupinga. Anasema, “Ni amri ya mume. Ndivyo nilivyolelewa na kufundishwa. Sharti nimutii mume wangu.” (uk. 127) Baadaye
Ushirikiano - Mkewe Jairo kujumuika pamoja na Bi. Sera katika kazi zote shambani na hata nyumbani. Walikuwa na mlahaka mwema.
Utu - Mwalimu Mosi analazimika kuikimu familia ya Jairo. Kwa mfano, kuwaelimisha wanawe.
Umbeya - Watu kumwambia Jairo kuwa Mwalimu mosi alitorokea mjini na bintiye Sabina ili kumfanya mkewe (uk, 128-129). Hizi zilikuwa ni tuhuma tu kwa sababu Mwalimu Mosi alimpeleka kwenye shule ya bweni naye akarejea nyumbani anakoendelea kuuguzwa.
Ukatili- Jairo kwenda kwa Mwalimu Mosi akiwa na nia ya kumuua kwa kumtorosha bintiye na kumfanya mkewe. (uk. 129-130)
Ukosefu wa lishe- makuzi ya Mashaka yalikuwa ya tikiti maji na tango ya kuponea umande (uk. 70)
Mashaka kuachwa yatima baada ya mamake kufa muda mfupi baada ya yeye kuzaliwa. Vilevile, babake aliaga dunia baadaye kidogo. Ililazimu Mashaka kuielewa na Biti Kidege- mwanamke mzee, maskini na tena mgonjwa.
Kushiriki katika ajira katika umri mdogo- Mashaka alifanya kazi za kibarua ili kujikimu binafsi pamoja na mlezi wake Biti Kidege.
Mashaka kusoma kwa taabu hadi akamaliza chumba cha nane. Punde tu baada ya kukamilisha masoma yake ya msingi, mamake mlezi akaaga dunia.
Mashaka kufungishwa ndoa ya lazima na Mzee Rubeya kwa kusubuhiana na bintiye Waridi. (uk. 74) Mzee Rubeya alifanya hivi ili kujiondolea aibu na baada ya hapo akamahia Yemeni. Hii ilikuwa ni ndoa ya kimaskini kwa sababu ilikosa harusi.
Kuishi katika makazi duni- baada ya kuoana na Waridi, waliendelea kuishi kwenye chumba kile kile kibovu- paa lilikuwa ni la madebe na lilivuja wakati wa mvua.
Kuishi kwenye mazingira ya uchafu- pale kwao hapakuwa na vyoo, mifereji ya maji taka ilitema uchafu wake kwenye mito na uvundo ulikirihi. Mambo yalikuwa mabaya zaidi wakati wa mafuriko. (uk. 75)
Kuzaa idadi kubwa ya watoto- (watoto saba)- nafasi ya kuwahifadhi haikutosha. Binti zao walibanana na mama yao kwenye chumba hicho usiku na wavulana walilala jikoni mwa Chakupewa kama nyau.
Mashaka kufanya kazi duni – alikuwa mlinzi wa usiku. Aidha hakuwa na nafsi ya kutosha kushiriki kikamilifu malezi ya watoto wao.
Mshahara duni- Mashaka anasema mshahara ulikuwa ni mkia wa mbuzi (uk. 76) Haungemwezesha kununua vitu vingi.
Waridi kumtoroka Mashaka- Aliondoka pasi na kuaga. Mashaka anaporejea kutoka kazini, anawakosa nyumbani na hata baada ya kuwatafuta anaambulia patupu. (uk 76)
Mashaka kutamauka- Hata baada ya kuachwa na mkewe, alikuwa na matumaini kuwa mambo yangekuwa mazuri. Anasubiri hadi anakata tamaa.(uk. 79)
Please
log in
or
register
to add a comment.
Related questions
0
votes
1
answer
Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza
asked
Jul 23, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anonymous
tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
hadithi fupi
fasihi andishi
ndoto ya mashaka
0
votes
1
answer
Kwa kurejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Nizikeni Papa Hapa , Mtihani wa Maisha na Mkubwa, eleza changamoto zinazowakumba vijana. (al.20)
asked
Jul 2, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anonymous
tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
hadithi fupi
fasihi
0
votes
1
answer
"...dunia imenikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza fimbo yake aushi yangu yote."
asked
Jul 2, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anonymous
fasihi
hadithi fupi
ndoto ya mashaka
0
votes
1
answer
"...dunia imenikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza fimbo yake aushi yangu yote."
asked
Jul 2, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anonymous
hadithi fupi
fasihi
ndoto ya mashaka
0
votes
1
answer
“Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
asked
Jul 23, 2021
in
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
by
anonymous
tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine
hadithi fupi
shibe inatumaliza
fasihi andishi
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.
Categories
All categories
Mathematics
(632)
English
(287)
Kiswahili
(559)
Sarufi na Matumizi ya Lugha
(260)
Chozi la Heri
(83)
Kigogo
(60)
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
(43)
Fasihi
(67)
Ushairi
(3)
Isimu Jamii
(33)
Insha
(10)
Chemistry
(663)
Physics
(604)
Biology
(659)
Geography
(537)
History
(568)
CRE
(365)
IRE
(53)
Agriculture
(519)
Business Studies
(379)
Computer Studies
(20)
Home Science
(60)
General Questions
(432)
6.4k
questions
9.6k
answers
6
comments
590
users
...