0 votes
4.3k views
in Fasihi by
Eleza kwa hoja tano udhaifu wa hojaji kama njia ya kukusanya Fasihi Simulizi.

1 Answer

0 votes
by
  1.  Huenda watu wakakosa kujaza hojaji kwa kikamilifu kutokana na hofu ya kulaumiwa au kukataa tu.
  2. Maswali yenye utata husababisha fasiri mbalimbali ambazo hufanya matokeo yasitegemeke.
  3. Sifa za uwasilishaji kama vile toni havipatikani kwani mtafiti hapatani ana kwa ana na mhojiwa.
  4. Huenda walio na habri muhimu hawajui kusoma na kuandika. Husaidiwa na huenda wasaidizi wasiandike kila kitu.
  5. Hojaji zinaweza kuchelewa kufikia wahojiwa na basi ujumbe usiopatikane kwa wakati ufaao.
  6. Huenda wahojiwa wasiandike ukweli na mtafiti hawezi kuthibitisha kwa urahisi iwapo habari ni za ukweli.
  7. Huenda wahojiwa wakakataa kujaza hojaji ikiwa ndefu.
  8. Uchanganuzi huchukua muda mrefu hasa hojaji wazi.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...