0 votes
11.5k views
in Fasihi by
Ni mambo gani ambayo huchangia kubadilika kwa kazi za fasihi simulizi?

1 Answer

0 votes
by
  1. Hadhira- fanani kulazimika kubadilisha mtindo wa uwasilishaji ili kukidhi mahitaji ya hadhira yake.
  2. Fanani- kila fanani ana mtindo wake tofauti wa uwasilishaji. Kwa mfano matumizi ya mbinu ya ufaraguzi miongoni mwa fanani mbalimbali.
  3. Teknolojia- mambo ya zamani kubadilika kutokana na athari za teknolojia ya kisasa hasa taknohama.
  4. Wakati- kadri wakati unavyoendelea kupita, ndivyo mambo mengi katika maisha ya jamii huweza kubadilika. Mambo hayo huweza kuleta athari ya mabadiliko katika sanaa ya jamii.
  5. Mazingira- kuhama kwa watu katika eneo fulani kunaweza kuwanyima mahali mahususi pa kuwasilishia kazi fulani. Kwa mfano miviga.
  6. Video- kazi za kisanaa zilizorekodiwa hutofautiana na zile za kuwasilishwa moja kwa moja kutokana na kuathiriwa kwa sauti na picha wakati wa kurekodi.
  7. Uhamaji na uhamiaji- kuingiliana kwa tamaduni mbalimbali kunaweza kuathiri jinsi kazi fulani ilivyokuwa tangu mwanzo iwapo kutakuwa na kukopa baadhi ya vipengele vya sanaa ya jamii moja na kuvijumuisha na vya jamii nyingine.
  8. Maandalizi- fasihi simulizi inapohifadhiwa kwa maandishi huwa si ya mdomo tena bali ni ya kusomwa.
  9. Ukengeushi wa jamii- watu wanaacha utamaduni wao na hivyo baadi ya vipera vya fasihi simulizi huweza kutoweka au vikawa vinajitokeza kwa nadra sana, Kwa ujumla sanaa husika huathirika kutoka na hili. Utafiti- watu kujijazia kile wasichokijua bila ya kwenda nyanjani ilipo jamii husika ili kupata taarifa kamili.

Related questions

Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...