0 votes
2.6k views
in Fasihi by
Kwa kutumia vipengele vitano, onyesha maingiliano yaliyopo baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi.

1 Answer

0 votes
by
  1. Maudhui- fasihi andishi hujenga maudhui yake kutokana na yale ya fasihi simulizi.
  2. Utendaji- kazi za fasihi simulizi zina utendaji. Tamthilia kama kazi ya fasihi andishi ina utendaji pia.
  3. Lugha- fasihi simulizi na fasihi andishi hutumia lugha kama nyenzo kuu yakupitisha mafunzo yake.
  4. Usimulizi- usimulizi hutumiwa katika fasihi simulizi kuelezea na kusimulia visa. Fasihi andishi huwasilisha ujumbe wake kwa njia ya masimulizi.
  5. Dhamira- kazi za fasihi simulizi huwa na dhamira mahususi kama vile kuelimisha, kuadilisha, kuendeleza utamaduni n.k. Fasihi andishi kwa upande wake huwa na dhamira zizo hizo.
  6. Fani- mbinu kuu za kuwasilisha maudhui (ploti, wahusika, lugha n.k.) huweza kubainika wazi katika fasihi simulizi sawa na ilivyo katika kazi za fasihi andishi.
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...