Login
Remember
Register
EasyElimu Questions and Answers
Questions
Unanswered
Tags
Users
Ask a Question
Ask a Question
“Haidhuru kuwa huenda wimbo huu unawaghasi waliolala. Atakalo mwimbaji huyu ni kutakasa hisia zake.” Bainisha jinsi mrejelewa alivyotakasa hisia zake kwenye wimbo wake kwa mifano mwafaka.
0
votes
860
views
asked
Jul 6, 2021
in
Chozi la Heri
by
anony mous
“Haidhuru kuwa huenda wimbo huu unawaghasi waliolala. Atakalo mwimbaji huyu ni kutakasa hisia zake.” Bainisha jinsi mrejelewa alivyotakasa hisia zake kwenye wimbo wake kwa mifano mwafaka.
chozi la heri
riwaya
kuandika
Please
log in
or
register
to answer this question.
1
Answer
0
votes
answered
Jul 6, 2021
by
anony mous
Ulevi kumpa utulivu uliosababishwa na kuwepo kwa shinikizo kutoka kwa wenye uwezo- Majabali (uk. 129) ulevi kwake ni suluhisho la kuyakimbia matatizo.
Kubaguliwa na mahasidi wenye uwezo/tabaka la juu kumbagua.
Kuchekwa na matajiri wakiwa kwenye roshani za nyumba zao. Walikuwa wamekula na kushiba (uk. 130) Wanamkejeli kwa kumuita Bwana Dengelua.
Watu wanamkejeli tu pasi na kutaka kujua ni nini kilichosababisha uraibu wake wa pombe.
Kutwaliwa kwa shamba lao la asili na Bwana Mabavu ambaye anahalalisha wizi huo kwa hatimiliki bandia. Wao walishindwa kumpinga (uk. 131)
Ananwonea babake huruma kwa kumenyeka kwa kazi za sulubu ili apate riziki na karo.
Yeye alifanya bidii chuoni ili kuivua aila yake kutoka kwenye umaskini. Alipohitimu alikosa kazi.
Nafasi za kazi zilitolewa kwa mapendeleo ya kinasaba. (uk. 133)
Kazi aliyoipata ni duni – ya kufutia mchozi na mshahara wake ulikuwa mdogo. (uk. 133)
Wanapodai nyongeza ya mshahara, mwajiri wao anawarejelea kama 'unskilled labourers' hivyo waridhike na mshahara duni waupatao.
Walipoandamana kuomba wafikiriwe kama wataalamu wengine kazini na kutaka wapandishwe cheo, walifukuzwa walikokaa mabandani na kufutwa kazi.
Babake Shamsi kufanya kazi ya sulubu hata katika umri wake mpevu bila kuonewa imani na mwajiri wake. (uk. 131)
Babake 'anaaga dunia kwa njaa - alilazimika kula vijasumu vilivyomuua.
Mfumo duni wa afya- hamna hospitali pale kijijini. Babake alikosa matibabu ya dharura hivyo kuaga dunia.
Wanaomcheka kutokana na ulemavu wa mali, bila shaka hata nao yatawafika.
Chakula kinapatikana kwa taabu. Shamsi ana matumaini kuwa Bi. Halua ameambulia kibaba cha unga kutokana na ujira mdogo.(uk.135)
Kuna watu wanaomsifu kwa kuwa wa kwanza kuhitimu masomoni na hivyo kuwa mwanga wa jamii- hilo halikutimia.
Ndoto zake za ujana zimezimwa na watu waliomzidishia umaskini. (uk. 137)
Anabahatika hakupofuka wala kufa kutokana na unywaji wa pombe haramu kama wenzake.
Wagema kuitia pombe haramu vijasumu ili iive haraka- matokeo yake ni upofu na vifo. Shamsi anawalaumu kwa hilo.
Please
log in
or
register
to add a comment.
Related questions
0
votes
1
answer
"Mara moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili yake kusimama wima. Anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang'anyiro kikali cha upiganaji masumbwi. Kwa mbali anasikia mbisho hafifu ... Anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu ... Mara anasikia moyo wake ukimwambia, "Yako ya arobaini imefika," ...
asked
Jun 21, 2021
in
Chozi la Heri
by
anony mous
riwaya
kuandika
chozi la heri
0
votes
1
answer
“Dada Umu, Di, ni mimi, Ni ndugu yenu. Ni hai . Auntie Sauna alishikwa na polisi.” Weka dondoo hili katika muktadha wake.
asked
Aug 17, 2021
in
Chozi la Heri
by
anony mous
chozi la heri
riwaya
0
votes
0
answers
"salama,salama Rohoni,rohoni Ni salama,rohoni mwangu" (a)Eleza kinyume kinachojitokeza katika wimbo huu ukirejelea riwaya ya chozi
asked
Jan 22, 2023
in
Chozi la Heri
by
0797039XXX
chozi la heri
0
votes
1
answer
Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri
asked
Jul 23, 2021
in
Chozi la Heri
by
anonymous
chozi la heri
riwaya
0
votes
1
answer
Jadili kwa hoja nane suala la ukoloni mambo leo lilivyoshugulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri
asked
Jul 2, 2021
in
Chozi la Heri
by
anonymous
riwaya
fasihi
chozi la heri
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.
Categories
All categories
Mathematics
(632)
English
(287)
Kiswahili
(559)
Sarufi na Matumizi ya Lugha
(260)
Chozi la Heri
(83)
Kigogo
(60)
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
(43)
Fasihi
(67)
Ushairi
(3)
Isimu Jamii
(33)
Insha
(10)
Chemistry
(663)
Physics
(604)
Biology
(659)
Geography
(537)
History
(568)
CRE
(365)
IRE
(53)
Agriculture
(519)
Business Studies
(379)
Computer Studies
(20)
Home Science
(60)
General Questions
(432)
6.4k
questions
9.6k
answers
6
comments
590
users
...