0 votes
1.4k views
in Fasihi by

Umepewa jukumu la kutafiti kuhusu michezo ya watoto katika jamii yako.

  1. Taja eneo ambalo utafanyia utafiti wako. 
  2. Fafanua mbinu ambazo utatumia kukusanyia data huku ukionyesha sababu za uteuzi wako.

2 Answers

0 votes
by
  1. Taja eneo ambalo utafanyia utafiti wako.
    • Mandhari ambapo pana watoto wachanga wanaocheza. 
  2. Fafanua mbinu ambazo utatumia kukusanyia data huku ukionyesha sababu za uteuzi wako. 
    • Kusikiliza-mtafiti anaweza kuwasikiliza Watoto wanapocheza na kusimulia visa vyao.
    • Mtafiti atapata ujumbe asilia na halisi kwa sababu Watoto hawatatia chuku michezo yao
    • Kushiriki-mtafiti anaweza kujiunga na Watoto katika michezo yao na kujirekodia anachokibaini katika ushirika huo.
    • mtafiti huja karibu na Watoto na kupata habari za kuaminika moja kwa moja.
    • Kurekodi-mtafiti anaweza kutumia vinasasauti, kanda za video, filamu au upigaji picha.
    • mtafiti hupata habari za kutegemewa na anaweza kuzirejelea baadaye/kumbukumbu
    • Uchunzaji/kutazama-mtafiti anashuhudia kwa macho michezo ya Watoto inapoendelezwa.
    • mbinu hii ni bora kwani utendaji hautaadhiriwa kwani wachezaji/washiriki hawatajua kuwa wanatazamwa.
    • Kutumia Hojaji-mtafiti anaweza kutayarisha hojaji ambayo ataipelekea mhojiwa ambaye anapaswa kuijaza.
    • mbinu hii ni bora kwani mtafiti anaweza kuwafikia watoaji wengi wa habari kwa wakati mmoja.
    • Mahojiano-mtafiti anaweza kukabiliana ana kwa ana na waahusika anaonuia kupata maarifa kutoka kwao.
    • mbinu hii inamwezesha mtafiti kupata ufafanuzi wa papo kwa hapo
0 votes
by
Mohojiano baina ya kachero na mshukiwa

Related questions

0 votes
1 answer
Welcome to EasyElimu Questions and Answers, where you can ask questions and receive answers from other members of the community.

6.4k questions

9.6k answers

6 comments

590 users

...