MASWALI
Soma taarifa ifuatayo huku ukijaza pengo kwa neno lifaalo zaidi kati ya yale manne uliyopewa
Takriban _1_ imetupasa kufanya kazi. Tunafanya kazi ili tujimudu maishani. Kazi_2_uti wa_3_wa maisha_4_binadamu. Iwapo binadamu yeyote anataka kuishi maisha_5_ni sharti ajikaze_6_kazini. Ikiwa mitume watukufu walifanya kazi_7_ sisi ambao daraja_8_ni ndogo mbele ya Mwenyezi Mungu. Kazi humpa mtu_9_na vilevile kumwezesha kuikidhi_10_yake. Isitoshe, ataweza kuishi raha mustarehe.
-
- zote
- sote
- wote
- nyote
-
- ndio
- ndilo
- ndicho
- ndiyo
-
- mgongo
- moyo
- roho
- mkono
-
- wa
- la
- ya
- cha
-
- njema
- mema
- jema
- vyema
-
- sauni
- kizabuni
- kisabuni
- kwa sabuni
-
- Ingawa
- Sembuze
- Licha ya
- Seuze
-
- letu
- chetu
- yetu
- wetu
-
- taadhimu
- taadhima
- tathmini
- thamini
-
- jamii
- jama
- jamani
- jamaa
Rehema alifurahi sana kukutana na nyanya yake. Pindi tu akamwamkua "_11__"Naye Nyanyake akaitikia" _12_ mjukuu wangu."Hapo wakaanza kupiga _13_ kuhusu mambo kadha wa_14_ Kulipokuchwa, wakaagana" _15_ ".
-
- Hujambo
- Sijambo
- Habari
- Shikamoo
-
- nzuri
- vyema
- marahaba
- salama
-
- gumzo
- kasia
- mbinja
- stori
-
- kadhaa
- kadha
- kadhia
- kadhalika
-
- sabalheri
- masalheri
- macheo
- alamsiki
Kutoka swali la 16-30 chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo
- Kamilisha sentensi kwa tanakali zifaazo.
Yusufu alitumbukia majini ............... na kuzama .................- tumbwi, zii
- tumbwi, jii
- chubwi, zii
- chubwi, jii
- Tumia 'amba' kwa usahihi katika sentensi ifuatayo.
"Tafadhali nionyeshe mfereji .............................. nyinyi huteka maji ya kunywa."- ambapo
- ambao
- ambayo
- ambamo
- Kamilisha: Penye miti
- pana wajenzi.
- kuna misitu.
- hapana wajenzi
- hakuna watu.
- Chagua jibu sahihi.
- mmoja mmoja.
- moja moja.
- mmoja kwa mmoja
- kimoja kimoja
- Kamau alisema angesafiri ndege.
- na
- kwenye
- penye
- kwa
- Kifungu kimoja cha shairi huitwa
- mshororo.
- ubeti.
- kibwagizo.
- mizani.
- Msichana yule ana nywele........................... na pua ............................
- mrefu, dogo
- refu/dogo
- ndefu/ndogo
- ndevu/ndogo
- Kutokana na kitenzi KUFA, tunapata nomino
- mfu.
- maiti.
- mkufa.
- mfua.
- . Kamilisha:
Unataka nyumba yako ijengwe- vipi
- yupi
- ipi
- upi
- Akisami inaitwaje?
- Thumuni tatu
- Humusi tatu
- Tusui tatu.
- Subui tatu.
- Kikembe cha simba ni sibli, je kikembe cha nguruwe ni
- kisui.
- kiyoyo.
- kinda.
- kivinimbi.
- Neno unyasi liko katika ngeli gani?
- U-ZI
- U-U
- I-ZI
- A-WA
- Soma, kula, tembea, cheza ni
- nomino.
- vielezi.
- ngeli.
- vitenzi.
- Kanusha sentensi hii
Johana ameandika kisha akalala.- Johana hakuandika na hakulala.
- Johana hajaandika wala kulala.
- Johana haandiki na halali.
- Johana hataandika wala hata lala.
- Andika kwa wingi.
Ulezi mwema umenisaidia.- Malezi mema yamemsaidia.
- Ulezi mema yametusaidia.
- Malezi mema yametusaidia.
- Malezi mema yamenisaidia.
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 31-40
Fatuma aliachwa na mamake akiwa mchanga. Alipofikia umri wa miaka kumi naye babake mpendwa pia aliaga dunia. Kifo cha babake kilimtia sana simanzi.
Fatuma alibaki yatima na hakuwa na budi kuishi na ami yake Maina. Kwa kuwa lisilokuwa na budi hutendwa, Fatuma aliishi na Maina bila wasiwasi. Maisha ya Fatuma yalikuwa mazuri hadi Maina alipochukua jiko. Hapa acha ale mwata kwa huyo mkazaami wake!
Babake Fatuma alipoaga dunia aliacha mali ya kutosha lakini hayakumfaidi mwanawe wa kipekee. Kidosho aliyeolewa aliukatiza upendo baina ya mtu na mpwa wake. Mwanamke huyo alikuwa nduli mkubwa aliyemletea Fatuma madhila makubwa. Kwa hakika kidosho alileta mfarakano katika ukoo huo. Fauka ya hayo Fatuma alijikaza kisabuni na kuendelea kuishi hapo.
Bi. Kidosho alikazana kwa fitina bila kuchoka, kwani kinolewacho hupata."Naye Maina alisalimu amri kwa ua lake la moyo. Kwa ghafla, Maina alimgeuka mpwa wake mithili ya hewa inavyobadilika. Acha Fatuma aone cha mtema kuni. Jambo la kwanza alikatizwa masomo na kuwekwa nyumbani. Alitumwa kama kijakazi. Ungepata fursa ya kumwona ungemwonea huruma. Nguo alizokuwa akivaa zilikuwa nyeusi kama chungu, na uso wake ungedhani ni ule wa kipaka jiko.
Ni kweli kuwa mja akifunga wake wa Maulana u wazi. Haukupita muda mrefu kabla ya habari ya mateso ya Fatuma kusambaa kama moto wa nyasi. Bila ya tatizo lolote habari ilimfikia afisa msimamizi wa watoto katika sehemu hiyo. Fedheha kubwa ilimpata Maina kwani alishtakiwa kwa kumnyima Fatuma haki zake. Alionekana kuwa amevunja kufungu cha sheria ya watoto. Bila ya kusita hakimu alimhukumu Maina kifungu cha miaka sita au faini ya shilingi laki saba. Pia aliamrishwa arudishe urithi wa Fatuma. Fatuma aliambiwa arudi shuleni aendelee na masomo yake.
- Fatuma aliishi na
- mjomba wake.
- kakake baba.
- kakake mama.
- dadake mama.
- Ni kweli kusema kuwa
- mamake Fatuma alimwachia mali nyingi.
- kidosho alileta mapenzi katika jamii hiyo.
- kifo cha babake Fatuma hakikumletea upweke.
- Kidosho ndiye aliyekuwa chanzo cha masaibu ya Fatuma.
- Kulingana na habari mama yake Fatuma alikuwa
- ameaga.
- ameenda safari.
- mzima.
- akifanya kazi mbali.
- Mwanamke ni kwa kijakazi kama vile mwamume ni kwa
- topasi.
- mjakazi.
- kitwana.
- mzegazega.
- "ale mwata” katika habari ina maana ya
- kuona ujasiri.
- kupata nafuu.
- kupata ujasiri.
- kupata taabu.
- Nimethali gani inayowiana na habari hii?
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Mola hamtupi mja wake.
- Usitupe mbachao kwa mswala upitao.
- Ukipanda pankwisha utavuna pantosha.
- Kilichomwokoa Fatuma kilikuwa ni
- kufanya kazi kwa bidii.
- askari waliopiga nduru.
- kuenea kwa habari zake za mateso.
- kuacha shule na kukaa nyumbani.
- Maina aliaibika wakati
- aliposhtakiwa.
- alipofungwa jela.
- alipoamriwa kurudisha urithi.
- alimwoa kidosho.
- Maina alitozwa faini ya shilingi?
- 7000
- 70,000
- 700,000
- 7.000.000
- Kichwa mwafaka kwa hadithi hii ni
- Mnyonge hana haki.
- Meskia hachoki.
- Tupuuze haki za watoto.
- Ajira ya watoto.
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali 41-50
Rehema alikuwa mtoto wa tatu katika familia ya Mzee Kazamoyo. Alikuwa mziwanda kwa kuzaliwa na mama penda raha. Nduguze walikuwa Yusufu na Yohana
Hawa walikuwa wavulana watanashati sana. Rehema alikuwa banati mmoja tu miongoni mwa ghulamu wawili. Mzee aliwalea vizuri sana wanawe, kwa heshima na adabu, kwa utu na ubinadamu. Wavulana walikuwa wacheshi kama vinyago. Naye binti alikuwa malaika. Kwa upole na wema, Rehema alikuwa nambari moja. Watu wengi walimpenda na kumheshimu sana. Kweli heshima si utumwa. Lakini Mzee Kazamoyo alikuwa simba.
Mzee Kazamoyo alikuwa mwindaji haramu kwa jina jingine,jangili. Aliwaua wanyama pori kisha akauza nyama kwa wenye hoteli na vilabu vya starehe vya mjini. Kitendo hiki cha kuwaua wanyama, hakikumpendeza Rehema.
“Wanyama lazima walindwe badala ya kuwaua" alisema kimoyomoyo. “Mbona baba anaharibu maliasili? alizidi kuuliza. "Watalii wakija kwetu watawaona wanyama gani? Msichana alisikitika zaidi.
Kusema kweli wanyama wakiwindwa kiholela na kuuwawa ovyo ovyo, hatutakuwa na wanyama pori siku zijazo. Tunapohifadhi mazingira, tunawahifadhi wanyama pia. Siku moja Mzee Kazamoyo alimshika kasuku kwa mtego akaja naye nyumbani. Alitengeneza tundu akamtia kasuku huyo ndani. Tundu lenyewe akalitundika kwenye dari upenuni.
Rehema alikuwa akimwangalia babake kwa makini sana tangu alipokuwa na kasuku mpaka kumfungia kwenye tundu. Hakumwona baba akimpa ndege yule punje ya mchele au mtama.
- Katika aya ya pili Mzee Kazamoyo aliwalea wanawe kwa njia ifuatayo isipokuwa?
- Kwa taadhima.
- Kwa ukatili.
- Kwa utu na ubinadamu.
- Kwa adabu.
- Kulingana na habari uliyoisoma Mzee
Kazamoyo alikuwa akifanya kazi gani?- Alikuwa akifanya kazi ofisini.
- Alikuwa akiuza ndege aina ya kawaida.
- Alikuwa mkulima hodari.
- Alikuwa mwindaji wa wanyama pori.
- Ni kweli kusema kuwa
- Mzee Kazamoyo alikuwa kitinda mimba kwa kuzaliwa.
- Mzee Kazamoyo alikuwa mzalendo halisi ya nchi yake.
- Rehema alikuwa mchapakazi shuleni.
- Rehema ndiye aliyekuwa mtoto wa kwanza katika familia hiyo.
- Neno wanyamapori kama ilivyotumika katika makala haya unaweza pia kuitwa !
- binadamu.
- vimelea.
- hayawani.
- nyuni.
- Kinyume cha utumwa ni
- uwazi.
- undugu.
- ufungwa. .
- uhuru.
- Mwandishi ametaja Mzee Kazamoyo kuwa simba maanake?
- Alikuwa mfalme katika kijiji hicho.
- Alikuwa mkali kwa hivyo aliogopwa kwake.
- Ni mzee aliyependa simba.
- Aliwinda simba sana.
- Kati ya orodha ifuatayo ni gani ndege pekee?
- Chiriku, kasuku, mbayuwayu, njiwa.
- Kasuku, korongo, mjomba, kuku.
- Kasuku, nzige, tandu, mbuni.
- Sibli, njiwa, kaka, korongo.
- Kulingana na taarifa ni nini hakikumfurahisha Rehema?
- Maisha yake mwenyewe.
- Hatujaambiwa.
- Kitendo cha babake.
- Kitendo chake baadaye.
- Baada ya Mzee Kazamoyo kumnasa ndege aliweka wapi?
- Alihifadhi kwenye ghala.
- Aliweka juu ya nyumba yake huku akaingiza kwenye paa.
- Alimtengengezea nyumba mzuri nje ya nyumba.
- Alimwua na kuuza kwa wenye hoteli.
- Kichwa mwafaka cha taarifa hii ni
- Wanyamapori.
- Kisa cha simba.
- Mwindaji hodari wa ndege.
- Mzee Kaza moyo na familia yake.
Marking Scheme
Insha
Andika insha ya kuvutia kuendeleza maneno uliyopewa.
Tulisikia kelele kwenye barabara iliyopo karibu na shule yetu. Sote tukatoka madarasani mwetu na ........................................
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 6 End of Term 2 2021 Exams Set 2 with Marking Schemes.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students