Monday, 01 November 2021 11:31

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 Exam 2021 Set 2

Share via Whatsapp

INSHA

Andika Insha ya kusisimua itakayoanzia hivi

Asubuhi moja nilipokuwa nikielekea shuleni, nilimsikia mtoto akilia katika vichaka vilivyokuwa kando ya barabara ......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

LUGHA

Chagua jibu mwafaka kwa yale uliyopewa ujaze nafasi zilioachwa

Ni jambo la ____1____ kuona kuwa waja wengi____2____ usafi wa mazingira, Utembeapo kila mahali 3 mijini____4____ utaona watu wakiangushaangusha takataka bila___5___zozote zile. Mate na vikohozi ___6___ovyoovyo nusura wawachafue wenzao.____7____kuona wengine hata___8___kando ya barabara zetu.

Ajabu ni kuwa, watu____9____ watasikika wakilaumu___10___ ya jiji eti kwa kushindwa___11___ usafi. Ni kweli kuwa wanaohusika katika usafi wameshindwa kwa njia moja au nyingine. Lakini, mbona tuwaongezee mzigo? Kumbukeni ni sisi tutakaoteseka ___12____ni____13____ wa maradhi. Tutamlaumu___14___? Ikumbukwe ____15____.

  1.  
    1. kusikitisha
    2. kutatizika
    3. kuchosha
    4. kuumiza
  2.  
    1. hawajali
    2. hawaijali
    3. hawazijali
    4. hawakujali
  3.  
    1. katika
    2. kwa
    3. mnamo
    4. hususan
  4.  
    1. yetu
    2. mwetu
    3. zetu
    4. yote
  5.  
    1. hisia
    2. haraka
    3. nia
    4. ujasiri
  6.  
    1. vinatowa
    2. yanatemwa
    3. wanatemwa
    4. zinatemwa
  7.  
    1. Ni ajabu
    2. Si ajabu
    3. Si kawaida
    4. Ni nadra
  8.  
    1. wakitabawahi
    2. wakitanabahi
    3. wakitawahi
    4. wakiwahi
  9.  
    1. hawa wawa
    2. wawa hao
    3. wao hao
    4. wawa wale
  10.  
    1. kamati
    2. halmashauri
    3. ukumbi
    4. manispaa
  11.  
    1. kudunisha
    2. kudumisha
    3. kudhararisha
    4. kuidhinisha
  12.  
    1. kunapokuwa
    2. kutakapokuwa
    3. kukawa
    4. kunakuwa
    1. mkurupuko 
    2. mlipuko
    3. kuzika
    4. janga
  13.  
    1. nini
    2. gani
    3. nani
    4. kwa nini
  14.  
    1. msinacho hafaidi aliye nacho
    2. mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
    3. yaliyopita si ndwele tugange yajayo
    4. kinga na kinga huwa moto

Kuanzia swala la 16-30 jibu swali kulingana na maagizo

  1. Kati ya mavazi yafuatayo, ni yapi ambayo huvaliwa na wanawake pekee? 
    1. Sidiria na suaruali. 
    2. Kaptura na surupwenye.
    3. Chepeo na bushati. 
    4. Gagro na kanchiri.
  2. Chagua sentensi ambayo ni sahihi kisarufi.
    1. Manyani waliharibu mimea yangu."
    2. Zulia ambayo imetandikwa sakafuni maridadi.
    3. Watu wengi huharibu masaa wakicheza.
    4. Gari ambazo zimenunuliwa zina rangi nzuri. 
  3. Kanusha
    Wachenje angekuja angetiwa mbaroni.
    1. Wachenje asingekuja angetiwa mbaroni.
    2. Wachenje hangekuja hangetiwa mbaroni. 
    3. Wachenje hangekuja asingetiwa mbaroni.
    4. Wachenje asingekuja asingetiwa mbaroni.
  4. Tumia kirejeshi -amba kwa usahihi
    Koja _______________  hupendeza ni ghali sana.
    1. ambacho
    2. ambalo
    3. ambayo
    4. ambao
  5. Nini ufupi ufupisho wa mwana wetu?
    1. Mwanetu.
    2. Mwanawetu. 
    3. Mwanaetu. 
    4. Mwanayetu. 
  6. Katika kujua usawa wa ukuta wa nyumba utatumia chombo kipi? 
    1. Pimamaji.
    2. Utepe. 
    3. Mizani.
    4. Timazi.
  7. Sentensi inayoonyesha hali ya kutendesha.
    1. Alisikia sauti ya mgeni. 
    2. Wimbo uliimbwa vizuri gwarideni. 
    3. Alipoteza kalamu ya jirani yake.
    4. Mshitakiwa alitozwa faini kubwa.
  8. Mke wa mwana ni
    1. mkazamwana.
    2. mka ahau.
    3. mwanyumba.
    4. mavyaa. 
  9. Jaza kwa kiunganishi kifaacho.
    _________________ mgeni akafika leo. 
    1. Labda
    2. Huenda
    3. Yakini
    4. Yamkini
  10. Baada ya Juma kusoma aliviweka vitabu katika
    1. dari.
    2. kigoda. 
    3. zulia.
    4. rafu.
  11. Nini udogo wa
    "Mwanamke ameenda" 
    1. kijanajike kimeenda.
    2. kijike kimeenda.
    3. kike kimeenda.
    4. kijimke kimeenda.
  12. Aina ya ngoma ndogo na nyembamba. Imewambwa upande mmoja na kutiwa vibati kwenye kingo zake, huchezwa kwa kutikiswa. Ala iliyoelezwa ni _______________
    1. zeze.
    2. mbiu.
    3. tarumbeta.
    4. dafu.
  13. Tambua sentensi iliyo na "kwa" ya umilikaji
    1. Yeye anaishi kwa nduguye. 
    2. Nyumbani kwao ni paradiso. 
    3. Mtalii huyo alitembea kwa madaha.
    4. Alipigwa kwa utovu wa adabu.
  14. Dada ni kwa kaka kama vile tembe ni kwa 
    1. kipora.
    2. dawa. 
    3. beberu.
    4. fahali.
  15. Malipo ya kuingilia ukumbini ni _________________
    1. mtaji.
    2. kiingilio.
    3. masurufu.
    4. koto.

Soma ufahamu huu taratibu kisha uyajibu maswali yote 31-40

Matatizo yalianza kumwandama binti Jamila alipojiunga na chuo kikuu na baadaye alipohitimu. Chaguo !a Jamila la kusomea siasa chuoni lilimwingiza kwenye uwanja wa wanaume wenye siasa kali kali. Ilikuwa vigumu kwake kupata kazi ya kudumu kwani wanaume walipinga sera na maoni yake hata yalipokuwa mazuri. Sehemu kadhaa alizozitembelea kuomba kazi, waajiri walimwangalia, wakamwuliza maswali na kumtakia asubiri majibu baadaye. Haikuwa vigumu kwake kujua kwamba kampuni ama mashirika hayo yalikuwa tayari kumwajiri mwanamume hata ingawa alikuwa amefaulu kuwazidi katika chuo kikuu

Jamila alianza kuhudhuria mikutano ya kuwahamasisha wanawake na kusoma katiba za vyama kadhaa vya kisiasa. Akiwa na imani kubwa kwamba wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri, alianza kuonyesha matumaini yake ya kugombea udiwani katika uchaguzi mkuu uliofuata. Pia alitembea vijijini na kuwashawishi wanakijiji kuhusu umuhimu wa kuwachagua wanawake zaidi ili wawe katika nafasi ya kutoa uamuzi wao. Alikuwa akiandika mfululizo wa makala kuhusiana na haki za wanawake yanayowaathiri. Waliowadharau wanawake na kudai kwamba kazi ni za nyumbani tu na wala sio kufanya uamuzi, iliwafaa kupata funzo kuwa hata mtoto wa kike anaweza kutoa maamuzi ya busara na anazo haki sawa na mtoto wa kiume.

  1. Nijinsia ngapi zimezungumziwa katika ufahamu huu? 
    1. Mbili. 
    2. Moja.
    3. Tatu.
    4. Nyingi.
  2. Shida za Jamila zilianza lini?
    1. Alipojiunga katika chuo kikuu.
    2. Kabla na baada ya kujiunga kwenye masomo chuoni.
    3. Baada ya kujiunga na kuhitimu chuo kikuu.
    4. Wakati wowote alipozungumza na wanaume kazini.
  3. Kutokana na kitenzi kuajiriwa tunapata nomino ipi?
    1. Mwajiri. 
    2. Mwajiriwa. 
    3. Majira.
    4. Ajira.
  4. Jamila alikuwa akisomea nini chuoni?
    1. Upigaji kura.
    2. Somo la sheria za wanawake.
    3. Haki za wanawake
    4. Siasa.
  5. Kwa nini kampuni na mashirika yalithamini wanaume kuliko wanawake?
    1. Wanawake hawakuwa na kisomo cha kutosha.
    2. Wanawake hawajui kufanya uamuzi kazini.
    3. Umuhimu wa wanawake haukuzingatiwa kwa sababu walidharauliwa na kuonekana kama waamuzi wa nyumbani.
    4. Wanazifahamu tu kazi za nyumbani na kazi za mashirika hawajazifahamu sana kama wanaume.
  6. Umoja wa wanawake ni mwanamke. Je, umoja wa wanaume ni
    1. mwanaume.
    2. mwanamume.
    3. mwanamme.
    4. kijana.
  7. Ni kweli kusema kuwa Jamila
    1. ana imani kuwa hata mke anaweza kuongoza vizuri.
    2. hana imani na wanaume wowote katika uongozi.
    3. anaamini kuwa hatapata kazi muradi wanaume wamo kazini.
    4. ni mwanamke mjane apiganiaye haki za wanawake.
  8. Maana ya kushawishi ni ____________
    1. kudanganya
    2. kufanya mtu avutike kutenda jambo fulani.
    3. kuchochea mtu kufanya jambo fulani.
    4. kuelimisha watu kuhusu jambo bila kushauriana.
  9. Sheria za vyama vya kisiasa zimo ____________
    1. vitabuni.
    2. bungeni.
    3. katibani
    4. shuleni.
  10. Unapata funzo gani kutokana na ufahamu uliousoma?
    1. Wanawake na wanaume sio sawa. 
    2. Ni vizuri kuwatia wanawake hamu ya kutenda mambo na kuwazingtia. 
    3. Sheria haijaruhusu mwanamke kuwa kiongozi na kufanya maamuzi yoyote.
    4. Elimu ya mtoto wa kiume ina manufaa kuliko ile ya mtoto wa kike.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50

Ukiyasoma majarida mbalimbali utazipata takwimu za kushangaza. Nyingi za takwimu hizi zinasababisha mtu hata akose matumaini. Takwimu zinaonyesha kuwa, watoto wanaokufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano bado ni wengi. Wafao wakati wa kuzaliwa bado ni tele. Watu waambukizwao virusi vya ukimwi kila dakika ni wengi. Watu wanaokufa mikononi mwa majambazi wanazidi kuongezeka nao wafao katika ajali barabarani si haba. Watoto wetu wa kike wanaobakwa na wanyama katika ngozi za binadamu, idadi yao inazidi kuongezeka kila kukicha.

Utazidi kupoteza matumaini ukisoma na usikie kuwa, vijana wetu wanazidi kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na pia vitendo vya ngono. Takwimu za watoto wafao kutokana na maradhi ya malaria nazo zinatisha.Sisemi wafao kwa maradhi mengine kama vile kifaduro. Ifahamike kuwa, wengine hufa kutokana na utapi wa mlo.

Upande wa uchumi, hakuna habari njema vilevile. Bila shaka kufikia sasa umezoea kusikia kuwa, zaidi ya sudusi ya raia nchini wamo katika kitovu cha umaskini. Hawawezi kupata hata angalau shilingi themanini kwa siku. Hebu fikiria kuhusu kiongozi wa jamii aliye na watoto sita ilhali hawezi kupata angaa shilingi themanini kwa siku. Nafasi za ajira nazo ni haba. Idadi ya wasio na kazi wala bazi inazidi kuongezeka

Kulingana na takwimu hizo, lile linaloonekana kukua kwa haraka ni mitaa ya mabanda katika miji yetu. Na je, unaelewa kuwa zaidi ya asilimia sabini ya wakazi wa mingi ya miji yetu huishi katika mitaa ya mabanda?
Tafadhali lifikirie hilo.

Nalo pengo kati ya matajiri na maskini linazidi kushamiri.Kila kukicha, matajiri wanazidi kunawiri huku maskini wakiendelea kudidimia na wengine hata kufifia kabisa.

Hali ya mazingira nayo haijaonyesha lolote la kuinua nyoyo zetu. Takwimu zinazidi kuonyesha misitu yetu inazidi kuangamizwa. Mito nayo inazidi kukauka. Maziwa yetu yanazidi kukauka na kuchafuka. Navyo viumbe vya majini kama vile samaki vinazidi kufariki dunia. Inasemekana pia kuwa kiwango cha joto duniani kinazidi kuongezeka. Si ajabu kujkosa theluji kileleni mwa mlima Kenya miaka michache ijayo. Nayo maradhi ya ngozi na ya saratani ya ngozi yazidi kuathiri na kufilisi ndugu na wazazi wetu.

Swali ni hili, je,tunaelekea wapi? Je, mambo haya yanatokea kwa kuwa hatuna uwezo wa kuyadhibiti au ni kwa sababu tunayavalia miwani? Katu, siamini kuwa hatuwezi kuyashinda. Uwezo tunao lakini nia haipo. Pasipo na nia njia haipo. Lakini tumaini lipo. Si tumaini pekee. Hata suluhisho. Nayo hayo ya mikononi mwenu enyi vijana. Kumbukeni mnao uwezo. Ni nyinyi viongozi wa kesho. Someni kwa bidii mwajibike ili muinusuru dunia.

  1. Katika aya ya kwanza, mwandishi ameyataja majanga mangapi?
    1. Sita.
    2. Matano.
    3. Saba.
    4. Manne.
  2. Kulingana na kifungu, mbali na maradhi, watoto wachanga aidha wanatishwa na :
    1. ukimwi.
    2. dawa za kulevya. 
    3. ukosefu wa chakula.
    4. wizi.
  3. Ni maelezo yapi sahihi?
    1. Ugonjwa wa malaria huwakumba watoto pekee. 
    2. Vijana wetu wametupilia mbali uovu wa ngono.
    3. Kifaduro ni uwele uwatishao watoto.
    4. Mengi ya maradhi yanadidimia.
  4. Kwa mujibu wa mwandishi, uhaba wa ajira unaweza kuzua matokeo yapi?
    1. Uhalifu.
    2. Kumarika kwa uchumi.
    3. Gharama ya maisha kupanda.
    4. Hatujaelezwa. 
  5. Kwa mujibu wa mwandishi, saratani ya ngozi inasababishwa na
    1. lishe bora.
    2. uchafuzi wa mazingira.
    3. mitaa ya mabanda.
    4. manukato yenye kemikali hatari.
  6. Je, unadhani hali ya mambo inayoelezwa hupatikana wapi? 
    1. Nchi zilizoendelea.
    2. Ni vigumu kujua.
    3. Katika mataifa yote duniani.
    4. Ulimwengu wa tatu.
  7. Kulingana na kifungu, ni takriban kiasi kipi cha wakazi wa mjini hakiishi katika mitaa ya mabanda? 
    1. Asilimia sabini.
    2. Ushuri tatu.
    3. Asilimia kubwa.
    4. Sudusi.
  8. Ni bayana kuwa uharibifu wa mazingira utasababisha?
    1. Kuzuka kwa maradhi kama vile ukimwi. 
    2. Kuangamia kwa viumbe mbalimbali.
    3. Kuongezeka kwa viwanda
    4. Kupunguka kwa kiwango kati ya wakwasi na walalahoi.
  9. Kulingana na taarifa, ni kipi kiini cha matatizo yote yaliyozungumziwa?
    1. Ugumu wa maisha. 
    2. Mazingira. 
    3. Matendo ya binadamu.
    4. Umaskini. 
  10. Ni sahihi kusema kuwa:
    1. Mwandishi ni mkwasi wa mali.
    2. Tamaa ya mwandishi ya kushuhudia. 
    3. Vijana wana fursa na satua ya kuboresha mambo.
    4. Binadamu hana uwezo wa kuyatatua matatizo yaliyozungumziwa.


MARKING SCHEME

  1. A
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. A
  7. B
  8. A
  9. C
  10. B
  11. B
  12. B
  13. A
  14. C
  15. B
  16. D
  17. A
  18. D
  19. B
  20. A
  21. D
  22. C
  23. A
  24. B
  25. D
  26. A
  27. D
  28. B
  29. A
  30. B
  31. A
  32. C
  33. D
  34. D
  35. C
  36. B
  37. A
  38. C
  39. C
  40. B
  41. A
  42. C
  43. C
  44. D
  45. C
  46. D
  47. B
  48. B
  49. C
  50. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 Exam 2021 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students