Thursday, 14 April 2022 08:59

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End of Term 1 Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi lumepewa majibu manne. Chagua lifaalo zaidi.

Katika kijiji _1_ Gatiku _2_sehemu _3_ Monyo. Ni pahali _4_ na pa kuvutia kiasi _5_ mimi siwezi kuelezea _6_ maneno, labda uende ujionee kwa macho yako_7__ Mvuto wa Monyo hukamilishwa na _8_ ya kipekee yasiyo na _9_ , chemi chemi ya ajabu inayobubujikwa kwa lahani ya _10_ za kuliwaza. Wapo viboko na samaki _11_ wanaoogelea kwa madaha na ulimbwende madaha na ulimbwende _12_ wanyama wote majini. Kwa hakika chemi chemi ya Monyo, katika mbuga  _13_ Manila _14__ pahali _15_ na maajabu ya mwenyezi Mungu Kijijini Gatiku.

  1.                
    1. ya
    2. wa
    3. la
    4. cha
  2.                  
    1. ina
    2. lina
    3. wana
    4. kuna
  3.                  
    1. linaloitwa
    2. unaoitwa
    3. kunakoitwa
    4. inayoitwa
  4.                
    1. mzuri
    2. nzuri
    3. pazuri
    4. mazuri
  5.              
    1. ambamo
    2. ambalo
    3. ambacho
    4. ambayo
  6.                  
    1. na
    2. kwa
    3. ya
    4. kwenye
  7.                  
    1. yenyewe
    2. penyewe
    3. mwenyewe
    4. kwenyewe
  8.              
    1. mandari
    2. mahali
    3. uzuri
    4. mandhari
  9.              
    1. nishani
    2. sahani
    3. kifani
    4. shani
  10.                
    1. wimbo
    2. nyimbo
    3. mashairi
    4. maneno
  11.                
    1. maridadi
    2. wabora
    3. nyingi
    4. mengi
  12.                  
    1. kuwaliko
    2. kuiliko
    3. kuliko
    4. kumliko
  13.                  
    1. la
    2. wa
    3. ya
    4. mwa
  14.                  
    1. ndipo
    2. ndiyo
    3. ndilo
    4. ndiko
  15.                  
    1. penye
    2. pako
    3. palipo
    4. kuko

Kutoka swali la 16 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Mwalimu wetu ni mkali.
    1. Mwalimu watu ni mpole.
    2. Mwanafunzi wao ni mpole.
    3. Mwalimu wao si mrefu.
    4. Mwalimu wetu si mkali.
  2. Jibu la alamsiki ni:
    1. chewa
    2. binuru
    3. marahaba
    4. ya mafanikio
  3. Leo ni siku ya jumatano. Mtondogoo itakuwa siku gani?
    1. Jumapili
    2. Jumanne
    3. Jumamosi
    4. Ijumaa 
  4. Chakula kilicholala huitwa?
    1. Makombo au masalia
    2. Mwikokipo 
    3. Kiporo au mwiku
    4. Mabaki au staftahi
  5. Andika wingi wa sentensi ifuatavo:
    Mtume anaheshimika.
    1. Watume wanaheshimika.
    2. Matume yanaheshimika.
    3. Mitume yamcheshimika
    4. Mitume wanaheshimika 
  6. Teua sentensi inayoonyesha "ki" ya masharti.
    1. Nilipomwona rais, alikuwa akikagua gwaride la heshima.
    2. Kijikaratasi hiki ndicho chenye maandishi.
    3. Alipowasili alitupata tukipiga domo.
    4. Tukitia bidii ya mchwa, tutafua dafu.
  7. Jaza pengo kwa kiashiria radidi kinachofaa
    Nyangumi ....................... ndiye amenaswa na mtego ule. 
    1. huyu huyu 
    2. huyu huyo
    3. lo hiyo
    4. yuyu huyu 
  8. Shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti huitwa:
    1. tarbia
    2. tathlitha
    3. takhmisa
    4. tathnia 
  9. Ipi si zana ya kivita?
    1. Nyambizi 
    2. Manowari 
    3. Parafujo
    4. Kombora
  10. Akifisha sentensi ifutayo vyema.
    Mama wee dadangu alishtuka
    1. “Mama wee!" Dadangu alisema.
    2. "Mama wee?" dadangu alitamka.
    3. “Mama wee" dadangu alikiri.
    4. Mama wee! "Dadangu alisema." 
  11. Unda kitenzi kutokana na neno mpishi.
    1. upishi
    2. pika 
    3. upikaji
    4. upiki 
  12. Tumia neno la heshima kujaza pengo.
    ......................... niazime kitabu chako nitakurudishia nikimaliza kufanya zoezi.
    1. Tafadhali
    2. Samahani 
    3. Pole
    4. Aisee
  13. Mchezo huu ..................... vizuri sana asubuhi.
    1. unachezesha 
    2. unachezana
    3. unachezeshana
    4. unachezeka 
  14. Neno "pua" hupatikana katika ngeli gani?
    1. LI-YA
    2. U-ZI
    3. I-ZI
    4. I-I 
  15. Chagua neno lililo sawa na lililopigwa kistari.
    Mfanyikazi aliyepigwa kalamu alikuwa mlegevu.
    1. mjuzi
    2. mwenye bidii
    3. mwerevu
    4. mzembe

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.
Kuna maradhi yanayowatinga adinasi katika dunia hii. Mojawapo ya mawele hayo ni ugonjwa wa kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu huathiri mapafu na inakadiriwa huua mamilioni ya watu kila mwaka duniani. Maradhi haya husababishwa na bakteria. Bakteria hawa huathiri kila sehemu ya mwili hasa mapafu. Aidha kifua kikuu huenezwa kwa haraka aliyeambukizwa anapokohoa au kuchemua na kutoa vijitone vya bakteria hao ambao huingia hewani na wengine huvuta.
Hata hivyo, watu wengi hawajui kwa sababu bakteria huvamiwa na kuingia mwilini. Kati ya mtu mmoja kwa watu ishirini inakadiriwa kuwa bakteria wengine huvamiwa na kuambukiza miezi au miaka kadhaa baadaye.
Dalili za maambukizi huanza kwa kikohozi chenye mwasho, ambacho huendelea kwa muda mrefu. Kikiendelea kuwa kikao kwa muda huo, mwele huwa na kikohozi ambacho huenda kikawa na matone ya ngeu. Dalili nyingine ni homa kali, kutokwa na jasho, kupoeza uzito, uchungu kifuani na kupoteza hamu ya chakula.
Ugonjwa huu usipotibiwa haraka huleta tatizo la kupumua, hatimaye huenea katika sehemu nyingine mwilini. Takribani nusu ya wote wanavkosa kutibiwa hufa. Inakisiwa kuwa katika mataifa maskini, watu milioni tatu hufa kila mwaka. Aidha maradhi hayo huandamana na Ukimwi ambao unadhoofisha mwili. Watu hupewa chanjo wakiwa wachanga ili kukinga uwele huu. Kwenye hospitali waganga hutumia njia kadhaa kuchunguza maambukizi ya kifua kikuu. Mgonjwa anapopewa dawa ni vizuri amalize kipindi chote cha dawa hata kama amepona huenda akasababisha kuibuka kwa ugonjwa wa kifua kikuu sugu.

  1. Kulingana na kifungu hiki ni ukweli kusema ugonjwa wa kifua kikuu huadhiri:
    1. mapafu pekee
    2. mbavu na mapafu
    3. kila sehemu ya mwili
    4. miguu na mapafu 
  2. Mwele wa kifua kikuu huambukiza watu wengine ugonjwa huu haraka kupitia; 
    1. Kukohoa na kuendesha 
    2. Kukohoa na kuchemua
    3. Kuchemua na bakteria
    4.  Bacteria na joto mwilini 
  3. Ni asilimia gani ya watu wanaokadiriwa bacteria huweza kujificha na kuambukiza miezi na miaka kadhaa baadaye.
    1. Asilimia ishirini 
    2. Asilimia moja
    3. Asilimia kumi
    4.  Asilimia tano
  4. Mwandishi ametaja dalili ngapi za kifua kikuu?
    1. Mbili
    2. Sita
    3. Tano
    4. Saba
  5. Kifua kikuu husababishwa na:
    1. ukosefu wa kinga mwilini
    2. viini viitwavyo bakteria
    3. ukosefu wa usafi
    4. mtu kukohoa karibu na mwingine
  6. Ipi si njia ya kukinga kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu?
    1. Alkupewa chanjo ukiwa na umri mdogo 
    2. kujikinga kutokana na baridi
    3. kuepuka makao ya wagonjwa wenye ugonjwa huu.
    4. kuwatibu wagonjwa wa ugonjwa huu 
  7. Mgonjwa anapopewa dawa ni vizuri:
    1. atumie dawa hizo kulingana na uwezo wake. 
    2. anywe dawa hizo zote mara moja 
    3. awache kutumia dawa hizo mara tu anapopona 
    4. atumie dawa hizo hadi kipindi chote kikamilike hata kama amepata nafuu. 
  8. Kati ya watu hawa, ni yupi asiyepatikana hospitalini?
    1. Mganga
    2. Daktari
    3. Mkutubi
    4. Muuguzi 
  9. Ni nini maana ya kifua kikuu sugu?
    1. Ugonjwa wa kifua kikuu unaotibiwa haraka.
    2. Ugonjwa wa kifua kikuu unaotokana na ukimwi.
    3. Ugonjwa wa kifua kikuu usioweza kutibiwa kwa urahisi.
    4. Ugonjwa wa kifua kikuu usiokuwa na by dalili 
  10. Kichwa gani kinachofaa kifungu hiki:
    1. Kifua kikuu sugu
    2. Maradhi bandia ya ukimwi. 
    3. Ugonjwa wa kifua kikuu
    4. Dalili za kifua kikuu.

Soma habari inayofuata kisha ujibu maswali 41 hadi 50,
"Majambazi waliowateka nyara na kuwaua waja watatu katika tariki ya kutoka Kikochi kuelekea Kinango wangali wanasakwa na polisi. Taarifa ya hivi karibuni inatuarifu kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo hayajabainika.
Yaaminika kuwa gari la aina ya V8 lenye rangi ya samawati lilikuwa na banati mmoja na maghulamu wawili. Vijana hawa walikuwa wa rika moja. Polisi wanasema kwamba mahuluki hao walistarehe katika hoteli moja va kifahari miini Kikochi kwa muda mrefu kabla ya kutoka hapo na kuelekea Kinange. Wakiwa njiani, watu hao walitekwa nyara na majambazi wasiojulikana na kuelekezwa hadi pahali pasipojulikana
Siku mbili baadave, mwili wa mwanamme mmoja aliyetambuliwa kama Juma ulipatikana ukiwa umetupwa kichakani kilichopewa jina la Wahaka huku amevujwa vunjwa mbavu. kichwa limevunjwa na meno yalikuwa yameng'olewa pamoja na macho.
Mwah mwingine wa mwanaume alivetambulika kama Kalembe, ulipatikana mtoni Mjengo ukiwa umekwama kwenye gogo la mti Askari wanaamini kwamba banati yule mmoja ann
mmoja aliyekuwa ganini mie pia aliuawa la sivyo majambazi hao wanamficha. Walakini cha mno ni kwamba kufikia sasa hakuna familia yoyote inayodai kumpoteza mwanamwali. Polisi wanauliza mja yeyote aliye na habari yoyote ile iwezayo kufumbua fumbo hilo asisite kuielezea kwenye kituo chochote cha usalama

  1. Majambazi waliowateka watu nyara:
    1.  wako kizuizini 
    2. hawajulikani walipo 
    3. wametiwa mbaroni
    4.  wamekamatwa
  2. Gari walilosafiria waliotekwa nyara lilikuwa la rangi ya:
    1. kijani
    2. manjano
    3. nyeusi
    4. buluu 
  3. Mojawapo ya mambo ambayo bado hayajabainika ni: 
    1. gari waliosafiria waliotekwa nyara 
    2. miili yote ya waliotekwa nyara ilipo 
    3. alipo mmoja wa watekwa nyara
    4. waliokuwa wametoka kabla ya kutekwa nyara 
  4. Ni kweli kusema:
    1. watu hawa walitekwa nyara kabla ya kujivinjari huko kikochi 
    2. miili ya watekwa nyara wote ilipatikana wakiwa wafu 
    3. yakini majambazi wanamficha mwanamke aliyetekwa nyara 
    4. uchunguzi wa polisi kuhusu uhalifu huu umefana 
  5. Watu waliotekwa nyara huitwa:
    1.  Mahabusu 
    2. Majangili
    3. Mateka
    4. Majambazi
  6. Kulingana na taarifa hii, polisi wanashuku: 
    1. mwanamke mmoja haeleweki vyema kuhusu mauti au uhai wake.
    2. waliouawa pia walikuwa majambazi
    3. mwanamke yule alishiriki mauaji ya waliokufa.
    4. waliotekwa nyara walijisalimisha kwa hiari. 
  7. Miili ya waliouawa ilikuwa:
    1. imeoza
    2. imehifadhiwa 
    3. kando
    4. pamoja 
  8. Neno wahaka lina maana ya:
    1. wasiwasi 
    2. giza
    3. vichaka
    4. hakika
  9. Jambo ambalo ni gumu kuelewa kama vifo hivi huitwa: 
    1. kizunguzungu 
    2. kikweukweu 
    3. kitefutefu
    4. kizungumkuti 
  10. Mada mwafaka ya habari hii ni:
    1. Sitofahamu ya mauaji 
    2. Msitu wa wahaka
    3. Polisi wazembe 
    4. Taaluma ya utekaji nyara  

MARKING SCHEME

swa marking scheme

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End of Term 1 Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students