Friday, 01 July 2022 07:10

Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi / mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi.
Kutokana na hali _1_ya hewa taifa la Kenya huwavutia watalii_2_kutoka kila pembe ya dunia. _3_. hali ya hewa hutofautiana sana kutoka sehemu moja hadi_4_ Ukizuru maeneo ya milimani hasa milima Kenya na Abadea utapata hali ya baridi. _5_ kilele kuna theluji ilhali kwenye nguu kuna msitu. Iwapo utatembelea maeneo ya Pwani na Ziwa Viktoria utapata kuna viwango vya juu vya joto. Aidha ipo misitu iliyojaa wanyamapori wa kila aina. Isitoshe zipo mbuga na hifadhi za wanyamapori. Hali ya uchukuzi_6_ kuelekea kwenye mbuga _7_. Pia kuna hoteli za kifahari. Hoteli hizo zinawahudumia wageni hawa. Ukitembea kwenye baadhi ya mito kuna maanguko ya maji. _8_. janibu za Thika kuna Thika na Chania. Maeneo ya Nyahururu kuna Thompson. Kenya kweli imebarikiwa sana.

  1.        
    1. shwari
    2. shari
    3. swali
    4. hali
  2.        
    1. chungu kubwa 
    2. chungu kizima
    3. chungu nzima
    4. chungu mzima
  3.        
    1. Kwa hivyo 
    2. Hata hivyo
    3. Kama vile
    4. Kwa vile
  4.        
    1. kwingine
    2. pengine
    3. jingine
    4. nyingine
  5.        
    1. Kwenye
    2. Penye
    3. Katikati
    4. Kati ya
  6.      
    1. imedunishwa
    2. imedidimishwa
    3. imeimarishwa
    4. imechukiza
  7.      
    1. hizo
    2. hiyo
    3. ile
    4. hilo
  8.      
    1. Maadamu
    2. Mathalani
    3. Minghairi
    4. Aghalabu

Maridhia alikuwa kijana _9_ kwa mapenzi _10_ na wazazi wake. Ingawa walikuwa mafukara, wazazi wote wawili walijitolea kwa _11_kumkidhia mtoto wao mahitaji yake ili akue kama mtu _12_angeifaidi jamii Hawakukosa kumrudi au kumtahadharisha dhidi ya hulka _13_ ya utu kwani walielewa kuwa _14_. Maridhia alifuata mwongozo wa wazazi na akatokea kupendwa na wengi kwa sababu ya nidhamu _15_

  1.      
    1. aliyelewa
    2. aliyelelewa
    3. aliyekopoa
    4. aliyezaa
  2.      
    1. makubwa
    2. kidogo
    3. kubwa
    4. matele
  3.        
    1. udi na uvumba
    2. uta na upote
    3. maji na maziwa
    4. kinu na mchi
  4.      
    1. ambao
    2. ambazo
    3. ambayo
    4. ambaye
  5.      
    1. yenye
    2. isiyo
    3. iliyo
    4. zisizo
  6.       
    1. juhudi si pato
    2. sikio halipiti kichwa
    3. kinolewacho hupata
    4. cha kuvunda hakina ubani
  7.      
    1. yake
    2. yao
    3. zetu
    4. yangu

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

  1. Kutokana na nonimo tiba, tunapata kitenzi 
    1. matibabu
    2. tabibu
    3. utibaji
    4. tibu
  2. Andika wingiwa:
    Mnyororo ulikatwakatwa ukatupwa jaani. 
    1. Minyororo zilikatwakatwa zikatupwajaani. 
    2. Minyororo ilikatwakatwa ikatupwa majaani, 
    3. Minyororo ilikatwakatwa ikatupwa jaani. 
    4. Maminyororo ilikatwakatwa ikatupwa majaani
  3. Ni sifa gani kati ya zifuatazo isiyochukua kiambishi cha nyeli?
    1. -bora
    2. -ororo
    3. -chafu
    4. -ekundu
  4. Ni sentensi ipi iliyoandikwa katika hali tegemezi?
    1. Nitakuletea kikapu unitilie mboga. 
    2. Zeda hukanza maji kabla ya kuoga. 
    3. Hawajakuwa wakipita huku. 
    4. Shule yetu ingepata ufadhili ingejengwa vizuri.
  5. Chagua kikundi kilicho na vivumishi pekee.
    1. Pole, sana, taratibu, tangu.
    2. Ebo! Ala! A kha! Lo! 
    3. Sisi: wewe, wao, nyinyi.
    4. Wote, salibaya. yake.
  6. Kati ya nomino hizi.ipi iliyo katika ngeli ya LI-YA? 
    1. Manukato
    2. Mali 
    3. Madoa
    4. Manowari 
  7. Nilijipaka poda usoni 
    1. Wangu
    2. pangu. 
    3. yangu.
    4. mwangu.
  8. Tunasema eupe kama theluji na zito kama
    1. nanga
    2. mzigo 
    3. usuli
    4. kanini
  9. Ni sentensi gani iliyo sahihi?
    1. Wanafunzi huenda shuleni kwa miguu. 
    2. Nyanya aliingia kwa kanisa akasali.
    3. Mlangoni wenye kufuli umefungwa. 
    4. Tutaenda ziarani na basi.
  10. Ni sentensi ipi iliyotumia kirejeshi amba ipasavyo?
    1. Majaribio ambao yalifanywa yalifaulu. 
    2. Gari ambalo lenye tuliabiri ni la mjomba.
    3. Huo ndio wimbo ambao nilitamani ucheze 
    4. Sukari ambayo iliyotiwa katika chai ni nyingi
  11. Ni sentensi gani inayoonyesha wingi wa sentensi hii? Mama yangu amewasili. 
    1. Mama yetu amewasili. 
    2. Mama wetu amewasili. 
    3. Mama zetu wamewasili 
    4. Akina mama zetu wamewasili.
  12. Jaza kwa vivumishi vifaayyo:
    Kiatu____ ni hiki 
    1. wenye, jingine 
    2. vyenyewe, vingine
    3. chenyewe, kingine
    4. zenyewe. nyingine
  13. Kanusha:
    Umesafiri mapema sana. 
    1. Haujasafiri mapema sana. 
    2. Hujasafiri mapema sana. 
    3. Hakusafiri mapema sana.
    4. Huwa husafiri mapema sana.
  14. Nilikuwa wa kwanza kufika darasa ndiko
    kusema, nilifika___watu wote.
    1. baada ya
    2. mbele ya
    3. kabla ya
    4. nyuma ya
  15. Andika udogo wa:
    Mkono wake ni mkubwa. 
    1. Kono lake ni kubwa. 
    2. Makono yake ni makubwa. 
    3. Mikono yake ni mikubwa. 
    4. Kikono chake ni kikubwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Kila mwanadamu ulimwenguni ana haki ambazo ni faradhi kila mmoja kuzingatia kile kinachonitia kiwewe ni kwamba wengi wetu tumekuwa tukizipigania haki zetu na kuzizika katika kaburi la liliwala zile za watoto. Ajabu zaidi ni kwamba wazazi wa watoto hawa ndio waliotia fora katika kuji watoto. Wanazivalia miwani hasa. Ninashikwa na jitimai na kibuhuti kikubwa, nikiona namna wavyele hawa wanavyosahau dhima na wajibu wao wa kuwatunza watoto wao. Wao, uajibikaji wa kuwalea watoto wao kwa njia nyofu na ongofu wameutia katika kaburi la sahau. Ikumbukwe kuwa kila mtoto ana haki zake na ni sharti kama mauti haki hizo zipewe kipaumbele na yeyote aliyewikwa jukumu hilo na Mola Mkawini.
Mathani, tunaelewa kuwa watoto wana haki ya kupata elimu. Wazazi wapende wasipende, watake wasitake, ni jukumu lao kuwapeleka watoto wao shuleni kusoma. Kwani haijawafikia masikioni kuwa climu ni taa gizani huzagaa? Enzi za zamani za uwaacha watoto kuzurura mitaani kivoloya bila lengo wala nia, zimepitwa na wakati. Elimu ndiyo nuru ya jamii. Tukiwaclimisha wana wetu, tutaupiga vita ulalahoi. Tutakuwa na wataalamu waliotaalamika katika nyanja na bila shaka tutajivunia watoto wetu.
Mtoto anayo haki ya kulelewa vizuri. Mlezi ama mzazi wake hana budi kuhakikisha kuwa mtoto amepatilo chakula cha kutosha na chenye lishe bora. Isitoshe watoto wanayo haki ya kuvishwa mavazi yatakayowakinya dhidi ya baridi yabisi na jua kali. Ukipita mitaani, utapigwa na butwaa kuviona vitoto vikicheza cheza vikiwa raham: wazazi hawa kwani hawaoni soni? Vikiwa katika harakati zao za kucheza, hujipata wakichezea takataka vilizosheheni makombo ya vyakula vilivyooza na kuozeana. Kwa hivyo, wanajipata wakivitumbukiza vinywani na hatimaye kuugua maradhi mbalimbali.
Sikonei hapo katu, lazima aidha nikujuze kuwa watoto wana haki ya kupata malazi bora na kuishi katika nyumba ili kumkinga na mabadiliko ya hali ya anga kama vile mvua, baridi na jua. Alalapo sharti pawe pazuri.
Asiachwe alale sakafuni penye baridi kali kama barafu. Husemwa, mwana wa yungi hulewa sembuse wa mwanadamu?
Familia iwe na watu watulivu, wenye mapenzi na wanaowajibika. Tusiwarushie watoto maneno makali ya kuwaumiza kwa udhuru wa kuwarekebisha. Akikosea, mtoto ascmezwe kwa upendo na aonyeshwe kuwa alilolifanya si zuri na asirudie. Endapo atarudia, basi aadhibiwe kama mwanadamu bali si kama mbwa aliyetabawali msikitini
Mtoto akilelewa vyema katika mazingira mazuri na matulivu, atainuka kuwa mwajibikaji wa kutegemewa na jamii yote. Aidha akilelewa vibaya, atakua akiwa mzigo sio tu kwa wazazi wake, bali pia jamii nzima. Sote tushirikiane zaidi ya kiko na digali, kinu na mchi ili kwa pamoja tumlee mtoto vizuri kwa kuzingatia haki zote zote ili tukijenge kizazi kijacho..

  1. Ni jambo lipi kulingana na aya ya kwanza, linamtia wasiwasi mwandishi? 
    1. Watu wengi wanazingatia haki za watoto. 
    2. Watu wengi wanazingatia haki zao. 
    3. Watu wengi wanazipigania haki zao na kuzisahau za watoto."
    4. Watoto huzipigania haki zao wenyewe.
  2. Maneno "waliotia fora" yametumika, yana maana gani? 
    1. Waliofanikiwa kim: 
    2. Wasiotetea haki za watoto. 
    3. Waliopata ufanisi katika kupigania haki za watoto. 
    4. Waliopendelea haki za watoto kuliko zao. 
  3. Ni akina nani wanaostahili kuwa katika mstari wa inbele kupigania haki za watoto?
    1. Watoto wenyewe. 
    2. Wazazi na watoto. 
    3. Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
    4. Wote walitwika jukumu la kuwalea watoto.
  4. Ni kwa nini inasemekana kuwa ni lazima watoto wapate elimu? Elimu 
    1. itayaboresha maisha ya baadaye ya mtoto. 
    2. inatolewa bure na serikali.
    3. inapatikana popote.
    4. ni vigumu kuipata maishani.
  5. Elimu ni taa, gizani huzagaa ni
    1. methali.;
    2. balagha.
    3. nahau.
    4. msemo.
  6. Wazazi watajivunia watoto wakati gani?
    1. Watakapocheza pamoja na kujichafua.
    2. Watakapoelimika na kuwa watu wa. kutegemewa. 
    3. Watakapovaa mavazi mazuri kila siku.
    4. Watakapokaidi kukosolewa na wakubwa wao
  7. Taka wazichezeazo watoto,
    1. huwa majalalani na zimefunikwa vizuri. 
    2. huchezwa tu na mbwamwitu. 
    3. huwa ni chafu na zer ye mabaki ya chakula 
    4. huwa zinatumiwa na watoto kutoka familia tajiri.
  8. Kulingana na aya ya nnc, mtoto
    1. ana haki ya kukomewa anapokosea. 
    2. anahitaji kulishwa vyema.
    3. anastahili kupata elimu ya kutosha.
    4. anafaa apewe malazi ya kuishi
  9. Aghabu sakafu nyingi,
    1. zina baridi kama barafu.
    2. hutengenezwa vizuri. 
    3. Lulaliwa na watoto wengi
    4. huwa makao mazuri ya familia nyingi.
  10. Watu hushirikiana kwa namna zote hizi ila
    1. kiko na digali. 
    2. tui na maziwa. 
    3. jembe na mpini. 
    4. kinu na mchi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Maisha yangu yalikuwa yale ya Sultan bin Jerere. Nilichokihitaji nilikipata bila kutoa jasho hata. Wazazi wangu walinionyesha mapenzi ya dhati. Nyumbani kwetu kulikuwa peponi. Hakuna kilichokosa na endapo kilikosa, kilikuwa kimeendewa popote ulimwenguni. Nguo zetu hazikutengenezwa barani sembuse nchini? Magari ya kifahari yaliyonunuliwa ghali yasingehesabika. Nilipelekwa shuleni kwa shangingi na kusubiriwa na dereva wangu mpaka wakati ule ningemaliza masomo. Sikupata masaibu katu na niliishi maisha ya raha mustarehe kweli.
Hata hivyo, raha yangu ilifikia tamati ya ghafla. Ajali isiyojali ilinipokonya wazazi wangu wapenzi. Ndege waliyokuwa wakisafiria ilianguka baada ya kupata hitilafu za kimtambo na kuwasafirisha jongomeo abiria pamoja na wote waliokuwa humo. Vifo hivyo vya ghafla bin vuu, viliyabadilisha maisha yangu. Maajabu ni kuwa mali ya wazazi wangu yalitoweka ghafla. Sijui mali hiyo walitoa kupi wazazi wangu.
Wajomba wangu pamoja na jamaa kwa jumla walitoweka nyusoni. Nilibaki peke yangu bila wa kunilea wala kuniongoa. Hakuna aliyenijali, marafiki wa wazazi wangu nao waliniambaa na kutoweka zaidi ya umande wa alfajiri jua lichomozapo,
Hapo ndipo wazazi wa rafiki yangu Zena walipoamua kuingilia kati na kunichukua. Hii ni baada ya rafiki yangu kuwasimulia masaibu yaliyokuwa yamenisibu. Faraja iliyoje! Bwana Fadhila alikuwa mzee aliyebugia chumvi si haba. Aliishi na mkewe Bi. Moyo. Ingawa walikuwa hawana hawanani, waliona ni heri umaskini wa mali na utajiri wa utu na wema, Bwana Fadhula na mkewe walishirikiana kama kiko na digali kulusomesha mimi na rafiki yangu wakinichukua kama mmoja wa watoto wao. Tulipokosa, walituadhibu sawia bila kutubagua Chakula tulikula pamoja, kiwe wali ama pure. Upendo ulikuwa katika familia hii ulizidi utajiri wowote.
Nami niliamua kukaza kamba masomoni ili nisije nikawaibisha wafadhili wangu. Aidha nilimhimiza Zena kuuma uzi shuleni ili kujijengea mustakabali aula. Shuleni tulitia fora na kuenziwa na kila mmoja shuleni. Tulimaliza masomo ya shule ya upili na kujiunga na chuo kikuu ambapo mimi nilisomea udaktari naye Zena akiridhika na uhasibu. Pamoja, tulikuwa kama mtu na kivuli chake.
Kwa kurudisha mkono wa fadhila, tuliwajengea nyumba nzuri na kuwaajiri wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na shambani. Niliamini kuwa miili yetu ni kama mimea. Ikitunzwa inanawiri vyema. Wazee hawa walibadilika na kuwa kama vijana. Waliishi maisha ya raha mustarehe walifurahia juhudi walizozifanya kumtunza mtoto wa watu, mwanamkiwa ambaye sasa amegeuka kuwa mwana wa maana katika uzee wao.

  1. Maisha ya mwandishi yalikuwa ya aina gani?
    1. Ya kikabwela. 
    2. Ya kilalahoi. 
    3. Ya kitajiri.
    4. Yakimaskini.
  2. Maisha yake mwandishi yalitatizwa na nini? 
    1. Masaibu
    2. Sherehe 
    3. Kutosoma
    4. Vifo vya wazazi wake
  3. Jamaa na marafiki wa wazazi wake mwandishi
    1. walikuwa wenye huruma na utu. 
    2. walikuwa wanafiki ambao hawakumsaidia. 
    3. walikuwa wengi na walimfaa sana.
    4. walikuwa watu wazuri lakini mikono mirelu.
  4. Mali ya wazaziwe mwandishi ilipatikana vipi?
    1. Biashara walizofanya.
    2. Ajira ya donge nono. 
    3. Mwandishi hakubaini.
    4. Kufuga mifugo mengi.
  5. Ni nani aliyemsaidia mwandishi hamda ya kukosa mhisani? 
    1. Zena rafikiye. 
    2. Wazazi wa Zena 
    3. Wajomba wake wandishi
    4. Marafiki wake mwandishi
  6. Taarifa ya uhitaji wake mwandishi uliwafikiaje wazazi wa Zena?
    1. Zena ndiye aliyewaambia wazazi wake
    2. Wazazi wa mwandishi waliwasiliana na Bwana Fadhila kabla ya kifo chake
    3. Wazazi wake mwandishi walikuwa wameandika urithi. 
    4. Wajombawe walimwomba Bw. Fadhila amsaidie mwandishi.
  7. Kulingana na aya ya nne, ni sahihi kusema
    1. Bwana Fadhila na mkewe walikuwa wazee
    2. Bwana Fadhila na mkewe walikuwa matajiri sana.
    3. Familia ya Fadhila ilikuwa na watoto wengi.
    4. Wazazi wa Zena walimbagua mwandishi.
  8. Nami niliamua kukaza kamba. Maneno haya yana maana kuwa mwandishi 
    1. aliaga dunia
    2. alianza kuzembea. 
    3. alifanya bidii.
    4. alihuzunishwa na kifo cha wazaziwe.
  9. Rafikiye mwandishi alisomca kazi gani?
    1. Wanasheria
    2. Uhandisi 
    3. Uandishi
    4. Uhasibu
  10. Ni methali gani inayoweza kuelezea kifupi taarifa hii?
    1. Asiye na wake aeleke jiwe. 
    2. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.
    3. Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina
    4. Aisituye mvua imemnyea

INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Kamilisha insha hii kwa kuifanya iwe ya kusisimua zaidi.
Tulimaliza kula chajio na kuingia vyumbani mwetu kulala. Punde si punde......



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. A
  2. C
  3. B
  4. D
  5. A
  6. C
  7. A
  8. B
  9. B
  10. A
  1. A
  2. D
  3. B
  4. C
  5. A
  6. D
  7. B
  8. A
  9. D
  10. D
  1. C
  2. B
  3. A
  4. A
  5. C
  6. D
  7. C
  8. B
  9. C
  10. D
  1. C
  2. B
  3. D
  4. A
  5. A
  6. B
  7. C
  8. D
  9. A
  10. B
  1. C
  2. D
  3. B
  4. C
  5. B
  6. A
  7. C
  8. A
  9. D
  10. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Standard 7 Term 2 Opener 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students