Thursday, 09 September 2021 09:02

Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 2

Share via Whatsapp

 Tumia msamiati ulio mwafaka zaidi ujaze kwenye vihasho 1 hadi 15.

Ni kweli kwamba jinsi tunavyoendelea kukua ndivyo __1__ kujifunza mambo mengi aushini. __2__ya hayo ni kazi. Kazi ndiyo _3_ wa maisha ya binadamu. Kazi ni kazi, iwe ya_4_au rahisi; usichagve. Kwani kazi_5_hutusaidia_6_ riziki yetu. Tujizoeshe, tupende na__7__ kazi mapema. Wajibu_8_nyumbani ni kuwasaidia wazazi katika kazi zote. Ubwete haufai_9_ hauwezi kutulisha. Tuchape kazi kwanza_10__tupumzike.

  1.  
    1. tunazidi
    2. tunavyozidi
    3. tunakozidi
    4. tunakozidi
  2.  
    1. Mmojawapo
    2. Mojawapo
    3. Kimojawapo
    4. Umojawapo
  3.  
    1. uti wa mgongo
    2. uti wa mkono
    3. uti wa kichwa 
    4. uti wa mguu
  4.  
    1. suluhu
    2. sulu
    3. zulu
    4. sulubu
  5.  
    1. ndicho
    2. ndiyo
    3. ndilo
    4. ndio
  6.  
    1. kusunbua
    2. kuzubua
    3. kuzumbua
    4. kusafirisha
  7.  
    1. kuendeleza
    2. kuendelesha
    3. kuendelea
    4. kuendeleshwa
  8.  
    1. yetu
    2. zetu
    3. letu
    4. wetu
  9.  
    1. na
    2. wala
    3. ingawa
    4. lakini
  10.  
    1. ndiyo
    2. ndio
    3. ndipo
    4. ndiko

Je_ 11_ wajua kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu? Ni kwa kutambua jambo hili _12_serikali ya Kenya ilitangaza kuwa itatoa elimu bila malipo kwa watoto wote ili kila _13__ apate nafasi ya kujipatia elimu ya msingi. Hali kadhalika watoto wa_14_wa kwenda shule hawapaswi kuajiriwa mahali_15 .

  1.  
    1. ,
    2. ?
    3. !
    4. .
  2.  
    1. ambako
    2. ambao
    3. ambaye
    4. ambapo
  3.  
    1. moja
    2. mmoja
    3. mamoja
    4. mojawapo
  4.  
    1. rika
    2. wakati
    3. umri
    4. muda 
  5.  
    1. pote
    2. kokote
    3. popote
    4. kote

Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Sentensi;
    Nilipigiwa mpira ina maana zifuatazo isipokuwa 
    1. mpira ulipigwa ukielekezwa kwangu
    2. nilisaidiwa kupiga mpira
    3. nilipigwa kwa sababu ya mpira
    4. mpira ulitumiwa kunipiga
  2. Umbo hili ni
             class 7 kiswa set 2 q17
    1. mstatili
    2. mche
    3. duara dufu
    4. pia
  3. Neno "maji" liko katika ngeli gani?
    1. I-I 
    2. YA-YA
    3. I-ZI
    4. LI-YA
  4. Kamilisha methali: Mchumia juani
    1. hulia kivulini 
    2. hali wali mkavu
    3. huumiza mkonowe 
    4. marejeo ni ngamani
  5. Chagua umoja wa sentensi hii:
    Watajiwakilisha wao wenyewe 
    1. Nitajiwakilisha sisi wenyewe
    2. Atajikilisha wewe mwenyewe
    3. Nitajiwakilisha mimi mwenyewe
    4. Atajiwakilisha yeye mwenyewe
  6. Petro alitia ________ masomoni na akuibuka mwanafunzi _______ zaidi.
    1. chumvi, mzuri
    2. bidii, upya
    3. fora, bora
    4. kauri, kauli
  7. Msichana alitumia __________ kulia vibanzi.
    1. umma 
    2. uma
    3. kijiko
    4. mwiko19. 
  8. Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vizuri?
    1. Nilinunua sukari, chumvi, mayai, biskuti
    2. Baba wa Wambui ni karimu
    3. Lo! Ameshindwa kufunga bao!
    4. Mji wa Mombasa unapendeza
  9. Ni vazi gani lisilovaliwa na wanaume?
    1. Chupi
    2. Kizibao
    3. Fulana
    4. Kanchiri
  10. Andika kwa wingi
    Mama yake alipoteza ufunguo
    1. Mama zao walipoteza funguo
    2. Wamama wao walipoteza funguo 
    3. Kina mame zao walipoteza funguo
    4. Mama zetu walipoteza funguo
  11. Chagua kiunganishi katika sentensi hii.
    Nilifika sokoni ijapokuwa nilichelewa.
    1. sokoni
    2. nilifika
    3. ijapokuwa
    4. nilichelewa
  12. Tambua kimilikishi katika sentensi ifuatayo:
    Tulimkuta mlevi akiwa amelala nyumbani kwake.
    1. mlevi 
    2. kwake
    3. nyumbani
    4. amelala
  13. Mnyama wa porini anayefanana na ng'ombe
    1. swara 
    2. twiga
    3. pundamilia
    4.  mbogo
  14. Kalamu yangu ______ jana
    1. iliibiwa
    2. iliiba
    3. iliibwa
    4. uliibwa
  15. Kifaa cha ufundi kinachotumiwa kukerezea mbao ni
    1. msumeno 
    2. patasi
    3. nyundo
    4. timazi

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali 31 hadi 40.

Siku ya kurudi shuleni iliwadia wazazi wa Pendo waliandamana naye kurudi shuleni. Ulikuwa mwisho wa mwezi na magari ya abiria yalijaa pomoni. Hata hivyo, walifika shuleni salama salimini. Pendo alikuwa amejawa na soni usoni. Hakutaka kumwona yeyote pale shule hasa wanafunzi. Hata hivyo alijikaza kwani alimaizi kuwa lisilobudi hutendwa.

Walimu walimweleza mzazi wa Pendo vile mwanao alivyopotoka zaidi ya kuwa na vipawa adinu. Waliwaeleza pia kuhusu Maria. "Huyu mtoto wa kitajiri ndiye anayempotosha Pendo. Ni lazima aachane naye kabisa ili afaulu katika maisha ya baada "Mwalimu mkuu alisema.

Babake Pendo aliposikia jina Maria likitajwa alianza kutafakari. “Mbona jina hili si geni kwangu?" Alijisaili moyoni. Jina lilo lilifanana n a mtoto wa mwajiri wake hata ingawa majina hufanana. Hakuona uwezekano wa mtoto wa mwajiri wake kuwa ndiye aliyemharibu mwanawe. Vilevile, hakuona kama kuna uwezekano kuwa mtoto wa tajiri angesomea hapo. .

Musa, babake Pendo, hakujua alikosomea mtoto wa kiwajiri wake. Hata hivyo, fikra na jina hilo zilimtatiza kwa muda baba mtu. Baada ya muda mapi kupita, Musa alimuuliza mwalimu jinsi ya kumsaidia Pendo. Mwalimu mkuu alieleza kwamba jambo lilo lingesuluhishwa vizuri kwa kuwahusisha wazazi wa Maria.

Mwalimu alielezea kwamba wazazi wa Maria walikuwa mabwanyenye katika mitaa ya kifahari Dhahiri shahiri kuwa haingekosa kuwa yule alikuwa mwajiri wake. Hakutaka mwalimu ajue hivyo licha ya kuwa hisia zake zilidhihisha mengi.

Mwishowe waliagana kwamba Pendo alipaswa kusauriwa na mwalimu na angeripoti katika ofisi ya mwalimu kila alasiri. Pia alipaswa kuadhibiwa kwa kosa lake la kutoroka na ashauriwe barabara na mwalimu kabla ya kwenda kulala.

  1. Magari yalijaa pomoni kwa nini?
    1. Ilikuwa siku ya kurudi shuleni
    2. Ilikuwa asubuhi
    3. Ni kawaida ya magari kujaa
    4. Ulikuwa mwisho wa mwezi
  2. Pendo alirudi shuleni
    1. kwa hiari yake
    2. siku ya kufungua shule
    3. kwa furaha mpwitompwito
    4. shingo upande
  3. Pendo alikuwa nyumbani kwa sababu
    1. ulikuwa mwisho wa mwezi
    2. ulikuwa wakati alikizo 
    3. alitumwa nyumbani kwa utovu wa nidhamu
    4. alitaka kuja shuleni ma mzazi wake
  4. Maisha ya baadaye ni maisha gani?
    1. Maisha ya kisogoni
    2. Maisha ya masomo
    3. Maisha yajayo
    4. Maisha ya furaha
  5. Pendo alisomea shule ya aina gani?
    1. Ya malazi
    2. Ya wavulana na wasichana
    3. Ya wasichana pekee
    4. Yakutwa
  6. Kwa nini Musa hakutaka wazazi wote wahusike kutafuta suluhisho?
    1. Wazazi wa Maria hakujulikana
    2. Walikuwa ndio waajiri wake
    3. Wangetumia wakati mwingi
    4. Wazazi wa Maria walikuwa bwanyenye
  7. Neno bwanyenye lina maana gani?
    1. maskini hohehahe
    2. mti anayeajiri wengine
    3. mtu mkubwa serikalini
    4. Mtu mwenye mali mengi
  8. Pendo alikuwa amefanya kosa gani?
    1. Hatujaambiwa
    2. Kupigana
    3. Kutoroka shuleni
    4. Kupendana ma Maria
  9. Ni jambo gani Pendo alipaswa kutenda?
    1. Kusauriwa kila siku
    2. Kuadhibiwa
    3. Kutumwa nyumbani 
    4. Kuachana ma marafiki wote
  10. Hisia za Bwana Musa zilidhihirisha nini?
    1. Kwamba mtoto alikuwa na shida
    2. Kwamba alimjua mzazi wa Maria
    3. Kwamba Pendo alikuwa hajafanya kosa
    4. Kwamba mtoto angeadhibiwa

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 had 50.

Ni wazi kama jua la mtikati kuwa demokrasia katika nchi yetu ya Kenya imekua kwa kiwango kikubwa. Bila shaka hili ni suala la kujivunia kwani inamaanisha kuwa tunaenda na wakati. Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu wenyewe. Tangu tulipojinyakulia uhuru yapata miongo mitano iliyopita, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika ulingo wa kisiasa.

Rais wa kwanza wa taifa letu tukufu hayati Mzee Jomo Kenyatta aliposhika hatamu za uongozi, alihakikisha kuwa amewaunganish wananchi wote wa taifa hili na kuwapa sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao. Aliasisi falsafa ya Harambee ambao ulikuwa mwito wa kuwahamasisha wananchi kushirikiana na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja. Mwito huo ulileta ari na mshawasha kwa wananchi wa Kenya na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi yao.

Aliposafiri kwa njia ya marahaba mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, hayati rais Daniel Toroitich Arap Moi alishikilia uzi huo huo na kuanzisha mwito wa Nyayo ambao ilimaanisha ya kuwa angefuata nyayo za mtangulizi wake na kuhimiza Wakenya kuishi kwa amani, upendo na umoja.

Hayati Rais Moi alikaa kwenye kiti cha enzi liwa miaka ishirini na minne. Ijapokuwa hakuna kapa isiyokosa usubi, alifanya mengi ya kujivunia pia. Hatimaye Rais Mwai Kibaki ambapo Kenya ilijipatia Katiba mpya ambayo hadi sasa imebadilisha sura ya uongozi katika nchi yetu. Kuna mabadiliko mengi ambayo yamejidhihirisha waziwazi hususan katika ulingo wa kisiasa, siyo jinsi mambo yalivyokuwa katika miaka ya awali.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa, wakati wa uchaguzi mpiga kura atahitajika kuwachagua viongozi zaidi ya watano. Atahitajika kumchagua rais, gavana wa jimbo lake, seneta, mbunge, mwakilishi wa wanawake bungeni na mwakilishi wa baraza la jimbo. Kwa ujumla, inatazamiwa kuwa katiba hii itaibua viwango vya hali ya juu vya uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa na wale wote walio katika nafasi za uongozi.

  1. Kidemokrasia, viongozi wa serikali hupigiwa kura na kuchaguliwa na ________ wa nchi husika.
    1. wabunge
    2. watu
    3. wazalendo
    4. raia
  2. Kiongozi mkuu kabisa wa nchi ambayo ni jamhuri na huchaguliwa kidemokrasia
    1. Gavana
    2. Waziri mkuu
    3. Rais
    4. Mfalme
  3. Ni kauli ipi si sahihi kwa mujibu wa kifungu?
    1. Kenya imekuwa nchi huru kwa zaidi ya miaka hamsini
    2. Kenya ilijinyakulia uhuru wake mwaka wa hamsini
    3. Rais wa kwanza na wa pili kwa sasa hivi ni hayati
    4. Kenya tulibadilisha katiba wakati wa Rais Mwai Kibaki
  4. Katika aya ya pili, mwandishi hatudokezei kuwa
    1. Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliwapa wananchi wa Kenya sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao .
    2. Hayati Daniel Toroitich Arap Moi aliaga mwa wa elfu moja mia tisa sabini na nane
    3. Rais Moi alianzisha kauli mbiu ya kufuata nyayo za Mzee Kenyatta
    4. Mwito wa Harambee ulianzishwa 
  5. Msemo"................ Aliposafiri njia ya marahaba ........." haumaanishi? 
    1. alipoaga
    2. aliposafiri jongomeo
    3. alipofariki
    4. alipoenda na kucheza ngoma
  6. Kulingana na kifungu
    1. Hayati rais Moi aliongoza nchi ya Kenya kwa zaidi ya miongo miwili
    2. Kauli mbiu ya Harambee ilihimiza Wakenya kutoishi kwa amani, upendo na umoja
    3. Rais Kibaki alibadilisha sura ya uongozi
    4. Katiba mpya imeibua maswala mengi mazito
  7. Methali nyingine yenye maana sawa na
    "Hakuna kapa isiyokosa usubi" ni
    1. hakuna kovu la masimango
    2. hakuna masika yasiyokuwa na mbu
    3. kila shetani na mbuyu wake
    4. haba na haba hujaza kibaba
  8. Nchi ya Kenya ilipatia uhuru mwaka wa
    1. 1973
    2. 1964
    3. 1963
    4. 1978
  9. Katika aya ya mwisho tunadokezewa ya kwamba
    1. mpiga kura atapiga kura kuwachagua viongozi watano 
    2. katiba mpya itaibua viwango vya ajabu
    3. bunge litakuwa na wawakilishi wa wanawake
    4. rais, makamu wake, spika na seneta ni baadhi ya viongozi wa serikali ambao watachaguliwa wakati wa uchaguzi
  10. Neno miongoni mwa limepigwa mstari katika ufamu liko katika kitengo kipi cha sarufi?
    1. Kihisishi
    2. Kihusishi 
    3. Kiunganisho 
    4. Kivumishi

KISWAHILI INSHA

  • Soma kichwa cha insha kwa makini na uandike insha

Andika insha ya kusisimua sana ukimalizia maneno yafuatayo

....................................................................................................... Kwa kweli niligundua ya kuwa, Mungu akifunga nafasi moja, hufungua nyingine.

 

MARKING SCHEME

  1. C
  2. B
  3. A
  4. D
  5. B
  6. C
  7. A
  8. D
  9. B
  10. C
  11. A
  12. D
  13. B
  14. C
  15. C
  16. D
  17. D
  18. B
  19. A
  20. D
  21. C
  22. B
  23. C
  24. D
  25. A
  26. C
  27. B
  28. D
  29. C
  30. A
  31. D
  32. D
  33. C
  34. C
  35. A
  36. B
  37. D
  38. C
  39. A
  40. B
  41. D
  42. C
  43. B
  44. B
  45. D
  46. A
  47. B
  48. C
  49. C
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students