Thursday, 08 September 2022 08:20

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 1

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo. Viina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.. Chagua lifaalo zaidi kati ya uliyopewa

   1       siku hiyo, Karanga      2     umuhimu wa ujirani      3     . Makuu     4      yalikuwa funzo kwake. Aliufahamu ukweli kuwa      5   .       6      mtaa wa kifahari        7     aliwabeza majirani       8      Aligaagaa pale kitandani kwa maumivu ya       9    . Alipoteza fahamu.    10      macho yake, alikuwa amezingirwa na madaktari!

  A B C D
1  Tangu  Kweli  Hadi  Madhali
2  alidharau  aliukumbatia  aliudharau  aliubeba
3  nzuri  duni  mwema  mbaya
4  yaliyompiga   yaliyomsumbua   yaliyomgonga  yaliyomfika
5  mtegemea cha nduguye hufa maskini  fimbo ya mbali haiui nyoka  damu ni nzito kuliko maji  ndugu mui heri kuwa naye
6  Katika  Humo  Kule  Pale
7  aliishi  aliishia  alikoishi  alikuwa
8  wake  yake  wao  zake
9  ghafla  sasa  kali  taratibu
10  Alipovumba  Alipovumbua  Alipofumbua   Alipofunba


Migomo    11     taifa letu sana. Ule wa madaktari    12     Disemba mwaka elfu mbili na kumi na sita    13     ndio mbaya zaidi.    14     wa ajali waliohitaji matibabu ya dharura waliachwa hoi    15    wa kuwajali.

  A B C D
11   imeathiri   imeliathiri  imeliadhiri   imeadhiri
12   kwanzia  kuanzia  mnamo  tangu
13   labda  bora   ilhali  Kweli
14  Majeraha  Manusura  Majeruhi  Matapeli
15  bali  kweli  na  bila


Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu swali kulingana na maagizo.

  1. Nomino kombamwiko yaweza kuorodheshwa katika ngeli ipi?
    1. U-I
    2. A-WA
    3. I-I
    4. I-ZI
  2. Ni ala gani kati ya hizi hutumiwa pamoja na mkwiro?
    1. Firimbi.
    2. Marimba.
    3. Zeze.
    4. Parapanda.
  3. Ni sentensi gani iliyo na karibu ya  nusura?
    1. Kombo ameketi karibu na baba yake.
    2. Karibu anisukume aliponipita mlangoni.
    3. Kina Yohana ni karibu arobaini darasani mwao.
    4. Mtihani u karibu kuanza.
  4. Kitenzi shona katika kauli ya kutendua ni
    1. shonwa.
    2. shonua.
    3. shonesha.
    4. shonewa.
  5. Kamilisha methali:
    Ajidhaniaye kasimama
    1. miti yote huteleza.
    2. hafikilii mbinguni.
    3. aangalie asianguke. 
    4. huja kinyume...
  6. Chagua kauli yenye kiashiria radidi
    1. Nguo zizo ndizo za kina Rita.
    2. Mto huo huo ndio wenye mamba hatari.
    3. Tutawapelekea zawadi zizi hizi.
    4. Udongo huo nao ni wa nani?
  7. Fagio 10 001 kwa maneno ni fagio
    1. kumi elfu na mmoja.
    2. elfu kumi na moja.
    3. laki moja na mmoja. 
    4. laki moja na moja.
  8. Chagua kinyume cha; Ajuza alianika nguo jioni. 
    1. Shaibu alianua nguo asubuhi.
    2. Ajuza hakuanua nguo asubuhi.
    3. Shaibu hakuanua nguo jioni. 
    4. Ajuza alianika nguo jioni.
  9. Ni nomino gani inayoweza kuundwa kutokana na sifa -ema?
    1. Sema.
    2. Jema.
    3. Wema.
    4. Mema.
  10. Chagua sentensi yenye kivumishi cha pekee.
    1. Watu wengine hupenda kula kwa vijiko.
    2. Mtoto huyu naye ni mdogo.
    3. Abiria walioumia ajalini walikuwawanne tu.
    4. Mwanamke wa tatu kuwasilialikuwa Bi. Leo
  11. Mama alimwambia bintiye kuwa angefaulu angempa tuzo katika usemi halisi ni
    1. "Ukifaulu utanipa tuzo," mama alimwambia bintiye..
    2. “Ukifaulu nitakupa tuzo," Mama alimwambia bintiye.
    3. "Mama alimwambia bintiye,"  ukifaulu nitakuyla tuzo.
    4. “Nikifaulu utanipa tuzo," mana  alimwambia bintiye.
  12. Tambua matumizi ya ki.
    Tasha amekibeba kitoto chake.
    1. Masharti.
    2. Ngeli. .
    3. Udogo.
    4. kiwakilishi.
  13. Mama ameenda sokoni kwa wingi ni
    1. kina mama wameenda masokoni.
    2. mama wameenda sokoni.
    3. kina mama wameenda sokoni.
    4. mama wameenda masokoni.
  14. Kanusha:
    Ningepita ningetezwa.
    1. ningepita nisingetuzwa..
    2. nisingepita nisingetuzwa.
    3. nisingalipita nisingelituzwa.
    4. nisingelipita nisingalituzwa.
  15. Ni chombo gani cha usafiri kilicho tofauti?
    1. Teksi.
    2. Daladala.
    3. Lori,
    4. Meli.

Soma taarifa ifuatave kisha wilbu maswali 31 hadi 46.

             Ajira ya watoto ni kazi ambazo zinawatumia na kuwaathiri vibaya watoto kati ya miaka mitano na kumi na saba kwa namna fulani kama vile kiakili, kimwili hata kimakazi. Madhila yanayowakumba watoto katika ulimwengu wa ajira ya w duniani ni mengi.
             Sababu moja ya ajira ya watoto ni itikadi fulani katika jamii. Itikadi ni imani. fulani katika jambo fulani. Katika baadhi ya jamii, wazazi huzaa watoto wengi kwa minajili ya kuwatumia kuchuma. Wao huwalazimisha watoto hao kuajiriwa kuteka maji, kutema kuni, kufua nguo, shughuli za shambani miongoni mwa kazi nyingine nyingi. Waajiri huwapokea kwa mikono miwili kwa kuwa masharti ya kuwaajiri huwa nafinu..
             Sekta inayowaajiri watoto wengi ni ile ya nyumbani. Jambo la kusikitisha ni kuwa zaidi ya asilimia tisini ni wasichana. Hawa nao mara kwa mara hutendewa unyama na ukatili na waajiri wao. Wakati mwingine, hawalipwi mishahara.
             Duniani kuna visa vingi vya watoto kuingizwa katika shughuli za ukahaba na zile za kuchukuliwa video za ngono kwa malipo duni. Jambo hili limekithiri katika maeneo yenye shughuli za kitalii. Majiji tajika duniani nayo pia yana shughuli hizi. Isitoshe, watoto huhusishwa katika uchuuzi wa mihadarati.
             Hatari ni kuwa wasipoangamizwa na ulevi wanaouchưuza, hupoteza uhai, katika vita vya magenge. Uwezekano wa watoto hao kuambukizwa UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa huwa jw sana,
             Ni wazi kuwa njia moja na madhubuti ya kuangamiza jamii ni kuwaajiri watoto, Ustawi wa kiuchumi wa baadhi ya nchi za bara Asia unatokana na ukweli kuwa nchi hizi zinawatunza watoto wao, kizazi cha kesho, kizazi ambacho kimerithishwa elimu na maarifa ya kuendeleza na kukuza uchumi.
             Mataifa hayana budi kuungana kuzua mikakati ya kutokomeza ajira ya watoto., Hatua ya kwanza ni uongozi. Lazima serikali za nchi ziwajibike.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza, ni kweli kuwa
    1. watoto wanaoajiriwa huwa wamepita umri wa kuwa shuleni.
    2. huenda watoto wanaoajiriwa hawapotezi makao.
    3. baadhi ya watoto wanaoajiriwa hupata majeraha mwilini.
    4. ajira ya watoto huwadumisha.
  2. Madhila ni
    1. shida.
    2. maono.
    3. mawazo.
    4. maoni.
  3. Kifungu hiki hakidhihirishi kuwa 
    1. imani huchangia ajira ya watoto. kuangamizwa na
    2. ajira ya watoto ni chanzo cha mateso yao.
    3. ajira ya watoto hueneza uovu.
    4. uchumi wa nchi hukua kwa minajili ya ajira ya watoto. -
  4. Baadhi ya wazazi huwazaa watoto kwa kuwa wanawachukulia kama 
    1. mtaji.
    2. kitegauchumi. 
    3. riba.
    4. fola.
  5. Huenda waajiri wanapenda kuwaajiri watoto kwa kuwa
    1. wanataka kutumia pesa kidogo.
    2. kazi zao ni nyepesi.
    3. watoto hawana nafasi katika jamii.
    4. ni rahisi kuwalazimisha kufanya kazi.
  6. Jinsia kubwa ya waajiriwa katika kifungu hiki ni ile ya 
    1. kiume. 
    2. wasichana
    3. wavulana. 
    4. kike.
  7. Video za ngono huendeleza 
    1. maadili.
    2. uozo jamiini. 
    3. vizazi. 
    4. uadilifu.
  8. Watoto wanaochınıza dawa za kulevya  wanakodolewa macho na hatari ya
    1. UKIMWI.
    2. magonjwa mengine. 
    3. wahalifu.
    4. vita.
  9. Kuwaajiri watoto 
    1. ni kuendeleza ukuaji wa uchumi.
    2. hukosesha jamii wakuzauchumi. 
    3. hurithisha jamii uchumi ulionawiri. 
    4. ni kurithisha jamii maarifa.
  10. Methali murua kujumlishia aya ya mwisho ni 
    1. baada ya dhiki faraja. 
    2. mchumia juani hulia kivulini. 
    3. mchuma janga hula na wa kwao.
    4. kidole kimoja hakivunji chawa. 

Soma tagrifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50.

             Raha na Tele walikuwa marafiki wa chanda na pete. Urafiki wao ulishinda hata udugu. Uchungu wa mmoja aliyeuhisi ni mwenzake. Waliishi katika mtaa wa Timayo na kusoma katika shule ya Matokeobora.
             Shuleni, walifanya bidii za mchwa. Mungu aliwajalia vichwa vyepesi. Raha alikuwa hodari katika somo la Kiswahili naye Tele alikuwa mweledi katika Sayansi na Kiingereza. Katika masomo haya, hakuna aliyeweza kuwapiku. Hata hivyo, katika mtihani wa mwisho wa muhula, Raha hakufanya vizuri katika somo la Kiswahili. Mwalimu alishindwa kusoma hati yake, jambo ambalo lilimpotezea alama kumi. Mawazo yake katika insha alikuwa ameyapanga vizuri lakini tatizo lilikuwa ni kukosa kuandika kila wazo katika aya yake. Tele naye alikuwa ameanguka katika Kiingereza kutokana na makosa yayo hayo. Mwalimu alishindwa kusoma mwandiko wake mbaya.
             Bwana Busara, mwalimu wao wa darasa, aliwaita afisini mwake ili kufahamu sababu zao za kuanguka. Walikiri kuwa wangeutilia maanani mwandiko wao. Waliahidi kufanya kila wawezalo kuirekebisha hati yao. Tele aliwashangaza walimu katika chumba chao cha shughuli rasmi aliposema bayana kuwa yeye hunakili somo la Hisabati kutoka kwa wenzake. Hilo lilikuwa jambo ambalo mwalimu hakuwa amelishuku.
             Mwalimu aliwaarabia kuwa ni kosa kunakili kazi za wengine. Hatimaye, mwalimu aliwashauri wasaidiane katika masomo yote kwa kuwa kila mmoja amejaliwa kipawa tofauti.
             Wanafunzi wale walifuata ushauri wa mwalimu kwa makini. Mwisho wa muhula uliofuata, Raha na Tele walifua dafu: Waliibuka washindi na kuwa na raha tele. Hati yao ikawa ya kupigiwa mfano kote shuleni.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa Raha na Tele 
    1. hawakuwa wakiishi katika mtaa mmoja. 
    2. walikuwa ndugu.
    3. walisomea shule tofauti.
    4. walikuwa marafiki wakubwa.
  2. Aliyekuwa stadi katika somo la Kiswahili alikuwa
    1. Tele.
    2. Tele na Raha.
    3. Raha
    4. Mwalimu.
  3. Mwandishi wa kifungu anasema kuwa 
    1. ingawa Tele na Raha walifanya vibaya, waliongoza katika darasa lao. 
    2. Tele na Raha walishindana katika darasa lao.
    3. Tele na Raha walikuwa watukutu
    4. mwalimu aliwapenda sana Tele na Raha.
  4. Kwa nini mwalimu alishindwa kusoma insha ya Raha?
    1. Hati hiyo ilikuwa ndogo.
    2. Mwandiko ulikuwa mbaya.
    3. Mwalimu hakujua kusoma.
    4. Herufi zilikuwa kubwa.
  5. Ni kwa nini mwalimu Busara aliwaita Raha na Tele afisini?
    1. Alitaka kuwaadhibu.
    2. Ili ajue sababu za kuanguka kwao.
    3. Alitaka kuwafunza kuandika kwa hati nadhifu.
    4. Ili kuwatuma nyumbani.
  6. Ni jambo gani ambalo mwalimu  hakuwa amelishuku? 
    1. Tele kunakili Hisabati.
    2. Raha kunakili Kiswahili. 
    3. Tele kufanya vizuri katika Sayansi. 
    4. Raha kuanguka katika Kiswahili.
  7. Chumba kinachorejelewa katika aya  ya tatu ni 
    1. msala.
    2. sebule.
    3. majilisi.
    4. ghala.
  8. Tele alikuwa
    1. mzembe.
    2. mwaminifu. 
    3. mjanja.
    4. mkora. .
  9. Kushinda kwa Raha na Tele katika mtihanini kulionyesha wazi
    1. walipuuza ushauri wa mwalimu. 
    2. walidharau ushauri wa mwalimu. 
    3. walikuwa werevu zaidi. 
    4. walitilia maanani ushauri wa  mwalimu;
  10. Walifua dafu ni sawa na
    1. waliendelea vizuri.
    2. walifanya bidit zaidi.
    3. walifanya uamuzi
    4. walifanikiwa. 

INSHA

Andika insha inayomalizika kwa naneno yafuatayo:
Zamani kidogo katika msitu wa Patapotea wanyama waliishi kwa amani na upendo. Walisaidiana katika mambo mengi. Siku moja ...........

Majibu

  1. A
  2. B
  3. C
  4. D
  5. B
  6. A
  7. C
  8. D
  9. A
  10. C
  11. B
  12. C
  13. A
  14. C
  15. D
  16. B
  17. B
  18. B
  19. A
  20. C
  21. B
  22. A
  23. A
  24. C
  25. A
  26. B
  27. C
  28. A
  29. B
  30. D
  31. C
  32. A
  33. D
  34. B
  35. A
  36. D
  37. B
  38. A
  39. B
  40. D
  41. D
  42. C
  43. A
  44. B
  45. B
  46. A
  47. C
  48. B
  49. D
  50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students