Thursday, 08 September 2022 12:13

Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 2

Share via Whatsapp Written by
Rate this item
(6 votes)

Maswali 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15.Kwa kila pengo, umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.

Wavyele na washikadau wengine katika      1     ya elimu       2       na wazazi kuhusu     3      la kudumisha nidhamu      4    watoto wa shule. Walimu wanawanyoshea kidole cha     5    wavyele hasa baada ya       6     ya kiboko       7     nchini. Kwa upande wao, wazazi wanajitetea kuwa walimu ndio kushutumiwa maadamu wanashinda      8     watoto hawa      9     . Hata hivyo, suala la nidhamu linahusisha kila mmoja katika jamii.

  A B C D
1  shirika  taasisi   sekta  kazi
2  wamehitilafiana  wameelewana  wameulizana  wamekubaliana
3  dhima  wadhifa  juhudi  jukumu
4  dhidi ya  miongoni mwa  mbali na  zaidi ya
5  lawama  laana  baraka  ushindi
6  vita  adabu  adhabu  mapigano
7  kupigwa vijembe  kupigwa dafrau  kupigwa kalamu  kupigwa marufuku
8  kwa  na  ya  pa
9  mchana kutwa  usiku kucha  usiku kutwa  mchana kucha

 

Wakazi wengi wa mjini     10     na tatizo la uhaba       11    maji     12   . Jambo hili hufanya    13    yao kushindwa kuyatunza mazingira yao.    14    serikali ichukue hatua ya kusambaza maji kote ili kuepuka kuzuka kwa maradhi kama vile    15   .

  A B C D
10  wamekutwa  wanakabidhiwa  wanakabiliwa   wamejuzwa
11  la   ya  za  wa
12  masafi  safi  yasafi  msafi
13  baadhi  wengi   wengine  baina
14  Bora tu  Yamkini  Kama  Ni bora
15  pepopunda  kifaduro  waba  surua


Kutoka swali la 16 hadi 30. jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Tambua sentensi yenye tashbihi,
    1. Kaka yake ni msini kama usiku.
    2. Maneno yake yalikuwa msumari moto.
    3. Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona.
    4. Unywaji pombe husababisha balaa na belua
  2. Mfinyanzi ni kwa finyanga kama vile msasi ni kwa;
    1. msako
    2. saka
    3. uasa 
    4. uasi
  3. Tunasema Mkungu wa ndizi na ________ cha ufunguo
    1. kicha  
    2. kifurushi
    3. kitita 
    4. chane
  4. Andika tarakimu 100,001 kwa maneno.
    1. Laki moja elfu na moja
    2. Laki moja na moja elfu
    3. Laki mia moja na moja
    4. Laki moja na moja
  5. Alikiona kilichomtoa kanga manyoya. 
    Kiambishi 'ki' kimetumikaje katika sentensi hii?
    1. Kuonyesha masharti
    2. Kuonyesha hali ya kuendelea
    3. Kuonyesha kiwakilishi
    4. Kuonyesha udogo
  6. Ni sentensi gani yenye kihisishi?
    1. Mchezaji yule ni hodari sana
    2. Kitoto kimezaliwa chini ya mti
    3. maneno yake yaliniumiza sana.
    4. Sote tulikimbia mkikimkiki.
  7. Majira baina ya saa tisa mchana na magharibi
    1. alasiri
    2. adhuhuri
    3. mawio
    4. macheo
  8. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Dhahabu yangu haishuki bei.
    1. Macho
    2. Almasi
    3. Shamba
    4. Jiwe mtoni
  9. Chagua maelezo sahihi ya viungo vya mwili.
    1. Taya ni nyama zinazoshikilia meno
    2. Kwapa huwa chini ya bega
    3. Nyonga huwa juu ya kiuno
    4. Kisugudi ni scheinu baina ya muundi na wave
  10. Kanusha sentensi ifuatayo kwa usahihi.
    Mtoto akila sana hunenepa.
    1. Mtoto asipokula sana hunenepa
    2. Mtoto akila sana hanenepi.
    3. Mtoto akila sana huwa hanenepi.
    4. Mtoto asipokula sana huwa hanenepi
  11. Sentensi gani imetumia 'kwa' ya umilikaji?
    1. Wageni walikuja kwangu jana.
    2. Sherehe iliandaliwa kwa Maria. cha funguo
    3. Bi. arusi alikaribishwa kwa vishindo.
    4. Tulienda moja kwa moja hadi mjini.
  12. Farasi ni mnyama wa jamii ya punda. Farasi pia 
    1. elimu ya mienendo ya nyota
    2. chombo cha kufumia nyuzi
    3. anayefuga wanyama wa kupandwa 
    4. fremu ya baiskeli
  13. Shughuli yoyote ikitendwa kupita kiasi  huharibika.
    Chagua methali inayolingana na maelezo haya.
    1. Ngoja ngoja huumiza matumbo
    2. Ngoma ikilia sana hupasuka kiwambo
    3. Tamaa mbele mauti nyuma
    4. Chombo cha kuzama hakina usukani
  14. Kikembe cha papa huitwaje?
    1. Kinengwe
    2. Kitekli
    3. Kiwavi
    4. Kipura
  15. Andika katika usemi wa taarifa;
    “Tafadhali niletee miwani yangu nisome gazeti,"  babu akaniambia.
    1. Babu alimwambia ampelekee miwani yake asome gazeti.
    2. Babu aliniagiza nimpe miwani yake asome gazeti.
    3. Babu aliniomba nimpelekee miwani yake asome gazeti
    4. Babu alimwamuru ampelekee miwani yake asome gazeti

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 - 40.

               Waziri wa Afya nchini. Bwana Bora, amesema kuwa huduma za afya nchini zimeimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka iliyopita. Akiwahutubia wananchi waliokuwa wamejumuika katika, zahanati mpya ya Pona Bw.Bora alisema kuwa wizara yake imeongezea zahanati takriban mia tatu katika kipindi kifupi, hasa katika sehemu ambazo wananchi walikuwa wakitembea kwa mwendo mrefu kusaka huduma. Alisema kuwa zahanati nyingi zilizojengwa majuzi zina vifaa vya kutosha kutoa huduma za kimsingi na kukabiliana na magonjwa yanayowataabisha wananchi kama vile malaria na homa ya matumbo. Aliongeza kuwa wizara yake imejenga maabara na kutoa mitambo ya kisasa katika zahanati hizo itakayoweza uhakika wa magonjwa yanayowasumbua wagonjwa. Alisema kuwa zahanati dawa za kutosha. 
               Aliongeza kuwa wizara yake imeongezea vituo vingi vya afya ili kuwahudumia wananchi. Vituo hivi vina  mitambo iliyo na uwezo wa kupiga picha viungo vya ndani  ili kuweza kutambua magonjwa ya ndani kwa ndani  yanayowasumbua wananchi. Aliongezea kuwa kila kituo kina wodi ndogo zenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa takribani thelathini. Hii ni hatua nzuri ikikumbukwa kuwa awali hata kupata dawa ilikuwa shida jambo lililowapelekea watu wengi kufariki.
               Bw. Bora alitoa wito kwa wananchi wajitahidi kuyatunza mazingira. Hali hii itaweza kuwaepusha na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama vile malaria na homa ya matumbo. Akitoa vyandarua vilivyotiwa dawa, Bw. Bora alisema kuwa sasa idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huu imepungua sana katika maeneo megni humu nchini. Alitoa mwito wa watu hasa kina mama wajawazito na watoto walale chini ya vyandarua. Waliougua  walihimizwa  kutafuta matibabu haraka iwezekanavyo.  Aliwakumbusha kuwa matibabu ya malaria sawa na yale ya ugonjwa wa kifua kikuu na UKIMWI hutolewa bure kote nchini. Aliwahimiza  wananchi kujua vianzo vya magonjwa mbalimbali ili waweze kujiepusha nayo.

  1. Kulingana na waziri wa Afya Bw. Bora;
    1. afya imeweza kuimarishwa kote nchini
    2. watu wengi nchini watakuwa wenye afya
    3. matatizo ya kiafya yanashughulikiwa vizuri
    4. serikali itaanza kutoa huduma bora za afya
  2. Maana ya neno ‘wamejumuika' kwa mujibu wa kifungu ni; 
    1. wamefumukana
    2. wamefungamana
    3. wametandazika
    4. wametengamana 
  3. Kwa sasa, zahanati zilizopo ni; 
    1. zaidi ya mia tatu
    2. mia tatu kamili
    3. chini ya mia tatu
    4. kama mia tatu hivi 
  4. Ugonjwa wa malaria husababishwa na nini?
    1. Mbung'o
    2. Maji yaliyotuama
    3. Mbu
    4. Viroboto
  5. Malaria na homa ya matumbo;
    1. ndiyo maradhi pekee yanayohangaisha wananchi
    2. ni baadhi tu ya shida za wananchi hawa
    3. ni maradhi yanayowashika watoto
    4. ni magonjwa yasiyotibika kwa urahisi
  6. 'Mitambo iliyo na uwezo wa kupiga picha  viungo vya ndani.' Hii ni mitambo ipi? 
    1. Kamera
    2. Uyoka 
    3. Hadubini
    4. Machela 
  7. Watu wengi walifariki kutokana na; 
    1. uhaba wa hospitali
    2. ukosefu wa wodi 
    3. uhaba wa matibabu 
    4. ukosefu wa matibabu
  8. Kutunza mazingira ni muhimu kwa kuwa; 
    1. husaidia kuponya magonjwa yawezayo kuzuilika
    2. huzuia kuenea kwa ugonjwa wowote ule 
    3. hudhibiti kuenea kwa maradhi yawezayo  kuzuilika
    4. ndio njia pekee ya kutunza afya zetu 
  9. Ni magonjwa mangapi yanayotibiwa bila malipo  kwa mujibu wa makala haya? 
    1. Mawili
    2. Matatu 
    3. Yote
    4. Manne 
  10. Kichwa mwafaka kwa makala haya ni; 
    1. Huduma za afya
    2. Hotuba ya Rais 
    3. Afya bora
    4. Ugonjwa wa malaria

Yasome makala yafuatayo kisha ujibu maswali 41 - 50.

                 Hamasa hakuwa mwenda guu. Aliamua kufanya lolote ambalo lingempa posho ya siku.  Akaona bora asibague kazi. Nguo zake zilizochakaa sana na viatu vyake vilivyokuwa vimepasuka soli vingefaa sana katika  kazi nyingine. Akamwendea mwenye mikokoteni mjini kuomba afaliwe, awabebee watu mizigo kisha amlipe jioni. jioni. Akaambiwa kuwa katika dunia hii ya nipe nikupe malipo huwa ya asubuhi. Maskini Hamasa hakuwa na senti zozote. Ilimbidi kuwabebea watu mizigo katika maduka makuu kwa mikono kwa muda akiwapelekea katika vituo vya magari ili apate chochote. Hatimaye aliweza kukusanya pesa za kutosha kukodi rukwama. Msomi mwenzetu akawa hamali. 
                 Alifanya kazi hii kwa moyo wake wote, akawa akirauka alfajiri kuenda kuwapelekea wachuuzi mizigo yao sokoni. Hakusahau kumshukuru Mungu kila uchao kwa hali yake na kumwomba siku njema baadaye. 
                 Baada ya siku nyingi za kazi hii ya sulubu, mwenzetu aliweza kujinunulia suti moja na jozi la viatu akajiwekea nyumbani. Alikuwa na matumaini kuwa siku moja jua la baraka lingemwangaza. Akaendelea kuvaa magwanda ya kazi ya mkokoteni.
                 Siku moja kilitokea kisa ambacho kilikuwa mchanganyiko wa simanzi na baraka - wakati mwingine baraka hujia motoni. Alikuwa ameiburura rukwama yake nzito kwa msaada wa kijana mmoja aliyekuwa akishirikiana naye wakati ambapo mizigo ingekuwa mizito zaidi. Walikuwa wamechoka niki. Mara likatokeza gari moja la kifahari, likakosa mwelekeo likaugonga mkokoteni na kuwaumiza vibaya. Mwenzetu hakujua lililofuata.
                 Alipozinduka, alijikuta hospitalini baada ya siku kadhaa. Alikuwa kavunjika mguu wa kulia na mkono wa kushoto. Juu ya dawati lake aliziona nakala za vyeti vyake vya chuo ambavyo daima alivibeba mfukoni
                 Vilikuwa vimechakazwa na wingi wa damu iliyommwagikia wakati wa ajali ile. Alimwona msukuma rukwama mwenzake katika kitanda kingine upembeni. Karibu naye pia walikuwa mahamali wenzake waliomzuru kumjulia hali. Pia alikuwepo mtu mmoja aliyeonyesha wazi kuwa ukwasi ulikuwa umemwota si haba.
                 Mtu yule alimpa pole na kujitambulisha kwake kuwa yeye ndiye aliyemgonga Hamasa. Ni jambo lililomhuzunisha sana. Ila alikuwa na jingine. Alinhakikishia kuwa angelipwa fidia na shinika lililomkatia bima. Pia alimweleza kuwa yeye alikuwa mkurugenzi wa shirika kubwa zaidi nchini lisilo la kiserikali. Alivichukua vyeti vya Hamasa na kuvikagua. Akamwomba akavidurusu. Alipovirejesha, akajiendea zake na kuahidi kurudi baadae. Japo alikuwa akishetasheta, mkurungezi yule alikuwa pale na hakikisho. Alitabasamu, akamkabidhi barua iliyomwatua moyo kijana yule - yaliyoandikwa yalikuwa ya kuacha kinywa wazi. Alikuwa ameajiriwa tayari kama meneja mkuu wa shirika lile. Hii ndiyo kazi aliyokuwa arneisomea chuoni. Alikuwa aripoti kazini baada ya miezi miwili, muda uliotosha kupona kwake.

  1.  'Hamasa hakuwa mwenda guu' ndiko kusema;
    1. alikata tamaa
    2. hakufa moyo
    3. hakutembea kwa miguu
    4. alikuwa na masomo ya juu
  2. Hamasa alimwendea mwenye mikokoteni kwa lengo la;
    1. kuomba kazi ya uhamali
    2. kukopeshwa mkokoteni
    3. kumweleza matatizo yake aliyopitia
    4. kupewa mkokoteni ili alipie kodi baadaye
  3.  Anayebeba mizigo kwa rukwama ni hamali ilhali muuzaji maji ni;
    1. mzegazega
    2. mchuuzi
    3. mwanamaji
    4. dalali 
  4. Jambo alilozingatia sana Hamaşa maishani ni;
    1.  kurauka mapema na kujihurumia maishani
    2. kuwafaa wengine na kuomba maishani
    3. kushukuru kwa hali yake na kuomba neema
    4. kuomba asubuhi na kuwashukuru wateja
  5. Hamasa alinunua suti na viatu kwa kuwa;
    1. alivihitaji wakati asipokuwa kazini
    2. alitarajia kuvitumia baada ya kuneemeka
    3. alitaka kuwa tofauti na mahamali wengine
    4. angevihitaji atakapowatembelea wazazi
  6. 'Wakati mwingine baraka hujia motoni'
    Kifungu hiki kinaeleza kuwa;
    1. baraka huja matumaini yakiwa hafifu
    2. baraka huwaendea waonekanao duni
    3. baraka huwafuata wenye imani kubwa 
    4.  baraka huja kwa njia inayodhaniwa kuwa ya taabu
  7. Gari lililomgonga Hamasa lilikuwa;
    1. shangingi
    2. kachara
    3. karandinga
    4. rukwama
  8. Mzee mkwasi alionyesha kuhuzunishwa na;
    1. hali mbaya ya Hamasa
    2. ajai aliyoisababisha
    3. damu kwenye vyeti
    4. kutomakinika barabarani
  9. Mafanikio ya Hamasa yanaweza kuelezwa na  methali kuwa;
    1. mgaagaa na upwa hali wali mkavu
    2. dawa ya moto ni moto
    3. Mungu akiziba hapa huzibua pale
    4. dau la mnyonge haliendi joshi
  10. Maana ya neno 'a kishetasheta' kulingana na  muktadha ni;
    1. alitetemeka sana 
    2. akienda kwa mkongojo kwapani
    3. akichechemea
    4. akijikokota 

INSHA

Andika insha ya kusisimua inayohusu methali hii;
MCHUMIA JUANI HULIA KIVULINI.

Majibu

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. C
  7. D
  8. B
  9. A
  10. C
  11. D
  12. B
  13. A
  14. D
  15. C
  16. A
  17. B
  18. A
  19. D
  20. C
  21. B
  22. A
  23. C
  24. B
  25. D
  26. A
  27. D
  28. B
  29. A
  30. C
  31. C
  32. B
  33. D
  34. C
  35. B
  36. B
  37. D
  38. C
  39. B
  40. A
  41. B
  42. D
  43. A
  44. C
  45. B
  46. D
  47. A
  48. B
  49. C
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 7 End Term 2 2022 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 1742 times Last modified on Thursday, 08 September 2022 13:16

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.