KISWAHILI
DARASA LA 8
MWISHO WA MUHULA WA 2
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.
Nchi 1 Kenya hujivunia umoja na 2 wa hali ya juu. 3 kuna makabila mengi, lugha ya Kiswahili 4 na wakenya wa makabila mbalimbali ili 5 Vilevile wimbo wa taifa, michezo na bendera ya taifa husaidia 6 magugu ya ukabila na chuki. Kila binadamu, bila 7 kabila wala lugha yake, ana umuhimu mkubwa. Tunapoishi 8 amani na umoja, bila shaka uchumi wetu utaimarika Ni vyema kukumbuka kuwa 9
- A.la B.ya C.mwa D. kwa
- A. mgawanyiko B. utengano C. utangamano D. vurugu
- A. Ingawa B. Licha ya C. Lakini D. Hata hivyo
- A. hutangazwa B.husomwa C. huandikwa D. hutumiwa
- A. kuwastawisha na kuwalenga
B. kuwadunisha na kuwajenga
C. kuwaunganisha na kuwatambulisha
D. kuwahamasisha na kuwalinganisha - A. kupanda B. kupalilia C. kung'oa D. kunyunyizia
- A. kujua B. kujali C. kuthamini D. kutambua
- A. katikati B. kwa C. ndani ya D. kwenye
- A. umoja ni nguvu utengoni ni udhaifu
B. chururu si ndondondo
C. akiba halozi
D. haba na haba hujaza kibaba
Kijana 10 aliketi pale 11 baada ya hakimu kuamua kwamba afungwe kwa miaka kumi. Alifungwa kwa sababu ya utapeli 12 aliufanya akitumia simu. Pesa hizo za wizi zilimtajirisha hadi 13 katika jumba la kifahari. 14 siku yake ya arubaini ilikaribia, nayo ilipofika alikula 15 kwelikweli.
- A. yeyote B. ambaye C. mwenye D. mwenyewe
- A. gerezani B. rumande C. kizimbani D. chupani
- A. ambao B. ambayo C. ambalo D. ambaye
- A. akahama B. akaguria C. akahamishwa D. akagurisha
- A. Kumbe B. Pengine C. Kwa sababu D. Labda
- A. njama B. nyama ya ulimi C gumzo D. kalenda
Kuanzia nambari 16 mpaka 30. jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.
- Chagua orodha yenye vielezi vya idadi pekee.
- mmoja, wengi, wachache
- polepole, vizuri, haraka.
- mapema, asubuhi, jana,
- sana, tena, aghalabu.
- Maneno yafuatayo yatakuwaje katika kamusi kuanzia la kwanza hadi la mwisho?
- Bahati
- Babaika
- Bahari
- Baidika
- (iii), (i), (iv). (ii)
- (i), (iv) (iii) (i)
- (ii).(iii) .(i) (iv)
- (ii), (iii), (iv), (i)
- Ni orodha ipi yenye nomino za ngeli ya YA-YA pekee?
- maji, mate, mapishi.
- mazingira, mapishi, malezi.
- magonjwa, maumbo, maisha.
- manukato, mafuta, maradhi.
- Sentensi gani iliyo sahihi kati ya hizi?
- Mbuzi wowote watachinjwa kesho.
- Kitabu chenyewe kiliandikiwa ni chake.
- Nguo ile ingine itafuliwa
- Gari jeupe ni ya mwalimu.
- Chagua sentensi iliyotumia ki kuonyesha wakati endelezi.
- Ukienda nyumbani uniambie.
- Mbuzi alikuwa akilala fisi alipompata
- Watoto walimwona alipotembea kijeshi
- kijibwa chake kimepotea.
- 'Mawazo, hasira, furaha' ni mifano ya nomino za aina gani?
- Nomino za pekee
- Nomino za dhahania .
- Nomino za kawaida
- Nomino za wingi.
- Tambua sentensi ambayo inaonyesha istiara kati ya hizi.
- Wageni wote waliowasili ni malaika
- Mji ule ulimpokea kwa mikono miwi
- Wazazi wamekaa nyumbani wakisubiri watoto wao wachanga wawanunulie chakula
- Watu walijaa uwanjani hadi nafasi ya nzi kutua ikakosekana.
- Chagua ukanusho wa sentensi: Kitabu kilichopotea kimepatikana.
- Kitabu kilichopotea hakikupatikana.
- Kitabu kisichopotea hakijapatikana
- Kitabu kisichopotea hakikupatikana
- Kitabu kilichopotea hakijapatikana.
- Neno gani lililo na silabi nne kati ya haya?
- Potelea
- Lala
- Mbuzi
- Mbaya
- Chagua sentensi inayomaanisha kuwa Musa hakuchelewa kazini kwa kuwa aliamka mapema
- Musa asingechelewa kazini angeamka mapema
- Musa asingeamka mapema angechelewa kazini
- Musa angeamka mapema angechelewa kazini.
- Musa angechelewa kazini angeamka mapema
- Maelezo gani ambayo si sahihi kuhusu neno shinda?
- Kuwa na ugumu wa kutendeka.
- Ni kuwa wa kwanza katika mashindano.
- Ni kukaa mahali mchana wote.
- Ni dhiki au matatizo
- Sentensi ipi iliyotumia kiunganishi kwa usahihi?
- Maadamu alimshauri vizuri hakufaulu.
- Ilhali mtoto ameanguka hajalia.
- Umeshindwa kununua baiskeli sembuse gari!
- Minghairi ya kununua gari alisafiri haraka
- Chagua orodha yenye aina za mashain pekee.
- Utenzi, mizani, kibwagizo
- Ngojera, tarbia, utenzi.
- Ukwapi, utao, mwandamizi.
- Mwanzo, mloto, mleo.
- Tambua sentensi iliyotumia kivumishi cha idadi ya nafasi katika orodha
- Mwanafunzi wa pili anajua kuogelea.
- Madawati mengi yamepakwa rangi
- Mama amenunua marinda mawili.
- Mipira michache imenunuliwa.
- Wakati wa macheo, jua huwa upande gani wa dira?
- Mashariki
- Magharibi
- Kaskazini
- Kusini
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kutoka 31 hadi 40.
Ni nani mwenye akili razini awezaye kupata hata lepe la usingizi usiku kama huo? Niligaagaa kitandani huku nimetawaliwa na kiwewe na wasiwasi uliopiku ule wa mwasi. Niliwaza na kuwazua jinsi siku iliyofuata ingekuwa keshoye, ilikuwa siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa gatuzi letu Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa gavana wetu kufumwa na mvi wa manaya katika ajali ya barabarani. Bila shaka, hakuna aliyetarajia kwamba ningekuwa nambari ya pili, sembuse nambari ya kwanza? Ilikuwa wazi kama pengo kuwa ningeburura mgwisho. Tangu lini mja asiyekuwa na misuli ya kihela akaibuka mshindi katika kinyang'anyiro chochote cha uchaguzi? Licha ya kuwa mkata aliyekatwakatwa na ukata, nilitoka katika kabila lenye watu wachache mno.
Asubuhi ilipofika, nilichukua baiskeli yangu na kuiendesha polepole huku wafuasi wangu wakinishangilia nilipopita. Tuliwasili katika ukumbi wa kaunti ya Ingusi, ambapo matokeo ya uchaguzi huo yangetangaziwa. Ukumbi huo ulijaa sisisi ya watu wake kwa waume, wazee kwa vijana, waliosoma kwa wasiosoma. Mashangingi ya wapinzani wangu yalikuwa yameegeshwa pale nje. Maafisa wa polisi walizunguka hapa na pale ili kuhakikisha kuwa hakuna uhalifu uliotokea.
Afisa wa tume ya uchaguzi alipokichukua kinasasauti, kila mtu alitulia tuli kama maji mtungini. Kimya cha makaburini kilitanda kote, hata unywele ungedondoka chini ungesikika kama mlipuko wa bomu katika ukimya huo, afisa huyo alikoroma na kupasua ukimya uliokuwa umetawala. "Mshindi wa uchaguzi huu ni Amani Mlachake". Wote walionipinga waliduwaa kama mja aliyedungwa sindano ya ganzi. Wengine wote waliokuwa wakigombea kiti hicho walidhani kuwa walikuwa katika ndoto mbaya. Rafiki yangu Nyangweso na kundi lake la watumbuizaji walianza kupiga isukuti. Akina mama walisakata densi ya mabega yao. Vijana wenzangu waliniinua juu kwa furaha. Sherehe na shangwe hizo zilifanyika bila kujali mipaka ya ukabila.
Hewaa! Jua la mabadiliko lilikuwa limechomoza. Hiyo ilikuwa siku mpya. Tofauti na hapo awali, uchaguzi wa kiongozi ulikuwa umefanyika bila kuzingatia kuwa mkono mtupu haulambwi. Wale waliodhani kuwa wangechaguliwa madhali walikuwa wakiwarambisha wapigakura asali walinamisha vichwa vyao kwa tahayuri Walikuwa wamekula inwande. Aidha, waliokuwa wakijipiga kifua kuwa kiongozi alichaguliwa kwa kuegemea dhana ya ukubwa wa kabila lake waliinamisha vichwa na kujiendea zao.
Niliutuliza umati uliokuwa umepandwa na jazba. Hamrerehamrere na chereko zilipotulia, nilichukua kinasasauti ili niwashukuru raia walioniunga mkono. "Ninawapa shukrani za dhati kutoka sakafuni pa mtima wangu. Ninawakumbusha kwamba ahadi zote nilizowapa hazikuwa ahadi za Kiswahili. Vilevile, ninawapa shukrani kwa uzalendo wenu. Shughuli za uchaguzi zilifanyika bila fujo wala vurugu. Hata baada ya mshindi kutangazwa, sijaona visa vya uharibifu wa mali kama hapo awali. Nyinyi ni mashujaa na wazalendo kindakindaki."
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza:
- msemaji alishindwa kulala kwa kuwa hakujua kama matokeo ya uchaguzi yangetangazwa
- msemaji hakutarajiwa kuwa nambari ya pili bali ya kwanza
- watu walitarajia kuwa msemaji angekuwa wa mwisho katika uchaguzi
- msemaji alikuwa tajiri aliyetoka katika kabila la watu wachache mno.
- Juhudi za msemaji kuwa kiongozi zilikumbwa na changamoto gani hasa?
- Umaskini na ukabila
- Ufisadi na utepetevu
- Utapeli na unyanyapaa
- Ukata na utapeli
- Nahau zifuatazo zina maana sawa na 'kufumwa na mvi wa manaya' ila
- kukata kamba
- kuaga dunia
- kuacha mkono
- kuenda nguu
- Maneno, hata unywele ungedondoka chini ungesikika kama mlipuko wa bomu ni mfano wa Tani yani ya lugha?
- tashbihi
- istiara
- chuku
- tanakali
- Matokeo ya uchaguzi yalipotangazwa
- kila mtu alifurahia matokeo
- kila mtu alienda nyumbani
- watu wengi walifurahi lakini wengine hawakuamini
- watu wote walimwinua msemaji kwa furaha.
- Maneno, hiyo ilikuwa siku mpya' yana maana kwamba ilikuwa siku ya
- uchaguzi
- mabadiliko
- sherehe
- matokeo
- Kulingana na aya ya nne, ni kweli kuwa
- jua lilipochomoza lilileta mabadiliko
- uchaguzi huo ulikuwa tofauti na wa siku za awali
- watu walishindwa kuulamba mkono mtupu
- ushindi wa msemaji ulifanya watu wajipige kifua
- Ufahamu huu unatufundisha kwamba:
- tusiogope kujaribu jambo hata kama hali ni ngumu
- tuheshimu watu wa makabila yetu kushinda wa makabila mengine
- tuchague viongozi ambao wana pesa pekee
- watu ambao hawana pesa hawawezi wakafaulu katika jambo lolote.
- Kwa nini msemaji anawashukuru wapigakura katika aya ya mwisho?
- Walimpigia kura vizuri.
- Waliungana kusherehekea ushindi wake
- Walipiga kura kwa amani bila fujo wala vurugu
- Walifanya kazi kwa bidii na umoja
- Kulingana na mwandishi, alipanga kuzingatia methali gani katika aya ya mwisho?
- Jitihada haiondoi kudura.
- Dau la mnyonge haliendi joshi.
- Mkono mtupu haulambwi.
- Ahadi ni deni na dawa ya deni ni kulipa
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Ukeketaji ni dhuluma ambayo huendelezwa na baadhi ya jamii humu nchini. Licha ya serikali kujifunga kibwebwe ili kukabiliana na jinamizi hili, bado linatishia kuendelea kuharibu mustakabali wa vijulanga wa kike humu nchini. Kuna viongozi wa kidini hapa nchini ambao huegemea mila na desturi za jadi katika jamii na ambao kisiri huunga mkono ukeketaji, hivyo basi kuhujumu vita dhidi ya ukeketaji. Pia hali ni tofauti kabisa ambapo shughuli hiyo ambayo zamani iliendeshwa kisiri vichakani hasa huko mashinani, leo hii imekuwa ni biashara ya faida na ambapo kuna wauguz ambao hulipwa ili kukeketa katika usiri wa vyumba vya kifahari na pia katika hospitali
Aidha, kuna wakuu wa kiusalama ambao wamethibitisha kuwa wauguzi wengine wamejiunga na wale ambao wamekataa katakata kutupilia mbali tohara ya wanawake katika jamii. Wengi wac wanachochewa na tamaa ya kujipa pato. Hii ni ithibati ya kutosha kuwa umaskini ni mojawapo ya vizingiti vikubwa katika vita dhidi ya ukeketaji. Hata hivyo, si umaskini tu bali pia unyama. Unyama huu unatokana na ukweli kwamba ukeketaji huu una madhara si haba kwa yule anayekeketwa. Kwa hivyo, mtu anayethamini hela anazopewa kushinda maslahi ya mwenzake ni mwovu anayefaa kutiwa mbaroni na kuozea katika jel
Uchunguzi wa hivi karibuni umedhihirisha kuwa idadi kubwa ya wale waliokumbatia ukeketaji huu ama hawajui madhara yake au wanajitia tu hamnazo. Kuna wale ambao kwa kupofushwa na kauli kuwa mwacha mila ni mtumwa, wanajitolea mhanga kiasi cha kuwakeketa hata wasichana ambao wangali tumboni. Ni faradhi kila mkenya afahamu kuwa njia za kitamaduni za ukeketaji zina madhara si haba. Uvujaji wa damu kiasi cha kusababisha kifo ni mojawapo tu ya athari hizo Isitoshe, ngariba alikuwa na mazoea ya kutumia kijembe kimoja kuwapasha wasichana kadhaa tohara. Hali hii ilitokea kuwa rutuba ya kukuza maangamizi.
Ukeketaji wowote ule, uwe wa kale au wa kisasa, humwathiri mhusika kisaikolojia. Dhuluma hii huweza kumfanya mhusika huyo asijichukie tu bali pia jamii nzima iliyochangia kumletea madhila. Baadhi ya wale waliopitia ukatili kama huu, wasiposaidiwa kupona majeraha ya moyoni, huweza kulipiza kisasi kwa wenzao au hata kuishi maisha yaliyosheheni uchungu na maumivu ya ndani kwa ndani.
Ni jukumu la kila mkenya kutathmini faida tunazopata kutokana na mila na desturi zetu. Mila na desturi zisizokuwa na umuhimu wowote zitupiliwe mbali. Ukeketaji una faida gani? Wale waliokeketwa wanawashindia nini wale ambao hawajakeketwa? Tukilipiga suala hili darubini tutang'amua kuwa ukeketaji hauleti faida yoyote. Ni msisitizo utokao kwa wanajamii wanaodai kuwa mwacha mila ni mtumwa. Je, hawajui kuwa mwacha mila potovu ni mtume?
- Aya ya kwanza inadokeza kuwa ukeketaji
- huendelezwa na jamii zote humu nchini
- unatishia kuimeza serikali humu nchini
- unaendelea ingawa serikali imekuwa ikijaribu kukabiliana nao
- unaunga mkono kisiri viongozi wa kidini.
- Makala yanaeleza kuwa ukeketaji siku hizi;
- hauna tofauti kubwa na wa hapo awali.
- hauendeshwi kabisa huko mashinani na vijijini
- ni biashara ambayo inaleta faida kote nchini
- hufanywa kisiri hospitalini na katika majumba ya kifahari.
- Ni nini hasa kinachowafanya wauguzi wajiunge na shughuli ya ukeketaji?
- Uzalendo
- Umaskini
- Utamaduni
- Ukale
- Kwa mujibu wa aya ya pili, imebainika kwamba;
- tunafaa kuwathamini wenzetu kushinda hela tunazoahidiwa
- umaskini ndiyo sababu pekee inayoendeleza ukeketaji
- idadi ya wauguzi ambao wanaendeleza ukeketaji inazidi kupungua.
- waliopatikana wakiendeleza ukeketaji walitiwa mbaroni na kuozea jela.
- Maneno, 'wanajitia tu hamnazo' yana maana gani jinsi yalivyotumika katika kifungu?
- Wanajipeleka jela
- Wanajifanya kuwa hawajui.
- Wanajiletea shida
- Wanashirikiana na wakeketaji.
- Aya ya tatu inadokeza kuwa madhara ya ukeketaji ni;
- kifo na athari za kisaikolojia
- ugonjwa wa UKIMWI na athari za kisaikolojia
- kifo na kusambaza ugonjwa wa UKIMWI
- uvujaji wa damu na madhara ya kisaikolojia
- maumivu ya ndani kwa ndani' ni yale ambayo:
- hayana athari zozote
- yanaonekana na kila mmoja
- hayawezi yakatulizwa
- yanamtesa mtu ingawa hayaonekani
- Makala haya yanaeleza kuwa ukeketaji wa kale au wa kisasa;
- haumwathiri mhusika kisaikolojia
- hufanya mhusika asijichukie
- hufanya mhusika ajichukie na pia kuichukia jamii iliyohusika
- hulipiza kisasi kwa wenzao.
- Ili kukabiliana na ukeketaji, tunafaa
- kufunza athari za UKIMWI na kuwatia mbaroni
- kuimarisha uchumi na kufunza jamii madhara yake.
- kuonyesha jamii madhara na kuondoa umaskini
- kufunza jamii madhara ya umaskini na kuimarisha ukeketaji.
- Aya ya mwisho inabaini wazi kuwa,
- mila zinaweza zikawa na faida na nyingine zina madhara
- mila zina madhara pekee
- mila hazina faida yoyote
- tufuate mila zote za kiafrika
MARKING SCHEME
- B
- C
- A
- D
- C
- C
- B
- B
- A
- D
- A
- A
- B
- A
- D
- D
- C
- D
- A
- B
- B
- A
- D
- A
- B
- D
- C
- B
- A
- A
- A
- A
- D
- C
- C
- B
- B
- A
- C
- D
- C
- D
- B
- A
- B
- C
- D
- C
- B
- A
Download Kiswahili Questions And Answers - Class 8 End of Term 2 2021 Set 2.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students