Tuesday, 07 September 2021 11:48

Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 hadi 15, Kwa kila nafasi umepewa majibu manne, Chagua jibu lifaalo kati ya ale uliyopewa.

Wahenga ______1_______ waliposema kuwa ______2______. Watahiniwa wengi huandika insha ______3______ mithili ya vipofu pasi na kutambua _______4______uandishi wa insha. Kama yalivyo maswali mengine katika mitihani ______5______ uandishi wa insha vilevile ni ______6______ kujibiwa kwa kuzingatia ______7______ yanayotolewa kabla ya swali lenyewe. Jambo la ajabu ni kwamba, wengi wa wanafunzi huanza tu kuandika ______8______  ya kuisoma sehemu hii muhimu. Amri ya mtahini ni muhimu sana na ni sharti ifuatwe kikamilifu.

  1.  
    1. hawakukosea
    2. walikosea
    3. hawakutuandaa
    4. walituandaa
  2.  
    1. asiyekujua hakuthamini
    2. kuyumbayumba sio kuanguka
    3. mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
    4. jambo usilolijua ni usiku wa kiza
  3.  
    1. kitamaduni
    2. kilevi
    3. kipopo
    4. kijuzi
  4.  
    1. sintofahamu inayoikumba
    2. suitafahamu inayoukumba
    3. suitafahamu inayoikumba
    4. sintofahamu inayoukumba
  5.  
    1. ;
    2. ,
    3. :
    4. ?
  6.  
    1. maswali ambalo yanafaa
    2. swali ambalo halifai
    3. maswali ambayo hayafai
    4. swali ambalo linafaa
  7.  
    1. mashauri
    2. maonyo
    3. maagizo
    4. ushauri
  8.  
    1. minghairi ya
    2. sembuse
    3. maadamu
    4. mintarafu

Fisi alikuwa amezoea _______9________ kwa muda mrefu sana. Maisha yake ya kuiparamia _______10______ na wanyama wengine yalikuwa yamemshinda. Hii ni ______11______ wanyama kama simba na chui waliyateketeza mabaki ya mawindo yao. Aliamua kuanza kufanya ______12______. Alitengeneza silaha kama mishale ili kuwawinda wanyama wengine,jambo ambalo lilikuwa limepingwa vikali na mfalme wao. Tendo hilo lilikuwa ______13______. Juhudi zake ______14______ kwani mishale yake ilikuwa ______15______ na haingemudu kumfuma mnyama yeyote.

  1.  
    1. kuvuna mahali ambapo hakupanda
    2. kupanda mahali ambapo alivuna
    3. kupanda kabla ya kwenda kuvuna
    4. kuvuna mahali ambapo alipanda
  2.  
    1. vyakula vilivyoliwa
    2. mizoga iliyosazwa
    3. wanyama waliouwawa
    4. nyama zilizoliwa
  3.  
    1. kwasababu
    2. kwa kuwa
    3. kwa sababu
    4. kwa minajili
  4.  
    1. jambazi
    2. ujambazi
    3. ujangili
    4. jangili
  5.  
    1. halali
    2. lilikataliwa
    3. likiharamia
    4. haramu
  6.  
    1. hazikufua dafu
    2. zilizaa matunda
    3. hazikuambulia patupu
    4. zilifua dafu
  7.  
    1. si butu
    2. butu
    3. kali
    4. bora

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi. 

  1. Chagua sentensi isiyoakifishwa vizuri
    1. Mwanafunzi bora-aliyeongoza katika mtihani-alituzwa.
    2. Mtu anayeipenda nchi yake (kwa dhati) huitetea zaidi.
    3. Sokoni mlikuwa na matunda mengi: mapera, maparachichi na karakara.
    4. Usilijibu swali lolote," mtahini alielekeza.
  2. Tambua sentensi yenye vivumishi vya pekee
    1. Mwanariadha hodari alizawadiwa.
    2. Wageni wenyewe waliula mkate wote. 
    3. Mtu mzuri ni anayevifanya vitendo vizuri kwa kuradidi.
    4. Shuleni palikuwa na bawabu mwenye maarifa tele.
  3. Ni kitenzi gani kilichoradidiwa katika sentensi zifuatazo?
    1. Anayetembea upesiupesi hufika kwa haraka
    2. Ukiwasemasema watu utakuwa mfitini.
    3. Machungwa yale yale ndiyo yaliyoliwa.
    4. Tulitembea asteaste kuelekea madhabahuni.
  4. Bainisha usemi wa taarifa wa:
    "Wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini, "mwalimu mkuu alisema.
    1. Wanafunzi wale wale ndio waliotia fora mihanini mwalimu mkuu alisema.
    2. Mwalimu mkuu alisema kuwa wanafunzi wale wale ndio waliotia fora mtihanini
    3. "Mwalimu mkuu alisema" wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini. 
    4. Mwalimu mkuu atasema kuwa wanafunzi wale wale ndio watakaotia fora mtihanini. B.C. mgawa
  5. Neno mwanasesere ina silabi ngapi?
    1. 9
    2. 5
    3. 7
    4. 4
  6. Neni karibu limetumikaje katika sentensi ifuatayo?
    Wastaafu wote walilipwa zaidi ya karibu milioni moja.
    1. Kuonyesha nusura
    2. Kuonyesha maagano
    3. Kuonyesha umbali
    4. Kuonyesha makisio
  7. Tumia kiunganishi kifaacho.
    Ni kwa nini umenmpa funguo za nyumba yako ________________ unajua kuwa yeye ni mwizi?
    1. maadamu
    2. ilhali
    3. ingawa
    4. isitoshe
  8. Andika sentensi ifuatayo bila kirejeshi -amba
    Mfanyakazi ambaye atafanya bidii atapandishwa madaraka.
    1. Mfanyakazi afanyaye bidii atapandishwa madaraka
    2. Atakayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka.
    3. Mfanyakazi ambaye atakayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka.
    4. Mfanyakazi anayefanya kazi kwa bidii atapandishwa madaraka. 
  9. Ni upi wingi wa sentensi hii?
    Ubavu wa mnyama wangu umevunjwa na  jirani mwenye wivu. 
    1. Ubavu wa wanyama wangu umevunjwa na majirani wenye wivu.
    2. Mbavu za wanyama wetu zimevunjwa na majirani wenye wivu.
    3. Ubavu za wanyama zangu zimevunjwa na jirani wenye wivu. 
    4. Mabavu ya wanyama wetu yamevunjwa na jirani wenye wivu.
  10. Kama juzi ilikuwa Jumatano tarehe kumi na nane, mtondo itakuwa siku gani tarehe ngapi?
    1. Jumatatu tarehe ishirini na tatu
    2. Alhamisi tarehe ishirini na tisa
    3. Jumapili tarehe ishirini na mbili
    4. Ijumaa tarehe ishirini.
  11. Ni sentensi ipi yenye maana sawa na 
    Sio nadra wao hutembeleana.
    1. Wao hutembeleana mara chache
    2. Wao hutembeleana mara nyingi
    3. Si mara kwa mara wao hutembeleana
    4. Kutembeleana kwao ni adimu
  12. Ni methali gani yenye maana sawa na:
    Ngoja ngoja huumiza mtu matumbo?
    1. Asiyesikia la mkuu huvunjika glu bidii atapandishwa madaraka.
    2. Pole pole ndio mwendo D.
    3. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako
    4. Haraka haraka haina baraka
  13. Chagua sentensi iliyotumia sitiari.
    1. Maua ni sungura siku hizi.
    2. Moyo wake ulimshauri asikate tamaa.
    3. Alice alijifungua salama salimini.
    4. Ondigo ni mweusi mithili ya masizi.
  14. Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya majirani wenye wivu kutendewa
    Kaguai alienda uwanjani akaucheza mpira.
    1. Mpira ulichezwa na Kaguai uwanjani. 
    2. Kaguai aliuchezea mpira uwanjani.
    3. Mpira ulichezwa na Kaguai
    4. Uwanjani ulichezwa mpira na Kaguai.
  15. Makao ya mchwa si 
    1. kingulima
    2. kinyago
    3. lishirazi
    4. kichuguu

Soma taarifa ifuatayo kisha uiibu maswali 31- 40

Akiba ni nini? Kwa kifupi, akiba ni kitu kilichotengwa kwa ajili ya manufaa ya baadaye. Watu wanaoamini akiba huwa wanafahamu kuwa maisha yana nyuso mara mbili: wakati wa mavuno mema na wakati wa mavuno hafifu. Wanazaraa hawa wanafahamu fika kuwa kuna uwezekano wa kupata mavuno kama hayo mbeleni. Taifa linalowajali wazalendo wake huhakikisha kuwa maghala yamejaa vyakula nomi. Akiba maarufu zaidi ni ya kuhifadhi pesa benkini.

Watu wengi duniani wamebakia kuwa walalahoi kwa kutojua wala kutambua namna ya kuweka akiba. Utawasikia wengi wakisema kuwa hakiba huwekwa na waja wenye vipato vikubwa. Kabla ya kufikiria hivyo ni vyema ujue kuwa waliokuwa au walionavyo, mwanzoni hawakuwa navyo. Mtu anaweza kuweka akiba hata kama kipato chake ni cha chini kabisa. Kumbuka kuwa hakiba haiozi na kidogo kidogo hujazaa kibaba.

Wengine hulalamika eti hawawezi kuweka akiba kwani mapato yao huishia tu wanapokidhi matakwa
yao ya lazima. Hawajui kwamba iwapo wanataka kuwa na uchumi thabiti katika siku za usoni ni sharti kujinyima. Kukosa kuweka akiba eti kwa kusingizia mshahara mdogo ni kujipumbaza tu. Kuna baadhi ya watu vilevile wanaodhani kuwa wao ni wachanga zaidi kuanza kuweka hifadhi. Kuna wanaofanya mipango mizuri zaidi ya kuzitumia pesa zao lakini tamaa na uchu huwafanya tena kupotoka kabisa. Kupanga kufanya jambo na kisha ukakosa kulitekeleza ni kupoteza muda. Utawaona watu wanalipwa mshahara, wanatumia kila kitu na kuendelea kufanya kazi kungojea mshahara mwingine. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara bila kupiga hatua.

Ni jambo la busara sana kuanza kuweka akiba kutoka utotoni. Akiba hizi zinaweza kufanywa kwa njia ayami. Mwanzo mtu anaweza kuwa na mkebe mdogo uliotengenezwa kwa njia ya kipekee. Mkebe huo huwa na kishimo kidogo kinachomwezesha mtu kuweka pesa bila kutoa. Njia nyingine ni kuwa wazazi au walezi wao kuwawekea. Wazazi na walezi wanaweza kuwafungulia watoto wao akaunti kwenye benki. Kuweka pesa benkini ni bora zaidi kuliko akiba nyingine zozote. Hii ni kwa sababu ya ulinzi wa pesa pale benkini. Isitoshe, pesa zinazowekwa kwenye benki huzaa riba. Vilevile pesa hizo zinaweza kuwekezwa kwa njia ambazo faida zitaonekana na mtoto mwenyewe. Mtoto anaweza kununuliwa mifugo kama vile; kuku, sungura, mabata ambao watazaana na kumletea mtoto faida zaidi.

Mtoto anapoona kuwa pesa zake zinaweza kuendelea kuzaa huwa na motisha wa kuendelea kuweka
akiba. Mwana akilelewa kwa tamaduni hizi za kuwekeza, kamwe hataacha hata akiwa mtu mzima. Atakuwa na mshawasha wa kuendelea kuzalisha milele. Kuweka akiba kutoka utotoni humfanya mtoto kuwa na pesa za kutosha hata kuyaendeleza masomo yake bila kutegemea wafadhili. Huku ndiko kujitegemea. Mtu anayejitegemea huishi maisha ya amani na raha mstarehe.

Je, wewe tayari una akiba au utaanza kuweka leo? Kumbuka kuwa kuweka akiba ni ishara kubwa zaidi ya kuwa na nidhamu.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza,
    1. akiba muhimu zaidi ni za vyakula vya wakulima
    2. akiba huwekwa baada ya kupata mapato mengi
    3. mtu anafaa kuweka akiba hata kama mapato yake ni finyu
    4. maisha kamwe hayana nyuso mbili
  2. Ni kwa nini watu wengi wameishia kuwa maskini kulingana na taarifa uliyoisoma?
    1. Mapato yao ni machache
    2. Wanafahamu fika maana ya kuweka akiba
    3. Wanachelea kuweka akiba wakidhani hawana vya kutosha
    4. Walalahai wameyachukua mapato makubwa wakawamalizia
  3. Chagua methali iliyo kinyume na methali iliyotumiwa katika sentensi ya mwisho wa aya ya pili
    1. Chururu si ndo! ndo! ndo!
    2. Papo kwa papo kamba hukata jiwe 
    3. Haba na haba hujaza kibaba
    4. Mchumia juani hulia kivulini
  4. Serikali inawezaje kuwahakikishia watu wake uthabiti wa kiuchumi kulingana na ufahamu?
    1. Kuwashauri watu wake kuweka akiba
    2. Kuwalazimisha wananchi wake kuweka akiba
    3. Kuwapa wananchi wake mapato makubwa ili waweke akiba
    4. Kuwawekea wananchi wake vyakula vya kutosha kwenye maghala
  5. Watu wengi hawapendi kuweka akiba kwa sababu zote hizi ila
    1. wanadhani kuwa mapato yao hayatoshi
    2. wanaona kuwa umri wao ni mdogo mno 
    3. wanafanya mipango mizuri lakini hawaitekelezi 
    4. mapato yao yanawaruhusu kuweka akiba ndogo mno
  6. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara... Ni tamathali gani ya lugha iliyotumiwa hapa?
    1. Tashbihi
    2. Methali
    3. Istiara
    4. Semi
  7. Ni ijambo lipi linalowazuia watu wenye mipango mizuri kuweka akiba?
    1. Mipango yao huwa na kasoro fulani.
    2. Wanayapangia mapato bila kufahau kuwa hayatoshi
    3. Mshahara wao mdogo kukosa kuwaruhusu kuitekeleza mipango yao
    4. Hulka zao za kuvitamani sana vitu vingine
  8. Kati ya mbinu zifuatazo, ni mbinu gani si bora
    1. Kuweka pesa kwenye mkebe maalum
    2. Kuwapa wazazi wao pesa wawawekee
    3. Kuzitumia pesa ili kukirimia matakwa yao
    4. Kuweka pesa kwenye akaunti za benki
  9. Ni kwa nini mtu anafaa kuanza kuweka akiba akiwa na umri mdogo?
    1. Atakuwa tajiri kwa haraka mno
    2. Atakuwa na utamaduni huo maishani
    3. Pesa zake zitakuwa maradufu
    4. Mtu hahitaji kujipanga akiwa ameweka akiba
  10. Mtu anayepoteza kazi yake ilhali ameweka akiba;
    1. atakuwa mtegemeaji wa wengine
    2. anaweza kuanzisha biashara
    3. ataanza kuweka akiba kidogo kidogo
    4. ataweza kwenda ziarani kujivinjari na familia

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 41-50

Nyanya Matinda alikuwa ametualika twende kumsalimia. Mwanzo aliwauliza wazazi wetu iwapo sote tungepatikana wakati wa sikukuu ya Krismasi. Wengi waliitikia ualishi huo isipokuwa shangazi ambaye aljitetea kuwa binamu yetu Juma angekuwa na shughuli muhimu chuoni. Baada ya majadiliano ya kina na watu wote wa ukoo, uamuzi ulitolewa kuwa twende kumtembelea wakati wa kiburunzi.

Mimi sikuwa nimemwona bibi huyu kwa zaidi ya nusu mwongo. Nilikuwa na mchanganyiko wa furaha na maswali. Furaha kwa kuwa ningepata nafasi ya kuzuru watu wa nyumbani na maswali ya kujua tuliloitiwa. "Je, nyanya anataka kuishia ahera ama vipi? Niliwaza na kuwazua. Nilitaka kuingojea siku hiyo ili nijue dhahiri shahiri. Bibi alikuwa ametayarisha kuchinja ndume wake kuwa kitoweo chetu.

Kufikia saa tisa alasiri tarehe thelathini na moja Desemba, kila mmoja alikuwa amewasili. Mimi ndimi niliyefika karibu wa mwisho. Nilipofika kwa nyanya nilishangazwa na wingi wa watu. Ukweli ni kwamba, singewajua wala kuwatambua wote. Wengi walikuwa ajinabi machoni pangu. Kulikuwa na harufu nzuri ya vyakula hewani. Nilianza kudondokwa na mate bila kujua. Punde si punde, tuliombwa na ami mkuu tuingie ndani sote. Nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ya sebule. Tulimezwa sote na hakukuwa aliyetapikwa hata mmoja. Ilikuwani nyumba ya kisasa iliyojengwa kwa teknolojia mpya.

Pale sebuleni. kila mmoja alionekana akishughulika na simu za mkononi. Wengine walikuwa kwenye mtandao, wengine wakicheza michezo, wengine wakiandika jumbe na wengine wakipiga picha almaarufu 'selfie". Mara nyanya Matinda alinyerereka asteaste na kuingia ndani. Cha ajabu ni kwamba, hakuna aliyemwona isipokuwa mimi. Wote walikuwa na shughuli. Nyanya alionekana kukasirika. Alitoka shoti na kuingia katika chumba chake cha kulala. Aliporudi alikuwa amebeba gunia. Alikohoa. Kila mmoja aliinua kichwa na kumwangalia. "Hata hamna muda wa kuzungumza mjuane? Simu..simu.simu tu! Kila mmoja aiweke simu yake kwenye gunia hili." Nyanya alifoka kwa ukali. Tulitii amri ingawa kwa shingo upande.

Sote hatukufurahia lakini tukajibu, "Pole nyanya Matinda kwa kukuudhi'"kwa kauli moja. "Ni kwa nini mmechangamkia elimu ya ulimwengu na huku elimu ya ukoo mmeipoteza? Ni kwa nini hamuwezi kuzungumza mkajuane? Hamjui kwamba dunia imeharibika siku hizi? Hamjawaona ndugu wa damu wakioana kwa kutojua? Ni kwa nini dunia hii inawapotosha wajukuu wangu? Ama nyote mnajuana?" Hapana nyanya," tulijibu kwa pamoja. "Haya hebu sasa mwangalie mwenzako," alitoa kauli nyingine.

"Ah! Wajukuu wangu, mmedanganyika na kupotoka kabisa. Hebu tazameni humu mwangu, ni kitu
gani cha kisasa ambacho hakiko? Angalieni runinga yangu na simu yangu. Hivi vyote si vya kisasa? Sasa
hebu mniambie iwapo vimenikatiza kujua watu wa ukoo wangu?" Nyanya alisimulia kwa masikitiko.
"Vyombo hivi vyote vya teknolojia ni vyema. Nyinyi ndinyi mnavitumia isivyofaa. Mimi nilipozaliwa
nilipata kuwa kulikuwa na magazeti na televisheni. Baba yangu alikuwa na kijiredio cha mbao ambacho
hakuna hata mmoja aliyeruhusiwa kukigusa." Tuliangua kicheko. "Acheni kucheka. Hata tulikuwa na
televisheni ya "Sanyo' ambayo ilionyesha rangi nyeusi na nyeupe."tulicheka tena. "Isitoshe, kijiji kizima
kilifika kwetu wakati wa Magharibi kutazama taarifa ya habari!"

Wakati huo wote tulishindwa kuzuia vicheko. Nyanya pia aliongezea kuwa baba yake alikuwa na saa kubwa sana. Saa hiyo iliyotajwa kuwa ya "Majira' iikuwa kubwa zaidi kiasi kwamba iliwekwa sakafuni.
Alidokeza kuwa saa hiyo haikutumia betri. Kila mara ungesikia ikitoa sauti kwaa krabu zake, ch! ch! ch!
Saa ishirini na nne.

Wajukuu wangu, nimemaliza mizungu. Sasa karibuni tule na tufurahie kuwa watu wa ukoo mmoja." Sinia za minofu zilianza kuletwa mezani.

  1. Familia ya nyanya Matinda ilimtembelea lini kulingana na aya ya kwanza? 
    1. Wakati wa Krismasi
    2. Mkesha wa mwaka mpya
    3. Mkesha wa Krismasi
    4. Siku yake ya kuzaliwa
  2. Ni nani aliyetoa sababu ya mwanawe kutopata nafasi tarehe kamili za awali za ualishi?
    1. Binamu yake shangazi
    2. Mtoto wa kiume wa shangazi
    3. Ndugu wa kiume wa mama
    4. Ndugu wa kike wa baba
  3. Msimulizi hakuwa amemtembelea nyanya yake kwa muda wa
    1. zaidi ya miaka mitano
    2. takribani miaka kumi na miwili
    3. zaidi ya miaka kumi
    4. zaidi ya nusu ya mwaka
  4. Unafikiri ni kwa nini mwandishi wa makala haya alifurahia baada ya kupata ualishi?
    1. Alikuwa anajiuliza sababu kuu ya nyanya kuwaita
    2.  Alidhani kuwa siku za nyanya zilikuwa zimeyoyoma 
    3. Binamu yake alikuwa na shughuli na kwa hivyo hawangeenda
    4. Angepata nafasi ya kutembea nyumbani na kuwaona watu wao
  5. Kifungu, bahari ya sebule, kimepigiwa mstari. Kinamaanisha kuwa
    1. nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ndani
    2. sebuleni palikuwa na kidimbwi kikubwa
    3. sebule ilikuwa kubwa zaidi
    4. bahari iliyokuwapo ilitumeza sote tukapotea
  6. Kulingana na aya ya nne
    1. nyanya Matinda anaonyeshwa kutoipenda mitambo yoyote ya teknolojia
    2. nyanya Matinda anashangaa ni kwa nini wajukuu wamekuwa watumwa wa simu badala ya kujuana 
    3. nyanya Matinda anadhani kuwa simutamba huhifadhiwa kwenye gunia
    4. wajukuu wale waliziweka simu zao kwenye gunia kwa hiari
  7. Ni jambo gani linaloonyesha kuwa wajukuu wale walikuwa na heshima?
    1. Hawakuwa wanazungumziana kwa hivyo waliheshimiana
    2. Walimwambia nyanya Matinda pole baada ya kumkasirisha
    3. Walikubali kuziweka simu zao kwenye magunia kwa furaha
    4. Wajukuu wote walikuwa wamemiliki simu ya mkononi.
  8. Kifungu ulichokisoma kimebainisha kwamba elimu ya ukoo
    1. hutuwezesha kufahamu jamaa na koo zetu
    2. hutuwezesha kufahamu ulimwengu wa tovuti
    3. huturahisishia kujua elimu ya dunia
    4. haijapuuzwa na vijana hata kidogo
  9. Kauli zifuatazo zinazotolewa na nyanya zinaonyesha ucheshi isipokuwa masimulizi kuhusu
    1. kuwepo kwa magazeti yaliyosomwa na wakongwe
    2. saa kubwa ajabu ambayo haikutumia betri
    3. runinga iliyotazamwa na karibu kijiji kizima
    4. kuwepo kwa kijiredio cha mbao ambacho hakikuguzwa na yeyote
  10. Ni kauli gani iliyo sawa kulingana na makala uliyoyasoma?
    1. Elimu ya ukoo hufunzwa pamoja na elimu za dunia
    2. Hapakuwa na vyombo vya teknolojia hapo zamani
    3. Vyombo vya kiteknolojia ni vyema lakini vinatumiwa visivyo
    4. Vyombo vya teknolojia vililetwa ili kupoteza ukoo wa watu

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. C
  4. B
  5. B
  6. D
  7. C
  8. A
  9. A
  10. B
  11. C
  12. C
  13. D
  14. A
  15. B
  16. B
  17. B
  18. C
  19. B
  20. B
  21. D
  22. B
  23. A
  24. B
  25. A
  26. B
  27. C
  28. A
  29. B
  30. B
  31. B
  32. C
  33. A
  34. A
  35. D
  36. A
  37. D
  38. C
  39. B
  40. A
  41. B
  42. D
  43. A
  44. D
  45. C
  46. B
  47. B
  48. A
  49. A
  50. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students