MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo kwa makini. Vina vihasho kumi na vitano. Tumia viteuzi ulivropewa i kuchagua libiilifaalo zaidi kuiania vihasho.
Uwanjani _1_ palijaa mashabiki _2_ Walikuwa tayari kujionea mchuano _3_ timu ya Simba naile ya Dubu. Timu hizi mbili zilikuwa maadui katika mchezo wa_4_ Hivyo basi hata mashabiki_5_ timu hizi walijipata na uadui. Kwa sababu ya _6_ wao, ilibidi polisi wawe pale uwanjani kwa wingi sana. Walijaa pale ili kuzuia vurugu yoyote baina ya mashabiki na wachez wa timu hizo.
_7_ muda wa kujiandaa hapa na pale, refa alipuliza kipenga ishara kuwa mchezo ulianza rasmi. Wanatimu wa Simba walikuwa waanzilishi. Walisakata dimba kama kwamba hawakuwa na mifupa. Hata bila ya timu ya Dubu_8_ mpira, bao la kwanza lilikuwa wavuni. Wacha basi mvua _9_ ianze kunyesha. _10_ukawa mwisho wa mchezo huo.
-
- kule
- mle
- ile
- pale
-
- wengi
- mengi
- wingi
- haba
-
- Miongoni mwa
- mkabala wa
- baina ya
- ndani ya
-
- kambumbu
- soka
- kadanda
- kambubu
-
- za
- la
- ya
- wa
-
- hasira
- uhasama
- chuki
- usuhuba
-
- Kabla ya
- Baadaye
- Baada ya
- Baada
-
- kuuguza
- kuugusa
- kuuona
- kuigusa
-
- nzito
- mzito
- mazito
- Kizito
-
- Hiyo
- Hapo
- Huo
- Hicho
Nyuki ni _11_ wa ajabu sana. _12_ kuwa mkali sana na kuogopwa na binadamu, _13_ anapendwa sana na binadamu_14_ Nyuki ana uwezo wa kuua mtu. Si mtu tu lakini inaweza kuua mnyama yeyote yule hata awe simba. La ajabu ni kwamba, mdudu huyu hutengeneza asali _15_ ina manufaa chungu nzima kwa binadamu na kwa wanyama wengine.
-
- mdudu
- kimelea
- mnyama
- hayawani
-
- Baada ya
- Licha ya
- Mighairi ya
- Badala ya
-
- Kwani
- pia
- senbuse
- japo
-
- Wawa hawa
- hawa wawan
- huyuyuyu
- wawa wawa
-
- ambazo
- ambacho
- ambaye
- ambayo
Kuanzia swali la 16 - 30. jibu kila swali kulingana na maagizo
- Chagua sentensi ambayo ni sahihi.
- Maseremala waliwaokota makinda wadogo mitini.
- Seremala waliyaokota makinda madogo mitini.
- Maseremala yaliyaokota makinda madogo mitini.
- Seremala aliliokota kinda dogo mtini.
- Kuna mambo ambayo yanafaa kushughulikiwa na kurekebishwa yakiwa bado mepesi. Tukisubiri sana, huenda yakawa magumu. Ni methali ipi inayoweza kutumiwa kueleza hiki?
- Jitihada huiondoi kudura
- Maji yakimwagika hayazoleki.
- Udongo upatilize uli maji.
- Fimbo ya mbali haiui nyoka.
- Chagua neno ambalo lina silabi funge.
- Mauzo
- Maksai
- Marekebisho
- Shati
- Tegua kitendawili hiki Ninacho ila siwezi kukiona kwa urahisi.
- Goti
- Chanda
- Kisogo
- Wayo
- Chagua ukubwa wa neno dirisha.
- Jijidirisha
- Dirisha
- Jidirisha
- Kijidirisha
- Ni kipi kiwakilishi katika sentensi hii?
Lolote atakalolisema, nitalikubali kwa moyo mkunjufu.- Mkunjufu
- Moyo
- Lolote
- Kwa
- Alama hii ya kuakifisha huitwa vipi?
- Kiulizi au kisaili
- Alama ya hisi
- Parandesi
- Mabano
- Chagua orodha yenye viunganishi pekee.
- Lau, sembuse, kando ya
- Hadi, yule, chochea
- Lo! Yamkini, sana
- Licha ya, ijapokuwa, bali
- Nomino Mungu inapatikana katika ngeli ipi?
- i-zi
- a-wa
- a-a
- u-i
- Chagua nomino ambata ambazo pia ni visawe.
- Kifunguamimba - kitindamimba
- Kiamshakinywa - kifunguakinywa
- Kichinjamimba - kifunguamimba
- Kiamshakinywa - kifunguamimba
- Je, kiambishi-na-kimetumikaje katika sentensi hii?
Mwanajuma ana huzuni kwa sababu ya kumpoteza shangazi yake.- Kuunganisha sentensi
- Kuonyesha wakati uliopo
- Kuonyesha umilikaji
- Kuonyesha hali.
- Mimi ni fundi stadi wa kuunda vifaa kutoka kwa udongo. Mimi ni nani?
- Seremala
- Mfinyanzi
- Mwashi
- Mhunzi
- Pale shuleni, wanafunzi wote walikusanyika katika jumba la ili kukila kishuka
- maamkuli
- maakuli
- maankuli
- makuli
- Ni mchezo gani ambao huchezwa tu na watoto?
- Kodwa
- Riadha
- Soka
- Kuogelea
- Chagua sentensi ambayo imetoa matumizi ya kiambishi-ka-cha kusudi.
- Mgonjwa ataenda kwa daktari akatibiwe.
- "Simameni mkaimbe kwa sauti!" Mwalimu aliwaamuru wanafunzi.
- Baba alipoingia nyumbani, alioga, akaketi, akala, akasoma gazeti na akalala.
- Chakula kimepikwa kikapikika.
Soma barua ifuatave kisha mwaibu maswali 31-40
Simba Mwana Marara,
S.L.P. 675, Maskani.
12-12-2012.
Kwa sahibu Dubu,
U hali gani kaka? Maisha huko mwituni yanakupelekaje? Ni tumaini langu kuwa unaendelea vizuri licha ya kwamba unaishi msituni. Mimi niko vivi hivi tu hapa Maskani. Wenzangu pia wako lakini si wazima sana. Sote hapa tuna mengi ya kusema lakini cha umuhimu ni uhai. Naam, bora maisha.
Nina mambo mengi ya kukuambia ndugu yangu. Tangu tuachane, ninajutia sana uamuzi wangu wakukuacha kichakani ili nije kuishi na binadamu. Nilidhani kuwa maisha ya hapa Maskani yalikuwa asali kumbe wapi! Laiti ningalijua, nisingalipapia jambo hili. Kweli, ni wazi kuwa utamu wa chai si rangi. Kwanza kabisa, chakula hapa ni kama dawa. Tunapatiwa chakula kidogo sana. Huwa tunakula mara mbili kwa siku kando na kule msituni ambako tulikula hata mara nne kwa siku moja. Watoto wangu wamekonda na kukondeana utadhani wana maradhi. Mimi mwenyewe ngozi yangu imekauka kana kwamba ninaishi katika jangwa la Sahara.
Mbali na hayo, Chumba chetu kina uchafu wa ajabu. Hatuwezi kukisafisha kwa sababu tumefungiwa kama mahabusu. Tunakubaliwa tu kutoka nje usiku kwa sababu ya kazi. Naam! Kazi ya ulinzi wa boma la binadamu huyu katili. Hata tunapotolewa nje, bado huwa tumefungwa kwa nyororo nzito pale karibu na lango kuu. Wakati huu wote, huyu binadamu na jamaa zake huwa wamelala wakikoroma. Hawajali hata wakati ambapo kuna mvua au baridi ya kuzizima. Aisee! Maisha haya yamenichosha sana.
La kuhuzunisha sana ni kwamba, watoto wangu hawana uhuru wowote ule. Kila wanapozaliwa, huwa wameshapangiwa maisha yao pasi hiari yao. Wengi huuzwa kwa binadamu wengine. Tumesikia fununu kwamba kuna binadamu ambao huwafanya kitoweo na wengine huwafanya watumwa wao.
Kila nikumbukapo jinsi ulivyonikanya kuwafuata binadamu, machozi hunitiririka sana. Najuta mwenzangu. Maisha ni magumu. Magumu hata kuliko mwamba. Upatapo barua hii, ya mkini unaweza kuwaeleza ndugu zetu wengine kuhusu matatizo yangu. Waeleze kina mbwa mwitu, fisi, chui na duma. Mnaweza kusuka mpango ili mfanye mashambulizi ya kuniokoa. Mkija usiku, huenda mashambulizi haya yatafua dafu. Wasalimu wote na Mola awabariki sana. Wako wa dhati, Simba Mwana Marara
- Mwandishi wa barua hii ni nani?
- Dubu
- Maskani
- Sahibu
- Simba Mwana Marara.
- Jambo gani sahihi kwa mujibu wa aya ya tano?
- Watoto wa mwandishi hawakuwa na uhuru wowote.
- Mwandishi alikuwa amekanywa na Dubu dhidi ya kugura mwituni,
- Kulikuwa na uhasama mkubwa kati ya mwandishi na chui.
- Kuna uwezekano kuwa binadamu huwala vilebu.
- Neno wakikoroma lina kisawe kipi?
- Waking'orota
- Wakingorota
- Wakiforota
- Wakinguruma
- Gani si tatizo analopitia mwandishi?
- Kupewa chakula kidogo.
- Kubebeshwa mizigo mizito.
- Kunyimwa haki ya uhuru.
- Watoto wake kuuzwa.
- Usemi huu umetumiwa katika barua. Je, umetumia tamathali gani ya lugha? Nilidhani kuwa maisha ya hapa Maskani yalikuwa asali kumbe wapi!
- methali
- istiara
- methali
- tashbihi
- Aya ya pili imedhihirisha kuwa;
- Mwandishi anaishi katika mazingira machafu.
- Mwandishi anamhimiza inwenzake asuke mpango wa kumwokoa.
- Kabla ya kuhama mwituni, mwandishi alikataa kukubali mawaidha aliyopewa.
- Mwandishi anafurahia Maisha ya Maskani ila tu wanawe wanateswa.
- Mwenye kupokea barua hii ni nani?
- Simba Mwana Marara
- Fisi
- Chui
- Dubu
- Taja tarehe ya kuandikwa kwa barua hii.
- 12/12/2021
- 12/12/2012
- 12/12/2202
- 12/12/2002
- Eleza maana ya usemi kusuka mpango kama ulivyotumika katika ufahamu.
- Kupanga njama.
- Kutengeneza mpango kwa kutumia uzi.
- Kukaa faraghani.
- Kupiga vijembe
- Yape makala haya kichwa kifaacho.
- Uzuri wa kuyu ndani mabuu.
- Mwenda tezí na omo, marejeo ni ngamani.
- Mbwa hafi maji akiona ufuo.
- Baniani mbaya kiatu chake ni dawa.
Soma ufahamu kisha ujibu maswali yafuatayo.
Kuchubora alijipata katika panda shuka pale mjini Pendaraha. Alikuwa tu ameyakamilisha masomo ya shule ya msingi. Huo ulikuwa wakati ambao alikuwa ameusubiri sana. Akiwa shuleni, alishinda akikaidi amri na maagizo ya wazazi na walimu. Alijiona kama mfungwa aliyetaka kupatiwa uhuru. Alijiona kama nyuni aliyefungwa mbawa na alitamani sana kufunguliwa ili aruke juu angani.
Hakuwa peke yake. Wapo wanafunzi wengine waliokuwa na hamu kama yake Kuchubora. Ingawa hawakuwa na uwezo wa kufika mjini, hamu yao ilikuwa ya juu sana. Kuchubora alikuwa na shangazi ambaye ndiye angekuwa mwenyeji wake wa mjini. Alisismama pale stanini kwa muda wa dakika arobaini akisubiri shangaziye ajitokeze. Alikuwa na fikra chungu nzima. Je, dharura ingetokea ambayo ilihitajiwa tu kukimbia, Kuchubora angefanya nini? Angekimbia akielekea wapi?
Akiwa katika harakati hizo za kupambana na mawazo, alihisi mkono baridi ukimgusa begani. Alipogeuka, alimwona mwanamke mrembo akiwa amebeba mkoba mkononi. Mwanamke huyo alitabasamu na
kumwita Kuchubora kwa jina kamili. Kuchubora ingawa hakumjua, alitabasamu na kuitika. Hata bila kusemezana mawili au matatu, mwanamke huyo alimwashiria waende. Kuchubora alianza kumfuata bila kujisaili maswali yoyote. Wakavuka barabara mbili zilizokuwa na umayamaya wa watu. Hapo. Kuchubora akawa hajijui waia lajifahamu.
Alipozinduka, alijipata katika chumba kimoja katika jumba la kifahari. Jumba la mabwenyenye. Msichana wa watu kwa mara ya kwanza alidhani kwamba nyumba hiyo ilikuwa ya shangaziye. Kumbe wapi? Ghafla, mwanamke yule aliyempokea kule mjini akaingia chumbani. Kuchubora alipewa maagizo pamwe na masharti makali ambayo alifaa kuyatii kila uchao. Akatembezwa mle jumbani kwa utaratibu. Akaonyeshwa vyumba ambavyo hakustahili kuvitazama sikwambii kuingia ndani. Mahali pake rasmi palikuwa jikoni na roshani mahali pa kufulia nguo.ro
Marucrue yakamtoka machoni. Akafahamu kuwa ni dhahiri alikuwa ametekwa nyara na kufanywa mjakazi. Maisha aliyoyatamani ya mjini yakabaki ndoto tu.Alitamani ajinasue kutoka kwenye utandabui huo lakini jambo hilo lilikuwa sawa na kumkama chui. Alijuta majuto ya mjukuu. Akakumbuka wosia alioupuuza kutoka kwa walimu na wavyele wake. Akakumbuka jinsi alivyokuwa msumbufu mithili ya mkia wa mbuzi. Akakumbuka jinsi alivyowaona wanafunzi wenzake kama mazuzu wasiofahamu maisha. Sasa alikuwa ameanguka motoni. Kiburi chake kikawa sawa na cha mende ambacho hatimaye huishia motoni.
- Kuchubora aliingia mjini wakati gani?
- Alipoguswa begani na mwanamke.
- Muda mfupi tu kabla ya kuyakamilisha masomo ya msingi.
- Pindi tu alipoyakamilisha masomo ya shule ya upili.
- Baada tu ya kuyakamilisha masomo ya al shule ya msingi..
- Hoja gani ya kweli kulingana na aya ya kwanza?
- Pale mjini, Kuchubora alipewa wosia ingawa aliupuza.
- Walimu na wazazi wa kuchubora waliwajibika alipokuwa shuleni.
- Pale shuleni palikuwapo mahali pa kuwafungia wanafunzi wa tukutu,
- Kuchubora alikuwa amefungwa mbawa zake hivyo basi asingeweza kupaa.
- Mjakazi ni:
- Mfanya kazi wa kiume wa nyumbani ambaye pia huitwa kitwana
- Mtumwa wa kike wa nyumbani ambaye pia huitwa mtwana.
- Mfanyakazi wa kike wanyumbani ambaye pia huitwa kijakazi
- Mfanyakazi wa nyumbani ambaye kazi yake ni kumlea na kumtunza mtoto mdogo.
- Eleza maana ya usemi: jambo hilo lilikuwa sawa na kumkama chui
- Ilikuwa kazi ngumu ya kumkama chui.
- Kuwezekana kwa jambo hilo kulikuwa kugumu sana.
- Jambo hilo lilikuwa rahisi sana mithili ya naia wa ya chui.
- Aghalabu jamoo hilo lilitendeka.
- Kwa mujibu wa aya ya pili, ni kweli kusema kuwa:
- Ni Kuchubora tu aliyetamani kufika mjini baada ya kukamilisha masomo ya shule ya msingi.
- Kuchubora alikuwa miongoni mwa wanafunzi wengine waliotamani kufika mjini baada ya masomo ya shule ya msingi.
- Wanafunzi kadhaa akiwemo Kuchubora walifika mjini baada ya kukamilisha masomo ya shule ya msingi.
- Shangazi yake kuchubora alimpokea pale mjini.
- Aya ya tatu imedhihirisha haya yote isipokuwa:
- Kuchubora alipoguswa begani, hakuwa na mwao kuhusu aliyemgusa.
- Alipoguswa begani, Kuchubora alikuwa katika hali ya kuwaza.
- Kuchubora hakuweza kumfahamu shangaziye alipomgusa begani.
- Aliyemgusa Kuchubora begani, ingawa hakuwa mbiomba wake, alimfahamu kwa jina.
- Mahali pake rasmi palikuwa jikoni na roshani mahali pa kufulia nguo.' Hili ni thibitisho kuwa:
- Alitengewa mahali maalum ambapo asingesumbuliwa
- Kulikuwa na watu wengi mle nyumbani.
- Alipendwa sana hivyo basi akateuliwa mahali spesheli pa kuvinjari.
- Alidunishwa na kudharauliwa.
- Majina ya Kiswahili yanayotumiwa kutaja mahali au wahusika huku ya kionyesha sifa zao huitwa:
- Chuku
- Balagha
- majazi
- Uhaishaji
- Eleza maana ya neno maruerue.
- Ndoto
- Ruiya
- Jinamizil
- Hali yakuona mambo yasiyo ya kweli. 50. Methali ipi inaweza kutumiwa kama mada ya ufahamu huu?
- Jitihada haiondoi kudura
- Pema usijapo, ukipema si pema tena hadi zizini.
- Usimwage kuku penye kuku wengi.
- Ng'ombe akivunjika mguu hujikokota
INSHA
Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:
MUI HUA MWEMA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
|
|
|
|
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 2 Opener Exams 2022 Set 2.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students