Friday, 10 September 2021 08:26

Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 2

Share via Whatsapp

DARASA LA 8, MWISHO WA MUHULA WA 1
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE...............................

Soma vifungu vifuatavyo vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu munne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaulo zaidi.

  1    marafiki wote   2   kuwa nao, siwezi kumsahau Tito asilani. Yeye   3   kuainisha aina mbalimbali    4    maneno.    5    alinifahamisha kwamba maneno kama vile   6   huitwa vielezi. Isitoshe,   7   ya kushirikiana na wengine katika shughuli za kimasomo kwani   8  ,  9  nilifaidika sana kutokana na urafiki wetu.

  1. A. Baadhi ya                       B Miongoni mwa             C. Fauka ya                              D. Licha ya
  2. A. niliyewahi                       B. aliowahi                       C. niliyowahi                             D. niliowahi
  3. A. ndiye aliyenifunza          B. ndio alionifunza           C. ndivyo alivyonifunza            D. ndiye alionifunza
  4. A. ya                                   B. na                                C. za                                         D. wa
  5. A. Mathalan                        B. Ihali                             C. Kwani                                   D. Kumbe
  6. A. mbali, ila. njema             B. tamu, nzuri, bora         C. hizo, vile, tena                     D. taratibu sana, vizuri
  7. A. alinivunja moyo              B. alinitia shime               C. alinipiga kumbo                    D. alinionea gere
  8. A. Mchumia juani hulia kivulini
    B. Jirani ni akiba
    C. Kofi hazilii ila kwa viganja viwili
    D. Jua vimeundwa
  9. A. Yakini                              B. Katu                              C. Kamwe                                D. Asilani

Elimu ina manufaa   10   Mtu    11   elimu ya kumfaa, maisha yake hugubikwa na giza    12  . Kwa mfano, kupitia elimu ya mazingira, tunajifunza jinsi     13  kuongeza    14    katika mazingira yetu. Vijana nao hufunzwa kutumia vipawa    15    kujikimu kimaisha

  1. A. anuwai                          B. nyingi                               C. mingi                                  D. kiasi
  2. A. asiopata                        B. asingepata                       C. asipopata                          D. asikopata
  3. A. tiriri                                B. totoro                               C. kochokocho                       D. furifuri 
  4. A. tunaoweza                    B. tunayoweza                      C. tunaweza                          D. tunavyoweza
  5. A. thamani                         B. dhamani                           C. ridhaa                                D. riba
  6. A. zao                                В yao                                    C. vyao                                  D. chao

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagmujawahu lifaalo zaidi kwa kila swali

  1. Bainisha matumizi ya kiambishi-ka kwenye sentensi.
    Mwalimu alituita akatushauri
    1. Kuonyesha masharti
    2. Kuonyesha hali ya kuendelea
    3. Kuonyesha kutegemeana kwa vitendo
    4. Kuonyesha kufuatana kwa matukio
  2. Chagua maelezo ambayo ni sahihi.
    1. Kikuku ni pambo la shingoni.
    2. Kipuli huvaliwa upande wa kushoto wa pua
    3. Kishaufu ni pambo la puani.
    4. Bangili ni pambo la mviringo la shingoni.
  3. Tunasema jua, juza na nawa
    1. navya
    2. nawia
    3. nawishwa
    4. nawika
  4. Andika katika wingi. Jirani ameniazima uteo wake.
    1. Jirani wamelazima uteo wao.
    2. Jirani wametuazima teo zao.
    3. Majirani wametuazima teo yao.
    4. Majirani wametuazima teo zao.
  5. Kamilisha: Mgonjwa alibebwa na wauguzi kwa _____ hadi kwenye wodi.
    1. ambulensi 
    2. machela
    3. toroli
    4. nyoka
  6. Kanusha: Mtoto alipoangukaaliumia.
    1. Mtoto alipoanguka hakuumia.
    2. Mtoto hajaanguka wala hakuumia
    3. Mioto asipoanguka hataumia.
    4. Mtoto hakuanguka na kuumia.
  7. Kutokana na kitenzi tii tunapata sifa gani?
    1. Utiifu
    2. Katii
    3. Mtiifu
    4. Tiliwa
  8. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya udogo.
    Mtoto alifurahi aliponunuliwa mkoba
    1. Kitoto alifurahi aliponunuliwa kikoba
    2. Toto lilifurahi liliponunuliwa koba.
    3. Vitoto vilifurahi viliponunuliwa vikoba.
    4. Kitoto kilifurahi kiliponunuliwa kikoba
  9. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Mlima wa Kwale hupandwa kwa kucha.
    1. Kula sima.
    2. Kusuka nywele
    3. Muwa
    4. Jiwe
  10. Sentensi gani kati ya hizi ni tashbihi?
    1. Sikio la kufa halisikii dawa.
    2. Jina jema ni hazina maishani.
    3. Mikono yake ni baridi kama barafu
    4. Wezi wale walikimbia mkiki mkiki.
  11. Fahali ni kwa mtamba kama ilivyo kipora kwa
    1. jogoo
    2. tembe
    3. beberu 
    4. kuku
  12. Andika katika usemi halisi.
    Kaka aliniambia kuwa tungeenda shambani siku ambayo ingefuata.
    1. "Utaenda shambani kesho" Kaka aliniambia.
    2. "Kesho wanaenda shambani" Kaka aliniambia
    3. "Tungeenda shambani kesho", Kaka aliniambia.
    4. "Mtaenda shambuni kesho," Kaka aliniambia.
  13. Msemo 'kuwa na kichwa kizito' una maana ya,
    1. kuwa na usingizi
    2. kutosikia
    3. kuwa na kichwa kikubwa
    4. kuwa mwerevu
  14. Kamilisha: Angalijua huko kulikuwa na wezi _______mlango.
    1. angefunga
    2. asingefunga
    3. hangalifunga
    4. angalifinga
  15. Chagua methali nyingine yenye maana sawa na hii.
    Akutanguliaye chanoni hukuzidi tonge.
    1. Mwenda mbio subiri achoke. 
    2. Ukiona vyaelca jua vimcundwa.
    3. Atanguliaye kisimani hunywa maji mengi.
    4. Mchimba kisima huingia mwenyewe.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40.

Hakuna kitu muhimu maishani kuliko afya ya akili. Kwa hakika afya hii ya akili ndiyo humwezesha mtu kutenda mambo jinsi anavyotakikana. Mtu mwenye afya ya akili huweza kutangamana vyema na wenzake bila kuwabughudhi kwa lolote. Aghalabu mtu huyu huwa mfurufu wakati wote, jambo ambalo humsaidia kudumisha hata afya ya mwili.

Matendo ya watu wengi katika siku za hivi karibuni yanadhihirisha kuwa afya ya akili inazidi kudorora. Imekuwa kawaida kama sheria kusikia kuwa mtu fulani amechukua silaha na kumwumiza mwenzake vibaya. Wengine wanatumia silaha za maangamizi ya halaiki pasi na kisa wala sababu. Baadaye watu hawa wakipelekwa mbele ya sheria huonekana kuchanganyikiwa; yaani hawajijui hawajitambui.

Je, ni nini hasa kinachochangia kuvurugika kwa afya ya akili? Kwanza, binandamu anapokabiliwa na hali ngumu ya maisha kila uchao, hujipata akihangaika kimawazo. Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu pasipo kushughulika ipasavyo, akili ya mhusika huweza kuenda tenge. Watu wengi, wakubwa kwa wadogo wanaendelea kuhangaika kwa sababu mbalimbali.
Matumizi mabaya ya vileo yamewafanya baadhi ya watu kuwa punguani. Kwa mfano, uvutaji wa bangi ni sababu kuu ya vijana wengi kurukwa na akili. Ni vyema tujitenge na waraibu wa mihadarati kwani niazi mbovu ni harabu ya nzima.Kwa hakika dawa hizi hazina manufaa yoyote.

Ili kudumisha afya ya akili, ni lazima ushauri nasaha uimarishwe katika sekta zote za kijamii. Kupitia ushauri walmarika shuleni kwa mfano, vijana watashauriwa kuhusu madhara ya kuandama sana starehe vilevile, watajifunza kuratibu muda wao na kuutumia kwa njia ya manufaa. Vilevile, wataelekezana kutambua mbinu mwafaka zaidi za kuepuka vishawishi vinavyoambatana na ujana.
Serikali haina budi kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya. Hili halitafanyika kwa kuwatia nguvuni waraibu tu. Huku ni kama kupogoa matawi ya mti na kuutarajia ukauke. Biashara hii sharti ikomeshwe kuanzia kwa wauzaji wa humu nchini na hata magenge ya kimataifa.

Mtu anapokabiliwa na tatizo, ni vyema kuwaendea washauri ili aongozwe kwa njia ifaayo. Wale walioathirika nao wajikubali na kutafuta matibabu kabla hali zao hazijazorota zaidi. Taifa halitaweza kupiga hatua bila raia wake kuwa razini.

  1. Chagua maelezo yanayolingana na aya ya kwanza.
    1. Afya ya akili ndicho kitu muhimu pekee maishani.
    2. Mtu akiwa na matatizo ya akili huoneakana waziwazi.
    3. Mtu asiye na afya ya akili ni mwendawazimu.
    4. Utendaji wa mtu huweza kuathiriwa na afya ya akili.
  2. Wanajamii wakiwa na afya ya akili,
    1. hudumisha uhusiano mwema baina yao.
    2. huvuruga maingiliano miongoni mwao.
    3. hawakabiliwi na shida zozote maishani.
    4. hukabiliwa na changamoto nyingi maishani.
  3. Kulingana na aya ya pili,
    1. malezi mabaya ya watoto yamewafanya wengi kupotoka.
    2. maovu yameongezeka kutokana na kuzorota kwa afya ya akili.
    3. matumizi ya silaha yanavuruga afya ya akili.
    4. si kawaida kwa watu siku hizi kuumizana kwa silaha.
  4. Maneno hawajijui hawajitambui yametumia tamathali gani ya usemi?
    1. Sitiari
    2. Tanakali za sauti
    3. Vielezi ya kutilia mkazo.
    4. Tashbihi
  5. Chagua jibu lililo sahihi.
    1. Wote wanaohangaika hupata shida za kiakili.
    2. Kukosa kusaidiwa husababisha matatizo ya akili.
    3. Kuhangaika kwa muda mrefu huathiri afya ya akili.
    4. Hali ngumu ya maisha ni mfano wa shida za kiakili.
  6. Hali anayopinga mwandishi hasa katika aya ya nne ni,
    1. hali ya vijana kurukwa na akili.
    2. madhara ya mihadarati hasa katika familia.
    3. watu wanaotumia pesa kununua mihadarati.
    4. matumizi mabaya ya vileo.
  7. Methali 'Nazi mbovu harabu ya nzima' ina maana kuwa,
    1. Ukifuatana na watu wabaya watakupotosha.
    2. Ukitumia mihadarati vibaya utahasirika.
    3. Vijana wakitumia mihadarati watakuwa punguani.
    4. Watu wazima wakiingilia ulevi vijana watawaiga.
  8. Yapi ni manufaa ya ushauri wa marika?
    1. Vijana huonyeshwa jinsi ya kuandama starehe.
    2. Vijana walioshauriwa hawapatani na vishawishi vyovyote.
    3. Vijana hujifunza kutumia muda wao ipasavyo.
    4. Vijana hushauriwa kuhusu dawa zifaazo.
  9. Kupogoa matawi ya mti kumelinganishwa na
    1. kuwanasa walanguzi wa mihadarati. 
    2. kuwashika wanaotumia mihadarati.
    3. kukabiliana na magenge ya kimataifa.
    4. kumaliza kabisa biashara ya mihadarati.
  10. Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni
    1. Madhara ya mihadarati.
    2. Umuhimu wa ushauri nasaha.
    3. Umuhimu wa afya ya akili.
    4. Serikali kupunguza shida za maisha.

Soma makala yanayofuata kisha ujibu maswali kuanzia 41 - 50.

Msenangu alifahamika katika kijiji chao na takriban kila mtu. Watoto walimfahamu kutokana na mtindo wake wa kutembea. Alitembea wima kama askarijeshi na kila alipokwenda kupiga chupa zake, alikuwa na mazoca ya kupiga kwata kama mwanajeshi gwarideni. Sababu nyingine iliyomfanya Msenangu afahamike ni ucheshi wake. Aliwasimulia vijana hadithi za kila aina na kuwavunja mbavu kwa umahiri wake wa kuzitamba hadithi zenyewe.

Ingawa Msenangu alikuwa na umri mpevu sana, alikuwa mmoja kati ya wazee wachache wa kwao waliojua kusoma. Idadi ya waliojua kusoma wakati huo ilikuwa akali sana na mzee huyo aliona fahari kuwa miongoni mwa hao wachache. Habari za kuandikwa kwa katiba mpya zilipofika kijijini, Msenangu alifurahi na kuchanua uso. Hii ni nafasi ya kuhakikisha kuwa nimewaeleza yote yanayohitajika kufanywa : alijitapa Msenangu. Wanakijiji walitaka kuteua vijana wawawakilishe ambapo tume ya kuandika katiba ampya ingefika pale kijijini. Hata hivyo, Msenangu alikazania kuwa ni lazima angekuwa mmoja wao. Licha ya uwezo wake wa kusoma, wanakijiji wengi hawakuamini kuwa alijua lolote kuhusiana na katiba.

Siku yenyewe, vijana walioteuliwa walitumia lugha ya kisheria ambayo ni dhahiri wanakijiji wengi hawakuielewa. Muda is muda, watu walianza kuondoka ukumbini mmoja mmoja. Ndipo bila kungoja aalikwe, mzee Msenangu alisimama. Watu waliokuwa nje ya ukumbi waliambiana, "Haya Msenangu huyo!' Alianza kuongea," Ndugu wanakamati, nimcisubiri fursa hii kwa hamu kubwa. Maneno yangu mimi si mengi kwani sikusoma mambo hayo ya "yesi" "yesi". Lakini ningependa kusema machache niliyo nayo moyoni. Nataka iandikwe katiba itakayoiendesha nchi yetu, kwa njia nzuri, kwa miaka mingi ijayo.Katiba hiyo ni lazima iwalinde raia wote, walemavu na wasio walemavu waonao na wasioona, waumini na walevi' alianza Msenangu. Watu walimtazama kwa mshangao mkubwa.
"Tulieni tumsikilize!” Wengine walisema. Wale waliokuwa wakiondoka ukumbini walirudi haraka kuketi. iangu akaendelea, “Katiba inayoifaa nchi ni ile isiyozingatia matakwa ya kundi moja la jamii tu... zima ziwepo njia za kuwadhibiti viongozi hawa kuhakikisha kuwa wanapotwaa madaraka hawatugeuzi sisi wanyonge kuwa wanase sere wao wa kuchezea, "alisema Msenangu na kutua. Ukumbi mzima sasa ukawa umemtegea sikio ndi!

Wanakumati walikuwa wakiandika huku wakiitikia kwa vichwa vyao. "Sisi wanyonge tunaoishi huku mashambani tuna shida. Wahenga walisema "Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma" Lakini kwetu huku haikati, inakala nyuma tu. Wenye vyeo wanapotamani vikataa vyetu wanavitwaa tu kwa njia rahisi wakitumia vyeo vyao. Tunaposhindwa kulipa pesa za michango ambazo hatuna, machifu wanaamuru mifugo yetu isombwe. Pawepo na sheria za kuwadhibiti watu kama hao. Kwa kifupi, iwe sheria inayotetea tajiri na maskini, mr yonge na mwenye nguvu, aliye nacho na asiye nacho.

Wanakamati wapendwa, usalama umeadimika kama mito jangwani. Sisi wenyewe tumegeuka walinda usalama. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba tuwatiapo wahuni hao mikononi mwa walinda usalama wanazunguka mbuyu na kuwa huru.
Katika nchi inayothamini raia wake, bei za bidhaa haziongezeki shaghalabaghala tu. Ningetaka katiba iangalie jambo hili."
Baada ya kusema haya Msenangu akachukua mkongojo wake na polepole akatoka ukumbini na kuuacha umati umeduwaa. Kisha ukumbi ukalipuka pu kwa makofi na vigelegele ukimshangilia Msenangu ambaye alikuwa tayari ameshaondoka.

  1. Chagua jibu lisilo sahihi
    1. Watu wote walimfahamu Msenangu.
    2. Msenangu alikuwa na tabia ya ulevi,
    3. Msenangu alizoca kuwafurahisha watu.
    4. Watoto walimfahamu Msenangu kwa kutembea kijeshi.
  2. Maana ya kuwavunja mbavu ni
    1. kuwaumiza mbavuni
    2. kucheka kisirisiri
    3. kuwachekesha sana
    4. kuwashangaza watu
  3. Ni jambo lipi alilojivunia Msenangu?
    1. Kupendwa na watu wengi.
    2. Elimu aliyokuwa nayo.
    3. Kuwashinda vijana kiclimu.
    4. Kuwa na wasomi kijijini.
  4. Msenangu alifurahishwa na habari za kuandikwa kwa katiba mpya kwa sababu,
    1. angeonyesha ubingwa wake kwa wale wasiomjua.
    2. angeshindana na vijana katika maarifa yao.
    3. aliwachukia viongozi waliokuwa mamlaka
    4. angependekeza njia za kuboresha utawala.
  5. Kwanini wanakijiji walianza kutoka ukumbini?
    1. Muda ulikuwa umeyoyoma.
    2. Hawakuzielewa hotuba ya wazungumzaji.
    3. Walikerwa na maneno ya Msenangu.
    4. Walipuuzwa na waandishi wa katibampya.
  6. Watu walishangazwa zaidi na Msenangu kutokana na,
    1. umaarufu wake wa kusema
    2. kupinga maovu ambayo hawakuyajua.
    3. kupigana na serikali iliyokuwa mamlakani.
    4. kuchangia hoja nzito zenye umuhimu.
  7. Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma kwani,
    1. haipendelei wala kumbagua yeyote.
    2. sheria haina manufaa kwa mtu yeyote.
    3. sheria wakati wote huwabagua wanyonge.
    4. huwaumiza watu wote katika jamii.
  8. Kulingana na maneno aliyoyasema Msenangu
    1. usawa ulikuwa ukizingatiwa huko zaidi.
    2. katiba ya zamani ilikuwa bora zaidi.
    3. wanyonge walikuwa wakidhulumiwa katika jamii.
    4. viongozi wa jamii walionyesha uzalendo.
  9. Nini kilichangia zaidi kudorora kwa usalama?
    1. Wananchi kukosa kushirikiana. 
    2. Uhaba wa kazi katika jamii.
    3. Kukosa sheria za kuwahukumu wahalifu.
    4. Ufisadi uliowafanya wahalifu kuachwa huru.
  10. Kilingana na aya ya mwisho
    1. Hotuba ya Msenangu ilikatizwa kwa makofi.
    2. Msenangu hakuwepo aliposhangiliwa.
    3. Bei za bidhaa zilikuwa juu sana.
    4. Msenangu alituzwa kwa mkongojo.

INSHA

Wewe ni mmojawapo wa wanafunzi wa darasa la nane shuleni mwako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wengine shuleni kuhusu jinsi ya kuimarisha matokeo yao katika mitihani.

MAAKIZO

  1. B
  2. D
  3. A
  4. C
  5. A
  6. D
  7. B
  8. C
  9. A
  10. A
  11. C
  12. B
  13. D
  14. A
  15. C
  16. D
  17. C
  18. A
  19. D
  20. B
  21. A
  22. C
  23. D
  24. A
  25. C
  26. B
  27. D
  28. A
  29. D
  30. C
  31. D
  32. A
  33. B
  34. C
  35. C
  36. D
  37. A
  38. C
  39. B
  40. C
  41. A
  42. C
  43. B
  44. D
  45. B
  46. D
  47. A
  48. C
  49. D
  50. B

 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - Class 8 End Term 1 Exam 2021 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students