MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne
Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.
Kusikiliza na kuongea ni stadi muhimu____1____kwa mwanafunzi__2__zinaimarisha usikivu na uelewaji mzuri wa mambo mbalimbali __3__hizi pia humtayarisha mwanafunzi ___4___ na kuyaendeleza maneno ya lugha hii ___5___Zinakusudiwa kumpa mwanafunzi ___6___ wa kujieleza bila woga. ___7___, ni sharti zifundishwe ____8____.
-
- katika
- kwa
- kwenye
- ndani ya
-
- kwa kuwa
- sana sana
- ama kweli
- kwa kweli
-
- Maoni
- MienendoMbinu
- Uerevu
-
- kuandika
- kutamka
- kusemewa
- kusoma
-
- vizuri
- nzuri
- mzuri
- wazuri
-
- bidii
- ujasiri
- uzembe
- mbinu
-
- Kwa hivyo
- Hata hivyo
- Mbali na hayo
- Kinyume na hivyo
-
- wanavyofaa
- wanavyohitajika
- vile inahitajika
- Kinavyohitajika
Gari___9___aina ya Mwamba ___10___ kwenye maskani ya kina Asmini, wengi wa wakazi waliingiwa na ___11___ wasijue la kufanya. Waama, wasiwasi huo wote ulitokana na jinsi ___12___ kuwa duni kiasi cha ____13___ na wakwasi wanaonuka pesa. Wasichokijua kilikuwa ni kwamba Asmini alikuwa kampata mfadhili wa kuyagharimia maradhi yaliyomzonga tangu zama za ___14___ hadi siku hiyo. Wallahi, ___15___.
-
- nyeupe
- leupe
- jeupe
- cheupe
-
- likaingia
- liliingia
- lilipoingia
- likiingia
-
- furaha kuu
- huzuni nyingi
- aibu kubwa
- tumbo joto
-
- walivyojichukua
- walichukulia
- walivyo
-
- kutembelewa
- kutotembeleana
- kutembeleana
- kutotembelewa
-
- kali
- zamani
- kitambo
- zama
-
- Mungu hamsahau mja wake
- siku ya nyani kufa miti yote huteleza
- mficha uchi hazai
- pole pole ndio mwendo
Kutoka swall la 16 hadi 30. Jibu kulingana na maagizo
- Vivumishi halisi pia huweza kuitwa vivumishi
- vya idadi.
- vya pekee.
- vimilikishi.
- vionyeshi.
- Mama ameenda sokoni katika hali ya wingi ni
- kina mama wameenda masokoni.
- mama wameenda sokoni.
- kina mama wameenda sokoni.
- mama wameenda masokoni.
- Kutokana na kitenzi andika, tunaweza kuunda nomino gani?
- Andika.
- Barua.
- Mwandishi.
- Insha.
- Chagua majina ya ngeli ya I-ZI pekee.
- Chuma, cheo, chupa.
- Rula, meza, kalamu,
- Nguo, ulimi, zeze.
- Darasa, shule, gwaride.
- Ni vazi gani kati ya haya huzuia mavazi ya ndani yasichafuke wakati wa kazi?
- Bombo.
- Kizibao.
- Buibui.
- Bwelasuti.
- Ni barua ya aina gani ambayo huwa na anwani moja? Barua ya
- kiofisi.
- kindugu.
- marafiki.
- kidugu.
- Teua sentensi yenye kivurishi cha sifa.
- Watu wanane wameangamia.
- Mwanafunzi yule ni mweledi.
- Maembe haya ni mabichi.
- Niletee kalamu nyingine.
- Tumia kiulizi ngapi. Marealiwa peremende
- mangapi?
- ngapi?
- mingapi?
- vingapi?
- Eleza matumizi ya ki.
Sakina amekichapa kitoto chake.- Masharti.
- Ngeli
- Udogo
- Kiwakilishi.
- Ni sehemu gani hupatikana shingoni?
- Ndewe.
- Kidakatonge
- Kiwiko.
- Kigasha.
- Jibu maamkizi yafuatayo:
U mzima?- Ni mzima.
- Tu mzima.
- Si wazima.
- Ni wazima.
- Akisami, 4/9 huitwaje kwa maneno?
- Robo tisa.
- Subui nne.
- Tusui nne.
- Sudusi nne.
- Kanusha sentensi ifuatayo:
Yaya anapiga deki. Yaya- hapigi deki.
- hajapiga deki.
- hakupiga deki.
- hatapiga deki.
- Dakika moja huwa na jumla ya sekunde ngapi?
- Sitini.
- Tisini.
- Arubaini na tano.
- Thelathini.
- Aliye na mtoto tumboni ni
- mtu mzito.
- mjamzito.
- mama.
- mimba
Soma kifungu kisha ujibu maswali 31 hadi 40.
Kila baada ya mtihani wa kitaifa kufanywa na matokeo kutangazwa rasmi na wanaohusika. huwa jambo la kawaida kuwaona wadau mbalimbali wakishangilia na kusherehekea matokeo ya bidii za wana wao na wanafunzi wao. Aghalabu, utawaona waliovuna pakubwa wakiinuliwa hanga hanga na kurushwarushwa hewani ovyo ovyo kwa kile ambacho kwa wakati huo huitwa shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa wanafunzi.
Aidha, katika barabara za mengi ya majiji na hata viungani, ni kawaida kuyaona magari ya manjano yakiongozana kwa milolongo huku "abiria" wakishangilia kwa shangwe, vifijo na cherekochereko. Ni kawaida pia kuyaona majina ya mabingwa wa shule mbalimbali yakiwa yamebandikwa ubavuni pa magari hayo katika karatasi pana angavu. Hakika, wakati huo huwa wakati wa kuvuna alichokipanda mpanzi. Waama, ukipanda pantosha, utavuna pankwisha.
Iwapo waliotia fora hustahili kushangiliwa hivyo na kuinuliwa hainehaine, je, wenzao ambao walikuwa na matokeo ya wastani au wale waliokuwa na alama zisizoridhisha hustahili zawadi gani? Si nao waliufanya mtihani huo huo? Ifahamike kuwa wanafunzi mbalimbali kote nchini hufanya mtihani mkuu wa kitaifa katika mandhari tofauti tofauti. Ni kweli kuwa baadhi yao hufanya mtihani huo wakiwa wodini na hata vizuizini. Wakati mwanafunzi mmoja analifurahia joto la darasa na mapochopocho wakati wa mafunzo, mwengine kwingine anangurumwa na tumbo huku akivumilia baridi shadidi chini ya mti, sehemu anayoiita darasa, ilhali wote wanausubiri mtihani huo huo. Kuna uwezekano wa wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu kufanya vizuri iwapo hali ya maisha itakuwa sawa kwa watahiniwa wote.
Kwa upande mwingine, si jambo la kawaida kuwaona walimu waliowaandaa wanafunzi wanaofuzu wakiangaziwa katika vyombo vya habari. Ama wanafunzi hawa hujielimisha wenyewe? Aghalabu, shule zao, baadhi ya watu wa familia zao na wao wenyewe ndio wapatao umaarufu. Ajabu ni kuwa, umaarufu huu huwa kama moto wa karatasi ambao haukawii kuzima. Hivi ni kwa sababu, pindi wafikapo sekondari, umaarufu wao hupotea na kuzima mfano wa kibatari kilichotumbukizwa majini ghafla. Hakuna ajuaye hali ya elimu yao katika shule za upili. Mwisho, heko kwa serikali hii ya tano kupitia Wizara ya Elimu kuibua mtindo mpya wa kuyatangaza matokeo baada ya kuyafanyia kazi kwa kipindi kifupi cha muda. Siku hizi ni mshindi tu ndiye atangazwaye, tena bila jina lake bali alama zake tu, kinyume na hapo awali ambapo majina ya wanafunzi, shule zao na alama zao yaliwekwa wazi.
Kaa Salama-Nawa mikono na uvae barakoa!
- Kwa mujibu wa aya ya kwanza.
- sherehe hupamba moto wakati wa mtihani mkuu wa kitaifa.
- walimu huhusika katika kutangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa
- ubingwa wa baadhi ya wanafunzi katika mtihani mkuu hushangiliwa.
- magari mengi hufuatana kama njia ya kusherehekea matokeo ya wanafunzi.
- Kwa maoni yako, wanaohusika ni kina nani?
- Wizara ya Elimu.
- Walimu wakuu katika shule zilizofuzu.
- Viongozi wakuu serikalini.
- Wanafunzi waliotia fora katika mtihani mkuu.
- Mwandishi ametaja namna ngapi za kuwashangilia wanafunzi waliofanya vizuri?
- Tatu.
- Nne.
- Moja.
- Mbili.
- Methali iliyotumika mwishoni mwa paragrafu ya pili inamlenga nani hasa?
- Mwanafunzi katika shule ya msingi.
- Walimu waliofanya bidii kuwafunza wanafunzi waliotia fora.
- Mwanafunzi ambaye ameukamilisha mtihani mkuu.
- Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Mwandishi anatudokezea kuwa wanafunzi waishio katika mandhari duni wakipata mandhari nafuu,
- ushindani utaimarika baina ya makundi haya mawili.
- wanaweza kufanya vyema zaidi katika mitihani.
- watawashinda wale wanaioshi katika mazingira salama.
- hali ya kielimu inaweza kuimarika maradufu.
- Taarifa imeweka wazi kuwa si jambo la kawaida
- walimu wa wanafunzi waliofuzu kuangaziwa.
- wazazi wa wanafunzi waliofaulu kuangaziwa.
- wanafunzi waliotia fora kuangaziwa.
- shule za wanafunzi waliofaulu kuangaziwa.
- Inawezekana kuwa wanafunzi wanaofanya mtihani mkuu wakiwa wodini huwa
- wauguzi.
- wahalifu.
- wagonjwa.
- washukiwa.
- Kidokezi ngarafu huu huwa kama mote wakeratasi ambao haukawii kuzima kinatoa wazo gani?
- Wanafunzi wanaofanya vizuri katika shule za msingi hupotea pindi wafikapo sekondari
- Baadhi ya wanafunzi huwa hawafanyi vizuri sekondari ama walivyofanya katika shule za msingi.
- Majina ya wanafunzi waliofuzu katika shule za msingi husahaulika wavukapo daraja.
- Wanafunzi waliotia fura katika shule za msingi huanza kuwa mazuzu.
- Msimulizi anaipa serikali ya tano mkono wa tahania kwa
- kuorodhesha majina ya wanafunzi waliotia fora.
- kuongeza muda wa kuhakiki matokeo ya mtihani mkuu.
- kuzua namna mpya ya kupeperusha matangazo ya matokeo ya mtihani mkuu.
- kupanga matokeo ya mtihani mkuu kulingana na kaunti.
- Hapo awali
- matokeo ya mtihani mkuu yalishughulikiwa kwa muda mfupi.
- majina na shule za wanafunzi yaliorodheshwa sambamba na alama zao.
- alama za mwanafunzi bora tu ndizo zilizotangazwa.
- wanafunzi wote waliofanya mtihani nchini waliangaziwa
Soma kifungu kisha ujibu maswali 41 hadi 50.
Sherehe nyingi kupita kiasi na anasa yalikuwa yamepita mpaka katika mji wa Peponi. Ingawa walikuwa na bidii kuliko za mchwa, mapato yao na mali waliyochuma yaliishia katika vileo haramu na sehemu nyinginezo za anasa.
Si hayo tu, mjini humo alitokea kidosho mmoja aliyekuwa na aina mpya ya kileo alichokiuza kisirisiri kwani kilikuwa haramu. Kileo hicho kiliwavutia sana wengi hususan wanaume ambao kila wakati walimwita kando ili awauzie pombe hiyo mpya. Siku zilizidi kusonga huku waliokionja kileo hicho wakawaita wenzao nao wapate kukionja bila kujua kuwa kileo hicho kilikuwa haramu na chenye sumu. Daima walijipa moyo kwa ule usemi usemao, kiingiacho mjini si haramu. Ole
wao!
Wave's wachanga walipopata ripoti kuhusu pombe ile mpya na kile walichokiita utamu wake, walijaribu kadiri walivyoweza ili angalau wapate fursa ya kuionja. Waliifurahia mno. Nyumbani kowe Bwana Chachandu, alikuwapo mwanawe aliyeitwa Sheshe na yaya aliyekuwa na jukumu la kumshughulikia kitindamimba katika familia hiyo, Majaliwa. Daima, Puza alimshughulikia Majaliwa bila kununa. Bwana Chachandu alipopata habari za kileo kile kipya, hakutaka kuachwa nyuma. Naye alipata fursa ya kukionja na hata kujibebea kiasi katika chupa ndogo ya plastiki. Si hunenwa kuwa akiba haiozi! Chachandu alilifahamu hili barabara.
Chachandu alipofika nyumbani, alimlazimisha Puza kukionja kileo kile. Ingawa Puza alijaribu kukataa, alitishiwa kuadhibiwa ikambidi naye apate kukionja kileo kile. Angurumapo simba hucheza nani? Siku mbili tatu, Puza alinyatia na kuichukua pombe iliyosalia chupani na kumwonjesha Sheshe. Bwamdogo alipokionja kileo kile, alifurahia mno.
Baada ya muda, ilifahamika kuwa pombe yenyewe haikuwa salama mwilini. Walioshiriki pombe hiyo walianza kufariki mmoja mmoja. Mama wa Majaliwa alipopata habari hizo, aliamua kuwaita waganga na waganguzi maana dalili mbaya zilianza kuonekana kwake nyumbani. Baada ya mama wa Majaliwa kushawishiwa na mumewe, naye akaonjeshwa kileo kidogo kilichokuwa kimebaki.
Baada ya kipindi cha muda, madhara ya pombe ile yalikuwa yamekolea mno mjini mote. Maskini nyumbani mwa Bwana Chachandu akabakia mmoja tu. Wengine wakasafiri jongomeo.
- Licha ya yaya, familia ya kina Majaliwa ilikuwa na watu wangapi?
- Watano
- Watatu
- Sita
- Wanne
- Kulingana na taarifa, ni kauli gani ni ya kweli?
- Mzee Chachandu alipewa pombe n mjakazi.
- Mjakazi alimpa S..she kileo hatari.
- Puza alipewa kileo hatari ne kidosho.
- Bi. Chachandu alijaribu kukataa kunywa pombe akalazimishwa.
- Wakazi wengi wa Peponi
- hawakuwahi kupatikana baani.
- hawakuwa walevi.
- hawakushiriki michezo sana sana.
- hawakupenda raha kupita kiasi.
- Ni kwa nini Puza alikipokea kileo cha sumu?
- Alitishiwa.
- Aliadhibiwa.
- Alikuwa akikitaka.
- Alikuwa akikitamani.
- Ni kundi gani kati ya haya lilifurahi mno baada ya kupata taarifa kuhusu pombe ya kigeni? Vijana
- wote.
- wa kike.
- wa kiume.
- kwa wazee.
- Mtoto wa mwisho katika familia ya Bwana Chachandu alikuwa nani?
- Sheshe.
- Puza.
- Kidosho.
- Majaliwa.
- Kulingana na makala haya, ni yupi alikuwa yaya?
- Sheshe.
- Puza.
- Majaliwa.
- Kidosho.
- Ni bwamdogo gani aliyerejelewa katika ufahamu?
- Sheshe.
- Puza.
- Majaliwa.
- Chachandu.
- Kwa maoni yako, ni yupi kati ya hawa hakufariki kutokana na kileo hatari?
- Puza.
- Chachandu.
- Mama wa Majaliwa.
- Majaliwa.
- Mwishoni, mwandishi anatueleza kuwa, licha ya mmoja, wengine wote
- walienda safari ya mbali.
- waliugua sana.
- waliaga dunia.
- waliathirika zaidi.
MARKING SCHEME
INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
Endeleza insha ifuatayo kwa maneno yake mwenyewe na ulfanye iwe va kusisimua.
Sote tulikuwa na furaha mpwitompwito kutia guni katika darasa la nane. Asubuhi hiyo, kipindi cha kwanza kilikuwa cha Kiswahili. Mwalimu alipoingia darasani........................................................................
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 6.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students